JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KITAMBULISHO NI BURE, GHARAMA ZA KUBADILI AU KUREKEBISHA TAARIFA ZA NIDA NI TSH. 20,000

Afisa Habari wa NIDA, Geofrey Tengeneza, amesema Moja ya mchakato wa kubadili jina lililopo kwenye NIDA ni kutakiwa kufanya mchakato wa kukana majina ya awali, kisha unatoa tangazo katika Gazeti la Serikali

Pia, kuna gharama ya kubadilisha au kurekebisha taarifa za NIDA kwa Tsh. 20,000 inayolipwa kupitia ‘Control Number’

Amesema hakuna rushwa wala fedha ambayo Mwananchi anatakiwa kutoa ili apate kitambulisho anapofanya mchakato kwa mara ya kwanza, ikitokea kuna mtu anaombwa rushwa ili afanikishe kupata Namba ya NIDA anatakiwa kutoa taarifa kwenye Mamlaka na Vyombo husika, hatua zitachukuliwa

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
👍51👎1
NIDA: UTARATIBU WA KUTOA NAKALA YA KITAMBULISHO UMESITISHWA

Afisa Habari wa NIDA, Geofrey Tengeneza amesema "Ni kweli kulikuwa na utaratibu wa kutoa Nakala ya Kitambulisho kwa wale ambao hawajapata Kadi lakini tulisitisha kutokana na matumizi mabaya ya mfumo huo"

Ameongeza "Tuna taarifa pia kuna watu wanawatapeli Wananchi kwa kuwaambia wanachapisha Nakala ya Kitambulisho, tunawaonya na tutawachukulia hatua kali"

#JamiiForums #NationalIDTZ #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
👍3
KENYA: Katibu Mtendaji wa Umoja wa Kitaifa wa Walimu (KNUT) katika Tawi la Nandi, Boniface Tenai ametoa wito kwa Serikali kutenga Rasilimali za kutosha kukabiliana na Ugonjwa wa Saratani ambao umeshambulia idadi kubwa ya Watu nchini humo

Umoja huo umesema Ugonjwa wa Saratani umekuwa mzigo kwa Wananchi kutokana na gharama kubwa za Matibabu na kwamba familia nyingi zimekuwa Maskini baada ya kutumia mali zao zote kuhudumia Wagonjwa wao

Kila mwaka nchi hiyo inakadiriwa kuwa na visa vipya 39,000 vya Saratani na zaidi ya vifo 27,000 vitokanavyo na Ugonjwa huo, huku
Saratani zinazoongoza zikiwa ni za Matiti, Shingo ya Kizazi, Tezi Dume na Koo

Soma https://jamii.app/SarataniKenya

#JamiiForums #Cancer #CancerAwareness #CancerInKenya #Afya #PublicHealth
👍43
CAF: SHANGWE TUPU, TANZANIA YAFUZU KUCHEZA AFCON

Timu ya Taifa ya #Tanzania “Taifa Stars” imeandika rekodi nyingine ya kufuzu kucheza michuano ya Afrika kwa mara ya tatu baada ya kuilazimisha #Algeria matokeo ya 0-0

Tanzania ambayo ilishiriki #AFCON Mwaka 1980 na 2019, imekamilisha michezo ya Kundi F ikiwa na pointi 8 nyuma ya Algeria yenye pointi 16 ambayo nayo imefuzu, #Uganda ina pointi 7, Niger imeshika mkia kwa kuwa na pointi 2

Michuano ya AFCON inatarajiwa kufanyika Januari 13 hadi Februari 11, 2024 Nchini #IvoryCoast

Soma https://jamii.app/CAFAFCON23

#JFSports #JamiiForums
🔥20👍6😁2
AFYA: Wizara ya Afya inatarajia kutoa Chanjo ya #Polio kwa Watoto katika Mikoa ya #Mbeya, #Katavi, #Rukwa, #Kagera, #Kigoma na Mkoa wa #Songwe unaotarajiwa Kuchanja Watoto 402,000

Ofisa Programu kutoka Idara ya Kinga, Penford Joel amesema zoezi litafanyika Septemba 21 hadi 24, 2023 na litawahusu Watoto wenye umri wa 0 hadi miaka 8

