JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
IRELAND: Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) inayosimamia Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPC) imeipiga faini kampuni ya #META baada ya kuendelea kuhamisha #Data za watumiaji wa #Facebook kwenda #Marekani, licha ya zuio la Mahakama

DPC ilitoa miezi 5 kwa #META kusitisha uhamishaji wa Taarifa Binafsi za Watumiaji wake ikiwa ni utekelezaji wa zuio la Mahakama ya EU lililotolewa mwaka 2020 dhidi ya kampuni zinazochakata na kuhifadhi #TaarifaBinafsi

Soma https://jamii.app/MetaFines

#JamiiForums #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #Accountability
πŸ‘3
MAREKANI: Kampuni #META inayomiliki Mitandao ya Kijamii ya #Facebook, #Instagram na #WhatsApp, imezundua 'App' nyingine ya Kijamii inayoelezwa kuwa itakuwa mshindani wa #Twitter

Mkurugenzi Mkuu wa META, #MarkZuckerberg amesema kuna kitu Twitter walipaswa kufanya na hawajakifanya hivyo 'Threads' inakuja kwaajili hiyo, japo itachukua muda kuifikia Twitter lakini Mtandao huo unalenga kuhudumia zaidi ya Watu Bilioni 1

Hata hivyo, Watumiaji wameonesha wasiwasi wao kuhusu kiwango cha 'TaarifaBinafsi zinazokusanywa na 'Threads' zikiwemo Taarifa za Afya, Fedha na aina ya Kivinjari (Browser), vyote vikiwa na uhusiano na Utambulisho wa Watumiaji.

Soma https://jamii.app/Threads

#JamiiForums #DigitalRights #Innovation #JFDigitali #DigitalWorld
πŸ‘9
NORWAY: Mamlaka ya Ulinzi wa #TaarifaBinafsi imeipiga Faini ya Tsh. Milioni 243.7 kampuni ya META kwa kutoweka wazi jinsi inavyotumia Faragha za Wateja wake na kuwatumia Matangazo ya Biashara bila Ridhaa yao

Faini hiyo italipwa kila siku kuanzia Agosti 14 hadi Novemba 3, 2023 na inaweza kuwa ya moja kwa moja endapo Bodi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Ulaya (EDPB) itaamua hivyo

#META ilipewa hadi kufikia Agosti 4, 2023 iwe imetoa taarifa kuhusu matumizi ya Data za Watu lakini haikutekeleza.

Soma https://jamii.app/METANorway

#JamiiForums #DataProtection #Governance #DataPrivacy #DigitalRights #Accountability
πŸ‘8
Ili Wakazi wa #UmojaWaUlaya (EU) waweze kufurahia Haki zao za Msingi za Faragha (ad-free service) chini ya Sheria ya Umoja wa Ulaya pindi wanapotumia #Facebook na #Instagram, watatakiwa kulipia Tsh. 35,138 kwa Mwezi, au 421,667 kwa Mwaka ili kupata Faragha hiyo

Kampuni ya #Meta inayomiliki Mitandao hiyo ya Kijamii imekuja na pendekezo hili kama jaribio la kutii Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya EU inayotishia kuzuia uwekaji wa Matangazo kwa watumiaji bila idhini yao

Soma https://jamii.app/MetaPayForYourRights

#JamiiForums #DataProtection #DataPrivacy #JFDigitali #DigitalRights
πŸ‘3❀1
Benki ya Dunia (WB) imeitaka Kenya kufanya mabadiliko ya Sheria inayoweka ulazima kwa Kampuni Nchini humo kutunza #TaarifaBinafsi kwenye 'Server' zilizopo ndani ya Nchi ikilenga kurahisisha Uwekezaji wa Huduma za Kidijitali kutoka Mataifa mengine

Kwa mujibu wa WB, Sheria hiyo inaweka vikwazo vya Kibiashara kwa Huduma za Dijitali hasa wakati ambao Kampuni kubwa Duniani ikiwemo #Google, #Meta, #TikTok, #Netflix, #Oracle, #Apple na #Microsoft zikizidi kufungua fursa za Uwekezaji Nchini humo na kuwa chanzo muhimu cha Ajira na Mapato ya Kodi

