JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#JFMDAU: Mdau wa JamiiForums.com anadai Vyoo vya Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya ni hatarishi kwa Watumiaji kutokana na kutozingatiwa kwa usafi

Je, Umewahi kukutana na changamoto ya mazingira machafu ya choo katika Hospitali au Kituo cha Afya?

Soma zaidi https://jamii.app/VyooHatarishiRufaa

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
👍3👎2
Unamshauri Mdau huyu atumie mbinu gani kukabiliana na Changamoto za kwenye Ndoa yake?

Mjadala zaidi https://jamii.app/AmaniNdoaMwezi1

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle #MarriageIssues #JFChitchats
3
Mshiriki wa Shindano la #StoriesOfChange2023 anasema ni kawaida kwa Watu kukosa huduma katika Ofisi za Umma kwasababu zitokanazo na Uzembe wa Watumishi

Amesema hatua kama za kupiga marufuku matumizi ya simu muda wa kazi, kulipa kwa saa na wale wanaofanya vizuri kuongezewa malipo zitapunguza uzembe na kukuza Uwajibikaji katika Ofisi za Umma

Unakubaliana na hoja za Mdau?

Mjadala zaidi https://jamii.app/UzembeOfisiZaUmma

#JamiiForums #SoC #StorieOfChange #CitizenJournalism #ImpactfulStories #Governance
👍4
#JFMDAU: Mdau wa JamiiForums.com anasema anashangaa Maji kutuama ndani ya Kituo cha Mabasi cha Magufuli pale Mvua inaponyesha

Anahoji iwapo Mkandarasi hakuona umuhimu na uhitaji wa kujenga njia za Maji hasa katika maeneo ambapo Mabasi yanapaki

Zaidi soma https://jamii.app/StendiKujaaMaji

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #Governance #Accountability
👍2
#BUNGENI: Naibu wa Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya ametoa kauli hiyo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Arumeru Magharibi, Noah Saputi aliyetaka kujua ni lini Serikali itazuia Magari ya Serikali kukutwa katika maeneo ya Starehe

Vipi Mdau, hali halisi ikoje Mtaani kuhusu muda wa matumizi ya Magari ya Serikali?

#JamiiForums #Governance #Accountability #JFQuote
👍81
Mdau wa Jukwaa la #Biashara, Uchumi na Ujasiriamali anasema Kama unaokoa kiasi fulani kutokana na kazi yako na unaingiza kipato cha ziada, utakuwa na dira nzuri ya kutokomeza madeni yanayokusumbua

Kama una maradhi ya kutosimamia pesa zako vizuri, basi weka Mtu unayemuamini kusimamia ulipaji wa madeni yako

Jifunze zaidi https://jamii.app/StressMadeni

#JamiiForums #Maisha #Uchumi
👍4
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Serikali imesema inatafuta Fedha zitakazotumika kuwafidia Wakazi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere katika eneo la Kipunguni Jijini Dar es Salaam, ambao madai yao yamehakikiwa

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema “Sasa, tunaendelea kutafuta fedha, ndani ya mwaka huu wa fedha unaoendelea ili kuweza kuanza kufanya malipo hayo.”

Aidha, ameongeza kuwa tathmini mpya ya ardhi na mali iliyofanyika kwa Wakazi 1,184 inaonesha Serikali italipa zaidi ya Tsh. Bilioni 144, ikiwa ni tofauti na tathmini ya Mwaka 2009 iliyoonesha malipo yalipaswa kuwa Tsh. Bilioni 15.5

Soma https://jamii.app/KipunguniKulipwa

#JamiiForums #Governance #SocialJustice #JFBungeni
👍21
SONGWE: Mdau wa JamiiForums.com anadai katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Ukiingia chumba cha Upasuaji hasa Idara ya Macho kunakuwa na kelele nyingi za kugombezwa na Wahudumu wa Afya hali ambayo inaweza kumpotezea mgonjwa utulivu

Je, Mdau, Umeshawahi kukutana na changamoto ya Kugombezwa na Wahudumu wa Afya katika Hospitali au Kituo cha Afya?

Soma https://jamii.app/SongweIdaraMacho

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #PublicHealth
👍3👏1