JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mila ya kumwekea Mtoto ahadi ya ndoa tangu akiwa tumboni inaimarisha wazo kwamba Wanawake hawawezi kufanya maamuzi binafsi na wanapaswa tu kufuata maagizo na mwongozo wa Mwanaume

Aidha, Wanawake waliofungwa na Mila hii wananyimwa fursa za Elimu, kujitegemea Kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika Maendeleo ya Kijamii, hivyo kusababisha kudorora kwa Maendeleo ya Jamii nzima

Taarifa zaidi https://jamii.app/AhadiZaNdoaKablaYaKuzaliwa

#JamiiForums #ChildRights #ChildProtection #WomenRights #JFWomen #HumanRights #HakiZaBinadamu #HakiMtoto
πŸ‘2
#JFAFYAAKILI: Kuwa na Mwenza asiyechaguliwa na mhusika mwenyewe kunaweza kusababisha uhusiano wa dhati kutoweka. Hii husababisha mtu kukosa uhusiano wa furaha na Mwenza wake, hali ambayo inaweza kuathiri furaha na ubora wa maisha yake yote

Vile vile, katika Jamii ambayo Mila ya kupangiwa Mume kabla ya Kuzaliwa inazingatiwa, mtu anayekataa maamuzi hayo anaweza kutengwa na kubaguliwa. Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya Kihisia, Kujisikia kutengwa na hata matatizo ya Kisaikolojia, kama Upweke na Msongo wa Mawazo ambayo huweza kusababisha hisia za kujidhuru

Soma Zaidi https://jamii.app/AhadiZaNdoaKablaYaKuzaliwa

#JamiiForums #JFWomen #HakiMtoto #SocialJustice #Depression #MentalHealth #MentalWelliness #ChildProtection #WomenRights
πŸ‘1
Mdau wa JamiiForums.com anasema tukikubali kuwa Watoto hawawezi kufanya maamuzi ya Ujira, kuendesha Vyombo vya Moto au kushiriki katika Uchaguzi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutosha, tunapaswa pia kutekeleza Kanuni hii katika suala la Ndoa kwa Watoto

Amesema Ndoa ni suala linaloweza kuwa na athari za kudumu kwa Watoto, Jamii itathmini Desturi zinazowalazimu Watoto kuolewa katika Umri Mdogo ili kuwalinda kwa kufahamu na kutambua kuwa Wanastahili kulindwa, kuwezeshwa kukua, kupatiwa #Elimu na kushiriki katika maamuzi yanayohusu mustakabali wao

Soma https://jamii.app/JukumuLaNdoa

#JamiiForums #SocialJustice #EarlyMarriages #NdoaZaUtotoni #JFWomen #HakiMtoto #WomenRights #ChildProtection
πŸ‘9
Kufuatia kusambaa kwa Video iliyowaonesha Watoto wakitoa Burudani kwenye Sherehe wakati wa Usiku na katika Miondoko isiyofaa kwa Umri wao, Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewatafuta Wazazi wa Watoto hao na kukemea kitendo hicho huku akiwataka Washereheshaji na Jamii kuzingatia Sheria inayokemea Udhalilishaji wa Watoto

Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 (iliyorekebishwa Mwaka 2019), kifungu cha 158 (1) (c) inazuia kumtumia Mtoto kwenye Maonesho ya Harusi, Mitindo ya Nguo au Maonesho mengine kama hayo wakati wa Usiku. Adhabu yake ni faini ya Tsh. Laki 5 au kifungo cha Miezi 6 jela au vyote kwa pamoja

Soma https://jamii.app/HarusiWatoto

#JamiiForums #HakiMtoto #JFWomen #ChildProtection #Governance #SocialJustice #JFUwajibikaji
πŸ‘18πŸ‘2❀1
Kufuatia Video iliyosambaa ikimwonesha Lilian Mwasha akiwa na Wanafunzi akiwataka wale wasiopendwa na Baba zao kutoka mbele na kutaja sababu za wao kuhisi hivyo kwa lengo la kuwapa Ushauri na Unasihi (Counselling), Waziri Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Lilian Mwasha amekosea, alichokifanya hakifai na kumtaka afute Video hizo kwenye Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii

Aidha, Dkt. Gwajima amesema 'Counselling' ni Huduma Patanishi na hufanyika kwa Usiri na utaratibu maalumu kwa kuzingatia pande zote mbili

