JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Uhuru wa kujieleza haumaanishi Uhuru wa upande mmoja tu. Ni Haki ya kila Mtu kusema, kusikilizwa, na kujibiwa kwa hoja

Wakati tunatetea Uhuru huu, lazima tukubali kwamba unafanya kazi kwa wote, wale tunaokubaliana nao au tunaowapinga

#FreedomOfSpeech #RespectAllVoices #SautiYetuUhuruWetu #FreedomOfExpression #JamiiForums #Democracy
Kila Mtu ana sauti, lakini si kila Mtu anapewa nafasi ya kusikika. Watu hupuuzwa, kunyamazishwa, au hata kukandamizwa ili wasiseme ukweli au kudai Haki zao

Dini, Serikali au Bendera haziwezi kuumizwa, ni Watu ndiyo wanaoweza kuumizwa. Ndiyo maana Haki za Binadamu zinalinda Watu na ni Watu wasio na Mamlaka walio hatarini zaidi na wanaohitaji ulinzi mkubwa zaidi

#FreedomOfSpeech #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #Democracy #FreedomOfExpression #RespectAllVoices #EveryVoiceMatters
Haki za Binadamu zipo kulinda Utu wa kila Mtu, si kulinda Mifumo ya Mamlaka

Serikali zinapojihami dhidi ya ukosoaji kwa kutumia Sheria kandamizaji, zinakandamiza Watu badala ya kuwalinda

Uhuru wa Kujieleza unapaswa kuwalinda wale wasio na sauti, sio kuimarisha Mamlaka ya walio Madarakani

#HumanRights #FreedomOfSpeech #ProtectPeopleNotPower #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #FreedomOfExpression #Democracy
Uhuru wa Kujieleza si Haki ya anasa, ni Haki inayowezesha Watu kudai Maisha bora. Bila sauti, mahitaji ya msingi ya Watu yanapuuzwa

Uhuru huu ndio njia ya kuhakikisha kuwa kila Mtu anaweza kuzungumza kuhusu Haki zake na kupigania Maisha yenye utu

#FreedomOfExpression #HumanRights #SautiYetuUhuruWetu #Democracy #JamiiForums #EveryVoiceMatters
DAR: Akielezea msimamo wa Kisheria wa Sheria ya Huduma za Habari, Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula amesema Serikali na nchi kwa jumla imekubali Uandishi wa Habari ni taaluma kama zilivyo nyingine, hivyo ni lazima kufuata matakwa ya Kisheria

Amesema hata kama Mtu ana kipaji kikubwa kiasi gani, kama hajasoma Taaluma ya Uandishi wa Habari haruhusiwi Kisheria kufanya kazi za Habari

Ameeleza “Kifungu cha 19 (1) cha Sheria ya Huduma za Habari, kinasema Mtu hataruhusiwa kufanya kazi ya Uandishi wa Habari, isipokuwa mtu huyo awe amethibitishwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria.”

Soma https://jamii.app/IthibatiMaelekezo

#PressFreedom #JamiiForums #Governance #FreeSpeech #Democracy #FreedomOfExpression
Katika Nchi ya Kidemokrasia, Watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kukusanyika bila hofu ili kueleza maoni yao, kupinga udhalimu na kudai Haki zao

Maandamano ya Amani na mikutano ya hadhara ni njia halali za kushinikiza mabadiliko ya Kijamii na Kisiasa. Serikali zinazozuia Haki hii zinadhoofisha Demokrasia na kuwanyima raia sauti yao halali.

#FreedomOfAssembly #Democracy #JamiiForums #SautiYetuUhuruWetu #FreedomOfExpression #EveryVoiceMatters
Teknolojia inapaswa kuwa nyenzo ya kukuza Uhuru wa Kujieleza, si chombo cha udhibiti au upotoshaji wa taarifa

Tunapaswa kuhakikisha AI inatumika kwa uwazi, kwa kuheshimu Haki za Binadamu, na kwa kuimarisha upatikanaji wa habari sahihi.

