JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com anasema ni kweli Elimu ni kitu muhimu kwa Watoto lakini kuna wakati Walimu wanasahau kwamba Wanafunzi nao wanahitaji kupumzika

Anaeleza hata Likizo ya Wiki moja bado Wanafunzi wanalazimishwa kwenda 'Tuition' kila Siku na bado kila Jumamosi wanakwenda kufanya Mitihani kwa kulipishwa Hela

Je, Shule wanaposoma Watoto wako wanapata muda wa kutosha kupumzika?

Mjadala zaidi https://jamii.app/WanafunziKupumzika

#JamiiForums #ChildRights #HakiElimu #ServiceDelivery
πŸ‘4
UWAJIBIKAJI: Wakurugenzi Watatu na Maafisa Waandamizi Watatu kutoka Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (#AICC) wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma za Ukiukaji wa taratibu na kanuni za Uendeshaji wa Mashirika ya Umma

Wakurugenzi waliosimamishwa ni Savo Mung'ong'o (Mkurugenzi wa Fedha wa Utawala), Victor Kamagenge (Mkurugenzi wa Miliki na Miradi) na Mkunde Mushi (Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko)

Maafisa Waandamizi ni Festo Mramba (Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu na Utawala), Augustine Karadoga (Mhasibu Mkuu) na Catherine Kilinda (Meneja JNICC)

Soma https://jamii.app/TuhumaAICC

#JamiiForums #Accountability
GEITA: Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba amesema anashangazwa na kitendo cha ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Kasamwa kutokamilika tangu Mwaka 2019 huku ikiwa imetumia zaidi ya Tsh. Milioni 100

Komba amesema tangu ameripoti kazini amekuwa akipokea taarifa mbalimbali kupitia miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ambayo imekuwa haikamiliki kwa wakati na hivyo kulazimika kutoa maagizo mapya ya ukamilishaji wake ikiwemo Zahanati hiyo

Amesema β€œTangu niliporipoti sikufurahishwa kukuta Miradi ya CSR haijakamilika, Zahanati ya milioni 100 imeanza kujengwa 2019 haijakamilika hadi leo tuko Mwaka wa 2024. Tunapokuwa na miradi mingi isiyokamilika tunawafanya Wananchi hawa wasione kama kuna Faida."

Soma https://jamii.app/GeitaZahanati

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #JFAfya #Accountability
πŸ‘6
RUKWA: Miundombinu ya Barabara inayopita maeneo ya Kasansa, Muze, Mtowisa, Ilemba, Kaoze, Kilyamatundu yenye urefu wa Kilometa 180 imeathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha hali ambayo imewapa changamoto Wakazi wengi wa Wilayani Sumbawanga

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amefika maeneo yaliyoathiriwa na kusema Serikali itashughulikia matengenezo sehemu husika kwa kuanza na maeneo korofi ya Nkwilo, Mtowisa, Zimba, Kisa, Kinambo, Ilemba na Solola ambayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa

Soma https://jamii.app/BarabaraRukwa

#JFHuduma #JFUwajibikaji #CivilRights #JamiiForums
πŸ‘1
DAR: Jeshi la Polisi pamoja na Maafisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF kuanzia Desemba 2023 hadi Aprili 2024 wamewakamata Watu 30 kwa tuhuma za kughushi nyaraka mbalimbali kwa lengo la kujipatia malipo kwenye Mfuko huo

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne amesema Watuhumiwa walikuwa na nyaraka bandia zinazohusu kuacha Kazi, Vyeti vya Huduma, taarifa za uongo za Ugonjwa, Hati za Uongo za kufukuzwa Kazi pamoja na fomu za kugushi za kuomba Mafao ya NSSF

Soma https://jamii.app/30KukamatwaNSSF

#JamiiForums #Accountability #Governance #Uwajibikaji
πŸ‘3❀1
Je, Wananchi wanawawajibisha vya kutosha Viongozi wanaorudi Majimboni kipindi uchaguzi unapokaribia?

Zaidi soma https://jamii.app/SiasaUchaguzi

#JamiiForums #Uwajibikaji #KemeaRushwa #Governance #Accountability #UtawalaBora #JFToons
πŸ‘3
Siku chache baada ya kufungwa na Al Ahly ya Misri kisha kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika (Hatua ya Robo Fainali), Timu ya #Simba imeendelea kuwa na wiki mbaya baada ya kupata kichapo kutoka kwa #MashujaaFC cha penati 6-5 baada ya matokeo ya goli 1-1 katika dakika 90

Mchezo huo wa Raundi ya Nne wa CRDB Bank Federation Cup 2023/2024 umechezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Mkoani Kigoma

Soma https://jamii.app/MashujaaSimba

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘9πŸ”₯1
UEFA: ARSENAL 2-2 BAYERN, MADRID 3-3 MAN. CITY

Michezo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepigwa ambapo Arsenal na Bayern Munich mechi imemalizika kwa sare ya magoli 2-2 kwenye Uwanja wa Emirate

Real Madrid ikiwa nyumbani imelazimishwa sare ya magoli 3-3 dhidi ya Manchester City ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabeu

Timu hizo zote zinatarajiwa kurudiana Aprili 17, 2024

Robo Fainali nyingine zinatarajia kupigwa leo Aprili 10, 2024, Atletico Madrid dhidi ya Borrusia Dortmund na Barcelona dhidi ya Paris Saint-Germain

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘12
JamiiForums inakutakia Sikukuu njema ya Eid yenye Furaha, Upendo na Amani kwako na wale uwapendao

#EidMubarak #JamiiForums #GoodMorning #AmkaNaJF
πŸ‘3
Unyanyasaji Mtandaoni unaweza kusababisha madhara makubwa ya Kisaikolojia kwa Waathirika, ikiwa ni pamoja na wasiwasi, sonona na hata Mawazo ya kujiua.

Shiriki Mjadala zaidi https://jamii.app/KusambazaConnection

#JamiiForums #DigitalRights #Cyberbullying #MentalHealthMatters
πŸ‘4
AFYA: Kuzingatia dozi ya dawa kunahusisha matumizi ya dawa kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Daktari au Maelekezo Yaliyomo kwenye Kibandiko cha Dawa (Label)

Wataalamu wa Afya wanashauri kuzingatia dozi ya dawa kwa usahihi, ili kuhakikisha matibabu yanakuwa na ufanisi na kuzuia madhara yanayoweza kutokea kama Usugu wa dawa au Ugonjwa kuongezeka

Soma https://jamii.app/KuzingatiaDozi

#JamiiForums #AfyaBora2024 #PublicHealth #Maisha #MatumiziYaDawa
πŸ’―5πŸ‘2❀1