JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya 2021/22 inaonesha Mwaka 2021, #TASAC ilifanya ukaguzi wa Kivuko cha #MVPangani na kubaini kimekuwa kikifanya kazi bila cheti cha kuthibitisha Usalama Baharini, huku Mabaharia wake wakiwa hawana Elimu ya Ubaharia

Pia, Jenereta mbili zilizokuwemo kwenye kivuko hazikuwa zikizalisha Umeme wa kutosha kuendesha Injini za propela za Azimuth na Magati mawili ya kushukia na kuegesha Kivuko yanafanya kazi kwa kutegemea nguvu kazi za Mikono na sio Umeme

Hata hivyo, ukaguzi wa #CAG wa 2021/22 ulibaini Kivuko hicho bado kilikuwa kikiendelea kufanya kazi licha ya mapungufu yaliyobainishwa. Hivyo, #TEMESA haikuwa imechukua hatua yoyote kushughulikia udhaifu wa uendeshaji wa MV. Pangani ulioripotiwa na TASAC

Soma https://jamii.app/UsimamiziRasilimaliZaUmma

#JamiiForums #RipotiYaUwajibikaji #UwajibikajiTaasisiZaUmma #UsimamiziTaasisi #JFUwajibikaji23
👍71
Rais Samia amemteua Kaimu A. Mkeyenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo akichukua nafasi ya Dkt. Elirehema Doriye atakayepangiwa kazi nyingine

Kabla ya uteuzi Mkeyenge alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (#TASAC)

Zaidi soma https://jamii.app/UteuziNov

#JamiiForums #Governance #Accountability
👍61
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mohamed Malick Salum kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (#TASAC)

Salum anachukua nafasi ya Kaimu Abdi Mkeyenge aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)

Awali, Salum alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Uchukuzi.

Soma https://jamii.app/UteuziTASAC

#JamiiForums #Governance #Accountability
2👍1
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa taarifa kuwa Watu 17 wameokolewa katika tukio la kuzama kwa Meli ya MV Maman Benita iliyokuwa inatoka #Kigoma kuelekea Kalemie Nchini #DRCongo katika Ziwa Tanganyika ikiwa na Abiria 27, Aprili 6, 2024

Taarifa imeeleza kuwa baada ya kuzama Aprili 7, 2024, Wavuvi walimuokoa Abiria mmoja raia wa China na hadi Saa 1:00 Usiku wa Aprili 7, 2024, Watu 17 waliokolewa (Wachina 2, Watanzania 3 na Wakongo 12). Chanzo cha kuzama kwa meli hiyo bado hakijajulikana huku Nahodha akiwa ni kati ya waliookolewa

#TASAC imeeleza meli hiyo iliyozama eneo la Kabimba, DRC iliyosajiliwa chini ya Bendera ya DRC ilikuwa na Raia wa Tanzania (5), China (4), DRC (16), Kenya (1) na mtoto mdogo

Soma https://jamii.app/AjaliMVBenita

#JFMatukio #JamiiForums #JFUwajibikaji
👍6