JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Zitto Kabwe (Kiongozi wa ACT-Wazalendo) amesema tukiendelea kujadili kuhusu nini kianze tutafika 2024/25 tukiwa hatuna tulichokipata. Tupate Sheria mpya ya Uchaguzi na Sheria ya Tume ya Uchaguzi ambayo inaweka utaratibu wa namna ya kuwapata Makamishna wa Uchaguzi ili tuondokane na utaratibu wa sasa ambao una Wakurugenzi na wote tunajua ni Makada wa Chama Tawala

Mtu aliyeshindwa Uchaguzi halafu akateuliwa kuwa Mkurugenzi na kwenda kusimamia Uchaguzi katika hali ya kawaida hata akiwa mtu wa kutenda haki haitumi taarifa nzuri za haki. Kwahiyo Sheria hiyo iangalie hayo yote

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘2
Mjumbe wa Mkutano wa Kujadili Hali ya Demokrasia Nchini kutoka NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amesema "Kilichofanyika 2019 na 2020 sio Uchaguzi, suala hili hatuwezi kuwa na ubishani mkubwa. Swali ni je nini kifanyike ili kufanikisha Uchaguzi wa 2024 na 2025. Sisi (NCCR-Mageuzi) tunasita kusema nini kifanyike kwa kuwa rejea hazioneshi kama kumewahi kufanyika Uchaguzi. Pia, hatuwezi kuzuia 2024/25 isije, hatuwezi kuzuia kilichofanyika 2019/20 kutofanyika 2024/25 lakini tunatamani mwaka 2024/25 kufanyike Uchaguzi"

Ameongeza "Tunaamini tukitaka kufanya uchaguzi Mkuu wa 2025 utakaotanguliwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, mtu wa kumuuliza yupo. Nasema haya kwa sababu hata Sheria za Uchaguzi zilikuwepo kwa Miaka iliyotangulia lakini 'jamaa' aliamua kwamba hataki Uchaguzi, hivyo tumuulize Rais aliyepo kama anataka uchaguzi ufanyike"

Fuatilia zaidi https://jamii.app/DemokrasiaTCD

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘8
Reginald Munisi (CHADEMA) amesema kama Chama tulipendekeza tutengeneze Chombo cha Kusimamia Mchakato wa Katiba kitakachoitwa Reference Group itakayoundwa na Rais, Viongozi wa Chama, Viongozi wa Dini, Asasi ya Kiraia na Sekta Binafsi ili kuhakikisha safari hii mchakato haikwami na penye tatizo lolote tunajua tuna chombo cha kukiendea

Ameongeza kuwa kwa mapendekezo ambayo tulitoa na tumekuwa tukijadiliana na Serikali kama Muswada ungepelekwa mwezi wa 9 Bungeni, mchakato ungekamilika na tungepata Tume Huru na namna itakavyopatikana na mambo mengine ambayo tungeyataka

Munisi anafafanua kuwa kwa mazingira ya sasa ya Uchaguzi, nikienda kuchukua Fomu nikanyimwa tayari nimeondolewa nafasi ya kwenda Mahakamani kushtaki na matokeo ya kuhojiwa ni ya Wabunge tu, ya Rais hayahojiwi, hivyo kuna migongano ya kurekebisha kwenye Katiba kabla ya Sheria

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘5
Anamringi Macha (CCM) amesema Mchakato wa Katiba unakwama kwa sababu ya kukosekana kwa maridhiano baina ya Vyama vya Siasa, ambapo ameeleza kwa kuna wengine walisema kuna Watu wamekuja na Katiba yao mfukoni nk.

Vilevile amesema kuwa Mchakato wa Katiba ni tofauti na kitabu cha hadithi hivyo utachukua muda lakini wamekubaliana kufanya mabadiliko ya Katiba ili kukidhi mahitaji ya Uchaguzi, hata hivyo baadhi ya hayo tayari yamefanyika kama kuondoa zuio la kufanya Mikutano ya Vyama vya Siasa

Macha ameongeza kuwa anafikiri Elimu ya Katiba pia inatakiwa kila wakati kwasababu hata kama tungepata Katiba Pendekezwa mwaka 2012/14, kuna mambo tungetakiwa kuyaangalia upya ili yaendane na mazingira ya wakati huu na ingetakiwa Watu wapate Elimu

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘4πŸ‘1
Akishiriki katika Mkutano wa Kujadili hali ya Demokrasia Nchini, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Hamis Issa Hamis amesema "Sisi kama Tume, tunasema Uchaguzi ni Mchakato Endelevu, unapoisha Uchaguzi mmoja tunaanza Uchaguzi mwingine. Utoaji wa elimu kwa Wapiga Kura ni mchakato ambao huwa hauishi, hausiti, kwa Zanzibar tunaendelea. Kwa sasa tunatumia TV kuwaelimisha Wananchi kuhusu Uchaguzi"

