JamiiForums
53.4K subscribers
34.2K photos
2.36K videos
31.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, leo Agosti 10, 2025, amefika kuchukua fomu ya urais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndejengwa akiwa na usafiri wa bajaji.

Amesema, lengo la kutumia usafiri huo ni kujali na kuwaza namna atakavyoshughulika na watu wa kawaida, pamoja na kuwaonesha vijana mwelekeo wa serikali yake endapo atashinda kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, amesema endapo ataingia madarakani, magari yoyote ya serikali yaliyogharimu zaidi ya Tshs. milioni 200 Yatauzwa, na serikali yake itatumia magari ya kawaida.

Zaidi Soma https://jamii.app/DoyoBajaj

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
1
Tembelea JamiiForums.com kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita.

#JamiiAfrica #JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza na Waandishi wa Habari, Agosti 10, 2025, Mgombea wa Urais kupitia Chama cha United People Democratic Party (UPDP), Twalib Kadege amesema endapo atakuwa Rais, atahakikisha Waandishi wa Habari wanapata uhuru wa kufanya kazi zao za Kihabari, kuwezeshwa vifaa muhimu na kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vya Habari kupanga mikakati ya kuweka Waandishi vijijini ili waripoti maendeleo na changamoto za Wananchi.

Aidha, Kadege amesema moja ya vipaumbele vyake endapo atapewa ridhaa na Watanzania ni kuleta mapinduzi katika Sekta ya Kilimo na kuhakikisha maliasili zinawekwa mikononi mwa Wananchi ili kila mmoja afaidike na keki ya Taifa.

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/KadegeUhuruHabari

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
1
MICHEZO: Kutoka Jukwaa la Sports ndani ya JamiiForums.com Mdau ameeleza mtazamo wake kuhusu Msimu wa 2025/26 utakavyokuwa na utabiri wake kutokana na aina ya usajili unaoendelea.

Je, Mdau una maoni gani kuhusu timu yako kuelekea msimu ujao wa soka?

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/UsajiliBongoUlaya

#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na East Afrika Radio, Agosti 7, 2025, kada wa Chama cha Ukombozi wa Umma (#CHAUMMA), James Mbowe amesema licha ya #CHADEMA kupendwa na Watu wengi, idadi ya wanaohudhuria kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, #TunduLissu haifiki Watu 300. Amesema ukilinganisha siasa za Kenya na Tanzania, zile za Tanzania zinataka ziende zaidi katika muktadha wa mazungumzo ya maridhiano.

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/LissuWatu300

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Democracy
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha United People's Democratic Party (#UPDP), Twalib Kadege amesema, "Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) iko vizuri sana, sijaona vikwazo vyovyote."

Akihojiwa na East Africa Radio, Julai 29, 2025, Kadege aliongeza "Sisi tunategemea sana Kura kutoka kwa Wananchi na fursa ya kwenda kuwaomba Kura ipo. Wananchi wanatuona na Tume Huru ya Taifa iko vizuri. Wameahidi kuwa atakayeshinda kuanzia Diwani, Mbunge hadi Rais atatangazwa."

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/KadegeMgombeaUrais

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Democracy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JF KUMBUKIZI: Aliyekuwa Mbunge wa Bumbuli, January Makamba alipokuwa kwenye mahojiano na Radio One, Aprili 1, 2019 kwenye kipindi cha Kumepambazuka alisema "Madaraka uliyobeba ni kama koti la kuazima na ukiwa na mbwembwe nyingi ukiwa umelivaa, siku koti likichukuliwa utakosama mahala pa kuficha uso wako."

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/JFKumbukiziMakamba

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFKumbukizi #Governance
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (#UDP), John Cheyo alipokuwa akiwasili kuhudhuria Mkutano Mkuu wa chama chake unaofanyika katika Ukumbi wa Lulu, Sinza kwa ajili ya kutimiza takwa la Kisheria la kumuidhinisha Mgombea Urais wa chama na Mgombea Mwenza, leo Agosti 11, 2025.

Kamati Kuu ya UDP itathibitisha jina, kabla ya kuwasilishwa kwa mkutano mkuu maalumu kwa ajili ya kuridhiwa.

Soma https://jamii.app/UDPMkutano

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Democracy
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Taifa, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ametangaza kuhusu harambee ya kukichangia chama hicho, amesema CCM sio taasisi ya kudhibiti fedha haramu, jibu ambalo limetokana na swali kuwa wataweza vipi kudhibiti fedha hizo wakati wa harambee yao ya kukichangia chama kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Amesema hayo wakati akizungumza na Wanahabari, leo Agosti 11, 2025 katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.

Soma https://jamii.app/CCMSioSerikali

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Governance #UchaguziMkuu2025 #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KILIMANJARO: Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa hivi karibuni vimejitokeza vikundi vya Watu kwa mwamvuli wa #siasa, #demokrasia na uanaharakati na kuanza kutoa maneno ya uchochezi yenye lengo la kuvuruga amani ya nchi.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, Agosti 11, 2025 katika Shule ya Polisi Tanzania, IGP Wambura alisema kwamba licha ya kuwepo kwa vikundi hivyo, Jeshi la Polisi limechukua hatua stahiki na kwa sasa hali ni shwari.