Soma https://jamii.app/WatotoUshauriNasaha

#JamiiForums #ChildProtection #JFWomen #HakiMtoto #Governance
πŸ‘9
Mdau wa JamiiForums.com anasema Utaratibu wa Kuwafungulia Watoto Akaunti kwenye Mitandao ya KIjamii kunahatarisha usalama na faragha yao kwa kuwa akaunti hizi hujazwa taarifa ambazo huweza kusababisha mtoto kunyanyasika Kimtandao

Ameshauri Wazazi kuzingatia Haki ya Watoto ya Kulindwa hasa Mtandaoni kwa kuepuka tabia kama hizo ili kuwaepusha na Ukatili au Unyanyasaji utokanao na taarifa zao zilizopo Mtandaoni

Vipi Mdau, kuna ulazima wowote wa Kuwafungulia Watoto akaunti za kwenye Mitandao ya Kijamii?

Soma https://jamii.app/WatotoNaMitandao

#JamiiForums #ChildProtection #ChildRights #HakiMtoto #JFWomen #DigitalRights #DigitalWorld
Mbinu za Malezi zinaweza kutofautiana kutokana na tofauti ya tabia na hulka za Watoto. Kama Mzazi/Mlezi, ni muhimu kubadili 'approach' pale ambapo unaona jitihada zako za malezi ya aina fulani hazizai matunda unayokusudia

Mdau anaomba ushauri wa namna ya kumlea Mtoto wa Ndugu yake anayeishi naye ambapo mbinu za malezi anazotumia yeye anaona zimegonga mwamba

Karibu tumshauri Mdau huyu

Kusoma Kisa chote bofya https://jamii.app/MtotoMtukutu

#JamiiForums #JFMalezi #ChildProtection #ChildRights #HakiMtoto
πŸ‘6😒1πŸ™1
Mdau wa JamiiForums.com anasema katika Shule jumuishi, changamoto hujitokeza linapokuja suala la kukosekana kwa Vyoo vya Wanafunzi wenye Ulemavu na mahitaji maalumu. Kundi hili huitaji Miundombinu maalum ya kuwasaidia kujihifadhi

Anaeleza athari kubwa ya ukosefu wa Vyoo bora kwa Wanafunzi wenye Ulemavu huathiri Afya zao pamoja na Kisaikolojia, kwasababu wanaona wanabaguliwa na kutengwa. Wengine hukatisha Masomo kutokana na adha wanayokumbana nayo Shuleni.

Soma https://jamii.app/VyooWalemavu

#JamiiForums #HumanRights #ServiceDelivery #Accountability #ChildProtection #StoriesOfChange2023
πŸ‘2
#MALEZI: Ni muhimu kutambua kwamba Mtoto hujifunza zaidi kwa kuona, hivyo Mzazi kuwa mfano bora wa Tabia na Maadili

Mawasiliano yenye Uwazi na Watoto hufanya wawe huru kujieleza na kutushirikisha katika Maisha yao

Usisahau kumsimamia Mtoto juu ya matumizi ya #Teknolojia na Mitandao ya Kijamii ili kuhakikisha anapata Maudhui yanayofaa kulingana na Umri wake.

Soma https://jamii.app/MaadiliTabiaWatoto

#JamiiForums #ChildProtection #DigitalSafety
πŸ‘2
Watoto ni kundi kubwa linalopitia Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia katika jamii, na hili linajitokeza kwa kiwango kikubwa katika tasnia ya Sanaa ya Uigizaji

Unyanyasaji huo unaweza kuwasababisha athari za kisaikolojia, matatizo ya afya ya akili, pamoja na Magonjwa ya zinaa.

Je, Wazazi na Walezi wenye watoto kwenye tasnia hii wana uelewa mzuri jinsi ya kuwalinda Watoto dhidi ya Unyayasaji?

Soma https://jamii.app/WatotoSanaa

#JamiiForums #Accountability #ChildProtection
πŸ‘2
DAR: Mwezi mmoja baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuripoti madai ya Mtoto kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza, Mama wa Mtoto ameomba mtuhumiwa achukuliwe hatua akidai ukimya umetawala tangu aripoti tukio hilo Februari 3, 2024, Kituo cha Polisi Mabatini

Baada ya andiko la Mdau, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dorothy Gwajima aliandika ujumbe wa kumtafuta Mama wa Mtoto, ambapo mama huyo anasema alimtafuta Waziri ambaye alimtuma Afisa Uhusiano kumsikiliza

Mama wa Mtoto amesema β€œNimeshatoa maelezo Polisi na Ustawi lakini ni mwezi sasa naona kimya na kila nikiuliza naambiwa wanafanyia kazi. Pia, sijapata ushirikiano kutoka upande wa muajiri wa Mtuhumiwa na sasa Mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana.”