Soma https://jamii.app/ServerKenya

#JamiiForums #Governance #PersonalDataProtection #DataPrivacy #Accountability
πŸ‘4
Andrew Karamagi (Uganda), akiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya AZAKI, ametambulisha dhana inaitwa 'Techno-Feudalism' yaani Ukabaila wa Kiteknolojia

Anasema Duniani kuna Kampuni kubwa Tano (5) za #Teknolojia yaani Alphabet (inamiliki #Google), #Meta (inamiliki Facebook, #Instagram, #WhatsApp), Amazon, #Apple na Microsoft

Kampuni hizi zinamilikiwa na Watu wachache na tunawapa taarifa nyingi mno ikiwemo alama za vidole, sura zetu n.k. Hatujui zinaenda wapi na Kampuni hizi zina pesa sana kiasi kwamba Bajeti ya kununua vifaa vya Ofisi tu vya #Google ni zaidi ya pato la Taifa la Nchi zetu.

Je, nchi zetu zikitaka kutengeneza #Sheria za kusimamia Kampuni hizi zitaweza?

Kila mara unapoenda Mtandaoni kununua kitu unaamini unanunua bidhaa, ila ukweli mchungu ni kuwa wewe ndio bidhaa. #Taarifa zako zinauzwa kwa Kampuni mbalimbali na zina thamani kweli kweli

#JamiiForums #DigitalWorld #TechnoFeudalism #TechGiants #CSOWeek2023 #WikiYaAZAKI2023 #Technology
πŸ‘2
MAREKANI: Majimbo 41 na D.C. yamefungua mashtaka dhidi ya Meta yakidai Kampuni hiyo inadhuru Watoto kwa kuunda vipengele kwenye Mitandao ya #Instagram na #Facebook ambavyo vinawafanya kuwa na uraibu

Uamuzi huo umetokana na uchunguzi wa Mwaka 2021 kuhusu madai kuwa #Meta inachangia changamoto ya Afya ya Akili kwa Vijana wengi

Inadaiwa Meta ilijihusisha kuwanyonya watumiaji Vijana kwa faida, kuwapotosha kuhusu vipengele vya Usalama na kuenea kwa Maudhui hatari, Kukusanya taarifa zao na kukiuka Sheria kuhusu #Faragha ya Watoto

Soma https://jamii.app/MetaIGFC

#DataPrivacy #DataProtection #JFDigitali #DigitalRights #PersonalDataProtection #JamiiForums #MentalHealth
😐4πŸ‘3
#BIASHARA: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kitendo cha Serikali kupitisha Kodi ya Matangazo Madogo ya Mitandaoni kitawarudisha nyuma Wafanyabiashara wanaotarajia kufungua Maduka siku za mbele

Kauli ya Mbowe inakuja baada ya Kampuni ya #META inayomiliki Mitandao ya #Facebook, #Instagram, #WhatsApp na #Thread kutangaza kuwa Wafanyabiashara wanaotangaza Bidhaa zao kupitia Mitandao wataanza kukatwa 18% ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuanzia Desemba 1, 2023

Amesema "Serikali inayotoa msamaha wa kodi kwa Kampuni zenye mitaji ya Mabilioni, imegoma kuwapatia Wananchi wake ahueni. Serikali inaendelea kujaza kodi kila sehemu huku ikishindwa kudhibiti wizi wa kodi ambazo Watanzania wamelipa"

Soma https://jamii.app/MboweVAT

#JamiiForums #Governance #DigitalRights #Accountability #FreeSpeech #Democracy
πŸ‘12❀4
#DIGITALI: Tume ya Udhibiti wa Maudhui Mitandaoni ya Umoja wa Ulaya (EU) imeitaka META, kampuni inayoendesha Mitandao ya Kijamii ya #Instagram, #Facebook, #Thread na #WhatsApp kujieleza namna inavyodhibiti maudhui ya Unyanyasaji wa Kingono dhidi ya Watoto

Wito wa kwanza ulitumwa META Novemba 2023 ukitaka maelezo ya Usalama wa Watoto Mtandaoni. #EU imesema mwisho wa wito ni Desemba 22, 2023, kinyume na hapo #META itachunguzwa kwa Mujibu wa Sheria za Umoja wa Ulaya

Sheria mpya ya Huduma za Dijitali ya Umoja wa Ulaya (DSA) inazitaka kampuni za #Teknolojia zinazojihusisha na Uchakataji wa Maudhui Mitandaoni kuhakikisha zinaondoa maudhui yasiyofaa na hatari kwenye mifumo yao.

