Unapoendesha Gari wakati wa Mvua au Ukungu unashauriwa kutumia Mwendo mdogo/wastani kwasababu Barabara nyingi huteleza na ni vigumu kuona njia vizuri. Mwendo Mdogo humsaidia Dereva kuweza kulimudu Gari vyema
Aidha, unashauriwa Usipite kwenye mafuriko au Maji mengi. Magurudumu ya Gari huelea kwenye Maji kutokana na Upepo ndani yake; hivyo hufanya iwe rahisi kuzolewa na Maji
Soma https://jamii.app/GariMvuaUkungu
#Driving #JFGarage #Maarifa #JamiiForums

👍8🙏2👎1
Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Kujiua/Kujitoa Uhai (#WSPD) ilianzishwa Mwaka 2003 na Chama cha Kimataifa cha Kuzuia Kujitoa Uhai kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO)
Septemba 10 kila Mwaka inalenga kuleta umakini kwenye tatizo hili la #AfyaYaAkili, kupunguza unyanyapaa, na kuongeza uelewa kwa Mashirika, Serikali na Jamii kwamba kujitoa uhai kunaweza kuzuilika.
Soma https://jamii.app/SuicidePrevention
#JamiiForums #JFAfyaAkili #MentalHealthMatters #WorldSuicidePreventionDay

👍2
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limeweka wazi sababu za kumshikilia Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu na wenzake watatu wa Chama hicho ambapo Jeshi hilo limesema ni kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za kufanya mikusanyiko isivyo halali na kuwazuia Askari Polisi kutekeleza majukumu yao
-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa #Arusha, Justine Masejo amebainisha kuwa baada ya mahojiano na taratibu nyingine, hatua nyingine za kisheria zitafuata
Soma https://jamii.app/LissuUpdate
#JFMatukio #Siasa #Democracy #JamiiForums

👍7
Kujitoa uhai ni tatizo kubwa la Kiafya lenye athari Kijamii, Kihisia, na Kiuchumi. Inakadiriwa kuna zaidi ya visa 700,000 vya kujitoa uhai kila Mwaka Duniani
"Kuleta Matumaini Kwa Vitendo" ndio Kaulimbiu inayotumika kwa Miaka mitatu kwenye Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Kujitoa Uhai kuanzia 2021-2023
Kaulimbiu hii inatoa wito wa kuchukua hatua na kukumbusha kwamba kuna njia mbadala za kutatua Changamoto badala ya Kujiua na kwa Matendo yetu, tunaweza kuleta matumaini.
Soma https://jamii.app/SuicidePrevention
#WorldSuicidePreventionDay #MentalHealthMatters #JFAfyaAkili #JamiiForums

Anadai Mwaka 2008 alichaguliwa kujiunga Chuo cha MUCE Iringa lakini hakujiunga kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake na akatoa taarifa, Mwaka 2009 akajiunga Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kuhitimu Mwaka 2012 huku akipata Mkopo wa Bodi ya Mikopo (HESLB)
Anadai alipopata ajira akawa anakatwa mikopo miwili kwa wakati mmoja (Wa #MUCEIringa na wa #UDOM), alipoenda kuhoji #HESLB na kutaka apewe uthibitisho wa malipo ya MUCE Iringa wanayodai walimlipa, hakupewa majibu ya kuridhisha
Anashauri mifumo ya mikopo iboreshwe kwa madai kuwa kuna changamoto kadhaa zinazohusu malipo
Je, wewe umepitia changamoto kama ya Mdau? Ulipata msaada kutoka kwenye Mamlaka husika?
Soma https://jamii.app/MkopoChuo
#JFUwajibikaji23 #JFHuduma #KemeaRushwa #JamiiForums

👍5
Makosa ya Jinai yapo ya Kati na Makubwa. #Uhaini ni moja ya Makosa Makubwa ya Jinai kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code), japokuwa zipo Sheria nyingine zinazofafanua kuhusu Jinai zikiwemo za Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Uhujumu Uchumi na Ugaidi
Tazama kwenye picha kusoma matendo ambayo yanaweza kuhesabika ni makosa ya Uhaini kwa mujibu wa Sheria Kifungu cha 39 (1) cha Kanuni za Adhabu
Soma https://jamii.app/Uhaini
#JFSheria #Governance #JamiiForums #Treason