Afisa Ustawi wa Jamii wa Sinza, Grace Ludovic akisema suala hilo lipo mezani kwao na linafuatiliwa

Soma https://jamii.app/KesiYaUkatili

#SocialJustice #JFMatukio #HumanRights #JamiiForums #ChildProtection #ChildRights
πŸ‘5❀1
DAR: Paroko wa Kanisa Katoliki la Sinza, Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi-Sinza, Padri Josephat Celestine Muhoza, amesema wamemuondoa Kazini Mlinzi anayefahamika kwa jina la Baraka, anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wa Darasa la Tano Kanisani hapo

Padri Muhoza amesema β€œSiku ya tukio nilikuwa kwenye Jumuiya, niliporejea Kanisani Mfanyakazi wa mazingira wa Parokia akasimulia kuwa alisikia sauti ya Mtoto akilalamika chooni 'Unaniumiza Unaniumiza', akaamua kwenda kutafuta msaada. Nikakuta mjadala unaendelea, nikapiga simu Polisi wakaja kumchukua mtuhumiwa.”

Ameongeza β€œNilipiga Simu kwenye Kampuni yake ya Ulinzi ya Multi-Lion Security Limited haikutoa ushirikiano wa haraka, baada ya hapo tumeachia Polisi wafanye kazi yao na huyo Mlinzi hapa hayupo.”

Soma https://jamii.app/TuhumaZaMlinzi

#SocialJustice #JFMatukio #HumanRights #JamiiForums #ChildProtection #ChildRights
πŸ‘12😁1
DAR ES SALAAM: Baraka Benedicto ambaye alikuwa Mlinzi wa Kanisa Katoliki la Sinza, Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi, amepandishwa kizimbani Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni na kusomewa shtaka moja la kumuingilia Mtoto wa miaka 14 kinyume na maumbile

Shtaka limesomwa na Wakili wa Serikali mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira ikielezwa mtuhumiwa alitenda tukio hilo Februari 3, 2024 ambapo amekana shtaka hilo na amepelekwa rumande Segerea

Mahakama imepanga kusikiliza tena shauri hilo Namba CC.5866, Machi 18, 2024. Ikumbukwe kuwa Februari 2024, Mdau wa JamiiForums.com aliripoti tukio hilo akiomba Serikali iingilie kati ili haki ipatikane ambapo alidai kuna mazingira ya suala hilo kuisha kimya kimya bila kufikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/KesiSinza

#SocialJustice #JFMatukio #HumanRights #JamiiForums #ChildProtection #ChildRights
πŸ‘4
Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeitaka #Somalia kutoruhusu marekebisho ya #Katiba ambayo yanalenga kupunguza umri wa Utu uzima kwa madai hali hiyo itadhoofisha Haki za Watoto

Mabadiliko yaliyopendekezwa ambayo yatajadiliwa #Bungeni leo, Machi 30, 2024 yanapendekeza Umri wa Utu Uzima wa Miaka 15 na Miaka 18 kama Umri wa kuwajibika Kisheria

Human Rights Watch imesema mabadiliko yaliyopendekezwa yatawaweka Wasichana katika hatari kubwa ya Ndoa za Utotoni, ambazo huathiri Afya zao, haswa Afya ya Uzazi, upatikanaji wa Elimu, na Ulinzi wao dhidi ya Unyanyasaji

Soma https://jamii.app/SomanChildAge

#JamiiForums #HumanRights #InvestInWomen #ChildProtection #HakiWatoto
πŸ‘8❀1
#HAKIMTOTO: Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia (Mei 15), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema lengo la Maadhimisho ni kutathmini nafasi ya #Familia katika Ustawi, Maendeleo na mchango wake kwa Taifa

Maadhimisho ya Mwaka huu (2024) yatafanyika Kimikoa kwa kugusa ngazi ya Jamii (Vijiji, Mitaa na Kata) huku Kaulimbiu ikiwa "Tukubali tofauti zetu kwenye Familia; Kuimarisha Malezi ya Watoto"