Ametaja sababu za kutoa Chanjo katika Mikoa hiyo ni kufuatia baadhi ya Nchi kubainika kuwa na Wagonjwa waliotokana na Virusi vya Polio

Soma https://jamii.app/ChanjoPolio

#JamiiForums #JFAfya #Governance #PublicHealth #JFAfyaJamii #PolioAwareness #JFHuduma
👍31👏1
UGANDA: Askari wa Usalama Barabarani wametangaza kufunga barabara Jijini #Kampala kwa ajili ya sherehe za kuadhimisha Miaka 79 ya kuzaliwa kwa Rais Yoweri Museveni, zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru leo, Septemba 8, 2023

Sherehe hiyo iliyoandaliwa na Vijana, wakiongozwa na Mratibu wa Kitaifa katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha National Resistance Movement (Chama Tawala), Hadijah Uzeiye Namyalo, inatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 100,000 kutoka nchi mbalimbali

Aidha, licha ya sherehe hiyo kufanyika leo, Siku ya kuzaliwa ya Rais Museveni itaadhimishwa Septemba 15, 2023, ambayo ndio tarehe aliyozaliwa Rais huyo

Soma https://jamii.app/BarabaraKampala

#JamiiForums #Governance #MuseveniBirthday
😁8👎7👍32🤔2💩2
#BURUDANI: Nyota wa Tamthilia ya #BreakingBad, Aaron Paul amedai kutolipwa Mirabaha yake na Kampuni ya #Netflix, inayoonesha Tamthilia hiyo

Japokuwa Breaking Bad imekuwa moja ya tamthilia ambazo zimetazamwa zaidi Netflix kwa miaka mingi, Paul anadai hapokei chochote kutoka kwao licha ya kucheza Mhusika Maarufu katika Misimu yote Mitano ya Tamthilia hiyo

Soma https://jamii.app/AaronPaul

#JamiiForums #JFEntertainment #Royalties
👍3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Baada ya Mdau wa JamiiForum.com kutoa wito kwa Serikali kuingilia mchakato wa kuwasaidia Wastaafu hao kwa madai kuna kikundi cha Watu kinataka kuwatapeli kwa kigezo cha kuwasaidia kulipwa stahiki zao, Serikali imesema hakuna stahiki wanazodaiwa na Wastaafu hao zaidi ya Malipo ya Pensheni yanayotolewa kwa baadhi

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema “Utaratibu wa Malipo ulifanyika na mirathi kwa waliofariki wapatao 31,831. Zoezi lilifanyika kwa miaka nane kuanzia Julai 2006 hadi Novemba 2013 lilipofungwa rasmi, kwa sasa Serikali inaendelea kulipa pensheni za kila mwezi kwa baadhi yao.”

Soma https://jamii.app/BungeSept8

#JFUwajibikaji23 #KemeaRushwa #Accountability #JamiiForums
👍3🤔1
Kwa mujibu wa Ripoti ya #UNESCO, Kipindi cha #COVID19, Elimu ya Mtandaoni ilifungua fursa ya Elimu kwa zaidi ya Wanafunzi bilioni 1 Duniani. Hata hivyo, takribani 31% ya Wanafunzi Duniani hawakuweza kufikia Elimu hii

Pia, 72% ya Wanafunzi wa familia za kipato cha chini hawakuweza kunufaika na Teknolojia husika. Hii inaonesha jinsi teknolojia inavyoendelea kuwa chanzo cha kutengeneza pengo la Elimu kati ya Matajiri na Masikini

Soma https://jamii.app/ElimuMtandaoni

#JFDigitali #ChildRights #JFHakiElimu #RightToEducation #JamiiForums
👍3
MDAU-MWANZA: KIVUKO CHA KIGONGO FERRY-BUSISI TIKETI HAZICHANWI NA ‘HAWAZI-SCAN

Mdau anadai tabia ya tiketi kutochanwa wala kutopitishwa kwenye mashine kwa ajili ya kuhakiki (scanner) imeanza miezi ya hivi karibuni na hivyo kutengeneza mazingira ya ‘upigaji’ kwa kuwa kuna uwezekano wa tiketi moja kutumika zaidi ya mara moja

Anadai abiria akinunua tiketi anatakiwa kumkabidhi Msimamizi mwingine kabla ya kuingia kwenye Kivuko, kisha inawekwa kwenye pipa dogo bila kuchanwa

