JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Kampuni ya kutoa Mikopo kwa Njia ya Mtandao ya #WhitePathLTD, imepigwa faini ya Ksh. 495,614 sawa Tsh. Milioni 8.6 kwa madai ya kuingilia na kutumia taarifa binafsi za Wateja kwa kigezo cha kufuatilia Madeni

Ofisi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ilipokea takriban malalamiko 150 dhidi ya Kampuni hiyo ikidaiwa kuwapigia Simu ndugu na jamaa wa wadeni wao wakiwataka kuwakumbusha kulipa madeni

Soma https://jamii.app/KampuniMikopoKE

#PersonalData #DataProtection
👏8👍4
KENYA: Mamlaka ya Mawasiliano (CA) na Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binfasi (ODPC) zimeonesha kutoridhishwa na hatua za Serikali juu ya Mradi wa Sarafu Mtandao ya Worldcoin iliyokusanya Taarifa za Wananchi zaidi ya 350,000

Licha ya Kusitisha shughuli za kampuni hiyo, Kamishna wa Taarifa Binafsi, Immaculate Kassait amehoji kutokuwepo kwa mfumo wa Udhibiti wa Taarifa unaoonesha Usalama wa Taarifa za Siri zilizokusanywa pamoja na Usalama wa Mtandao huo

Worldcoin hufanya Usajili kupitia Mboni za Jicho kama Utambulisho wa Kidijitali uitwao 'World ID', ambapo anayesajiliwa analipwa Tsh. 120,385

Soma https://jamii.app/DataBreachKE

#JamiiForums #DataProtection #DataPrivacy #Accountability #SocialJustice #DigitalRights #PersonalData
👍9
KENYA: Kutokana na kuongezeka kwa ripoti za vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kesi za mauaji, katika nyumba za makazi maarufu kama (AirBnB) na Hoteli, Mamlaka ya Udhibiti wa Taarifa Binafsi imetoa maagizo kwa Watoa Huduma Kurekodi na kutunza kumbukumbu za utambulisho wa wageni, kurekodi muda wa kuingia na kutoka kwa wageni na pia Kukusanya na kuhifadhi kwa muda Vitambulisho vya wageni

Mamlaka hiyo imesema Maagizo hayo yanalenga kuzuia vitendo vya Uhalifu, Unyanyasaji na hata Mauaji yanaweza kutokea katika kuhakikisha usalama wa Wakazi na Wageni

Usalama wa AirBnB nchini Kenya umekuwa mashakani katika siku za hivi Karibuni baada ya Matukio ya Mauaji ya Kinyama ya Wateja akiwemo Mwanamitandao #ScarletWahu na Mwanamke mmoja ambaye aliuawa kisha mwili wake kukatwa vipande na kuwekwa kwenye ndoo ya taka huko #Kasarani

Soma https://jamii.app/KenyaAirBnB

#JamiiForums #DataPrivacy #PersonalData #DataProtection #DataProtectionLaw #Governance #Accountability
👍31
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetangaza kuanza Usajili wa Wakusanyaji na Wachakataji wote wa #TaarifaBinafsi Nchini ambapo imetoa muda wa Miezi 6 kuanzia leo Aprili 10, 2024 kwa wahusika kukamilisha zoezi hilo

Watoa Huduma hizo wanapaswa kutekeleza wajibu huo kwa kufuata Kifungu Namba 14(1) cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Namba 11 ya Mwaka 2022

PDPC imeeleza kuwa Wakusanyaji na Wachakataji wote wanatakiwa kufanya Usajili kupitia Tovuti ya Tume ambayo ni www.pdpc.go.tz

Soma https://jamii.app/PDPCTZA

#JamiiForums #DataProtection #DataPrivacy #PersonalData #Governance
👍9
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anahoji sababu za Nyaraka zenye taarifa Binafsi za Watu kutumika kutengenezea vifungashio vya bidhaa kwani ni udhalilishaji na kutotunza faragha za Watu.

Je, umeshakutana na hali hii?

Soma https://jamii.app/NyarakaVifungashio

#JamiiForums #Accoutability #Uwajibikaji #DataProtection #DataPrivacy #PersonalData #Governance
👍3😁1
TAARIFA ZA WATU ZINATUMIKA VIBAYA, KWANINI HATUA HAZICHUKULIWI?

Mdau wa JamiiForums amelalamikia suala la #TaarifaBinafsi za Watu kutumika vibaya na kusambazwa bila ridhaa zao huku Mamlaka zikiwa hazijishughulishi kwa lolote

Amesema mara kadhaa amekutana na taarifa za Watu kwenye Vifungashio vilivyotengenezwa na nyaraka kama barua za kazini, matokeo ya mitihani, vyeti na nyingine nyingi

Amehoji kwanini Mamlaka haizichukulii hatua Taasisi zinazohusika na haya kwani Vifungashio hivi vipo kila sehemu na sasa vimeshamiri mno

Zaidi, tembelea https://jamii.app/VifungashioTaaarifa

#JamiiForums #DigitalSecurity #PersonalData #JFDigitali #PersonalDataProtection #DataPrivacy
👍1
Kadiri huduma na biashara zinavyozidi kuelekea kwenye Majukwaa ya Kidijitali, matumizi ya mtandao na uwepo wa watu mtandaoni kwa sasa haviepukiki.

Kutokana na ongezeko la uhalifu wa mtandaoni, kulinda taarifa kutokana na ulaghai na vitisho vya mtandaoni ni muhimu. Kulinda #TaarifaBinafsi huanza kwa kufanya mazoea salama ya kuvinjari mtandaoni

Zaidi tembelea https://jamii.app/UlinziKivinjari

#JamiiForums #DigitalSecurity #PersonalData #JFDigitali
👍4