JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Rais Abdel Fattah El-Sisi ametoa wito huo huku akieleza kuwa inatakiwa wastani wa Watu uwe 400,000 kwa Mwaka badala ya Watu Milioni 2.2 kama ilivyokuwa katika takwimu za Mwaka 2022 ambapo Taifa hilo lina Watu zaidi ya Milioni 112

Rais El-Sisi anaonya kuwa ongezeko la Watu linaweza kusababisha mzigo kwa Serikali na kushindwa kumudu maboresho ya Uchumi wa Nchi na wa Wananchi miaka ijayo

Awali, Waziri wa Afya wa Misri, Khaled Abdel Ghaffar alisema suala la mzazi kuwa na idadi kadhaa ya Watoto ni hiyari na uhuru wa mtu binafsi

Soma https://jamii.app/EgyptPopulation

#LifeStyle #SocialJustice #Governance #JamiiForums
πŸ‘6
#JamiiForums kupitia Jukwaa la #JamiiCheck imethibitisha kuwa si kila Mgonjwa wa Kifua Kikuu huwa na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Aidha, ikiwa mtu aliye na VVU atatumia vizuri dawa za kufubaza virusi anaweza asipate kabisa Ugonjwa wa Kifua Kikuu
-
Wagonjwa wanaoishi na VVU wanashauriwa kutumia dozi zao vizuri ili kuepusha maambukizi ya Kifua Kikuu ambacho huongeza athari za ukubwa wa tatizo pamoja na kufupisha Maisha
-
Soma https://jamii.app/KifuaKikuu

#FactsChecking #FactsCheck
πŸ‘5
UPDATE: Baada ya hukumu ya takriban saa 10, Majaji wa Mahakama ya Rufani Nchini #Nigeria, wameamua kuwa madai ya Wapinzani kuwa Uchaguzi ulitawaliwa na Udanganyifu hayakuwa na mashiko, hivyo kubariki Urais wa #BolaTinubu aliyeapishwa Mei 29, 2023

Uchaguzi huo unatajwa kuwa wenye ushindani mkali zaidi tangu kumalizika kwa Utawala wa Kijeshi Mwaka 1999, ambapo Tinubu alishinda kwa 37% ya kura zilizopigwa, dhidi ya 29% za Atiku Abubakar na 25% za Peter Obi

Soma https://jamii.app/PingamiziLatupiliwaMbali

#JamiiForums #NigeriaElections #Democracy #SocialJustice
πŸ‘2πŸ₯±2
AFRIKA KUSINI: Hendrietta Bogopane-Zulu ambaye ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, ametaka Wanawake wanaokunywa Pombe wakati wa Ujauzito washtakiwe kwa Unyanyasaji Watoto kutokana na Madhara wanayowasababishia Watoto kwenye Ubongo

Akizungumza katika Kongamano la Kukuza Uelewa Kuhusu Athari za Pombe kwa Watoto, amesema Shirika la Afya Duniani (#WHO) limeitaja Afrika Kusini kuwa na kiwango cha juu zaidi cha Walevi Duniani

Kwa mujibu wa takwimu, Matumizi ya Pombe Nchini humo yameripotiwa kufikia 41.5% kwa Wanaume na 17.1% kwa Wanawake. Wakazi wa Mijini ni 33.4% na wa Vijijini 18.3%

Soma https://jamii.app/FASDSA

#JamiiForums #Governance #Accountability #ChildRights #PublicHealth
πŸ‘8❀1😁1
Je, umewahi kukumbana na Changamoto wakati wa kupata Kitambulisho cha Taifa? Jiunge nasi katika Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini Leo, Septemba 7, 2023, kupitia 'X Spaces' ya #JamiiForums kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 2:00 usiku

Tutaangazia Mchakato wa Utoaji na Upatikanaji wa Vitambulisho ikiwemo Mafanikio, Changamoto wanazopata Wananchi na Mwitikio wa Mamlaka

Karibu kutoa maoni yako, Mamlaka( NIDA na TAKUKURU) zitakuwepo kusikiliza maoni yako

'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
πŸ‘3
Jeshi la Polisi linamshikilia #EstherLungu ambaye ni mke wa Rais wa zamani wa #Zambia, #EdgarLungu akituhumiwa makosa matatu likiwemo la wizi wa gari ambalo amekana kuhusika

Esther ambaye yuko kizuizini, amekamatwa pamoja na Watu wengine watatu kwa tuhuma hizo, pia Mawaziri kadhaa wa zamani, Maafisa wa Serikali na Wanafamilia wa Lungu wanachunguzwa kwa tuhuma za uhalifu licha ya wote kukana tuhuma hizo

Soma https://jamii.app/LunguZambia

#Governance #Accountability #JamiiForums
πŸ‘6❀2😁2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema wito huo kwa Msanii wa Bongo Fleva, #NayWaMitego ulihusu mazungumzo kuhusu wimbo wake wa #Amkeni lakini hakutokea na hiyo ndio sababu ya kuzuia vibali vya kufanya shoo Mkoani #Njombe

Mwanasheria wa #BASATA, Christopher Kamugisha amesema β€œTumempa wito kwa mara ya tatu afike Ijumaa hii (Septemba 8, 2023), tunasubiri kuona kama atafika au la.”

