JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mchezo wa #Yanga dhidi ya #Simba wa Raundi ya Pili ya Ligi Kuu Bara 2024/25 ambao uliahirishwa, sasa umepangwa kuchezwa Jumapili Juni 15, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa

Ikumbukwe, Yanga imetangaza kuwa haitashiriki mchezo huo na tayari iliwasilisha malalamiko yao kwa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), lakini shauri lao likakwama, wakatakiwa kurejea katika Mamlaka za Nchini, jambo ambalo wamesema hawawezi na hawatacheza Mchezo huo

Mdau, unadhani Yanga watashikilia msimamo wao au ‘mbungi’ itapigwa?

Soma https://jamii.app/DerbyJune15

#JFSports #JamiiForums #KariakooDerby
🤣2
DAR: Timu ya #Simba imeendeleza mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kasi, hiyo ni baada ya kuichapa #PambaJiji Magoli 5-1 kwenye Uwanja wa KMC Complex

Kiungo mshambuliaji Jean Ahoua amefunga magoli matatu (hat trick dakika ya 15, 36 na 48) huku mawili yakifungwa na Leonel Ateba (80 na 84), goli la Pamba Jiji limewekwa wavuni na Mathew Tegisi dakika ya 85

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 66 katika michezo 25 ikiwa nyuma ya #Yanga yenye pointi 70 katika michezo 26 wakati Pamba Jiji ipo nafasi ya 13 kwa kuwa na pointi 27 katika mechi 27

Soma https://jamii.app/SimbaPamba

#JamiiForums #JFLigiKuu25 #JFSports
👍1
DAR: Magoli yaliyofungwa na Steven Mukwala yameiwezesha Timu ya #Simba kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya #KMCFC ambayo imepata goli kupitia kwa Rashid Chambo katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa KMC

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 69 ikiwa nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi nyuma ya Yanga yenye pointi 70, timu zote hizo mbili zikiwa zimecheza michezo 26

Upande wa KMC imesalia katika nafasi ya 11 ikiwa na alama 30 katika michezo 27

Soma https://jamii.app/KMCSimbaDar

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
👍1
CAF: Mchezo wa Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) umekamilika kwa #Simba ya Tanzania kupoteza magoli 2-0 ikiwa ugenini dhidi ya #RSBerkane ya Morocco

Wachezaji waliosababisha kilio kwa Simba ni Mamasou Camara dakika ya 8 na Oussama Lamlaoui dakika ya 14

Kutokana na matokeo hayo sasa kila kitu kinaelekezwa katika mchezo wa pili ambao bado kuna utata kama utacheza kwenye Uwanja wa Mkapa (Dar es Salaam) au New Amaan Complex (Zanzibar)

Je, unadhani Simba inaweza kupindua matokeo au ndio imeisha hiyo?

Soma https://jamii.app/BerkaneSimba

#JamiiForums #CAFCC #JFCAF25
🔥1
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesema kuwa Ripoti ya Mkaguzi imeonesha maboresho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa hayawezi kukamilika kwa wakati kwa ajili ya kuandaa Mchezo wa Marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho uliopangwa kufanyika Mei 25, 2025

Taarifa ya CAF imeeleza kuwa (Kama ilivyotangaza awali) mchezo huo wa #Simba dhidi ya #RSBerkane unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Taarifa hiyo imeeleza kuwa #CAF itaendelea kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Serikali ya Tanzania na Wadau wote kuhakikisha Uwanja wa Mkapa na viwanja vyote vinakuwa tayari kwa Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) na kukidhi Kanuni na Viwango vya CAF yanayotarajiwa kuanza Agosti 2, 2025

Soma https://jamii.app/CAFMkapaStadium

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
👍21
ZANZIBAR: Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) inaendelea kwenye Uwanja wa Amaan Complex. Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika, #Simba inaongoza kwa Goli 1-0 dhidi ya #RSBerkane

