JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa siku 14 kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kufanya marekebisho ya Mabasi 70 yaliyoripotiwa kuwa Mabovu ili yarudi kutoa huduma za Usafiri na kuondoa kero kwa Wananchi

Hatua inakuja siku chache tangu JamiiForums iripoti hali ya Msongamano wa Abiria katika Kituo cha Abiria cha Kimara Mwisho ambapo Wananchi walilalamikia uchache wa Mabasi

Akizungumza baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho, RC Chalamila amesema anashangazwa kwanini idadi kubwa ya Mabasi ni mabovu licha ya kuwa mtoa huduma amekuwa akilipwa Fedha katika mradi huo huku Abiria wakiendelea kusumbuliwa na Kero hiyo

Hadi sasa #DART imesaliwa na Mabasi 140 yanayotoa huduma kati ya 210

Soma https://jamii.app/DARTBus

#JamiiForums #Governance #ServiceDelivery #SocialJustice #JFHuduma #Accountability
πŸ‘2
Mdau wa JamiiForums.com anasema Oktoba 29, 2022 kuliripotiwa habari ya kupatikana Mwekezaji mpya wa kuendesha Mabasi ya Mwendokasi ambaye ni Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu

Taarifa ya Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafiri wa #DART, Mhandisi Fanuel Kalugendo ilisema Kampuni hiyo ingeanza kazi Novemba 2022 ambapo mwanzoni ingeingiza Mabasi 177, na ndani ya Miezi 6 (kuanzia Novemba 2022) ingeingiza jumla ya Mabasi 750

Anahoji, hadi sasa tatizo ni nini? Magari mapya mbona hayaonekani wala Mwekezaji wake? Mbona Wananchi hawaelezwi mkwamo umetokea wapi?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MwekezajiDARTVipi

#ServiceDelivery #Governance #JamiiForums #Accountability
πŸ‘6
USAFIRISHAJI: MKURUGENZI WA MABASI YA MWENDOKASI ATENGULIWA

Rais Samia ametengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Kasi (#DART), Dkt. Edwin P. Mhede huku taarifa ikisema atapangiwa kazi nyingine

Aidha, Rais Samia amemteua Dkt. Athuman Kihamia kuwa Mtendaji Mkuu wa DART. Hapo awali, Dkt. Kihamia aliwahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha

Hatua hii inakuja wakati ambao kumekuwa na malalamiko ya Watumiaji wa Mabasi hayo wakieleza kutoridhishwa na ubora wa huduma zake

Soma https://jamii.app/DARTCEO

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #Accountability
πŸ‘7
Mtendaji Mkuu wa Mabasi Yaendayo Haraka (#DART), Dkt. Athuman Kihamia amesema amepata ripoti ya tukio la Dereva wa Mwendokasi kuwatelekeza Abiria Kituo cha Kivukoni na wanatarajia kumchukulia hatua za kinidhamu yeye pamoja na Wasimamizi wa Kituo cha Kivukoni

Amesema β€œNilipata taarifa na nikafika kituoni, nikakuta Dereva mwingine amewapeleka Abiria Kimara baada ya Dereva wa awali kuwapeleka Abiria Morocco kisha kuwarejesha Kivukoni na kuwatelekeza hapo. Hatua zitachukuliwa ili iwe funzo kwa kuwa kuna malalamiko mengi tunapata kuhusu huduma zetu.”

Awali, Mdau wa JamiiForums.com aliripoti juu ya tukio hilo na kusema Dereva husika aliungwa mkono na Msimamizi wa Kivukoni. Pia, alidai Abiria walipanda basi saa 1:00 Usiku lakini safari ya kwenda Kimara ilianza saa 3:25 Usiku

Soma https://jamii.app/MwendokasiUfafanuzi

#JFHuduma #Governance #JFUwajibikaji #JamiiForums
πŸ‘4❀1
DAR: Watumishi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Shabani Kajiru (Msimamizi wa Kituo cha Kivukoni) na Brown Mlawa (Afisa Ufuatiliaji wa Kituo) wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tukio la vurugu zilizotokea kituoni hapo Machi 26, 2024

