JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFYA: Septemba kila mwaka, ni Mwezi wa Uelewa wa Saratani ya Utotoni Duniani. Mwezi huu hutumika kutambua Watoto na Vijana walioathiriwa na aina mbalimbali za Saratani

Pia, siku hii hutumika kuheshimu Vijana wanaougua #Saratani, Familia zinazowatunza, Wataalamu wa Afya na Walezi wao, Watoto waliopoteza maisha yao na Wanasayansi waliojitolea kupambana Saratani ya Utotoni

Alama ya Mwezi huu ni Utepe wa Dhahabu unawakilisha aina zote za Saratani inayoathiri Watoto na Vijana

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
Kwa mujibu wa WHO, Katika Nchi za Kipato cha Juu, zaidi ya 80% ya Watoto walio na Saratani hupata Matibabu kamili na kupona, lakini Nchi nyingi za Kipato cha Kati na cha Chini, chini ya 30% ya Watoto ndio hupona

Sababu za viwango vya chini vya kuishi katika Nchi hizo ni pamoja na: kuchelewa kugundulika, kutokuwa na uwezo wa kupata Uchunguzi sahihi, Tiba isiyoweza kufikiwa na kuacha Matibabu

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
👎1
Saratani hutokea kwa Watu wa rika zote na inaweza kuathiri sehemu yoyote ya Mwili. Huanza na mabadiliko ya kijenetiki katika Seli moja, kisha hukua na kuwa Uvimbe (#Tumor), ambao huvamia sehemu nyingine za Mwili

Tofauti na kwa Watu wazima, idadi kubwa ya #Saratani za Utotoni hazina sababu inayojulikana. Tafiti nyingi zimebaini ni Saratani chache kwa Watoto zinazosababishwa na Mazingira au Mtindo wa Maisha

Takwimu za sasa zinaonesha takriban 10% ya Watoto wote walio na Saratani wana uwezekano walizipata kwasababu za Kijenetiki.

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
👍21
Dalili zinazoonekana sana ni Uvimbe ambao mara nyingi huchelewa kugundulika kwa kuwa huwa hauna maumivu. Hufanya Watoto wachoke sana, kudhoofika na kudumaa na baadae inaweza kubana Mishipa ya Mwili

Wakati mwingine Mtoto huweza kupata Homa ambazo hazisikii Matibabu ya kawaida.

Pia, Mtoto anaweza kuanza kukosa choo vizuri, kukojoa Damu, au kuishiwa Damu mara kwa mara. Dalili zote hizi zinategemea na aina ya Saratani aliyoipata

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
👍2
SARATANI ZINAZOWASHAMBULIA WATOTO

1. Saratani ya Damu (#Leukemia): Mtoto huishiwa Damu mara kwa mara au inawezekana akawa akitokwa na Damu ovyo kupitia sehemu za wazi za Mwili

2. Saratani ya Macho (#Retinoblastoma): Ni Saratani inayoathiri takriban Watoto 8000 Duniani kila Mwaka. Jicho la Mtoto hupatwa na Uvimbe mdogo, kuwasha na Uvimbe huongezeka mpaka Mtoto kushindwa kuona vizuri

3. Saratani ya Ubongo: Ni saratani ya pili inayosumbua Watoto baada ya Leukemia. Mtoto hupata Uvimbe kwenye Ubongo ambao huathiri mwenendo wake wa Ukuaji

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
Watoto wanaweza kuathiriwa na aina mbalimbali za Saratani ya Damu (Leukemia), lakini aina mbili kuu ni Leukemia ya #Lymphoblastic (ALL) na Leukemia ya #Myeloid (AML)

Leukemia ya Lymphoblastic (ALL): Ni aina ya kawaida zaidi ya #Leukemia kwa Watoto. ALL inaweza kutokea kwa Watoto wa Umri wowote, lakini mara nyingi hutokea katika Umri wa Miaka 2 hadi 4

Leukemia ya Myeloid (AML): Aina hii pia huathiri Watoto, ingawa ni nadra kuliko ALL. AML inatokea katika Seli za Myeloid, ambazo ni sehemu ya utengenezaji wa Seli za Damu mwilini

Zaidi Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
👍73
Saratani ya Ubongo kwa Watoto ni hali ambayo Seli za Saratani hukua katika Tishu za Ubongo au Uti wa Mgongo wa Mtoto. Mtoto huweza kupata Uvimbe kwenye Ubongo au Uti wa Mgongo lakini wakati mwingine Uvimbe huu huweza kuwa sio Saratani

Inakadiriwa Watoto 33 kwenye kila Watoto milioni 1 na Vijana 21 kwenye kila Vijana milioni 1 wataugua Ugonjwa huu kwa mwaka 2023

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
1👍1