Soma https://jamii.app/METAEU

#JamiiForums #DigitalRights #InternetSafety #CyberSafety #ChildRights #Accountability #JFDigitali
πŸ‘3
MAREKANI: Akihojiwa wakati wa kikao cha Bunge la Seneti, Mkurugenzi Mtendaji wa #Meta, #MarkZuckerberg ameomba msamaha kwa Familia zinazodai Watoto wao waliathiriwa au kujidhuru kutokana na maudhui ya Mitandao ya Kijamii

Zuckerberg anayemiliki #WhatsApp #Instagram na #Facebook amesema hayo katika kikao ambacho pia kilihusisha Viongozi wa TikTok, Snapchat, X (Twitter) na Discord ambapo wote kwa pamoja walihojiwa kwa Saa Nne

Pia, Shou Zi Chew kutoka TikTok aliulizwa kama kampuni yake inatoa 'data' za watumiaji wa Marekani katika mtandao wao na kuipa Serikali ya China, alikanusha jambo hilo

Soma https://jamii.app/MitandaoKwaWatoto

#DigitalWorld #DigitalRights #ChildRights #Technology #JFDigitali #JamiiForums
πŸ‘4
NIGERIA: Serikali imeitoza Kampuni ya META faini ya Dola za Marekani Milioni 220 (takriban Tsh. Bilioni 583.8) baada ya Mitandao ya WhatsApp na Facebook kukutwa na makosa ya ukiukwaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Haki za Wateja

Taarifa ya Tume ya Ushindani na Ulinzi wa Haki za Walaji ya Nigeria (FCCPC) imesema baadhi ya makosa ni kutoa Taarifa Binafsi za Wateja bila ridhaa yao, Kutowapa haki ya kujua taarifa zao zinatumikaje, vitendo vya ubaguzi na matumizi mabaya ya taarifa za masoko

FCCPC imesema, #META imeshindwa kuzingatia Kanuni ikiwemo kutowasilisha ripoti ya ukaguzi wa Kanuni za Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa miaka miwili. Nigeria inakadiriwa kuwa na Watumiaji wa Intaneti zaidi ya Milioni 154

Soma https://jamii.app/NGRDataPrivacy

#JamiiForums #DataProtection #DataPrivacy #DigitalRights #Governance #SocialJustice
πŸ‘5
NIGERIA: Kampuni ya #Meta imefuta akaunti 63,000 za #Facebook za Raia wa #Nigeria, kama hatua ya kudhibiti Utapeli wa Mtandaoni, akaunti 2,500 kati ya hizo zilikuwa zikifanya Utapeli wa Kingono

Imeelezwa kuwa, akaunti hizo zilitumika kulaghai pesa raia wa Marekani hususan Wazee na Watoto, kwa tishio la kuvujisha picha za utupu ambazo nyingine ni 'feki'

Pia, wamefungia akaunti za Matapeli wanaojifanya wawekezaji kwa kuahidi kiasi kikubwa cha fedha, huku wengine wakijifanya wawekezaji kwa kuahidi faida kubwa maarufu kama β€œ#YahooBoys”

Soma https://jamii.app/FacebookKuvutaAkauntiUtapeli

#JamiiForums #DigitalSecurity #Uwajibikaji #CyberSecurity #DigitalWorld #CyberThreats
πŸ‘4
DIGITALI: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Ireland (DPC) imeipiga faini ya takriban Tsh. Bilioni 273 Kampuni ya #META baada ya kubainika 'Passwords' za Watumiaji Milioni 600 wa Facebook zilivujishwa kwa Wafanyakazi

Kwa mujibu wa taarifa, META haikutekeleza hatua madhubuti za kiusalama za Shirika ili kulinda #TaarifaBinafsi za watumiaji dhidi ya Wadukuzi. Pia, ilishindwa kudhibiti hatari zinazoweza kuathiri taarifa zilizohifadhiwa katika 'Seva' zake

Tangu Mwaka 2018, META inakadiriwa kukumbwa na Kesi zaidi ya 8 za ukiukwaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, ambazo zimekuwa zikiigharimu Kampuni hiyo Mabilioni ya Fedha kupitia faini inazopigwa.

