JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza katika Uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Emmanuel Mkilia amesisitiza Watu Binafsi na Taasisi zinazokusanya na kuchakata Taarifa Binafsi kujisajili na kupata vibali vya kuendelea kufanya wanachokifanya

Aidha, amesema “Tume ilianzishwa rasmi Mei Mosi, 2023 na itatekeleza majukumu yake #TanzaniaBara na #Zanzibar kwenye masuala ya Muungano.”

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍21
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, #NapeNnauye, amesema Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni chombo muhimu katika kuimarisha Misingi ya #Demokrasia, Utawala Bora na Utawala wa Sheria na hivyo kuzidi kuvutia Wawekezaji kutoka Nje

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan akizungumza katika uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam amesema baadhi ya taarifa zinaweza kutumika kuhujumu Jamii

Amesema “Wakati mwingine taarifa ya Mtu inaweza kusababisha unyanyapaa, vurugu, vita na hata mauaji.”

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan ametoa maelekezo kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kuhakikisha Taasisi zote za Umma na Binafsi zinasajiliwa na zinatekeleza Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kabla au ifikapo Desemba 2024

Amesema hayo wakati akizindua Tume hiyo, leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan ameelekeza Ofisi ya Waziri Mkuu isimamie na kuhakikisha Mifumo ya #TEHAMA Nchini inasomana, ametoa maelekezo hayo baada ya kuzindua Mfumo wa Kisera na Kisheria wa Kulinda Taarifa Binafsi

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍1
Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wanasema kuna mtindo umezuka ambapo Wakopeshaji wa Mtandaoni wamekuwa wakisambaza taarifa binafsi za Wateja kwa Watu ambao huwa wanawasiliana nao kwa kuwaeleza kuwa wanamdai mhusika

Je, umeshawahi kukumbwa na Udhalilishaji wa aina hii baada ya kukopa Mtandaoni?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KudhalilishwaMkopoOnline

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #PersonalDataProtection #DataPrivacy #DataProtection
👍1😡1
HAKI ZA KIDIGITALI: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema hadi sasa zaidi ya Taasisi 300 zinazojihusisha na Ukusanyaji na Uchakataji wa #TaarifaBinafsi ziko katika hatua mbalimbali za Kujisajili katika Mfumo wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binfasi (PDPC)

Hatua hiyo ni moja ya matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Taasisi na Watoa Huduma wote Nchini ambao wanakusanya na kuchakata Taarifa Binafsi za Watu ili kuwezesha Mfumo kupokea Malalamiko endapo kutatokea Ukiukwaji wa Masharti ya Ulinzi wa Taarifa hizo na kuyashughulikia

Aidha, Tume ya PDPC inatarajia kusajili Wakusanyaji na Wachakataji wa Taarifa Binafsi 500,000 kwa Mwaka 2024/25

Soma https://jamii.app/HabariBajeti2425

#JamiiForums #Governance #DigitalRights #Accountability #JFDigitali #JFDATA #PersonalDataProtection
👍2
TAARIFA ZA WATU ZINATUMIKA VIBAYA, KWANINI HATUA HAZICHUKULIWI?

Mdau wa JamiiForums amelalamikia suala la #TaarifaBinafsi za Watu kutumika vibaya na kusambazwa bila ridhaa zao huku Mamlaka zikiwa hazijishughulishi kwa lolote

Amesema mara kadhaa amekutana na taarifa za Watu kwenye Vifungashio vilivyotengenezwa na nyaraka kama barua za kazini, matokeo ya mitihani, vyeti na nyingine nyingi

Amehoji kwanini Mamlaka haizichukulii hatua Taasisi zinazohusika na haya kwani Vifungashio hivi vipo kila sehemu na sasa vimeshamiri mno

Zaidi, tembelea https://jamii.app/VifungashioTaaarifa

#JamiiForums #DigitalSecurity #PersonalData #JFDigitali #PersonalDataProtection #DataPrivacy
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye, amesema Serikali imetoa maeleko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (#TCRA) Kitengo cha Cyber Crime Unit kuwafuatilia na kuchunguza Watu wanaotumia taarifa za waliowakopesha Mtandaoni kwa lengo la kudhalilisha Wakopaji

Wadau wa JamiiForums.com kwa wakati tofauti walizungumzia changamoto hiyo, Februari 21, 2024, Aprili 4, 2024 na Machi 19, 2024 wakisema ni tabia hatarishi kwa Faragha ya Mtu

Ikumbukwe Juni 4, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Emmanuel Mkilia, naye alizionya Taasisi na Watu Binafsi wanaofanya vitendo hivyo kuwa ni kinyume cha Sheria

Soma https://jamii.app/TCRAWakopaji

#JamiiForums #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #Accountability #PersonalDataProtection #JFDigitali
👍3
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka kuchukua hatua za kuhakikisha ulindaji wa taarifa binafsi katika kituo cha NIDA kilichopo Kawe akidai taarifa za Watu hazilindwi kama inayotakiwa

Anasema Mamlaka husika zitoe Elimu kwa Maofisa hao kuhusu ulindaji wa taarifa binafsi katika kituo hiko

