This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, #NapeNnauye ameitaka Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (#PDPC) kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyowekwa na si kwa Matakwa na Utashi wa watu fulani
Akizungumza katika uzinduzi wa Tume hiyo kwenye Ukumbi wa TCRA Jijini Dodoma, Januari 19, 2024, Nape amesema “Hatakiwi kutokea mtu kutweza imani tuliyowapa ya kulinda taarifa zetu wote, fanyeni kazi kwa kujiamini na mtimize majukumu kwa mujibu wa Sheria.”
Amesema "Kama kuna Tume tunataka iwe huru kutekeleza majukumu yake basi ni hii, nataka iwe huru na mlinde hilo, tusiingilie na nyie msikubali kuingiliwa, mlindwe na Sheria tulizotunga.”
Soma https://jamii.app/PDPC
#DataPrivacy #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #Faragha #DigitalRights #JamiiForums

❤2👍1
MOROGORO: Wateja wa Nyumba za Wageni wamejulishwa kuwa hawatakiwi kuandika taarifa za wanapotoka au wanapoelekea katika Vitabu vya nyumba hizo, kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Taarifa Binafsi
Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa (#PDPC), Stephen Wangwe amesema Watu wanatakiwa kujua Sheria ya #TaarifaBinafsi ili wasiingie matatizoni, kwa kuwa taarifa hizi hazina uhusiano na wao kufika katika nyumba hizo
Aidha, amesema tangu kuanza kutumika kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, mtu anapoona taarifa zake zimetumika bila ridhaa yake anaruhusiwa kulalamika kisha hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika au mhusika
Soma https://jamii.app/PDPCMarch1
#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako

👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (#PDPC), Innocent Mungy ameeleza umuhimu wa Tume kusimamia ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kusema "Tunalinda zisiende kwenye mikono isiyo sawa, isiyoruhusiwa kuwa na matumizi ya hizo taarifa."
Ameeleza hayo wakati wa mafunzo maalum Julai19, 2025, yakihusisha Maafisa Habari wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC).
Soma zaidi https://jamii.app/PDPCTaarifaBinafsi
#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #PersonalDataProtection #DataPrivacy #DigitalRights

❤1
DODOMA: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (#PDPC) imeiamuru Kampuni ya MI CASA kumlipa Abdul Naumanga fidia ya Tsh. Milioni 20 kwa kutumia picha na video zake kwenye akaunti yao ya Instagram bila idhini.
Tukio hilo lilitokea kati ya Februari na Aprili 2023, na kutolewa maamuzi Julai 10, 2025 kufuatia Malalamiko Na. 8 ya 2024. Abdul aliomba picha na video hizo ziondolewe lakini MI CASA walikaidi, hali iliyomlazimu kupeleka shauri hilo kwa Tume.
Tume imesisitiza ukiukwaji wa faragha Mitandaoni, hususan kwenye baa, kumbi za starehe na sherehe, umekithiri na lazima udhibitiwe, kwamba hatua hiyo inalenga kuwakumbusha wachakataji wa Taarifa Binafsi kuzingatia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022.
PDPC imeeleza kuwa ni lazima wachakataji wa taarifa wazingatie Sheria na kuhakikisha kuwa faragha za Wananchi zinalindwa.
Zaidi Soma https://jamii.app/KuvunjaFaragha
#JamiiForums #JamiiAfrica #DataProtection #DataPrivacy #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako

❤3