Soma https://jamii.app/FineMETA

#JamiiForums #DataProtection #DigitalRights #DataPrivacy #JFDigitali
πŸ‘1
MAREKANI: Kampuni ya #META imewafukuza Wafanyakazi zaidi ya 24 ambao walibainika kutumia Fedha ziliwekwa kwenye Kuponi za Chakula wakiwa kazini na kununua Mahitaji mengine zikiwemo Sabuni za Kufulia na Dawa za Meno

META imesema imechukua uamuzi huo kwa Wafanyakazi wa #WhatsApp, #Instagram na #Facebook ambao wamekuwa wakitumia kinyume na makubaliano marupurupu, pia imewahamisha vitengo wengine

Kampuni hiyo imekuwa ikitoa Chakula bure kwa Wafanyakazi katika Migahawa ya Ofisi za Silicon Valley, na walio nje ya ofisi hupewa Dola 70 (takriban Tsh. 190,750) kila siku kwaajili ya Huduma hiyo kila siku.

Soma https://jamii.app/LayoffMeta

#JamiiForums #Governance #Accountability #SocialJustice
πŸ‘2
MAREKANI: Kampuni ya #META imeshinda kesi iliyofunguliwa Mwaka 2019 iliyokuwa ikiituhumu Kampuni ya NSO Group ya Israel kutumia Programu yake ya 'Pegasus' kudukua mawasiliano ya Watumiaji wa Mtandao wa WhatsApp

Uamuzi wa Mahakama umetokana na kubaini kuwa #NSO ilikiuka Sheria za Mkataba wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi na hivyo kuingilia na kufuatilia Mawasiliano ya watumiaji 1,400 wa #WhatsApp wakiwemo Waandishi wa Habari, Watetezi wa Haki za Binadamu na Wapinzani

Katika utetezi wake, NSO imesema, #Pegasus husaidia Idara za Usalama kutekeleza Sheria za Kijasusi katika kupambana na uhalifu na kulinda usalama na kwamba Teknolojia yake inalenga kusaidia ukamataji wa Magaidi na Wahalifu wengine wasiopatikana kirahisi

Ripoti mbalimbali za masuala ya Haki za Binadamu zimekuwa zikiitaja NSO Group kushirikiana na Serikali za Mataifa yasiyofuata misingi ya Utawala Bora katika kutekeleza vitendo vinavyokiuka Haki za Binadamu.

Soma https://jamii.app/PegasusApp

#JamiiForums #DataPrivacy #HumanRightsViolations
πŸ‘4
DIGITALI: Taarifa ya Mmiliki wa #META, Mark Zuckerberg imesema majaribio ya utaratibu wa kutumia Madokezo ya Kijamii (Community Notes) kuhakiki Maudhui utaanza kwa Watumiaji waliopo Marekani na baadaye utaendelea kwa watumiaji Duniani kote

Awali, META ilikuwa ikitumia timu maalumu ya Uhakiki wa Maudhui na Mifumo ya Kiotomatiki, utaratibu ambao ulikuwa ukilalamikiwa kuwa unabana Uhuru wa Kujieleza

Inadaiwa kuwa hatua hiyo ni mkakati wa META kujenga uhusiano na Utawala mpya wa Rais #DonaldTrump atakayeingia Ikulu Januari 20, 2025.