Soma https://jamii.app/NidaKutunzaFaragha

#JFUwajibikaji #JamiiForums #JFHuduma #Accountabilty #DigitalRights #PersonalDataProtection #JFDigitali
👍4
Ukosefu wa Elimu ya Usalama wa Kidigitali unawaweka Watu katika hatari ya Ukiukwaji wa Haki zao za Faragha kwasababu mara nyingi, hujikuta wakitoa taarifa zao binafsi kwa urahisi bila kuzingatia hatari zinazoweza kutokea

15% tu ya Watu walioshiriki katika Utafiti wa Ripoti ya Haki za Binadamu (2022) walisema wameelimishwa vizuri sana/vizuri kuhusu Usalama wa Kidigitali, huku zaidi ya 55% wakiwa hawajaelimishwa/hawajui kuhusu Usalama wa Kidigitali

Fahamu zaidi https://jamii.app/DigitaliTHRR

#Teknolojia #JFDigitali #UsalamaMtandaoni #DigitalSafety #DigitalRights #PersonalDataProtection #DataPrivacy
Mdau wa JamiiForums.com anasema taarifa binafsi za Mtumishi anazijaza kwa mwajiri wake, je, Matapeli wanaopiga Simu wanawezaje kuzipata au wanazitoa wapi?

Anasema kitendo cha tapeli kutumia Taarifa Binafsi kutaka kuwatapeli Watumishi inaleta hofu juu ya Usalama wa Taarifa Binafsi na faragha za Watumishi

Soma https://jamii.app/TapeliTaarifaWatumishi

#JamiiForums #DataPrivacy #PersonalDataProtection #OnlineSafety
Nukuu hii imetolewa katika Chapisho la Dkt. Gwajima la Mei 8, 2023 katika Mtandao wa X, ambapo alisisitiza umuhimu wa kulinda faragha ya waathirika wa Ukatili dhidi ya Watoto

Kauli hii inalenga kuhamasisha jamii kutoeneza taarifa binafsi za waathirika kama majina, picha, au maeneo wanayoishi, ili kuzuia unyanyapaa na kuwalinda dhidi ya madhara zaidi. Tukumbuke, kuheshimu faragha ya Waathirika ni hatua ya kwanza ya Kupambana na Ukatili

#JamiiForums #JFNukuu #JFQuotes #PersonalDataProtection #DataPrivacy #ChildProtection #HakiMtoto
🔥2
#FARAGHA: Sheria ya #Tanzania ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 imeanisha Taarifa Binafsi kuwa ni taarifa zinazomtambulisha Mtu ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote

Taarifa Binafsi ni pamoja na zinazohusu Rangi, Asili ya Kitaifa au Kabila, Dini, Umri au Hali ya Ndoa ya Mtu, Elimu, Historia ya Matibabu, Jinai au Ajira, Namba yoyote ya Utambulisho, Anwani, Alama za Vidole au Kundi la Damu, pamoja na Jina la Mtu

Jina lako huchukuliwa kuwa Taarifa Binafsi kwasababu linakutambulisha na endapo litaunganishwa na Taarifa nyingine huweza kutoa Utambulisho wa kukutofautisha na Mtu mwingine

Soma https://jamii.app/PersonalInformation

#JamiiForums #JFDigitali #DataPrivacy #PersonalDataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
Mdau, unafanya nini kuhakikisha taarifa zako binafsi ziko salama mtandaoni?

Mjadala zaidi https://jamii.app/TaarifaBinafsiKutumikaVibaya

#JamiiForums #JFDigitali #DataPrivacy #PersonalDataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
👍1
Namba ya simu ni taarifa binafsi na kama taarifa nyingine yoyote nyeti, inapaswa kulindwa (Iwapo mwenye nayo hajaamua kuiweka wazi kwa Umma)

Kila wakati, uliza idhini kabla ya kutoa namba ya mtu mwingine, kwani ni sehemu ya kuheshimu faragha yao

Soma https://jamii.app/NambaYaMtuRidhaa

#JamiiForums #JFDigitali #DataPrivacy #PersonalDataProtection #TaarifaZakoMaishaYako #JFMdau2025
Kitambulisho chako (ID) kinachukuliwa kuwa Taarifa Binafsi kwasababu kina taarifa zako kama Jina, Nambari ya Utambulisho, Picha, Tarehe ya Kuzaliwa, n.k.

Unamshauri Mdau afanye nini hapo?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MkopoSimuKitambulisho

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #PersonalDataProtection #DataPrivacy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (#PDPC), Innocent Mungy ameeleza umuhimu wa Tume kusimamia ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kusema "Tunalinda zisiende kwenye mikono isiyo sawa, isiyoruhusiwa kuwa na matumizi ya hizo taarifa."

Ameeleza hayo wakati wa mafunzo maalum Julai19, 2025, yakihusisha Maafisa Habari wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC).

Soma zaidi https://jamii.app/PDPCTaarifaBinafsi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #PersonalDataProtection #DataPrivacy #DigitalRights
1