#FreedomOfExpression #WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍1
Sanaa katika aina zake zote (Uchoraji, Uandishi, Muziki, Filamu, au Ngoma) ni njia muhimu ya Watu kueleza mawazo yao na kuibua Mijadala ya Kijamii

Kupunguza Uhuru wa Sanaa ni sawa na kunyamazisha Sauti za Watu. Jamii huru huunga mkono Wasanii wake kwasababu Sanaa ina nguvu ya Kuhamasisha, Kuelimisha na kuleta Mabadiliko

#FreedomOfExpression #ArtIsFreedom #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #Democracy
👍1
#Demokrasia haiwezi kustawi bila Uhuru wa Mawazo. Kukataa kusikiliza maoni tofauti kunaua Maendeleo ya Kijamii na Kisiasa

Jamii yenye Afya ni ile inayoruhusu mijadala ya wazi, hata pale ambapo mawazo yanayotolewa ni magumu au yasiyopendwa na wengi

#FreedomOfSpeech #FreedomOfExpression #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #DemocracyNeedsFreedom
Sheria za kusimamia Matumizi ya Mitandao zinapaswa kuwepo ili kulinda Watu dhidi ya Unyanyasaji, Udanganyifu na Uhalifu wa Mtandaoni na si kama chombo cha kuminya Uhuru wa Kujieleza

Baadhi ya Serikali hutumia Sheria hizi kama silaha ya kunyamazisha Wakosoaji, Wanaharakati na Waandishi wa Habari kwa kisingizio cha "Usalama Mtandaoni"

#FreedomOfSpeech #SayNoToCensorship #FreedomOfExpression #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #DemocracyNeedsFreedom
Kama Haki nyinginezo, Uhuru wa Kujieleza na Kukusanyika unaweza kuwa na mipaka kwa madhumuni ya kulinda Usalama wa Umma, haki za Watu wengine au kuzuia Chuki na Ghasia

Hata hivyo, Serikali nyingi hutumia kisingizio cha "Usalama" kama njia ya kunyamazisha Wakosoaji na kuzima harakati za Mabadiliko

Mipaka ya Haki hizi inapaswa kuwa ya Haki na isitumike vibaya kwa maslahi ya wachache, kwasababu Uhuru wa kukusanyika kwa Amani ni njia muhimu ya kuwasilisha maoni na kudai Haki

#FreedomOfSpeech #SayNoToCensorship #FreedomOfExpression #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #DemocracyNeedsFreedom
1
Kueleza mawazo yako hadharani na kukusanyika kwa Amani si uhalifu, ni haki ya msingi ya kila Mtu, lakini katika Mataifa mengi, Watu wanaokosoa Serikali au Kuandamana kudai haki zao wanakamatwa, kunyanyaswa au hata kupotezwa

Kupaza sauti si uhalifu na Kukosoa Mamlaka si uhaini

#FreedomOfSpeech #SayNoToCensorship #FreedomOfExpression #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #DemocracyNeedsFreedom
Haki hizi hazitolewi kama fadhila za Serikali au Watawala, ni Haki za msingi za kila Mtu. Jamii inayodumisha Uhuru wa Kujieleza na Kukusanyika kwa Amani hujenga Mazingira ya Haki, Usawana Maendeleo

Haki hizi zinahakikisha Uwajibikaji wa Viongozi, huipa jamii nafasi ya kushiriki katika maamuzi yanayoathiri Maisha yao, pia zinaimarisha Utawala wa Kidemokrasia na kulinda Haki za Binadamu

#FreedomOfSpeech #SayNoToCensorship #FreedomOfExpression #SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #DemocracyNeedsFreedom
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Emmanuel Nchimbi, amezungumzia ripoti kadhaa na kueleza zimeonesha Uhuru wa Habari umeimarika Nchini

Amesema hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Wahariri, leo Aprili 4, 2025

Soma https://jamii.app/NchimbiAprili4

#PressFreedom #JamiiForums #Governance #FreedomOfExpression
#TANZIA: Sifa Bujuni aliyeimba wimbo wa “Tanzania Inaelekea Wapi?” yenye kionjo cha “Mnatuona Nyani tu” amefariki Dunia hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Baba Mzazi wa Marehemu amethibitisha taarifo za kifo chake

Ikumbukwe, Septemba 13, 2023, Sifa na wenzake Wawili walikamatwa huko Isyesye - Mbeya wakidaiwa kuandaa wimbo wenye maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuusambaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na mtandao wa kurusha maudhui wa YouTube