Soma https://jamii.app/FactCheckers

#DigitalRights #FreeSpeech #FreedomOfExpression #JFDigitali #JamiiForums
πŸ”₯1
MAREKANI: Kampuni ya #META imeanza kutekeleza mpango wake kwa kuwapunguza kazi Wafanyakazi 4,000 katika sehemu mbalimbali Duniani wanaoshindwa kufanya vizuri na kujiandaa kwa ajili ya uwekezaji mkubwa kwenye matumizi ya Akili Mnemba (AI)

Januari 2025, Kampuni ya Meta ilitangaza mpango wa kupunguza takriban 5% ya Wafanyakazi kwa kuzingatia utendaji wao kazini

Aidha, kampuni hiyo imewapa Wafanyakazi walioathiriwa na punguzo hilo nchini Marekani malipo ya kuachishwa kazi ya mishahara ya Wiki 16 na nyongeza ya wiki mbili kwa kila Mwaka wa utumishi

Soma https://jamii.app/MetaJobLayoff

#JamiiForums #Governance #SocialJustice
πŸ‘1
MAREKANI: Serikali kupitia Tume ya Biashara imeishtaki Kampuni ya #Meta, ikidai ununuzi wa Mitandao ya Kijamii ya #Instagram na #WhatsApp ulikuwa na nia ya kuondoa Ushindani katika Sekta ya Mitandao ya Kijamii

Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa leo Aprili 14, 2025, Washington DC inatarajiwa kuchukua Wiki kadhaa, huku Mwanzilishi wa Meta, Mark Zuckerberg, pamoja na aliyekuwa Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Sheryl Sandberg wakitarajiwa kutoa ushahidi

Imeelezwa, ingawa FTC iliidhinisha manunuzi ya Mitandao hiyo, imeendelea kufuatilia athari zake kwa ushindani wa soko na kama itashinda kesi hiyo, Meta inaweza kulazimika kuuza Instagram na WhatsApp

Meta si Kampuni pekee ya Teknolojia inayochunguzwa kwa tuhuma za ukiritimba. Google pia inakabiliwa na uwezekano wa kulazimishwa kuuza kivinjari (Browser) chake cha #Chrome ili kuvunja utawala wake katika soko la Utafutaji mtandaoni (Online Search)

Soma https://jamii.app/MetaKuuzaIgNaWhatsApp

#JamiiForums #EmbracingTechnology #DigitalWorld
Akizungumzia suala la Waandaa Maudhui kunufaika kupitia Majukwaa ya Kidigitali, Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica amesema "Tumezungumza na wenzetu #Meta, tunashirikiana nao na baadhi ya vikao kati yetu na wao tutafanya kwa njia ya Digitali ili Wadau wengine washiriki na waweze kutoa maoni yafanyiwe kazi. Mikutano hiyo itashirikisha Wadau mbalimbali wakiwemo wa Serikalini na Sekta Binafsi"

Awali Mwakilishi wa Meta, Mercy Ndegwa alisema wameona Majukwaa yao ya Whatsapp na Instagram yamekuwa yakifanya vizuri, hivyo kwa kushirikiana na Wadau wanatafuta namna ya kuweka njia ya kuwawezesha Watumiaji wa majukwaa hayo kujipatia Fedha (Monetization)

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
πŸ‘2
Kupitia Televisheni ya Taifa ya Iran, Wananchi wamehimizwa kuondoa programu ya #WhatsApp kwenye Simu zao, ikidaiwa (bila ushahidi wowote wa moja kwa moja) kuwa programu hiyo inakusanya taarifa za Watumiaji na kuzipeleka kwa #Israel

Katika taarifa yake, Kampuni ya #Meta ambayo inamiliki WhatsApp imesema β€œTunasikitishwa na ripoti hizi za uongo ambazo huenda zikatumiwa kama kisingizio cha kuzuiwa kwa Huduma zetu wakati Watu wanazihitaji zaidi.”

Serikali ya #Iran imekuwa ikizuia upatikanaji wa Mitandao mbalimbali ya Kijamii kwa Miaka mingi, lakini Watu wengi nchini humo hutumia mbinu za kukwepa vizuizi hivyo kama #proxies na Mitandao Binafsi ya Intaneti (VPNs) ili kuendelea kupata Huduma

Mwaka 2022, Iran ilipiga marufuku WhatsApp na Google Play wakati wa Maandamano makubwa ya kupinga Serikali yaliyotokana na kifo cha Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa na Polisi wa Maadili wa Nchi hiyo. Marufuku hiyo iliondolewa mwishoni mwa Mwaka 2024

Soma https://jamii.app/IranVSWhatsApp

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
❀1