Ameeleza mifarakano katika Familia huleta matokeo hasi kwenye Maendeleo na Ustawi wa Watoto

Soma https://jamii.app/SikuYaFamilia

#JamiiForums #SikuYaFamilia #Accountability #Uwajibikaji #HakiZaWatoto #ChildRights #ChildProtection
πŸ‘11
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Mwaka ifikapo Juni 16 kuwakumbuka Watoto waliouawa na Serikali ya Kibaguzi huko #Soweto Mwaka 1976 wakiwa katika Maandamano ya kudai Haki zao ikiwemo Haki ya kupata Elimu na kufundishwa kwa kutumia Lugha zao Asilia

Siku hii pia inaangazia Changamoto ambazo Mtoto wa Kiafrika anazipitia ikiwemo Ukosefu wa Elimu, Ukatili wa aina mbalimbali pamoja na uhitaji wa kuboresha Mazingira yake ya Kuishi

Soma https://jamii.app/DAC2024Day

#JamiiForums #ChildProtection #ChildRights #AfricanChild #DAC2024 #ChildSafety24 #ChildSafety #DayOfTheAfricanChild #YearOfEducation
#Education4All
πŸ‘2❀1πŸ‘Ž1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Ujumbe wa Mariam Sagini, Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake (UWT) akiitaka Jamii kutotumia imani za Kishirikina kuharibu Maisha ya Watoto, aliutoa Julai 4, 2024, alipozungumza na Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) katika Kata ya Nsemulwa, Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi

Soma https://jamii.app/WanaumeMajukumu

#JFNukuu #GoodMorning #Maisha #AmkaNaJF #HakiMtoto #HumanRights #ChildProtection #Quotes #ChildSafety24 #JamiiForums
πŸ‘3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
GEITA: Katibu Mkuu wa Chama cha #ACTWazalendo, Ado Shaibu amedai bado kuna taarifa za kupotea kwa Watoto katika maeneo ya Kanda ya Ziwa. Ametoa wito wa taarifa hizo ziripotiwe kwa kuwa ukimya utahalalisha matukio ya aina hiyo kuendelea

Amesema hayo alipozungumza na Wananchi wa Mbogwe, Septemba 29, 2024, ambapo ameongeza β€œWito wetu ACT ni lazima Serikali iwajibike, namuomba Rais Samia Suluhu Hassan alitazame jambo hili kwa uzito mkubwa sana. Mfano; ameunda Tume ya kuchunguza kifo cha Ali Kibao, Tume hiyo isiwe ya Mtu mmoja kwa kuwa visa ni vingi sana.”

Ameongeza β€œIundwe Tume yenye hadhi ya Kijaji, isiwe Jeshi la Polisi lijichunguze lenyewe. Tunataka chombo huru cha kuchunguza matukio ya upoteaji na kama halitafanyiwa kazi Waziri wa Mambo ya Ndani na Inspekta wa Jeshi la Polisi wajiuzulu.”

Soma https://jamii.app/AdoACT

#JFMatukio #JamiiForums #HumanRights #HakiMtoto #ChildProtection
πŸ‘1
DIGITALI: Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ametoa wito kwa wazazi kufuatilia 'Games' na Katuni wanazofuatilia watoto mtandaoni kwa kuwa baadhi yake hazina maudhui yanayofaa na huhatarisha usalama wa watoto mtandaoni

Ametoa wito kwa wazazi kuwaelimisha watoto kuhusu masuala mbalimbali yanayojitokeza kwenye jamii hasa upande wa kidijitali ili kuwasaidia na kuwajenga.

Soma https://jamii.app/GamesKatuniHatariWatoto

#JamiiForums #DigitalSecurity #ChildRights #ChildProtection
Nukuu hii imetolewa katika Chapisho la Dkt. Gwajima la Mei 8, 2023 katika Mtandao wa X, ambapo alisisitiza umuhimu wa kulinda faragha ya waathirika wa Ukatili dhidi ya Watoto

Kauli hii inalenga kuhamasisha jamii kutoeneza taarifa binafsi za waathirika kama majina, picha, au maeneo wanayoishi, ili kuzuia unyanyapaa na kuwalinda dhidi ya madhara zaidi. Tukumbuke, kuheshimu faragha ya Waathirika ni hatua ya kwanza ya Kupambana na Ukatili

#JamiiForums #JFNukuu #JFQuotes #PersonalDataProtection #DataPrivacy #ChildProtection #HakiMtoto
πŸ”₯2