Mdau anashauri Mamlaka za Serikali ikiwemo TAKUKURU ifuatilie kinachoendelea ili kama kuna michezo michafu inayokosesha Serikali Mapato idhibitiwe

Soma https://jamii.app/KigongoBusisi

#JFUwajibikaji23 #KemeaRushwa #JFHuduma #JamiiForums
👍9🤔1
Siku ya Kimataifa ya kujua Kusoma na Kuandika huadhimishwa kila Septemba 8, ikiangazia umuhimu wa Elimu katika Maendeleo ya binafsi na ya jamii

Siku hii iliyoanzishwa na Shirika la Elimu, Sayansi, na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), inasisitiza Elimu kama suala la Heshima na Haki za Binadamu.

Kulingana na UNESCO, angalau Watu takriban milioni 76 Duniani walikosa ujuzi wa Msingi wa kusoma na kuandika Mwaka 2020.

Soma https://jamii.app/LiteracyDay2023

#JamiiForums #WorldLiteracyDay #RightToEducation #JFHakiElimu
👏21👍1😁1
AFYA: Septemba kila mwaka, ni Mwezi wa Uelewa wa Saratani ya Utotoni Duniani. Mwezi huu hutumika kutambua Watoto na Vijana walioathiriwa na aina mbalimbali za Saratani

Pia, siku hii hutumika kuheshimu Vijana wanaougua #Saratani, Familia zinazowatunza, Wataalamu wa Afya na Walezi wao, Watoto waliopoteza maisha yao na Wanasayansi waliojitolea kupambana Saratani ya Utotoni

Alama ya Mwezi huu ni Utepe wa Dhahabu unawakilisha aina zote za Saratani inayoathiri Watoto na Vijana

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesema inachunguza tukio la Nyara za Serikali kukamatwa Australia, baada ya Video iliyosambaa mtandaoni kuonesha Maafisa Usalama wakichunguza picha za ‘X-Ray’ za ngozi ya Chui iliyotengenezwa kama zulia na fuvu la Simba lililoungana na ngozi (Full Mount) vinaodaiwa kutumwa kutokea Tanzania

#TAWA imeeleza uchunguzi wao wa awali unaonesha nyara hizo zilitumwa kama kifurushi kwenda #Australia, zikiambatanishwa na baadhi ya Nyaraka kama Hati ya Kusafirisha Nyara nje ya Nchi ambazo kwa mujibu wa Sheria, kibali hicho hakiwezi kutumika kusafirisha nyara za Wanyamapori hao

Soma https://jamii.app/NyaraAustralia

#JamiiForums #SocialJustice #Governance #Wildlife
🤔73👍1
Kulingana na UNESCO, takriban Watu milioni 775 Duniani hawana ujuzi wa Msingi wa Kusoma na Kuandika. Mmoja kati ya Watu watano bado hawajui kusoma, na pia kuna pengo kubwa la jinsia, kwani theluthi mbili ya Watu hawa ni Wanawake

Zaidi ya hayo, mamilioni ya Watoto hawapo Shuleni au wanahudhuria Shule kwa kusuasua, na athari za janga la #COVID19 zimezidisha changamoto hizi. Karibu Wanafunzi milioni 24 huenda wasirudi tena katika Elimu rasmi

Soma https://jamii.app/LiteracyDay2023

#JFHakiElimu #RightToEducation #WorldLiteracyDay #JamiiForums #ChildRights
1😁1
Je, kuna taarifa, tukio au jambo linakutatiza na hujui kama ni Kweli, Uongo au Nadharia?

