JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Baruani Mshale wa Taasisi ya #Twaweza anasema “Ni muhimu kujiuliza umuhimu wa mageuzi ni kwa maslahi ya nani? Lazima tuangalie raia wa kawaida anataka nini na yanagusa maisha yetu ya kila siku?”

Anaongeza “Mwananchi akisikia Wanasiasa wanazungumzia mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi anaona wanajitengenezea fursa za kuingia madarakani na kubaki kuwa na uhalali bila kujali maisha ya Mwananchi wa kawaida.”

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman amesema Rais Samia Suluhu Hassan amezielekeza Taasisi za Serikali zilizotajwa katika mapendekezo ya Kikosi Kazi kufanya mazingatio ya utekelezaji wa maoni yaliyopendekezwa

Amesema “Kupitia maoni hayo ya Kikosi Kazi hatua zimechukuliwa, Mikutano ya Hadhara na ya ndani imeendelea kufanyika. Serikali inaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo yote, yale yanayohusiana na utekelezaji wa masuala ya Sheria tunaendelea kuyafanyia mazingatio ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa ufanisi zaidi"

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Makamu wa Pili wa Rais wa #Zanzibar, Hemed Suleiman amewasihi Wanasiasa kutumia nafasi zao kuendeleza Amani iliyopo Nchini kwa kufuata Kanuni na Taratibu za Nchi hasa wakati wa kuendesha Mikutano ya Hadhara

Amesema “Lugha ambazo zimekuwa zikitumiwa na baadhi yetu sio nzuri na zinaweza kusababisha mpasuko wa umoja katika Taifa letu. Tusipokuwa makini jambo hilo linaweza kusababisha uvunjifu wa Amani.”

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍21
RUVUMA: Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (#MCT), Kajubi Mukajanga akiwa Songea amesema Vyombo vya Habari vinaendelea kupokea vitisho vya Kiutawala, changamoto za Kiuchumi, Kibiashara na nyinginezo, hivyo kukwamisha Utendaji wao

Pia, Wakili Fulgence Massawe akiwasilisha hoja kuhusu Sheria za kusimamia #UhuruWaKujieleza amesema matukio ya Watu kukamatwa, kukamata Mali, faini, kuharibiwa Vifaa, kuchunguzwa au kufuatiliwa Mawasiliano binafsi yanachangia kuminya #UhuruWaHabari

Mambo mengine ni kubambikiwa mashtaka, hofu ya kushtakiwa, kudhibitiwa kwa Maudhui katika Vyombo vya Habari au Mitandaoni

Soma https://jamii.app/UhuruWaHabari

#JamiiForums #PressFreedom #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
👍4🤔3
Kupungua kwa ushindani kati ya Vyama vya Siasa na mgawanyiko wa Kisiasa ni jambo baya kwa Demokrasia

Bunge hupata urahisi katika kufanya Maamuzi ya pamoja ikiwa Mawazo ya Wanachama wote wa Kisisasa yataheshimiwa. Ikiwa Mawazo yanatofautiana, wanaweza bado kusimamia tofauti zao kwa kujadiliana, kufikia makubaliano na mara nyingine kwa kupiga kura

Soma https://jamii.app/DemocracyChallenges

#JamiiForums #Democracy #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
👍4
Utulivu wa Serikali nyingi umekuwa ukivurugika kutokana na Serikali hizo kushindwa kutoa Usalama wa Kiuchumi kwa Raia wao

Kutokana na Serikali nyingi kushindwa kutimiza mahitaji ya Raia wao, kutoaminika na kupuuzwa kwa thamani ya Demokrasia miongoni mwa Raia kumeongezeka. Kutoaminika huku kunajionesha katika kupungua kwa idadi ya Wapiga Kura, maoni ya Umma, Maandamano na hata Mapinduzi kwa baadhi ya Nchi

Soma https://jamii.app/DemocracyChallenges

#JamiiForums #Democracy #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
👍61
JamiiForums imeandaa Mjadala wa Vijana katika kuadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani, ambapo Mada kuu ni 'Demokrasia ya Kidijitali: Kichocheo cha Utawala Bora Nchini'

Katika Mjadala huu Washiriki watajadili Jukumu la Demokrasia ya Kidigitali kama kichocheo cha Utawala Bora, Ushirikishwaji wa Vijana katika Demokrasia ya Kidijitali na Athari za Demokrasia ya Kidijitali katika Kukuza Utawala Bora

