JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Wakiwa kwenye Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), Rais Samia wa Tanzania na Rais William Ruto wa Kenya walitaniana kuhusu Matumizi Sahihi ya Lugha za Kiswahili na Kingereza

#JamiiForums #KiswahiliLughaYetu #TanzaniaVsKenya
👍3
MOROCCO: TETEMEKO LA ARDHI LAUA WATU 296

Tetetemeko kubwa limetokea usiku wa kuamkia leo Septemba 9, 2023 likiwa na ukubwa wa Richa 6.8 na kusababisha uharibifu mkubwa Mji wa #Marrakesh na Miji mingine ambayo ni Al-Haouz, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant

Inaelezwa vifo vingi vimetokea kwenye maeneo ya miinuko na milima ambapo ni vigumu kufikia. Ripoti ya Wizara ya Mambo ya Ndani imeeleza kuwa watu 153 wamejeruhiwa

Soma https://jamii.app/TetemekoMorocco

#EarthQuake #ClimateChange #JamiiForums
💔8😢3👍1
Rais #CyrilRamaphosa amesema Ukaguzi wa Mitindo ya Maisha ya Viongozi ulioanza Machi 2021 kwa sasa umewafikia yeye, #Makamu wake na #Mawaziri na ni lazima ukamilishwe hivi karibuni, ingawa hajaweka wazi tarehe kamili

Taarifa zinasema hadi kufikia Machi 2023, Watumishi 11,000 wa Serikali wamefanyiwa Mapitio, Uchunguzi na Ukaguzi wa Mtindo wa Maisha na zoezi hili linatakiwa kukamilika Machi 2024

Endapo Kiongozi atatiliwa mashaka ikiwemo kuwa na utajiri usioelezeka namna ulivyopatikana au kuwa na biashara zenye Mgongano wa Kimaslahi Serikalini, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake

Soma https://jamii.app/LifeStyleAudit

#JamiiForums #Governance #Accountability #LifeStyleAudit
👏32👍2
Haki ya kupata Elimu inaambatana na Haki ya kufikia Huduma ya Mtandao. Hata hivyo, upatikanaji wa #Teknolojia hii bado ni changamoto

Duniani, ni 40% tu ya Shule za Msingi, 50% ya Shule za Sekondari za chini, na 65% ya Shule za Sekondari za juu zinaunganishwa na Mtandao

Ripoti ya #UNESCO inasema ingawa 85% ya Nchi zina sera za kuboresha upatikanaji wa Mtandao kwa Wanafunzi na Shule, bado kuna safari ndefu ya kufikia usawa wa upatikanaji wake

Soma https://jamii.app/ElimuMtandaoni

#JFDigitali #ChildRights #JFHakiElimu #RightToEducation #JamiiForums
👍31
MOROCCO: Idadi ya Vifo kutokana na Tetetemeko la Ardhi la ukubwa wa Richa 6.8 lililotokea Usiku wa kuamkia Septemba 9, 2023, imefikia 632, huku zoezi la Uokoaji likiendelea kwa waathirika waliofunikwa na vifusi

Wizara ya Mambo ya Ndani Nchini humo imesema vifo vingi vimetokea katika maeneo ya Al-Haous, Marrakesh, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant, na kuongeza kuwa Watu wasiopungua 329 wamejeruhiwa

Soma https://jamii.app/TetemekoMorocco

#EarthQuake #ClimateChange #JamiiForums #MoroccoEarthQuake
👍3👎1👏1😢1
UPDATE: Taarifa mpya kutoka katika maeno ya Rabat na Marrakesh, Morocco zinaeleza kuwa idadi ya Watu waliopoteza maisha kutokana na Tetemeko la Ardhi lenye kipimo cha Richa 6.8 imefikia 820

Mbali na waliofariki, idadi ya Majeruhi pia inakadiriwa kuzidi Watu 670

Soma https://jamii.app/TetemekoMorocco

#JamiiForums #EarthQuake #ClimateChange #MoroccoEarthQuake
😢4👎2
UCHUMI: Mkutano wa Jukwaa Kuu la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa la G20 limetoa baraka za kuupa Umoja wa Afrika Ujumbe wa Kudumu katika Jukwaa hilo ambapo sasa AU itakuwa na hadhi sawa na Umoja wa Ulaya (EU)

Kwa uamuzi huo, AU itakua na sauti kwenye Kura za Maamuzi yatakayogusa Nchi 54 za Afrika, Nchi 19 za Mataifa Yaliyoendelea Kiviwanda na Umoja wa Ulaya

G20 ni Muunganiko wa Kiserikali unaojumuisha Nchi 19 pamoja na Umoja wa Ulaya. Majukumu yake ni kushughulikia masuala ya Uchumi wa Dunia ikiwemo Utulivu wa Kifedha, Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Maendeleo Endelevu