Ameongeza "Sheria zinataka tuandae mpango kazi na bajeti na vyote tumeshaandaa. Kuanzia mwezi Novemba tutaanza kuandikisha Wapiga Kura wapya kwa kuwa Serikali imeshakubaliana na bajeti yetu. Pia, mwakani zoezi la kuandikisha Wapiga Kura litaendelea. Kutokana na Sensa kuna ongezeko la Watu hivyo tutafanya Mapitio ya Majimbo"

Fuatilia zaidi https://jamii.app/DemokrasiaTCD

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘3
Hamad Masoud Hamad (CUF) amesema #Zanzibar imefanya Chaguzi 6, ni Chaguzi mbili tu hazikuwa na mauaji (2010 na 2015), hivyo jambo muhimu ambalo linaweza kufanyika ili kubadilisha hali hiyo ni 'Good Political Will'. Hakuna yeyote aliyeko madarakani atapenda aondoke madarakani, kwa hiyo cha kwanza cha kufanyika kipo ndani ya nafsi ya mtu

Kuhusu Uchaguzi wa Muungano, amesema wengi wanazungumzia kubadili Sheria na kadhalika lakini Uchaguzi zaidi ya 80% unasimamiwa na CCM. Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa hajatajwa kokote kwenye Sheria ya Uchaguzi, sasa anakuja kwenye Uchaguzi kufuata nini?

Fuatilia zaidi https://jamii.app/DemokrasiaTCD

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘5❀1
Akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Balozi wa Marekani, Michael Battle amesema Demokrasia sio lazima ifanane kwa kila nchi, na hivyo Demokrasia ya Tanzania, inabidi izingatie mazingira ya Tanzania, ifanane na Tanzania

Battle amesema Tanzania imekuwa ikipiga hatua vizuri na wao (Marekani) wataendelea kuwa washirika wa Tanzania ili kusaidia kukuza Demokrasia nchini

Marekani ni moja kati ya wadau waliofadhili Mkutano wa Demokrasia wa mwaka 2023, ambao kwa mwaka huu mgeni rasmi ni Rais wa Zanzibar, Hussein Ally Mwinyi

Zaidi soma https://jamii.app/BaloziUSDemokrasia

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘4
Prof. Lipumba (Mwenyekiti wa TCD) amesema Mkutano wetu ulikuwa unajadili hali ya Demokrasia Nchini kuelekea Chaguzi za 2024/25, tumetambua Mfumo wa Vyama Vingi umekuwepo kwa zaidi ya miaka 30 na Washiriki wanakubali mfumo huu ni muhimu katika kuhakikisha Usalama na Amani ya Nchi

Ameongeza kuwa sisi Wadau wa Siasa na Vyama 19, Mashirika ya Kimataifa na Asasi za Kiraia baada ya majadiliano, kuelekea katika Chaguzi zinazokuja tumefikia maazimio ambayo tutaandika na kuyawasilisha Serikalini

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘1
Prof. Lipumba (Mwenyekiti wa TCD) amesema kuhusu mabadiliko ya Katiba tumezingatia Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya inayotokana na Maoni ya Wananchi pamoja na kwamba ulikwama kidogo ni vizuri ukakwamuliwa na uweze kukamilishwa ili tupate Katiba yenye Misingi ya Kidemokrasia

Ameongeza kuwa Washiriki wametambua kwamba taratibu za Uchaguzi ni Muhimu zifanyike katika Chaguzi za 2024/25 na dhana kwamba tunaweza kukamilisha mchakato wa Katiba kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu tutakuwa tunajidanganya, hivyo Mkutano umejadili na kupendekeza mabadiliko yafanyike katika Katiba ya Sasa ili kuruhusu uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi

Fuatilia zaidi https://jamii.app/DemokrasiaTCD

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘5❀1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akifunga Mkutano wa Siku 2 wa Kijadili hali ya Demokrasia Nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Rais Hussein Ally Mwinyi amesema mapendekezo ya Wadau yaliyotolewa katika mkutano huu yatafanyiwa kazi

Miongoni mwa Mapendekezo yaliyotolewa na Wadau ni pamoja na kurejea mchakato wa Katiba Mpya, kubadili Sheria za Uchaguzi na kuwa na usimamizi mmoja kwa chaguzi zote

Aidha, amewapongeza TCD kwa kuandaa Mkutano huu kwa Kujadili hali ya Demokrasia Nchini na ametoa wito wa TCD kuendelea kuandaa Mikutano hii ili kuendeleza Demokrasia kwa kuwa inaonesha ukomavu wa kisiasa katika Nchi yetu

