JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Serikali imeamuru Kampuni za Mitandao ya Kijamii nchini humo kuwa na Ofisi chini ya Mamlaka ya Wizara ya Mambo ili kuboresha uwajibikaji na kupambana na matumizi mabaya ya Majukwaa ya Kidijitali

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema kuwa kumekuwa na ongezeko la Visa vya unyanyasaji, uchochezi wa vitendo vya chuki na vurugu katika mitandao ya kijamii na hivyo inahitajika njia ya kudhibiti matukio hayo

Aidha, Wizara hiyo imetoa wito kwa Watoa Huduma za Mawasiliano (Telecommunications Providers) na Wamiliki wa Majukwaa ya Kidigitali kuchukua hatua kali dhidi ya shughuli za Uhalifu Mtandaoni

Soma https://jamii.app/KampuniDigitaliKuwaOfisi

#JamiiForums #Accountability #FreedomOfSpeech #CyberSecurity
Mdau umewahi kutapeliwa Mtandaoni, ilikuwaje na ulichukua hatua gani baada ya tukio hilo?

Mjadala Zaidi https://jamii.app/UtapeliMtandaoBasi

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Mdau kabla ya kuagiza vitu mtandaoni huwa unazingatia vitu gani ili uepuke kupigwa au kutapeliwa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/BiasharaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Baadhi wa Wafanyabiashara 'feki' hutumia Mitandao ya Kijamii kufanya utapeli ambapo hutumia mbinu ya kuambiwa utume pesa ili utumiwe bidhaa yako

Aidha, unaweza kutuma pesa na kupokea bidhaa ambayo haina uhalisia na kile ulichoagiza au walichopost kwenye Mitandao

Mdau, ni dalili gani nyingine ukiiona unajua kuwa Mfanyabiashara ni tapeli wa Mtandaoni?

Mjadala zaidi https://jamii.app/BiashazaZaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
USIBOFYE ‘LINK’ USIYOIFAHAMU AU USIYO NA UHAKIKA NAYO

Utapeli umeongezeka Mtandaoni, njia mojawapo ni kutumiwa Kiunganishi (Link), ambapo wengi wametoa taarifa zao binafsi kama nywila (Password) za benki, za Mitandao ya Kijamii au taarifa nyingine muhimu baada ya kubofya kiunganishi wasichokifahamu au kuwa na uhakika nacho

Matapeli hutuma Viunganishi vilivyoambatana na ujumbe mfupi, mzuri wa kuvutia au unaoonesha hali ya dharura na wanatuma kama SMS ya kawaida au kupitia Mitandao ya Kijamii kama WhatsApp, Facebook na mingine

Je, umewahi kukutana na ujumbe gani ukajua unatapeliwa?

Zaidi soma https://jamii.app/ZuiaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #OnlineFraudAndScam #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli #JFDigitali
👍1
Utapeli mtandaoni umekuwa tishio kubwa kwa Watu Binafsi na Taasisi

Kila siku, Watu wanapoteza pesa na taarifa zao za siri kwa njia za ujanja zinazobuniwa na matapeli wa mtandao.

Je, ni hatua zipi zichukuliwe ili kukomesha vitendo vya kitapeli mtandaoni?

Mjadala zaidi https://jamii.app/TunajilindajeUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameelezea kisa chake ambapo alinusurika kutapeliwa Mitandaoni. Ameshauri watu kuacha tamaa kwani vile vya bure huja na gharama kubwa

Mjadala zaidi https://jamii.app/NilivyonusurikaKutapeliwa

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
👍2
Matapeli wa kupitia Mitandao huwa na mbinu mbalimbali za kulaghai na kuibia watu na mara nyingi huwalenga wenye tamaa, wenye shida, wajuaji na wasio na uelewa kuhusu utapeli, pia wanaopenda 'shortcut'

Mdau ni njia gani nyingine unazifahamu hutumika na matapeli mitandaoni?

Mjadala https://jamii.app/NjiaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
1
Mwanachama wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com, ameelezea kisa chake cha kutakiwa alipie gharama ya usafiri ili kupokea zawadi aliyotumiwa kutoka nje ya nchi na mtu ambae hawajawahi kuonana

Mdau, ushawahi kukutana na kisa kama hiki na ilikuwaje?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KamaVileNtapeliwa

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
1
Iwapo umepokea ujumbe kama huu usifuate maelekezo na kutoa nywila (neno siri), namba yako ya uthibitisho (OTP) au taarifa za akaunti yako kwa mtu yeyote, utaibiwa!