Soma Zaidi: https://jamii.app/WamburaKuhusuAmani

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #UchaguziMkuu2025
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Entertainment anasema Muziki wa #HipHop kwa sasa ni kama umekuwa mwepesi sana tofauti na Miaka ya nyuma, hiyo ni katika ‘mistari’ na hata staili ya ku-flow.

Anahoji ni Wasanii gani watatu wanaweza kushika nafasi tatu za juu, kwamba wao ni bora kuliko wengine bila kujali wana ‘hit’ au hawana nyimbo mpya kwa sasa?

Kushiriki mjadala zaidi bofya https://jamii.app/HipHopMusic

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFEntertainment #JFBurudani
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Taifa, Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wanahabari leo Agosti 11, 2025 katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba wakati wa kutambulisha harambee ya chama itakayofanyika Agosti 12, 2025, pia alitamka kuwa baadhi ya Waandishi wa Habari ni WanaCCM.

Soma https://jamii.app/RoboTatuWaandishiCCM

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) kupitia chama cha Union for Multiparty Democracy (#UMD), Mwajuma Noty Mirambo amesema sera za chama hicho zimejikita katika uchumi wa majimbo, ambapo kila Mtanzania atafurahia uchumi uliopo katika eneo lake.

Zaidi Soma https://jamii.app/MajimboUchumi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Taifa, Emmanuel Nchimbi akijibu hoja ya jinsi watakavyodhibiti pesa za Raia wa Kigeni wenye nia mbaya katika harambee ya chama hicho kuelekea katika Uchaguzi Mkuu amesema:

"Tutakapokuwa tukiipokea michango tutaianisha kujua hii inatoka wapi ile ambayo inadhalilisha heshima au inapoteza Uhuru wa Taifa letu hatuwezi kuipokea. Niwahakikishieni hatuwezi kupokea michango inayopoteza Heshima ya Nchi yetu na kudhalilisha Utu wa Watanzania."

Soma zaidi https://jamii.app/CCMMichangoNje

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Governance #UchaguziMkuu2025
Kupitia Jukwaa la JamiiForums.com Mdau ameibua changamoto anayodai inawakumba Walimu wa Mbeya DC wanaotaka kujitoa kwenye Chama cha Walimu Tanzania (#CWT) ili kujiunga na vyama vingine vya Wafanyakazi.

Anadai licha ya kujaza fomu za kujitoa, maombi yao yamegomewa kwa kisingizio kuwa Mwaka huu ni wa Uchaguzi na muda mwingine wakienda wanaambiwa “hatuna majibu ya kuwapa” na kuongeza kuwa majibu hayo wanayopewa hayaridhishi na yanakera.

Mdau anaeleza kuwa hali hiyo ni kama kuwalazimisha Walimu kubaki CWT kana kwamba vyama vingine havipo kisheria, akisisitiza Walimu wana haki ya kuchagua chama chochote cha Wafanyakazi.

Soma Zaidi: https://jamii.app/WalimuMbeyaCWT

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #Uwajibikaji #Accountability #JFMdau2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Aliyekuwa mtia nia wa Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia #CCM, Alphonce Temba akifanya mahojiano na East Africa Radio, Agosti 5, 2025 alisema aliwahi kushika nafasi ya mshauri wa juu wa viongozi wawili wa Afrika: Rais wa zamani wa Zambia, Michael Sata na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila.

Anaeleza kuwa aliwahi kumshauri Rais Joseph Kabila kuzimwa kwa Mtandao wa simu na Intaneti wakati wa kutangaza matokeo ya Uchaguzi kupitia CENI (Tume ya Uchaguzi ya DRC), kwa nia ya kudhibiti taarifa potofu na taharuki.

Soma zaidi https://jamii.app/KabilaKuzimaMtandao

#JamiiForums #JamiiAfrica #DigitalRights #Governance #Democracy
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama cha ADA TADEA, Georges Bussungu akiwa pamoja na Mgombea Mwenza Ali Makame Issa wamesindikizwa na kikundi cha ngoma cha Kabila la Wagogo wakiwa wanaenda kuchukua fomu ya Urais kwenye Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Bussungu amekuwa mgombea wa saba kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya Urais, Wagombea wengine ambao wameshachukua fomu za Urais ni Samia Suluhu Hassan (#CCM), Coaster Kibonde (Chama Makini), Doyo Hassan Doyo (#NLD), Kunje Ngombare Mwiru (#AAFP), Hassan Almas (#NRA) na Twalib Kadege (#UPDP).

Zaidi soma https://jamii.app/MgombeaUraisADATADEA

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Democracy #UchaguziMkuu
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mgombea Urais wa Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Hassan Alma, jana Agosti 10 alichukua fomu ya kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC).

Alma alichukua fomu hiyo mbele ya Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhani pamoja na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele.

Soma Zaidi: https://jamii.app/MgombeaUraisNRA

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu #Siasa #Democracy