Fuatilia zaidi https://jamii.app/DemokrasiaTCD

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
πŸ‘1
Rais Hussein Ally Mwinyi amesema Tanzania iliruhusu Mfumo wa Vyama Vingi Julai 1992 tokea wakati huo Jamhuri ya Muungano imeonesha nia ya Kukuza Utawala wa Kidemokrasia ikiwemo kusaini Mikataba yenye lengo la Kukuza Demokrasia

Amesema kuwa kuanzishwa kwa Mfumo huu kulipelekea kufanywa mabadiliko katika Sheria mbalimbali na kuanzishwa kwa Sheria mpya ikiwemo Sheria ya Vyama vya Siasa No. 5 ya mwaka 1992 ambayo iliwezesha kuratibu Usajili wa Vyama mbalimbali vya Siasa, Sheria ya Uchaguzi No. 1 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Rais Mwinyi ameongeza kuwa Tanzania ilifanya Uchaguzi uliohusisha vyama vingi mwaka 1995 na kufuatiwa na chaguzi nyingine 5 za Kidemokrasia kila baada ya Miaka 5 na katika kipindi chote hiki tumekuwa tukifanya mabadiliko kwenye Sheria zetu za Uchaguzi ili kufanya Chaguzi zetu kuwa Bora zaidi

Fuatilia zaidi https://jamii.app/DemokrasiaTCD

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Accoutability #Democracy #MkutanoWaDemokrasia23
❀1πŸ‘1
Akiongea katika Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Nchini, Rais Hussein Ally Mwinyi amesema "Serikali inatambua michango ya Wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Viongozi wa Dini, Watu Binafsi na tathmini mbalimbali ambazo wamekuwa wakiwasilisha Serikali kwaajili ya kufanyiwa kazi. Napongeza maoni yote yenye nia njema ya kuimarisha ujenzi wa Taifa letu"

Ameongeza "Ni mategemeo yangu mlipokuwa mnatafakari Demokrasia ya Nchi yetu kuelekea chaguzi zijazo mlizingatia nafasi ya Mfumo wa Vyama vingi katika kukukuza Demokrasi ya Makundi Maalumu kwenye Jamii, mlizingatia ushirikiwa Wanawake, Vijana na watu Wenye Ulemavu katika nafasi mbalimbali za maamuzi"

Rais Mwinyi amemalizia kwa kusema "Serikali itaendelea kudumisha Demokrasia Nchini mwetu na nashukuru kunialika mimi na wenzangu Serikalini kuja kushiriki katika hafla ya kufunga Mkutano huu ambao ni kielelezo cha ukomavu wa Demokrasia katika Nchi yetu"

#Governance #JFDemokrasia #Accoutability #MkutanoWaDemokrasia23
❀1
DAR: Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (#TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema hadi kufikia leo Oktoba 2, 2023, upungufu wa Umeme katika Gridi ya Taifa ni Megawati 300 hadi 350 ambapo Wiki iliyopita kulikuwa na upungufu wa Megawati 400

Aidha, Naibu Waziri Nishati, Judith Salvio Kapinga aliyetembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Gesi Asilia, Tegeta, Dar es Salaam kinachozalisha Megawati 43, amesema mtambo mmoja kati ya Mitano upo nje ya kituo kwa ajili ya matengenezo ya lazima

Soma https://jamii.app/GridiYaTaifa

#JFHuduma #Accoutability #JamiiForums
πŸ‘5
ARUSHA: Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), Jaji Iman Aboud amesema bado Serikali nyingi za Afrika hazikubali kushtakiwa pamojja kutekeleza Hukumu zinazohusu Haki za Binadamu zinazotolewa dhidi yake

Akizungumza katika Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki ya Binaadamu na Watu (ACHPR) kilichofanyika Jijini Arusha amesema kati ya Hukumu zaidi ya 200 zilizotolewa na Mahakama hiyo, zilizotekelezwa na baadhi ya Nchi ni chini ya 10%

Ameongeza kuwa suala la #HakiZaBinadamu ni muhimu kuzingatiwa kwasababu hakuna Maendeleo na Amani bila kuwepo na Haki. Pia, amezitaka Serikali kuruhusu kushitakiwa na Asasi za Kiraia (CSO's) na Watu Binafsi ili kulinda na kuendeleza Haki za Binadamu

Soma https://jamii.app/AfCHPR

#JamiiForums #Governance #SocialJustice #Accoutability #JFHakiRaia
πŸ‘2❀1πŸ‘1
Mdau aliyejitambulisha kuwa ni Mwanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (#DIT) anadai taasisi hiyo inachukua hadi miaka minne kurejesha malipo ya fedha ya Wanafunzi (refund) waliolipa ada wakati wa udahili kabla ya kuingiziwa mkopo kutoka Bodi ya Mikopo (#HESLB)