Goli limefungwa na Joseph Mutale dakika ya 17

Soma https://jamii.app/SimbaRSBerkane

#JFSports #JamiiForums #JFCAFCC
ZANZIBAR: Licha ya Timu ya #Simba kupata sare ya Goli 1-1 katika Fainali ya Pili ya CAF kwenye Uwanja wa Amaan Complex, hiyo haikuwa na faida kwao baada ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwenda kwa #RSBerkane ya Morocco

Simba ambayo imecheza pungufu muda mwingi wa kipindi cha pili baada ya Yusuph Kagoma kupata Kadi Nyekundu dakika ya 50 ilipata goli lake kupitia kwa Joshua Mutale dakika ya 17 huku wageni wakifunga kupitia kwa Soumaila Sidibe dakika ya 90+3

Hivyo, Simba imeukosa Ubingwa kwa kuwa mchezo wa kwanza RS Berkane ilishinda kwa magoli 2-0, hivyo matokeo ya jumla kuwa 3-1

Soma https://jamii.app/SimbaBerkane

#JFSports #JamiiForums #JFCAFCC
1
DAR: Goli pekee la Steven Mukwala katika dakika ya 42 limeipa Simba ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Singida Black Stars kwenye Uwanja wa KMC Complex

Ushindi huo unaifanya #Simba kufikisha alama 72 ikiwa nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya #Yanga yenye pointi 73, timu zote zikiwa zimecheza Michezo 27

Singida imebaki katika nafasi ya nne ikiwa na alama 53 katika Michezo 28

Soma https://jamii.app/SimbaSingidaMei28

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
👍2
Mwamuzi wa kati, Hery Sasii aliyecheza mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya #Simba dhidi ya Singida Black Stars SC, amefungiwa Miezi 6 kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo ambapo Simba ilishinda Goli 1-0 (lililofungwa na Steven Mukwala) baada ya kufanya maamuzi mengi yaliyoashiria kushindwa kutafsiri vema Sheria 17 za Soka

Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu imeeleza kuwa adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi

Aidha, Kocha wa Simba, Fadlu Davis ametozwa faini ya Tsh. Milioni 2 kwa kosa la kuishutumu Bodi ya Ligi Kuu wakati akihojiwa na Azam TV, kuwa ina ajenda tofauti kuhusiana na ratiba ya michezo ya klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC

Soma https://jamii.app/RefaKufungiwa

#JFSports #JamiiForums
2
DAR: Wakati Uongozi wa #Yanga ukitarajiwa kufanya kikao na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, leo Juni 9, 2025 kuhusu ajenda ya mchezo dhidi ya #Simba uliopangwa kuchezwa Juni 15, 2025, Klabu hiyo imesema matakwa yao yakisililizwa na kutekelezwa, timu itaingia uwanjani

Akijibu swali kupitia Wasafi FM, Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema “Yanga ni Klabu ya Mpira wa Miguu, kazi kubwa ni kucheza Mpira wa Miguu, matakwa ya Kamati ya Utendaji ya Yanga yaliyowasilishwa kwa Bodi ya Ligi yakisikilizwa na yakafanyiwa kazi bila shaka yoyote mbungi itapigwa.”

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Machi 8, 2025 lakini uliahirishwa baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa siku moja kabla, Yanga ilipeleka timu uwanjani na kueleza haipo tayari kucheza mchezo huo Namba 184 wakati mwingine kwa madai maamuzi ya kutochezwa yalikuwa kinyume na utaratibu wa Kanuni za Ligi

Soma https://jamii.app/KamweYanga

#JFSports #JFLigiKuu25 #JamiiForums #KariakooDerby
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Almas Kasongo amesema kikao chao na #Yanga kilichofanyika leo Juni 9, 2025 kilikuwa cha kupokea matakwa ya Klabu hiyo lakini sio cha kubadili maamuzi ya Mchezo wa Timu hiyo dhidi ya #Simba wa Juni 15, 2025

