PWANI: Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa taarifa kuwa imeanza kufikisha miundombinu ya ujenzi katika Mradi wa Maji Pangani – Kibaha kwa kuweka mabomba ya kusafirisha maji ya ukubwa wa inchi 6 yatakayolazwa kwa Mita 1,100, ikiwa ni utekelezaji wa Mradi ulioombwa na Wananchi wa eneo hilo kwa miaka kadhaa.
Ikumbukwe, Oktoba 8, 2023, Mdau wa JamiiForums.com alidai kuna mazingira ya ‘upigaji’ yaliyokwamisha mradi, pia Julai 21, 2024, Mdau mwingine alitoa wito kwa Rais Samia kuwapelekea huduma ya maji kwa maelezo kuwa wanapitia mateso kwa kukosa huduma hiyo.
Zaidi soma https://jamii.app/MajiPanganiKibaha
#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFMdau2025 #CivilRights #JamiiAfrica

❤2
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (#DART) kutafuta njia ya haraka kuboresha huduma ya usafiri wa Mwendokasi kwa maelezo kuwa inazidi kupungua ubora kila siku.
Anasema "Mabasi ni machache na hali hiyo inalazimu Watu kukaa zaidi ya Saa moja hadi mbili Kituoni kusubiria magari ambayo nayo yakifika kupata nafasi ya kuingia unatakiwa uwe 'umeshiba' kutokana na utaratibu mbovu uliopo."
Soma zaidi https://jamii.app/MdauMwendokasi
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025

❤2👏1
MOROGORO: Mdau ndani ya JamiiForums.com anadai jengo lililopaswa kuwa Zahanati ya Kijiji cha Lungongole lipo hapo takriban kwa Miaka mitatu na kwamba Machi 2025 alitembelea ukurasa wa Halmashauri ya Mji Ifakara akaona waliahidi Wakazi wa eneo hilo kuwa kufikia Oktoba 2025 litakuwa limekamilika, lakini haoni dalili hizo.
Amehoji ni kitu gani kinachokwamisha zoezi hilo kukamilika akidai Wanawake wanaoenda kliniki wanatembea hadi kijiji cha jirani kupata huduma muhimu, hivyo ni vizuri ujenzi huo ukakamilika.
Soma https://jamii.app/ZahanatiIfakaraNiGofu
#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025

❤1😁1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
PWANI: Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Usafirishaji wa Mizigo kwa SGR Kwala, leo Julai 31, 2025 Rais Samia amewataka Viongozi kuendelea kuhamasisha Wadau wa Sekta Binafsi ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa ya huduma ya reli kwa kununua vichwa vya treni na Mabehewa yao wenyewe.
Soma https://jamii.app/SektaBinafsiReli
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #ServiceDelivery

❤4🔥1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (#UDART), Waziri Kindamba amesema makosa ya nyuma katika usimamizi wa huduma hiyo yamechangiwa na kutokuwepo kwa mkazo katika matengenezo ya mara kwa mara (routine maintenance) ya mabasi.
Ameongeza kuwa kutokana na changamoto zilizojitokeza za mabasi, UDART imejifunza na sasa inaweka mkazo mkubwa kwenye usimamizi endelevu na wenye tija na mabasi mapya yatakapoletwa watazingatia uthibiti na utunzaji.
Mara kwa mara Wadau wamekuwa wakilalamikia huduma mbovu zinazopatikana katika usafiri huo pamoja na changamoto ya mbasi kuharibika mara kwa mara.
Zaidi https://jamii.app/HudumaMwendokasi
#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #Accountability #JamiiAfrica

👎2❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema ifikapo Agosti 15, 2025, mabasi 99 yataingia kwa ajili ya kutoa huduma njia ya Mbagala, pia Oktoba 1, 2025, mabasi mengine 250 yatawasili kwa ajili ya njia ya Mbezi - Kimara hadi Gerezani, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya mfumo wa usafiri wa umma.
Ameyasema hayo leo Agosti 1, 2025 kwenye ufunguzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) Ubungo.
Soma https://jamii.app/ChalamilaMabasiMapya
#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Uwajibikaji #Accountability #Governance

Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka kuwasaidia Wafanyabiashara wa Buguruni hususani katika kipande cha barabara kinachoelekea Buguruni kwa Mnyamani, akidai ujenzi unaoendelea wa barabara ya Mwendokasi, Mkandarasi anamwaga maji upande wa Barabara ya Mandela na Uhuru lakini upande wa Mnyamani hafanyi hivyo.
Anasema, vumbi linalotoka hapo linaathiri #afya na biashara katika maeneo hayo, na kwamba hali hiyo imedumu kwa muda wa mwezi sasa.
Zaidi Soma https://jamii.app/BuguruniMnyamaniVumbi
#JamiiAfrica #JamiiForums #ServiceDelivery #Uwajibikaji #ServiceDelivery #JFHuduma

DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko anadai tangu Julai 26, 2025, baadhi ya Abiria wanapata changamoto kutokana na utaratibu wa kutouzwa kwa kadi za kununua tiketi siku za wikiendi katika usafiri wa Mwendokasi, hali inayowalazimu wasiokuwa na kadi kutegemea msaada wa abiria wenzao.
Anahoji mantiki ya uamuzi huo akiuliza "Hivi wanadhani Wateja wao ni walewale wa siku zote? Hawajui Jiji la Dar es Salaam linapata Watu wapya kila siku, sasa unapoondoa uuzaji wa kadi Wikiendi maana yake hawataki Watu wapya watumie huduma hiyo?"
Fuatilia zaidi: https://jamii.app/KadiUsafiriDART
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma

Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Elimu anadai licha ya kukamilisha masomo yake takriban Mwaka mmoja sasa katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), bado hajakamilisha sehemu ya masomo yake ya Utafiti (Research) kwa madai ya kukosa ushirikiano wa Wahadhiri na Viongozi wa Chuo hicho.
Anaeleza alipata kazi nchini #Uganda, akaamua kubadilisha sehemu ya kufanyia 'Research' yake, lakini hapati mrejesho wowote kutoka OUT, simu na barua pepe (e-mails) hazijibiwi, na kwamba yupo mbioni kuondolewa kwenye ajira yake kwa kuwa hana matokeo kamili ya kuhitimu Shahada, hivyo analazimika kutumia Cheti cha Stashahada (Diploma).
Soma zaidi https://jamii.app/ChuoKikuuHuria1
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability

❤1
Mwanachama wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ametoa wito kwa Mamlaka ya Uchukuzi kutoa kauli rasmi kuhusu hali ya ufanisi wa Kamera za ulinzi kwenye Treni ya Kisasa ya Umeme (#SGR), akidai Usalama wa abiria na Mali zao ni wajibu wa msingi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na vyombo vingine vya ulinzi.
Anasema, kama Kamera zilizopo kwenye Treni zinafanya kazi mbona hakuna Ushahidi wa video, yaani ‘Footage’ zinazosaidia kubaini wahalifu au kusaidia upelelezi wa matukio yanayohitaji ufuatiliaji? Amedai kuna tatizo katika ufuatiliaji, usimamizi au upatikanaji wa taarifa kutoka kwenye kamera hizo.
Aidha, ameshauri kuwa Shirika litoe mwongozo wa hadharani kwa Watumiaji kuwa inapotokea kuna changamoto ya kuripoti kama hizo, mchakato wake utambulike unaanzia wapi na wanapoelekea ili kupunguza mzunguko kama ilivyo sasa.
Soma zaidi https://jamii.app/TRCToeniMaelezo
#JamiiForums #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #ServiceDelivery

Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (#HESLB) kushughulikia changamoto ya mfumo wa uombaji mikopo kwa Mwaka 2025 akidai kuwa unasumbua na unafunguka kwa saa kadhaa.
Pia anadai mfumo unashindwa kusomana vizuri na Mamlaka ya Vitambulisho (#NIDA), hali inayosababisha kushindwa kuidhinisha (validate) namba ya NIDA.
Anadai changamoto hizo zimemzuia kufanya maombi ya Mkopo ikizingatiwa mwisho wa maombi ni Agosti 31, 2025, hivyo ameshauri kuwa kama mfumo wa HESLB na NIDA hausomani vizuri, basi sharti la kutumia Namba ya NIDA liondolewe kwani linaweza kuwakosesha waombaji mikopo.
Zaidi Soma https://jamii.app/ElimuYaJuu
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability
Pia anadai mfumo unashindwa kusomana vizuri na Mamlaka ya Vitambulisho (#NIDA), hali inayosababisha kushindwa kuidhinisha (validate) namba ya NIDA.
Anadai changamoto hizo zimemzuia kufanya maombi ya Mkopo ikizingatiwa mwisho wa maombi ni Agosti 31, 2025, hivyo ameshauri kuwa kama mfumo wa HESLB na NIDA hausomani vizuri, basi sharti la kutumia Namba ya NIDA liondolewe kwani linaweza kuwakosesha waombaji mikopo.
Zaidi Soma https://jamii.app/ElimuYaJuu
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability
❤2
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuchukua hatua za haraka na kinidhamu dhidi ya baadhi ya vituo vya mafuta vinavyojihusisha na mchezo mchafu wa kuuza mafuta yaliyochakachuliwa akidai moja ya madhara yake ni kuharibu injini, gari kuzima na inaweza kusababisha ajali.
Shiriki kwenye mjadala huu kwa kubofya https://jamii.app/MafutaYamechakachuliwa
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability
Shiriki kwenye mjadala huu kwa kubofya https://jamii.app/MafutaYamechakachuliwa
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability
❤2
Mdau ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (#PSSSF) kufuatilia utendaji wa baadhi ya Watendaji wake wa Tawi la Dodoma akidai anapigwa 'danadana' nyingi bila majibu ya msingi tangu alipoanza kufuatilia madai ya malipo yake ya kupoteza ajira tangu Mwaka 2024.
Anadai awali aliwasilisha malalamiko kupitia JamiiForums.com akasaidiwa na Ofisi ya PSSSF Kinondoni lakini alipotakiwa kwenda Makao Makuu Dodoma huko ndipo shida ilipo, akidai huduma zinaenda polepole na kila hatua inahitaji wahusika wapigiwe simu ndiyo watimize majukumu yao.
Zaidi soma https://jamii.app/UmunguWatu
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability
Anadai awali aliwasilisha malalamiko kupitia JamiiForums.com akasaidiwa na Ofisi ya PSSSF Kinondoni lakini alipotakiwa kwenda Makao Makuu Dodoma huko ndipo shida ilipo, akidai huduma zinaenda polepole na kila hatua inahitaji wahusika wapigiwe simu ndiyo watimize majukumu yao.
Zaidi soma https://jamii.app/UmunguWatu
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability
❤1
DAR: Kupitia Jukwaa la JamiiForums.com, Mdau ameeleza leo Agosti 13, 2025 katika Kituo cha Mwendokasi cha Mbezi Luis (Mbezi Mwisho) kulikuwa na msongamano mkubwa wa abiria waliokata tiketi huku mabasi yakifika kwa nadra, akitoa mfano kuwa baadhi yao walifika tangu Saa 11 Alfajiri lakini hadi kufikia Saa Tatu Asubuhi yalifika mabasi mawili pekee.
Anadai Wahusika hawakutoa maelezo yoyote kuhusiana na changamoto hiyo ya mabasi, katika malalamiko yake Mdau huyo amehoji “Kama wanajua kuna shida kwa nini waliamua kukata tiketi na kuchukua fedha za Watu?”
Zaidi Soma https://jamii.app/MwendoKasiMbeziLuis
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amekemea hadharani huduma mbovu aliyokutana nayo katika Hospitali ya Mawenzi ambapo amesema alisubiri kwa muda mrefu ili kupata huduma hospitalini hapo.
Babu amesema baada ya kusubiri kwa muda mrefu alichukua uamuzi wa kupiga simu kwa wasimamizi na ndipo walipofika Madaktari sita na Watumishi wengine ili kumhudumia.
Zaidi Soma https://jamii.app/RCKilimanjaroHospitali
#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Uwajibikaji