#DART imeeleza kuwa wahusika hao walipewa taarifa mapema kuhusu Changamoto ya Usafiri iliyosababisha Abiria kupelekwa Kituo cha Morocco kisha kurejeshwa Kivukoni na kutelekezwa hapo kwa saa kadhaa, lakini hawakushughulikia suala hilo ambalo lilisababisha usumbufu

DART imesema kuwa inamuelekeza Mtoa Huduma wa Mpito (#UDART) kuwachukulia hatua na kuwasimamisha kazi Salehe Maziku na Chande Likotimo (Madereva), Lameck Kapufi (Msimamizi wa Kituo) na Erick Mukaro (Afisa Usafirishaji) ambao pia walihusika katika tukio hilo

Soma https://jamii.app/TamkoLaDART

#JFHuduma #JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums
πŸ‘1
USAFIRISHAJI: Taarifa ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (#DART) maarufu kwa jina la Mabasi ya Mwendokasi ya Aprili 23, 2024 imesema Barabara ya #Jangwani imefungwa kutokana na mafuriko, hivyo Mabasi kwa njia za #Kimara hadi #Kivukoni na Gerezani yataishia #MagomeniMapipa

Vilevile, huduma ya usafiri wa Mabasi ya DART inaendelea kutolewa kwa njia ya #Morocco kwenda Kimara na eneo la katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa njia ya #Muhimbili na #Gerezani

Soma https://jamii.app/UsafiriMwendokasi

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #JFHuduma #Governance
πŸ‘2
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (#DART) kutafuta njia ya haraka kuboresha huduma ya usafiri wa Mwendokasi kwa maelezo kuwa inazidi kupungua ubora kila siku.

Anasema "Mabasi ni machache na hali hiyo inalazimu Watu kukaa zaidi ya Saa moja hadi mbili Kituoni kusubiria magari ambayo nayo yakifika kupata nafasi ya kuingia unatakiwa uwe 'umeshiba' kutokana na utaratibu mbovu uliopo."

Soma zaidi https://jamii.app/MdauMwendokasi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025
❀2πŸ‘1
DAR: Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) imepiga marufuku Watoa Huduma Binafsi kutoa taarifa zozote kwa Vyombo vya Habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), ikiwemo mikataba na mipango mbalimbali ya uendeshaji.

Mtendaji Mkuu wa #DART, Dkt. Athumani Kihamia amesema mawasiliano yote ya umma yanayohusu sera, ununuzi wa mabasi au shughuli za waendeshaji wenzao lazima yatolewe na DART pekee. Amesisitiza baadhi ya taarifa zilizotolewa na watoa huduma binafsi ni batili na zinakiuka taratibu rasmi za mawasiliano na watoa huduma kuheshimu majukumu yao bila kuingilia mamlaka ya msimamizi.

Aidha, ameongeza kuwa DART inatarajia kuanza kutoa huduma kupitia Mradi wa BRT Awamu ya Pili – Mbagala katikati ya Agosti 2025, na kufikia Oktoba zaidi ya mabasi 930 yanatarajiwa kuwepo, yakiletwa na wawekezaji kupitia ushirikiano wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP).

Soma zaidi https://jamii.app/WatoaHudumaDART

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #JFHuduma
❀1πŸ€”1
DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza utaratibu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kutouza kadi za kununua tiketi za usafiri wa Mwendokasi siku za Wikiendi, ni kero na unasababisha Watu wengi kukosa huduma, DART imetoa ufafanuzi.

Mtendaji Mkuu wa #DART, Dkt. Athumani Kihamia amesema si lengo lao kuuza kadi siku za Jumamosi na Jumapili, kwani abiria anaweza kupata kadi hizo kwa siku tano za wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa na kwamba Wananchi wamehamasika na wamenunua kwa wingi kadi na zinaongeza ufanisi wa kukusanya mapato na kuepusha ubadhirifu.

Soma https://jamii.app/MajibuDART

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #Uwajibikaji #JFMdau
❀3