Awali, Mwanasheria wa Nay, Wakili Jebra Kambole akiongea na JamiiForums alisema β€œBASATA wamempa wito wa maandishi Nay afike ofisini kwao Ijumaa hii kwa sharti kuwa anatakiwa kwenda peke yake bila Mwanasheria, bado tunatafakari sharti hilo na kwa nini iwe hivyo.”

Soma https://jamii.app/NayNaBASATA

#Entertainment #Democracy #FreedomOfSpeech #FreedomOfExpression #JamiiForums
πŸ‘5😁2πŸ‘Ž1
Mdau wa JamiiForums.com anasema tukikubali kuwa Watoto hawawezi kufanya maamuzi ya Ujira, kuendesha Vyombo vya Moto au kushiriki katika Uchaguzi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutosha, tunapaswa pia kutekeleza Kanuni hii katika suala la Ndoa kwa Watoto

Amesema Ndoa ni suala linaloweza kuwa na athari za kudumu kwa Watoto, Jamii itathmini Desturi zinazowalazimu Watoto kuolewa katika Umri Mdogo ili kuwalinda kwa kufahamu na kutambua kuwa Wanastahili kulindwa, kuwezeshwa kukua, kupatiwa #Elimu na kushiriki katika maamuzi yanayohusu mustakabali wao

Soma https://jamii.app/JukumuLaNdoa

#JamiiForums #SocialJustice #EarlyMarriages #NdoaZaUtotoni #JFWomen #HakiMtoto #WomenRights #ChildProtection
πŸ‘9
Je, umewahi kukumbana na Changamoto wakati wa Kupata Kitambulisho cha Taifa? Jiunge nasi katika Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini Leo, Septemba 7, 2023, kupitia 'X Spaces' ya #JamiiForums kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 2:00 usiku

Tutaangazia Mchakato wa Utoaji na Upatikanaji wa Vitambulisho ikiwemo Mafanikio, Changamoto wanazopata Wananchi na Mwitikio wa Mamlaka

Karibu kutoa maoni yako, Mamlaka( NIDA na TAKUKURU) zitakuwepo kusikiliza maoni yako

'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Waziri Mkuu, #KassimMajaliwa amemuagiza Waziri wa Nishati ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko kukaa na Wadau wa Mafuta na kuja na majibu ndani ya siku 7 kuhusu upatikanaji wa Mafuta Nchini

Waziri Mkuu alikuwa akijibu Swali la Mbunge wa Lushoto (CCM), Rashid Shangazi aliyetaka kujua Serikali inaweka mkakati gani ili upatikanaji wa Mafuta uwe wa uhakika Nchini, ambapo amekiri uwepo wa changamoto ya Mafuta Nchini na kueleza kuna jitihada zinazochukuliwa na Serikali

Ikumbukwe ni siku moja imepita tangu Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (#EWURA) kutangaza Bei mpya za Mafuta ambazo zimeanza kutumika zikiwa na ongezeko la Bei kulinganisha na mwezi Agosti 2023

Soma https://jamii.app/PMOrdrersDPM

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #FuelCrisis #JFUwajibikaji23
😁5πŸ‘3πŸ‘1
Tamko hilo la EWURA linalofafanua kuhusu taarifa yao ya Septemba 4, 2023 linakuja muda mfupi tangu Waziri Mkuu akiri Bungeni kuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa Nishati hiyo katika baadhi ya maeneo Nchini

Kupitia taarifa yake kwa Umma, #EWURA imefafanua inaposema akiba ya Mafuta iliyopo inatosha kwa siku 19 maana yake inakidhi mahitaji ya Kisheria yanayotaka Maghala ya Hifadhi kuwa na Mafuta yanayotosha kwa siku 15

Aidha, EWURA umeongeza kuwa inaposema mafuta yanatosha kwa Siku 19 haina maana baada ya siku hizo kutakuwa hakuna Mafuta Nchini

Soma https://jamii.app/EWURAStock

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #FuelCrisis #JFUwajibikaji23
😁4πŸ‘3❀2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathmini kuhusu mfumo mpya wa uagizaji Mafuta Nchini ili kuondoa ongezeko la changamoto ya upatikanaji wake

Spika amesema "Haiwezekani Mafuta yanapatikana kwa wiki mbili na baada ya hapo yanakuwa hayapatikani, kisha Bei mpya zikitangazwa baada ya muda yanaanza kupatikana tena".

