RUVUMA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuliomba Jeshi la Polisi Wilayani Tunduru kutoa majibu juu ya Sheikh Abdulrazack Mohamed ambaye alidai kukamatwa na Watu wanaodhaniwa kuwa ni Askari Polisi, Machi 7, 2024 kisha kupelekwa kusikojulikana, Polisi imetoa ufafanuzi
Kamanda wa Polisi Mkoa, Marco Chillya amesema “Huyo mhusika alikuwa ana tuhuma za Ugaidi Arusha, baadaye akafanywa kuwa Mwangaliwa wa Polisi, akatakiwa awe anaripoti Kituo cha Polisi Tunduru alipokuwa anaishi.”
Ameongeza “Huu ni Mwaka wa Tatu amekuwa akipoti bila tatizo, Machi 7, 2024 alitakiwa kuripoti pia, hakufika, inadaiwa amepotea akiwa njiani anaenda kituoni. Polisi hawawezi kumkamata mtu ambaye mara zote aliitikia wito vizuri, tumefungua jalada kupeleleza kupotea kwake, inawezekana kuna mchezo unafanyika.”
Soma https://jamii.app/TundumaPolisi
#JFMatukio #JFUwajibikaji #CivilRights #JamiiForums

👍10😁1
Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa alitoa kauli hii Mwaka 2000 ikiwa ni hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa na kushika madaraka ya Kipindi chake cha Pili cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania
#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #AmkaNaJF #GoodMorning

👍6❤1
MSUMBIJI: Zaidi ya Watu 90 wameripotiwa kufariki katika ajali ya Kivuko kinachodaiwa kilikuwa na takriban Watu 130 katika eneo la jirani na jimbo la Nampula, huku Watu 5 wakiokolewa
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa eneo hilo, imeelezwa kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni Watoto na chanzo cha ajali ni uzito kuzidi kwenye Kivuko
Soma https://jamii.app/AjaliMSMBJ
#JamiiForums #JFMatukio #ServiceDelivery

👍2💔1
#JFMDAU: Mdau wa JamiiForums.com anasema Choo kilichopo ndani ya Kivuko cha MV KOME II kinachofanya safari Nyakarilo na Kome Kisiwani katika Halmashauri ya Buchosa, Wilayani Sengerema hakifai kwa matumizi ya Binadamu
Mbali na matobo yanayomuacha wazi aliyeko ndani lakini kinatoa harufu kali jambo ambalo ni kero kwa abiria
Ametoa Wito kwa Viongozi wa Serikali na #TEMESA kuchukua hatua haraka ili kumaliza kero hiyo na Udhalilishaji kwa abiria
Soma zaidi https://jamii.app/ChooMVKomell
#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery

👍2
#JFMDAU: Mdau wa JamiiForums.com anasema tabia ya Wamiliki wa Majengo, Nyumba na Fremu kupandisha Kodi kila baada ya muda mfupi inaweza kusababisha kuua #Biashara za wengi
Amesema ni vema kuweka Miongozo au Kanuni kuhusu masuala ya kupangisha; Miongozo iseme wazi ni wakati gani kodi inaweza kupanda na kwa kwa kiasi gani bila kumuumiza Mpangaji au Mpangishaji
Mjadala zaidi https://jamii.app/KodiKupandaOvyo
#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
Amesema ni vema kuweka Miongozo au Kanuni kuhusu masuala ya kupangisha; Miongozo iseme wazi ni wakati gani kodi inaweza kupanda na kwa kwa kiasi gani bila kumuumiza Mpangaji au Mpangishaji
Mjadala zaidi https://jamii.app/KodiKupandaOvyo
#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
👍1
Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wanasema kuna mtindo umezuka ambapo Wakopeshaji wa Mtandaoni wamekuwa wakisambaza taarifa binafsi za Wateja kwa Watu ambao huwa wanawasiliana nao kwa kuwaeleza kuwa wanamdai mhusika
Je, umeshawahi kukumbwa na Udhalilishaji wa aina hii baada ya kukopa Mtandaoni?
Mjadala zaidi https://jamii.app/KudhalilishwaMkopoOnline
#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #PersonalDataProtection #DataPrivacy #DataProtection

