JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Dalili zinazoonekana sana ni Uvimbe ambao mara nyingi huchelewa kugundulika kwa kuwa huwa hauna maumivu. Hufanya Watoto wachoke sana, kudhoofika na kudumaa na baadae inaweza kubana Mishipa ya Mwili

Wakati mwingine Mtoto huweza kupata Homa ambazo hazisikii Matibabu ya kawaida.

Pia, Mtoto anaweza kuanza kukosa choo vizuri, kukojoa Damu, au kuishiwa Damu mara kwa mara. Dalili zote hizi zinategemea na aina ya Saratani aliyoipata

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
πŸ‘2
SARATANI ZINAZOWASHAMBULIA WATOTO

1. Saratani ya Damu (#Leukemia): Mtoto huishiwa Damu mara kwa mara au inawezekana akawa akitokwa na Damu ovyo kupitia sehemu za wazi za Mwili

2. Saratani ya Macho (#Retinoblastoma): Ni Saratani inayoathiri takriban Watoto 8000 Duniani kila Mwaka. Jicho la Mtoto hupatwa na Uvimbe mdogo, kuwasha na Uvimbe huongezeka mpaka Mtoto kushindwa kuona vizuri

3. Saratani ya Ubongo: Ni saratani ya pili inayosumbua Watoto baada ya Leukemia. Mtoto hupata Uvimbe kwenye Ubongo ambao huathiri mwenendo wake wa Ukuaji

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
Watoto wanaweza kuathiriwa na aina mbalimbali za Saratani ya Damu (Leukemia), lakini aina mbili kuu ni Leukemia ya #Lymphoblastic (ALL) na Leukemia ya #Myeloid (AML)

Leukemia ya Lymphoblastic (ALL): Ni aina ya kawaida zaidi ya #Leukemia kwa Watoto. ALL inaweza kutokea kwa Watoto wa Umri wowote, lakini mara nyingi hutokea katika Umri wa Miaka 2 hadi 4

Leukemia ya Myeloid (AML): Aina hii pia huathiri Watoto, ingawa ni nadra kuliko ALL. AML inatokea katika Seli za Myeloid, ambazo ni sehemu ya utengenezaji wa Seli za Damu mwilini

Zaidi Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
πŸ‘7❀3
Saratani ya Ubongo kwa Watoto ni hali ambayo Seli za Saratani hukua katika Tishu za Ubongo au Uti wa Mgongo wa Mtoto. Mtoto huweza kupata Uvimbe kwenye Ubongo au Uti wa Mgongo lakini wakati mwingine Uvimbe huu huweza kuwa sio Saratani

Inakadiriwa Watoto 33 kwenye kila Watoto milioni 1 na Vijana 21 kwenye kila Vijana milioni 1 wataugua Ugonjwa huu kwa mwaka 2023

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
❀1πŸ‘1
#AFYA: Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameshauri Wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Saratani huku akieleza takriban Wagonjwa 40,000 wa Saratani wanagundulika kila Mwaka na kati yao 26,000 hufariki Dunia
-
Amesema idadi ya Wagonjwa wanaofika Hospitali ni 30% ambapo wengi wao wanafika wakati Ugonjwa huo ukiwa katika hatua ya tatu hadi hatua ya nne, hali inayosababisha ugumu kwenye matibabu, tofauti na kama wangewahi kupata huduma za Kiafya na kuanza matibabu mapema

Waziri Ummy amesema β€œNitoe wito kwa Watanzania wapime Saratani angalau mara moja kwa Mwaka kwa kuwa Saratani inayoongoza ni ya Mlango wa Kizazi iko kwa 25%, Matiti 10%, Tezi Dume 9%, Mfumo wa Chakula 6.5% pamoja na Saratani nyinginezo.”