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaDemokrasia2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍1
Dkt. Rodrick (UDSM): Demokrasia ya Dijitali inaondoa ile dhana ya kusubiri hadi uchaguzi ujao yaani miaka mitano kwa Tanzania ili kumuwajibisha Kiongozi wa Kisiasa

Teknolojia ya dijitali inachochea dhana ya Mwananchi kuwa sehemu ya Utawala wa kila siku

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaDemokrasia2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DemekrasiaYaKidijitali #DegitalDemocracy
👍1
Dkt. Muhidin Shangwe (UDSM): Uongozi wa Kisiasa huwa Una Ngazi (Hierrachy) kwamba Kiongozi yuko juu na Mananchi chini lakini uwepo wa majukwaa ya dijitali unasawazisha uwanja huu na kila Mtu sasa anaweza kumhoji yeyote, kuuliza swali lolote bila kujali Umri, Cheo wala Hadhi

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaDemokrasia2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍2
Dkt. Muhidin Shangwe (UDSM): Demokrasia ya Dijitali bado ina changamoto kutokana na “Digital Divide”. Kuna Watu hususan wa Vijijini bado hawana namna ya kufikia au kumudu huduma za dijitali

Ni wajibu wetu wenye uwezo wa kushiriki kwenye majukwaa ya kidijitali kuhakikisha tunawajumuisha na wenzetu wasioweza ili iwe Demokrasia kweli

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaDemokrasia2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DKT. HELLEN KIJO-BISIMBA: KUTOKUWA NA MGOMBEA BINAFSI KUNARUDISHA NYUMA DEMOKRASIA

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Demokrasia, Mkurugenzi Mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) amesema ushiriki wa Wananchi katika Chaguzi unakuwa na mikwamo kutokana na Mifumo iliyopo kulazimisha Wagombea kutoka katika Vyama vya Siasa

Amesema Suala la Uchaguzi linatakiwa kushirikisha Wananchi wote bila kujali upande wanaotokea Kisiasa na si kuwaachia Wanasiasa pekee. Pia, kesi ya kuwepo kwa Mgombea Huru katika Uchaguzi nayo ilifunguliwa ili kujaribu kuongeza Ushiriki wa Wananchi katika Uchaguzi bila kulazimika kuwa na vyama

Soma https://jamii.app/IDD2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍1👎1
Katika Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, Mkurugenzi wa Shirika la Haki Mawasiliano, Stephen Aloys amesema kuwa tunatakiwa kuwa na Sheria ambazo hazibani Uhuru wa kujieleza, Sheria na Kanuni ambazo ni rafiki zinazoweza kumfanya Binadamu aweze kujieleza kwa sababu kiasili Binadamu anatabia ya kutaka kujua zaidi na kujieleza zaidi

Akizungumzia Hali ya Demokrasia Nchini, amesema "Kwa sasa kuna Sheria nyingi zinazotoa uhuru na zipo zinazobana uhuru wa kujieleza, tunachoshauri ni kuwa kusiwe na mipaka inayoumiza watu kutoa na kupata taarifa"

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaDemokrasia2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍21
Mshiriki wa Maadhimisho ya Siku ya #Demokrasia Duniani, ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Abdul-Azizi Ally Carter amesema Mifumo iliyopo katika Vyuo Vikuu inakatisha tamaa kwenye suala la Demokrasia. Kuna vifungu vya Sheria vinazuia Wanafunzi kushiriki moja kwa moja kuleta Demokrasia Nchini tofauti na baadhi ya Vyuo vya Nchi nyingine ambapo Wanafunzi wanatumika kama tabaka la kushawishi Mabadiliko katika Taifa

Amesema "Mifumo iliyopo Tanzania inatengeneza Wanafunzi watiifu ambao hawana uwezo wa kuhoji, kupigania Jamii na mwisho wake inatengeneza ‘Chawa’. Kuna Sheria ya Vyuo Vikuu (University Act 346) inakataza Wanafunzi kujihusisha na Siasa awapo Chuo au katika Mazingira ya Chuo. Pia, kuna Sheria ndogondogo nazo zinasimamia msimamo huohuo"

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaDemokrasia2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #JFDemokrasia #DemokrasiaYaKidijitali
👍3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya #Demokrasia, Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi (Bara), Joseph Selasini amesema hali ya Kisiasa imekuwa ngumu, hata kushawishi Vijana kushiriki Uchaguzi Huru kwasasa si jambo rahisi

Amefafanua kuwa Wagombea wamekuwa wakiingia kwenye Uchaguzi kwa #Rushwa za Mamilioni na Mabilioni ya Fedha, kitendo kinachofanya Viongozi kuchaguliwa kwa kutumia Utajiri wao