👍1😡1
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa taarifa kuwa Watu 17 wameokolewa katika tukio la kuzama kwa Meli ya MV Maman Benita iliyokuwa inatoka #Kigoma kuelekea Kalemie Nchini #DRCongo katika Ziwa Tanganyika ikiwa na Abiria 27, Aprili 6, 2024
Taarifa imeeleza kuwa baada ya kuzama Aprili 7, 2024, Wavuvi walimuokoa Abiria mmoja raia wa China na hadi Saa 1:00 Usiku wa Aprili 7, 2024, Watu 17 waliokolewa (Wachina 2, Watanzania 3 na Wakongo 12). Chanzo cha kuzama kwa meli hiyo bado hakijajulikana huku Nahodha akiwa ni kati ya waliookolewa
#TASAC imeeleza meli hiyo iliyozama eneo la Kabimba, DRC iliyosajiliwa chini ya Bendera ya DRC ilikuwa na Raia wa Tanzania (5), China (4), DRC (16), Kenya (1) na mtoto mdogo
Soma https://jamii.app/AjaliMVBenita
#JFMatukio #JamiiForums #JFUwajibikaji

👍6
Mdau wa JamiiForums.com ametoa kero yake juu ya Waajiri wa Sekta Binafsi wasiowasilisha Michango ya Wafanyakazi huku akidai Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (#NSSF) unasuasua kuchukua hatua dhidi ya Waajiri wa aina hiyo
Vipi Mdau, umewahi kupata usumbufu gani katika kufuatilia Mafao yako?
Soma https://jamii.app/NSSFMichango
#JamiiForums #SocialJustice #Accountabity #Governance

👍5
#MICHEZO: Kocha wa #Liverpool, #JurgenKlopp ametoa kauli hiyo baada ya matokeo ya magoli 2-2 ya timu yake dhidi ya #ManchesterUnited katika #PremierLeague, akielezea sababu za mchezo baina ya timu hizo huwa unakuwa mgumu kwake hata kama United haina kiwango kizuri kwa wakati huu
Rekodi za Liverpool ya Klopp dhidi ya Man United ikiwa chini ya Kocha Erik ten Hag zipo hivi:
FA Cup (Machi 17, 2024)
Man. United 4-3 Liverpool
EPL (Desemba 12, 2023)
Liverpool 0-0 Man. United
EPL (Machi 5, 2023)
Liverpool 7-0 Man. United
EPL (Agosti 22, 2022)
Man. United 2-1 Liverpool
Kirafiki (Julai 12, 2022)
Man. United 4-0 Liverpool
Soma https://jamii.app/ManULiver
#JFSports #JFNukuu #JamiiForums

❤3👍2
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema leo Aprili 8, 2024 dunia inatarajia kushuhudia tukio la Kupatwa kwa Jua Kikamilifu (Solar Eclipse) ambapo Mwezi utazuia kabisa Mwanga wa Jua, hata hivyo tukio hilo halitakuwa na athari zozote kwa upande wa Tanzania
TMA imesema nchi zitakazoshuhudia zaidi tukio hilo ni za Bara la Amerika Kaskazini kupitia #Mexico, Marekani na #Canada. Kwa upande wa Tanzania hali hiyo haitaonekana kwasababu iko eneo la mbali kutoka njia ya Kupatwa kwa Jua Kikamilifu
Vipi Mdau, unakumbuka nini katika Matukio ya Kupatwa kwa Jua na Mwezi?
Soma https://jamii.app/TMASolarEclipse
#JamiiForums #ClimateChange #JFMatukio #SolarEclipse

👍4