Pia, usibonyeza kiungo 'link' itakayoambatana na ujumbe huu

Soma https://jamii.app/AinaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
GEITA: Jeshi la Polisi linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya matukio ya Utapeli, baada ya kukutwa na laini za simu 9,389 Machi 13, 2025 katika Kata ya Ludete.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Safia Jongo amesema “Watuhumiwa walikutwa na Laini mpya za mitandao mbalimbali 1,600, Mabaki ya laini za mitandao mbalimbali jumla 6189, Line za Yas (Tigo) zilizosajiliwa 2600 na begi 3 za mgongoni”

Waliokamatwa ni Ilege Charles (42), Shabani Abdallah (25), Daudi Omary (25), Alex Rashid (32), Jumanne Mageso (27), Meshack Bahebe (31), Alex Edward (29), Nkwabi Ipilinga (21), Dennis Ndihunze (33), Vicent Vedastus (25) na Hamduni Issa (30)

Soma https://jamii.app/MatapeliMtandaoniKukamatwa

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Ili kujilinda dhidi ya matapeli wa Mitandaoni, epuka kutoa taarifa zako binafsi na usiwe na haraka katika kufanya maamuzi unapopokea ujumbe ambao una mashaka nao

Mdau, ukigundua umetapeliwa unafanyaje?

Mjadala zaidi https://jamii.app/HatuaBaadaKutapeliwa

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
1
Kama umetumiwa SMS ya kitapeli, tuma ujumbe uliotumiwa kwenda 15040 kisha ingiza namba ya simu iliyokutumia na kama umepigiwa simu ya kitapeli tuma neno UTAPELI kwenda 15040 kisha ingiza namba ya simu iliyokupigia

Mjadala zaidi https://jamii.app/KuripotiNambaUtapeli

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Mdau, huwa unazingatia vitu gani kabla ya kununua bidhaa au huduma Mtandaoni ili kuepuka kutapeliwa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/BiasharaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Mdau wa Jukwaa la 'Tech, Gadgets & Science' ameelezea mbinu mbalimbali za kuepuka kutapeliwa Mtandaoni

Mdau, unazingatia nini ili kujiadhari na Matapeli wa mtandaoni?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KuepukaKutapeliwaMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Endapo utapokea ujumbe kama huu usiuzingatie, pia usifuate maelekezo kutoka kwa mtu anayejitambulisha kama mtoa huduma wa Mtandao wako wa simu, kwani Watoa Huduma wa Mitandao ya simu Nchini huwasiliana na wateja kwa namba 100 pekee

Mjadala zaidi https://jamii.app/ZuiaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameelezea kisa chake cha kutapeliwa Mtandaoni baada ya kununua kifurushi cha Intaneti Mtandaoni kwa Mtu asiyemfahamu

Mdau umewahi kukutana na tukio kama hili?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NimetapeliwaTena

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
👍1
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameshauri badala ya kupiga namba *106# ili kuangalia namba zilizosajiliwa kwa namba ya NIDA, mhusika wa namba atumiwe ujumbe wa SMS kila namba mpya inaposajiliwa ili kupunguza tatizo la Utapeli Mtandaoni.

Unakubaliana na Mdau huyu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/UjumbeBadalaya106

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema kilichoingiliwa ni akaunti za Mitandao ya Taasisi na sio Mifumo ya Serikali, akilihakikishia Bunge kuwa Mifumo ya #TEHAMA ipo salama na akaunti tayari zimerejeshwa

Akizungumza #Bungeni, leo Mei 21, 2025, Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga, ambapo amesema akaunti hizo ziliingiliwa kutokana na udhaifu wa taratibu za kiusalama katika usimamizi wa akaunti.

Soma https://jamii.app/KudukuliwaAkauntiJerry

#JamiiForums #JamiiAfrica #OnlineSafety #CyberSecurity #CyberAttacks
Watafiti wa Masuala ya Usalama wamethibitisha kuwa hili ni tukio kubwa zaidi la uvujaji wa taarifa kuwahi kutokea baada ya nywila bilioni 16 pamoja na taarifa za Watumiaji wa Mitandao mbalimbali kuvuja kuanzia Januari 2025

Watafiti wamedai taarifa na nywila hizo zilikusanywa kwa kutumia programu hatari za kuiba taarifa (infostealer malware)

Tukio hilo limesababisha Wadukuaji kuiba akaunti za Watu, kufanya udanganyifu wa utambulisho (Identity theft) pamoja na kutuma mashambulizi ya kimtandao (phishing) kwa Watu wengine

Soma https://jamii.app/WorldLargestBreach

#JamiiForums #JamiiAfrica #CyberSecurity #DigitalSecurity