Soma https://jamii.app/G20AU

#JamiiForums #Governance #Diplomacy #Accountability #WorldEconomy
👍3😁21👎1🤔1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Video hii ilisambaa mitandaoni mwaka 2020 ikimuonesha Afisa wa Nigeria anayedaiwa kuzimia Bungeni baada ya kuulizwa kuhusu Matumizi ya Fedha za Umma

#JamiiForums #JamiiForumsInsights #Accountability #JFUwajibikaji
😁11👍31
UPDATE: Wakati zoezi la uokoaji likiendelea, Maafisa wa Uokoaji Nchini humo wamesema Watu wengi bado wamenaswa kwenye vifusi vizito na idadi ya waliopoteza maisha inazidi kuongezeka kwa kasi ambapo hadi sasa imefikia Watu 1,037

Pia, imeelezwa kuwa Miili ya Watu wengine iko katika maeneo ambayo ni magumu kufikika huko #Marrakech

Usiku wa kuamkia leo Septemba 9, 2023, #Morocco imepigwa na Tetemeko la Ardhi lenye kipimo cha Richa 6.8 ambalo ni kati ya Matetemeko makubwa kuwahi kutokea Barani Afrika

Soma https://jamii.app/TetemekoMorocco

#JamiiForums #EarthQuake #ClimateChange #MoroccoEarthQuake
👍6😢2
Pima uwezo wa Macho hapa

Unasoma namba gani?

#JamiiForums #BrainTeaser #ChemshaBongo
👍3
ZANZIBAR: Bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Septemba 9, 2023 zimetangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) ambapo Petroli imeshuka kwa Tsh. 20, Dizeli imepanda kwa Tsh. 169 huku Mafuta ya Ndege yakipanda kwa Tsh. 83 na bei ya Mafuta ya Taa imebaki palepale

Bei mpya zilizotangazwa ni Petroli Tsh. 2,950, Dizeli Tsh. 3,012, Mafuta ya Taa Tsh. 2,921 na Mafuta ya Ndege ni Tsh. 2,448

Sababu za kuongezeka bei ni kuongezeka kwa bei katika Soko la Dunia kwa 21%, gharama za Bima na usafirishaji kwa 62% ikilinganishwa na Mwezi Agosti 2023

Soma https://jamii.app/NishatiZNZ

#Governance #JFHuduma #JamiiForums
👍4
Kwa hapa Nchini unadhani ni Kanisa gani linaweza kuvunja Rekodi hii?

#JamiiForums #Maisha #GWR
2
MOROCCO: Wizara ya Mambo ya Ndani imesema hadi kufikia sasa takriban Watu 2,012 wamefariki Dunia huku wengine 2,059 wakijeruhiwa na 1,404 kati yao wako katika hali mbaya kiafya

Shirika la Afya Duniani (#WHO) limesema zaidi ya Watu 300,000 wameathirika na Tetemeko hilo lililopiga maeneo kadhaa ya Jiji la #Marrakech ikiwemo Kijiji cha #Asni ambacho inaelezwa kuharibiwa karibia nyumba zote

Ni Tetemeko la pili kusababisha maafa makubwa ndani ya mwaka mmoja ambapo Miezi 7 iliyopita, takriban watu 50,000 walipoteza maisha kwa kupigwa na Tetemeko Nchini Uturuki

Soma https://jamii.app/QuakeUpdate

#JamiiForums #EarthQuake #ClimateChange #MoroccoEarthQuake #JFMatukio #JFUpdates
😢8👍5👎1
Kufuatia kusambaa kwa Video iliyowaonesha Watoto wakitoa Burudani kwenye Sherehe wakati wa Usiku na katika Miondoko isiyofaa kwa Umri wao, Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewatafuta Wazazi wa Watoto hao na kukemea kitendo hicho huku akiwataka Washereheshaji na Jamii kuzingatia Sheria inayokemea Udhalilishaji wa Watoto

Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 (iliyorekebishwa Mwaka 2019), kifungu cha 158 (1) (c) inazuia kumtumia Mtoto kwenye Maonesho ya Harusi, Mitindo ya Nguo au Maonesho mengine kama hayo wakati wa Usiku. Adhabu yake ni faini ya Tsh. Laki 5 au kifungo cha Miezi 6 jela au vyote kwa pamoja

Soma https://jamii.app/HarusiWatoto

#JamiiForums #HakiMtoto #JFWomen #ChildProtection #Governance #SocialJustice #JFUwajibikaji
👍18👏21
ARUSHA: Inadaiwa Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA, Tundu Lissu, amekamatwa asubuhi ya leo Septemba 10, 2023 wakati akiwa Wilayani Karatu

Wengine ambao nao inadaiwa wamekamatwa ni Walinzi wote wa Lissu, Catherine Ruge (Katibu wa BAWACHA), Mzee Hashim (Mwenyekiti Wa Baraza la Wazee CHADEMA Taifa), Suzan Kiwanga na Oscar ambaye ni Mwandishi wa Jambo TV

Soma https://jamii.app/LissuAkamatwaKRT

#JFMatukio #JamiiForums
👍7👎4😁2