Soma https://jamii.app/IDD2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #KemeaRushwa #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍1
Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema "Kuna kipindi Wanafunzi walicheleweshewa fedha za ada kutoka Bodi ya Mikopo ya #Elimu ya Juu (#HESLB) tukakubaliana tulipe kisha Bodi itarejesha hizo fedha Julai 2023, lakini hii ni Septemba hizo fedha hatujapata licha ya kufuatilia kwenye Mamlaka"

Ameendelea "Kuna Mwanafunzi akataka yafanyike Maandamano kwa kuwa ni haki ya Kidemokrasia lakini akaitwa na Kiongozi wa Wanafunzi (Dean of Student), kinachoendelea hapo ni vitisho ili kutoendelea na alichokipanga, hivyo tunatengenezewa hofu na Demokrasia inaminywa hapo"

Amemalizia "Athari ya Mifumo ya kutokuwa na Demokrasia Imara inawafanya Wanafunzi wanapohitimu masomo wanaingia Uraiani na kutengeneza Taifa lisilokuwa na nguvu ya kuhoji na kutambua #Haki zao za msingi"

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍5
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu wa BAWACHA, Catherine Ruge amesema Waraka wa Utumishi wa Umma No. 2 wa Mwaka 2009 unaotaka Mtumishi yeyote kuachia nafasi ya Kazi baada ya kuteuliwa kugombea nafasi za Kisiasa umekuwa kikwazo cha Wanawake kushiriki Chaguzi kwasababu wanakuwa hawana uhakika na Maisha yao

Amesema kwa jinsi mfumo wa Uchaguzi ulivyo Nchini #Tanzania, Wanawake ambao ni nguzo ya Malezi katika Familia wanakosa uhakika wa Kuchaguliwa na kuacha Kazi ni hatari kwao hivyo ameshauri Mabadiliko ya Sheria mbalimbali yalizingatie hilo

Soma https://jamii.app/IDD2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #JFDemokrasia #DemokrasiaYaKidijitali
👍3
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga amesema bado kuna shida kubwa ya Wanasiasa Nchini Tanzania kuzichukulia Asasi za Kiraia kuwa kama Vyama vya Upinzani, jambo ambalo halina ukweli

Amesema hali hiyo imekuwa ikijokeza mara kwa mara ikiwemo kuzinyima AZAKI Haki ya kuwa Waangalizi wa Uchaguzi hali iliyosababisha Wananchi wengi kukosa taarifa mbalimbali za Uchaguzi na waliojaribu walikamatwa kwa madai ya kujumlisha Matokeo ya Uchaguzi

Soma https://jamii.app/IDD2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa CHADEMA ametoa kauli hiyo kupitia Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Demokrasia na kueleza kuwa msimamo wa Serikali hadi sasa ni Uchaguzi huo kuendelea kubaki chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Amesema suala hilo linathibitishwa na uamuzi wa Serikali kutoweka kwenye mipago yake ya uwasilishwaji Bungeni wa Muswada unaogusa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Vikao vya Bunge linalokuja

Soma https://jamii.app/IDD2023

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali #JFDemocracy
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
STEPHEN ALOYS: DIJITALI INATOA UHURU WA KUJIELEZA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki Mawasiliano, Stephen Aloys akizungumza katika mjadala wa Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, ambapo ujumbe unaojadiliwa ni Jukumu la Demokrasia ya Kidijitali kama Kichocheo cha Utawala

Amesisiza umuhimu wa matumizi ya Dijitali katika fursa na kushauri kutokuwa na Sheria zinazominya Uhuru wa Kujieleza

#JamiiForums #SikuYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍4
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Demokrasia, Sept. 15, 2023, JamiiForums iliandaa Mjadala wa Vijana ambapo Mada kuu ilikuwa 'Demokrasia ya Kidijitali: Kichocheo cha Utawala Bora Nchini'

Katika Mjadala huu Washiriki walijadili Jukumu la Demokrasia ya Kidigitali kama kichocheo cha Utawala Bora, Ushirikishwaji wa Vijana katika Demokrasia ya Kidijitali na Athari za Demokrasia ya Kidijitali katika Kukuza Utawala Bora

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaDemokrasia2023

#JamiiForums #JFDemokrasia #DemocracyWeek2023 #DemocracyDay #Governance #DigitalDemocracy #DemokrasiaYaKidijitali
👍1