Septemba 19, 2023, Sifa na wenzake Salome Mwampeta (Mwimbaji) na Mtayarishaji wa Wimbo huo, Hezekiel Millyashi George walipandishwa Mahakamani na kusomewa Shtaka la Kusambaza Taarifa za Uongo kwa njia ya Mtandao ambapo wote walikana na baadaye kesi yao kufutwa

Soma https://jamii.app/SifaAfariki

#JamiiAfrica #JamiiForums #FreedomOfExpression #Demokrasia #UhuruWaKujieleza
👍1
Taasisi ya CIPESA (Collaboration on International ICT Policy for East and Southern Africa) kwa kushirikiana na wadau wengine, wamewasilisha kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, Safaricom na Airtel Kenya, kupinga vitendo vya kiholela na visivyo halali vya kuzuia huduma ya intaneti nchini humo

Kesi hiyo inajikita kwenye ushahidi wa kiteknolojia kutoka Mashirika ya Kimataifa kama Cloudflare, Open Observatory of Network Interference (OONI) na Internet Outage Detection and Analysis (IODA), ambayo yamedhihirisha kuwepo kwa vitendo vya makusudi vya kupunguza kasi ya intaneti na kufunga baadhi ya majukwaa kama vile Telegram

Zaidi https://jamii.app/KeepItOnKE

#DigitalRights #JamiiForums #JamiiAfrica #FreedomOfExpression #Governance #Accountability
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwanasiasa na Balozi Humphrey Polepole akizungumza kupitia ukurasa wake wa #Facebook amesema "Huu Mchakato wa kupata Wagombea (ndani ya Chama Cha Mapinduzi - #CCM) umekosewa, wakati mwingine inatakiwa kubomoa ili tujenge, nimeongea na mzee mmoja amekiri kuwa pale walichemka."

Soma https://jamii.app/PolepoleWagombea

#Democracy #JamiiForums #JamiiAfrica #FreedomOfExpression
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwanasiasa na Balozi Humphrey Polepole akizungumza kupitia ukurasa wake wa #Facebook amesema "Kwenye #CCM hakuna kuvuana nguo, wala wasisingizie kuwa tunakosoana kwenye vikao, sisi tusiokuwa na vikao tunakosoana hadharani."

Amesema hayo leo Julai 18, 2025 na kuongeza, "Hata walipokuwa wanafanya vibaya kwenye CCM, Mwalimu Julius Nyerere alitoka hadharani zaidi ya mara moja na kuwaambia waliokuwa wanakosea."

Soma https://jamii.app/WaojifanyaWanaCCM

#Democracy #JamiiForums #JamiiAfrica #FreedomOfExpression
1
IVORY COAST: Mahakama imemhukumu Tokpa Flan Japhet kifungo cha Miaka Mitatu jela na kumtoza faini ya Dola 8,500 (Tsh. Milioni 22.1) kwa kutoa maoni kwenye #Facebook akisema "Kama Mama wa Rais Alassane Ouattara angefanya 'utoaji mimba' angekuwa ameokoa Afrika." Kauli iliyotafsiriwa kama lugha ya kumdhihaki Rais.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka imesema adhabu hiyo ni sehemu ya juhudi za kudhibiti vitendo visivyofaa vinavyoongezeka kwenye Mitandao ya Kijamii.

Hukumu hiyo imetolewa miezi michache kabla ya uchaguzi wa Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, ambapo chama cha #RHDP kimemteua Rais Ouattara kuwania kwa mara ya nne.

Soma https://jamii.app/IvoryCoastRais

#JamiiAfrica #JamiiForums #FreedomOfExpression #UhuruWaKujieleza #Governance
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amesema Kiwango cha kupendwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiko chini kuliko wakati wowote katika Historia ya siasa za Tanzania huku akitolea mifano kuwa kuna Viongozi wanaofunga “comments” katika mitandao yao ya Kijamii kuhofia maoni ya Wananchi.

Ameyasema hayo leo Agosti 15, 2025 wakati anazungumza kwa njia ya Mtandao

Zaidi https://jamii.app/CCMKuchukiwaHistoria

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #FreedomOfExpression
1