❤1👍1
Mdau anadai Mikoa ya Kusini mwa #Tanzania mfano #Lindi na #Mtwara haifikiki kwa urahisi kwa njia ya Barabara kwa mtu anayetokea Kanda ya Kati, Magharibi, Kanda ya Ziwa na Kaskazini kwa kuwa kunakosekana muunganiko wa Barabara Kuu
Anatoa wito kwa Serikali kujenga Barabara Kuu kuanzia Iringa Mjini/Ipogolo kupitia Kilolo, Ifakara, Mahenge hadi Liwale
Mdau anasema barabara hiyo itatoa fursa za Utalii kwenye Hifadhi ya Nyerere (Selous) na ikitokea changamoto kwenye Barabara Kuu ya #Tanzam (Barabara Kuu kati ya Dar es Salaam na Lusaka) magari yatapitia Ifakara hadi Mikumi na maisha yataendelea bila usumbufu
Soma https://jamii.app/BarabaraKuuIringa
#JamiiForums #Governance #ServiceDelivery #JFHuduma

❤8👍5
TUNTEMEKE SANGA: MSOMI WA SHAHADA 7 ALIYEIKATAA FALSAFA YA UJAMAA YA MWALIMU NYERERE
Aliamini Siasa ya Ujamaa haiwezi kuleta maendeleo na kumtaka Mwl. Nyerere ampishe Urais ili ailetee nchi maendeleo kwa Falsafa za ubepari
Hiyo inadaiwa kumkera Nyerere na kwa kutumia Sheria alimuweka Tunte kizuizini Kijijini kwake Bulongwa na kumuamuru atoke kwa kibali maalumu
Zaidi, tembelea https://jamii.app/HistoriaTuntemekeSanga
#JamiiForums #JFHistoria #TuntemekeSanga

👍10❤1😁1
ARUSHA: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na wenzake wametakiwa kuripoti katika Kituo cha Polisi leo, Septemba 11, 2023 ikiwa ni baada ya kupewa dhamana baada ya yeye na Wanachama wengine kukamatwa Wilayani Karatu
Lissu na Wanachama wengine akiwemo Katibu wa BAWACHA, Catherine Ruge walikamatwa kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko isivyo halali na kuzuia Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yake ikiwa ni siku moja tangu wazuiwe kuingia Ngorongoro
Ikumbukwe, haya yanatokea siku chache tangu Lissu anukuliwe akisema mazungumzo ya Maridhiano kati ya CHADEMA na Chama Cha Mapinduzi (CCM) yamevunjika kutokana na CCM kukataa hoja zao zote
Soma https://jamii.app/LissuBailed
#JamiiForums #JFDemokrasia #JFSiasa #Governance

👍5🔥2🤔1
Winga huyo wa #ManchesterUnited aliyetakiwa kurejea mazoezini leo Septemba 11, 2023 amekubaliana na klabu yake kupewa muda wa kushughulikia tuhuma za unyanyasaji dhidi yake toka kwa aliyekuwa mpenzi wake #GabrielaCavallin na Wanawake wengine wawili
#Antony (23) hajasimamishwa lakini amepewa muda wa kuwa nje ya ofisi akiwa pia anaendelea kulipwa mshahara wake kama kawaida
Soma https://jamii.app/AntonyStayAway
#JFSports #SocialJustice #JamiiForums

👍3😁2
Kwa mujibu wa Ripoti ya Economist Intelligence Unit (EIU), ni kuwa Afrika ina 12% tu ya Nchi zenye kiwango bora cha Demokrasia zikiongozwa na Mauritius
Nchi zenye kiwango kibaya zaidi cha Demokarasia ni pamoja na Chad, DR-Congo, Afrika ya Kati, Guinea, Burundi, Zimbabwe, Libya, Sudan, Elitrea, Cameroon n.k.
Vielelezo vya Demokrasia vimekuwa vikipimwa kwa Michakato ya Uchaguzi, Utamaduni wa Kisiasa, Ushiriki wa Wananchi katika Siasa, Uwajibikaji wa Serikali na Uhuru wa Kiraia
Soma https://jamii.app/AfricanDemocracy
#JamiiForums #Governance #Accountability #JFDemokrasia #DemocracyWeek2023 #WikiYaDemokrasia2023