Ameongeza kuwa kama mfumo huo unaleta changamoto ni vema kurejea kwenye mfumo wa zamani kwa kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto

Soma https://jamii.app/SpikaMafuta

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #FuelCrisis #JFUwajibikaji23
πŸ‘8😁1
RWANDA: Mwanamume mmoja (34) amekamatwa nchini humo baada ya kupatikana kwa zaidi ya miili 10 ya watu iliyozikwa kwenye shimo Jikoni katika nyumba aliyopanga Mjini #Kigali

Mshukiwa anadaiwa kuwadadisi, kisha kuwarubuni na kuwapeleka waathiriwa hao nyumbani kwake, ambako alikuwa akiwaibia simu na mali zao kisha kuwanyonga hadi kuwaua na kuwazika kwenye shimo hilo huku baadhi yao akiwayeyusha kwa kutumia tindikali

Soma https://jamii.app/RwandaSerialKiller

#JamiiForums #RwandaSerialKiller #SocialJustice #Crimes
πŸ€”5πŸ‘4πŸ‘1🀨1
JE, UMEWAHI KUKUMBANA NA CHANGAMOTO WAKATI WA KUPATA KITAMBULISHO CHA TAIFA?

Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini unaendelea kupitia 'X Spaces' ya #JamiiForums kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi saa 2:00 Usiku

Shiriki kutoa maoni, Mamlaka (#NIDA na #TAKUKURU) zipo kusikiliza maoni yako

'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
πŸ‘1
NIDA: NAMBA YA NIDA NI MUHIMU KULIKO KADI YA KITAMBULISHO

Akizungumza kupitia Mjadala wa Changamoto za upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa NIDA, Godfrey Tengeneza, amesema Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imeanza kutoka katika matumizi ya β€˜Card Reader’, na inazungumza na Taasisi nyingine ili kuwa na umoja wa kupata taarifa za wateja

Amesema tayari wamefanya mazungumza na Taasisi za Serikali ambapo wanatumia kanzidata ya NIDA kuweza kuwahudumia wateja wao ili Mwananchi anapokwenda kupata Huduma katika Taasisi husika aende na namba tu

Amesema "Kitu muhimu ni namba ya Utambulisho, kwenye Mataifa mengine wamefikia hatua ya kuwa hakuna haja ya kuwa na kitambulisho kwa maana lile β€˜gamba’, namba pekee inatosha kumpatia Mtu Huduma na kumtambulisho"

#JamiiForums #NationalIDTZ #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
πŸ‘1
NIDA: KUPATA NAMBA YA NIDA NI SIKU 7 HADI 14, KADI NI WIKI 3 HADI MWEZI BAADA YA KUJISAJILI

Afisa Habari wa NIDA, Geofrey Tengeneza amesema kama hakuna matukio au mambo yanayosababisha msongamano, na taarifa za mhusika zikiwa hazina shida, kupata Namba ya NIDA ni ndani ya siku 7 hadi 14 tokea kujisajili, japokuwa kukiwa na changamoto inaweza kuwa zaidi ya hapo

Upande wa kupata kadi ya NIDA, amesema baada ya kupitia mchakato wote ikiwemo kushirikisha Taasisi nyingine wanazofanyanazo kazi, na Kukiwa hakuna matukio yenye msongamano pia, kupata kadi ni ndani ya wiki tatu hadi mwezi mmoja, lakini kukiwa na changamoto inaweza kuwa zaidi ya hapo

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
πŸ‘3πŸ’©2
NIDA: WOTE WENYE NAMBA ZA NIDA WATAPATA KADI KUFIKIA JANUARI 2024

Afisa Habari wa NIDA, Geofrey Tengeneza amesema Watanzania wote wenye Namba za #NIDA hadi kufikia Januari 2024 kila Mwananchi mwenye namba husika atakuwa amepata Kitambulisho chake cha Taifa

Aidha, amesema hadi kufikia sasa, tayari watu Milioni 24 wamesajiliwa, Namba za Utambulisho zilizotolewa ni Milioni 20 na Vitambulisho ambavyo vimechapishwa ni zaidi ya Milioni 17

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
πŸ‘1