Jukwaa la Jamii Check ndani ya JamiiForums.com lipo mahsusi kuondoa utata huo

Kutembelea Jukwaa hili, tafadhali bonyeza jamii.app/FactChecker

#JamiiForums #JamiiCheck #FactsChecking #FactsCheck
#UTAFITI: Uchunguzi wa DNA uliofanywa Ujerumani umefanikiwa kuwapata Watu waliopo Tanzania ambao ndugu zao ni miongoni mwa mafuvu yaliyoporwa na Ujerumani kipindi cha Ukoloni

Moja ya fuvu ambalo tayari liliashiria kuwa ni la aliyekuwa Mshauri wa Kiongozi wa Wachaga, Mangi Meli (1866-1900) limeonesha uhusiano wa moja kwa moja na mwanaume ambaye bado yupo hai

Makumbusho ya kihistoria ya Berlin imekuwa ikifanya utafiti kwenye mafuvu takriban 1,100 kutoka katika iliyokuwa inajulikana kama Ujerumani ya Afrika Mashariki (Rwanda, Burundi, Tanganyika-Tanzania na sehemu ya Msumbiji) tangu mwaka 2017, wakiwa na lengo la kurudisha mabaki hayo katika nchi husika

Uongozi wa Makumbusho hiyo umesema Ndugu na Jamaa pamoja na Serikali ya Tanzania watapewa taarifa haraka iwezekanavyo

Zaidi Soma: https://jamii.app/FuvuUjerumani

#JamiiForums #Historia #UgunduziTanzania #Utafiti
👍61
UGANDA: Kamati ya Bunge ya VVU/UKIMWI imeeleza kushangazwa na ripoti ya Mamlaka ya Taifa ya Dawa Nchini humo iliyokiri kufahamu Wafugaji wamekuwa wakitumia Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV) ili Kukuza na Kunenepesha Mifugo wakiwemo Kuku na Nguruwe na haikuchukua hatua zozote

Mkaguzi Mwandamizi wa Dawa kutoka NDA, Amos Atumanya amesema Mamlaka hiyo ilifahamu hatari hiyo miaka 10 iliyopita na ilifanya uchunguzi mwaka 2014 ili kuthibitisha madai hayo

Kwa upande wake Serikali imesema imeanza kampeni za uhamasishaji kwa Umma kuhusu hatari za kutumia Dawa hizo kama Chakula cha Mifugo

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Dawa (NDA), ulaji wa Kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV husababisha Watu kupata Usugu wa Dawa, pia huongeza hatari ya kupata Shinikizo la Damu na Magonjwa mengine ya Moyo

Soma https://jamii.app/ARVUganda

#JamiiForums #Governance #PublicHealth #SocialJustice
👍21😱1
AFRIKA KUSINI: Pendekezo la kumlipa #TrevorNoah Randi Milioni 33 (takriban Tsh. Bilioni 4.2) kwa Video ya Dakika 5 ya kuitangaza #SouthAfrica kama Kivutio cha Kitalii, limesababisha mpasuko baada ya baadhi ya Wabunge na Wananchi kupinga kwa kudai kuwa Nchi hiyo inapitia Mgogoro mkubwa wa kifedha kwa wakati huu

Waziri wa Utalii, Patricia de Lille amesema kuwa Mcheshaji na Mtangazaji huyo atalipwa na Baraza la Biashara la Utalii Nchini humo na sio kwa kupitia Fedha za Umma

Hata hivyo, Wadau wengine wameunga mkono pendekezo hilo wakisema ushawishi wa Nyota huyo unaweza kukuza Utalii wa Afrika Kusini

Soma https://jamii.app/UtaliiSA

#JamiiForums #SATourism #Utalii #Tourism #Governance #Democracy
👏3👍2
#NISHATI: Wananchi kutoka maeneo mbalimbali walioandika ndani ya JamiiForums.com wamesema TANESCO imekuwa na utaratibu wa kukata Umeme na kurejesha ndani ya muda mfupi kwa mfululizo bila taarifa yoyote hali inayosababisha kuungua kwa Vifaa

Akitoa mfano mdau kutoka Kilungule A, Kimara anasema "Tangu asubuhi TANESCO wanachofanya ni kukata na kuwasha Umeme kama vile wamepanga kutuunguzia Vifaa vyetu ambavyo wengine tumevipata kwa kukopa"

Mdau kutoka Mtwara Mjini anasema "Ni siku ya nne sasa toka huu mchezo uanze kufanyika. Tunateseka, baadhi ya vifaa vyetu vinavyotegemea umeme vinaharibika kwa sababu ya shoti ya umeme"

Je, wewe umepitia changamoto hii? Una maoni gani kwa TANESCO?

Soma https://jamii.app/KimaraUmeme

#JamiiForums #JFHuduma #JFUwajibikaji23 #Governance #SocialJustice
👍76👏1