Anadai kuna wakati wengine wanatakiwa kusubiri β€˜refund’ hadi watakapohitimu masomo au inaweza kuhamishiwa mwaka mwingine wa masomo kitendo anachoona si sahihi kwa sababu bajeti ya Wanafunzi si rafiki kutokana na wengi wao kutokuwa na ajira

Soma https://jamii.app/RefundDIT

#KemeaRushwa #ElimuBilaRushwa #Accoutability #JamiiForums
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima amesema kuna nchi ikitokea mtu hajaridhika na maamuzi ya Tume ya Uchaguzi yuko huru kupinga, hatua iliyojenga uaminifu wa Tume hizo kwa Wananchi

Amesema Afrika Kusini na Kenya Tume za Uchaguzi zinafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Haki, ila Tanzania kuna usanii mwingi, kujipendekeza, vikundi vya kupitisha watu na kupeana madaraka kiujanja ujanja

Zaidi soma: https://jamii.app/MjadalaUchaguzi

#JamiiForums #UtawalaBora #Uwajibikaji #Governance #Accoutability
πŸ‘11❀3
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anahoji sababu za Nyaraka zenye taarifa Binafsi za Watu kutumika kutengenezea vifungashio vya bidhaa kwani ni udhalilishaji na kutotunza faragha za Watu.

Je, umeshakutana na hali hii?

Soma https://jamii.app/NyarakaVifungashio

#JamiiForums #Accoutability #Uwajibikaji #DataProtection #DataPrivacy #PersonalData #Governance
πŸ‘3😁1
Mahakama ya Ushindani na Haki za Watumiaji Huduma (CCPT) ya #Nigeria, imeitoza Kampuni ya Matangazo ya Televisheni ya #MultiChoice takriban Tsh. Milioni 282.56 pamoja na kuwapa Wateja wake Kifurushi cha Matangazo ya mwezi mmoja bila malipo

Uamuzi huo unafuatia malalamiko ya Wateja wa MultiChoice ambayo inaendesha huduma zake kupitia #DTSV na #GOTV juu ya kupandishwa kwa gharama za Vifurushi kwa 25% kuanzia Mei 2024 ambapo CCPT ilijiridhisha kulikuwa na ukiukwaji wa Haki za Wateja

Awali, #CCPT iliizuia MultiChoice kupandisha bei za Vifurushi lakini kampuni hiyo ilikata rufaa na kupandisha bei wakati shauri likiwa Mahakamani, hivyo uamuzi huo umekuja kama adhabu ya kupuuza agizo la Mahakama.

Soma https://jamii.app/MultiChoiceNGR

#JamiiForums #DigitalRights #Governance #SocialJustice #Accoutability
❀3πŸ‘3🀣2
KATAVI: Mdau wa JamiiForums.com ameandika β€œNikiwa eneo la Mtemi Beda, Wilaya ya Mpanda nimekuta kero ya muda mrefu ya ubovu wa Barabara ya Mtaa wa Misukumilo kwenda Kitongoji cha Milala Shongo Kijiji cha Milala.”

Anaongeza β€œNilivyoona hivyo nikakumbuka Mkataba wa TARURA - Katavi waliosaini Oktoba, 2024 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na Daraja la Milala Shongo ambapo walituambia Tsh. Milioni 500 zitatumika na ujenzi utakamilika Juni 2025.”

Mdau anaeleza kuwa β€œJambo la kushangaza ujenzi pekee uliofanyika ni greda kuchimbua barabara na kuondoka, najiuliza kuna nini kinaendelea? Maana Wananchi tunateseka.”

Zaidi bofya https://jamii.app/DarajaMtemiBeda

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accoutability #Governance
❀2
GEITA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio analodai limetokea katika Hifadhi ya Msitu Kigosi, akidai kijana mwenye umri wa Miaka 20+ ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Hifadhi, jana Agosti 13, 2025.

Anadai Familia ya marehemu ilitoa taarifa Polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo kisha wakaambiwa wakauchukue mwili leo Agosti 13, 2025 kwa ajili ya mazishi lakini familia haitaki kufanya hivyo hadi itakapopewa majibu juu ya hatua zilizochukuliwa.

Alipotafutwa Meneja Uhusiano wa TFS, Johary Kachwamba amesema β€œTumepata taarifa kuhusu tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inafanya kikao leo (Agosti 14, 2025) itajadili kubaini ukweli wake, kukiwa na taarifa zaidi tutatoa mrejesho.”

Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Safia Jongo zinaendelea.

Soma zaidi https://jamii.app/KijanaAuawaGeita

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accoutability #Governance #HumanRights #CivilRights #JFMdau2025