Sehemu ya matakwa ya Yanga yaliyotajwa ni kuwataka Watendaji kadhaa wa Bodi ikiwemo Mwenyekiti, Afisa Mtendaji kuachia ngazi na kuona Bodi hiyo inakuwa Chombo huru

Baada ya kikao hicho, Yanga imetoa tamko kuwa haitashiriki Mchezo huo Namba 184 mpaka pale matakwa yao waliyoyawasilisha kwa Maandishi yatakapotimizwa, hivyo wanaitakia kila la heri Bodi ya Ligi na Shirikisho la Soka Tanzania katika kushughulikia Matakwa hayo

Soma https://jamii.app/KariakooDerbyUpdates

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
DAR: Klabu ya #Simba imesema Serikali imeruhusu watumie Uwanja wa Mkapa kufanya mazoezi Juni 14, 2025 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya #Yanga unaoratajiwa kuchezwa Juni 15, 2025

Barua hiyo imeeleza kuwa uwanja upo tayari kwa mchezo na wameruhusiwa kwa mujibu wa Kanuni kwa kuwa Simba itakuwa ugenini katika mchezo huo ambao Yanga imekuwa ikisisitiza haitaingiza timu uwanjani

Barua imeandikwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Boniface Tamba kwenda kwa Simba na nakala kwa Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu

Soma https://jamii.app/SimbaMazoezi

#JFSports #JamiiForums
2
BAADA YA SAMIA KUKUTANA NA VIPNGOZI WA YANGA, SIMBA; VIONGOZI TPLB WAJIUZULU

Baada ya mgogoro wa muda mrefu kuhusu Yanga na Simba kucheza mchezo wa Ligi Kuu, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Steven Mnguto amewasilisha barua ya kujiuzulu huku Rais wa #TFF, Wallace Karia akimsimamisha Kazi Afisa Mtendaji Mkuu wa #TPLB, Almasi Kasongo

Haya yametokea ikiwa ni saa chache baada ya Rais Samia kufanya mazungumzo na Viongozi wa Klabu za #Simba na #Yanga na kisha taarifa kutoka kuwa mchezo huo uliokuwa uchezwe Juni 15, 2025 umeahirishwa hadi Juni 25, 2025

Soma https://jamii.app/TPLB_Wajiuzulu

#JamiiAfrica #JFSports
1
Mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa 2024/25 zinaendelea kushika kasi, #Yanga imeendelea kubaki katika nafasi ya kwanza kwa kufikisha Pointi 76 baada ya kuiunga Tanzania Prisons Magoli 5-0, #Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 75 baada ya kuichapa KenGold Magoli 5-0 pia

Yanga imeshinda ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya wakati Simba nayo ilikuwa ugenini kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora

Timu hizo mbili zimesaliwa na michezo miwili kukamilisha Ligi, ukiwemo unaozikutanisha zenyewe mnamo Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, ambapo ni mchezo unaotarajiwa na wengi kuwa utaamua bingwa wa Ligi

Soma https://jamii.app/MbioZaUbingwa

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
1
MICHEZO: Timu ya #Yanga imeshinda Magoli 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC na hivyo kuendelea kubaki kileleni katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha Pointi 79, nafasi ya pili inashikwa na #Simba ambayo imefikisha alama 78 baada ya kuifunga Kagera Sugar Goli 1-0

Kutokana na matokeo hayo bingwa wa ligi hiyo msimu huu anatarajiwa kujulikana wiki ijayo Jumatano Juni 25, 2025 ambapo Yanga itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa mwisho kabisa wa Ligi Kuu Msimu wa 2024/25

Soma https://jamii.app/LigiKuuMatokeo

#JFSports #JFLigiKuu25 #JamiiForums
DAR: Siku moja kabla ya mchezo dhidi ya #Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Uongozi wa #Simba haujatuma wawakilishi katika Mkutano uliohusisha Wanahabari ambao ni maalum kwa ajili ya kuzungumzia mtanange huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano Juni 25, 2025