😁1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza na Kituo cha Redio, Mwenyekiti wa Wapangaji, Abdullah Msagama amesema Sheria ya Kodi inamtaka mpangaji kulipa kodi ya nyumba kwa Mwezi mmoja mmoja, na kuongeza kuwa utaratibu wa malipo ya Miezi mitatu mpaka sita umeletwa na madalali kwa manufaa yao binafsi.
Vipi Mdau mpangaji, mwenye nyumba anaweza kukubali kodi ya Mwezi mmoja?
Mjadala zaidi soma https://jamii.app/KodiDalaliNyumba
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery

Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Serikali kuingilia kati kiwango cha faini kinachotozwa na kampuni inayoshughulika na ukamataji wa magari maeneo ya Ubungo, akieleza kuwa faini inayosomeka kwenye fomu ni Tsh. elfu 80 bila kuendana na aina ya kosa.
Amedai kuwa kampuni hiyo imekuwa ikikamata magari licha ya magari hayo kuwa tayari yamekaguliwa (scanned), na wakati mwingine wanakamata hata pale ambapo dereva amesimama kwa dharura.
Zaidi soma https://jamii.app/UonevuKwaMadereva
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025
Amedai kuwa kampuni hiyo imekuwa ikikamata magari licha ya magari hayo kuwa tayari yamekaguliwa (scanned), na wakati mwingine wanakamata hata pale ambapo dereva amesimama kwa dharura.
Zaidi soma https://jamii.app/UonevuKwaMadereva
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ametoa wito kwa Mamlaka ya Jiji kutafuta suluhisho la Maegesho maeneo ya Ferry ili kuondoa usumbufu kwa madereva wa Taksi Mtandao kukamatwa na kutozwa faini wanaposhusha au kubeba Abiria.
Soma zaidi https://jamii.app/MaegeshoDar
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery

MWANZA: Mwanachama wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Fichua Uovu ametoa wito kwa mamlaka husika kufuatilia changamoto ya muda mrefu ya Walimu ambao ni Ajira Mpya kutopata malipo ya Fedha ya Kujikimu Wilayani Sengerema licha ya kufuatilia kwa takribani miezi sita.
Mdau anaandika "Majibu ya Afisa Elimu tukiulizia tunaambiwa Mwezi Julai (2025) huwa Mifumo ya Fedha haijakaa sawa, kwa hiyo endeleeni kusubiri”.
Soma zaidi https://jamii.app/MdauSengerema
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #Uwajibikaji #JFMdau2025 #ServiceDelivery

DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai huduma ya Kampuni inayokamata Vyombo vya Moto vinavyoegeshwa kimakosa ndani ya Wilaya ya Ubungo na kueleza faini ya Tsh. 80,000 inayotozwa haiendani na kosa, ufafanuzi umetolewa na Mamlaka inayosimamia.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imesema dereva anayekutwa na kosa hataruhusiwa kuondoka eneo la tukio hadi awe amelipa faini tofauti na utaratibu wa Polisi ambapo faini inaweza kulipwa baadaye hata baada ya kuondoka eneo la tukio.
Halmashauri hiyo pia imetoa maelekezo kwa Watendaji wa Boss Kazi Ltd kufanya kazi kwa kufuata masharti ya mkataba na Sheria za nchi, kuhudumia Wananchi kwa staha, heshima na weledi, kupiga picha kabla ya kutoa faini ili kuepusha sintofahamu na kutoa elimu ya kutosha kwa kila Mwananchi anayekamatwa kuhusu kosa lake na namna ya kulipa.
Zaidi https://jamii.app/WrongParkingUbungo
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025 #Accountability