Taratibu za Ligi hiyo ni kuwa siku moja kabla ya mchezo, timu husika zinatakiwa kutuma Kocha na Mchezaji kuzungumza na Wanahabari kuhusu mchezo unaofuata ambapo ni ratiba pia inayofuatwa na Azam TV ambao wanahusika kurusha matangazo ya Ligi

Soma https://jamii.app/SimbaMkutanoni

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
🤣4
DAR: Timu ya #Yanga imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 kwa kuifunga #Simba Magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Mkapa ikiwa ni ushindi wa Tano mfululizo dhidi ya Wapinzani hao wa Jadi

Ushindi huo uliotokana na Magoli ya Pacome Zouzoua na Clement Mzize unaifanya Yanga kumaliza Ligi kwa kuwa na Pointi 82 huku Simba ikibaki na alama 78

Michezo mingine iliyopita ya timu hizo Simba 0-1 Yanga (Oktoba 19, 2024), Yanga 1-0 Simba (Agosti 8, 2024), Yanga 2-1 Simba (Aprili 20, 2025) na Simba 1-5 (Novemba 5, 2023)

Soma https://jamii.app/YangaBingwa25

#JFSports #KariakooDerby #JamiiForums #JFLigiKuu25
ZANZIBAR: Timu ya Yanga imethibitisha kuwa Msimu wa Mwaka 2024/25 ni ‘mali yao’, baada ya kutwaa Fainali ya CRDB Bank Federation Cup 2024/2025 kwa kuifunga Singida Black Stars Magoli 2-0 katika Fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan

Wafungaji waliopeleka furaha kwa #Yanga katika mchezo wa leo Juni 29, 2025 ni Duke Abuya dakika ya 40 na Clement Mzize dakika ya 50

Ikumbukwe, Yanga ilianza msimu huu kwa kubeba Ngao ya Jamii, ikashinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya nne mfululizo, na kwa kunogesha zaidi ubingwa huo ilishinda michezo yote miwili dhidi ya #Simba ambao ni Wapinzani wao wa Jadi, pia ilitwaa Kombe la Muungano

Soma https://jamii.app/FainaliZanzibar

#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica
2
Kiungo wa #YoungAfricans (Yanga), Peodoh Pacome Zouzoua ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Juni katika Ligi Kuu Bara 2024/2025, akiwashinda Clatous Chama wa #Yanga na Kibu Denis wa #Simba baada ya kuisaidia timu yake kushinda mechi tatu alizocheza Juni.

Kwa upande wa Kocha Bora, Miloud Hamdi wa Yanga amenyakua tuzo hiyo kwa kuiongoza timu yake kushinda mechi tatu akiwashinda kocha Rashid Taoussi wa Azam FC na Fred Felix wa Pamba Jiji.

Aidha, Meneja wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Jackson Mwendwa, ametangazwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi huo

Shiriki Mjadala https://jamii.app/PacomeTuzoJune

#JamiiForums #JFMatukio #JFSports
1👍1
MICHEZO: Mtibwa Sugar Sports Club yenye makazi yake Mkoani Morogoro, Wilaya ya Mvomero, ilianzishwa na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa. Madhumuni ya awali yalikuwa kushiriki Ligi katika Ngazi ya Wilaya na kutoa burudani kwa Wafanyakazi, baadaye iliendelea na kushiriki Ligi Daraja la Nne (4th Division League).

Mtibwa Sugar ni moja ya timu yenye historia kubwa katika soka la #Tanzania, iliwahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mbele ya vigogo wa ligi #Simba na #Yanga mara mbili mfululizo.

Tukumbuke #MtibwaSugar ilipobeba taji la Bara na Mdau una kumbukumbu ipi kuhusu wakati huo?

Soma Zaidi https://jamii.app/MtibwaSugar

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports #JFKumbukizi