Soma https://jamii.app/SarataniTZA

#JamiiForums #JFAfya #PublicHealth #CancerAwareness
πŸ‘2
#AFYA: Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Moyo ya Marekani (Heart.Org) kwa Watu wenye miaka kati ya 20 hadi 70 umeonesha Watu wasiopata muda mrefu wa Kulala Usingizi kati ya Saa 7 hadi 8 kila siku wanakuwa hatarini kupata Saratani au Kifo cha Ghafla

Utafiti huo uliochapishwa kupitia Journal of the American Heart Association (JAHA) umebaini Watu wenye matatizo yoyote yanayohusisha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Ubongo (CBVDs) wako hatarini zaidi Kupoteza Maisha endapo watakuwa hawalali vizuri

Usingizi unatajwa kuwa moja kati ya Tiba Bora za Mwili zinazofanya kazi wakati Mtu amelala kwa kurekebisha maeneo yenye shida, hivyo Mtu asiyelala angalau kwa Saa 7 au 8, anapunguza ufanisi wa Mwili kujitibu ambapo madhara yake huongezeka kadri Mtu anapokosa Usingizi wa kutosha

Soma https://jamii.app/UsingiziSaratani

#JamiiForums #PublicHealth #CancerAwareness #JFAfya #JFAfyaJamii
❀3πŸ‘2
#JFAFYA: Takwimu za Wizara ya Afya Tanzania zinaonesha aina 4 ya Saratani zina idadi kubwa ya Wagonjwa nchini kulinganisha na Saratani nyingine

Saratani ya Mlango wa Kizazi inaongoza kwa 23% ya Wagonjwa ikifuatiwa na Saratani ya Mfumo wa Chakula 11%, Saratani ya Matiti 10.4% na Saratani ya Tezi Dume 8.9%

Ungana nasi leo Aprili 27, 2024, Saa 10:00 Jioni katika Mjadala utakaokuwa na Wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki Mjadala Bofya https://jamii.app/HPVSpaces

#JamiiForums #PublicHealth #CancerAwareness #AfyaBora2024 #JFAfyaJamii #JFXSpaces
πŸ‘2
JE WAJUA: Msichana anayeanza kushiriki Ngono katika umri mdogo, anakuwa katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi endapo atakuwa hajapata Chanjo ya #HPV?

Leo Aprili 27, 2024, Madaktari na Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (#MEWATA) watazungumza kuhusu Umuhimu wa Chanzo ya Kuzuia Saratani hiyo

Ni kupitia XSpaces ya JamiiForums kuanzia saa 10:00 Jioni. Kushiriki Mjadala Bofya https://jamii.app/HPVSpaces

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #JFAfya
πŸ‘4❀3
Saratani ya Mlango wa Kizazi inaweza kuzuilika kwa kupata Chanjo na kutibika endapo Mgonjwa atawahi Matibabu, lakini Saratani hii inabaki kuwa moja ya sababu kuu za vifo kwa Wanawake Duniani

Saratani ya Mlango wa Kizazi ni ya 4 kati ya zinazowapata zaidi Wanawake. Inakadiriwa takriban Wagonjwa wapya 604,000 wanagundulika kila Mwaka na vifo vikifikia 342,000 huku 90% ya athari zikiwa katika Nchi Masikini

Kufahamu zaidi, ungana nasi katika Mjadala kupitia XSpaces ya JamiiForums kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (#MEWATA) leo Aprili 27, 2024, Saa 10:00 Jioni

Fuata kiunganishi hiki https://jamii.app/HPVSpaces

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘3
AFYA: Chanjo ya Human Papillomavirus (#HPV) inatolewa na Serikali kwa Wasichana wenye umri wa Miaka 9 hadi 14 kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi

Saratani hiyo inaweza kuzuilika kwa kupata Chanjo na kutibika endapo Mgonjwa atawahi Matibabu

Kujua zaidi kuhusu chanjo na Ugonjwa huo, Shiriki katika Mjadala unaoendelea muda huu kupitia #XSpaces ya JamiiForums kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (#MEWATA)

Fuata kiunganishi hiki https://jamii.app/HPVSpaces

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
❀1πŸ‘1
Mkurugenzi Kinga, Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe, amesema Serikali imeamua kutoa Chanjo ya #HPV kwa kuwa Saratani ya Mlango wa Kizazi imekuwa changamoto kubwa Nchini ambayo inaongoza kwa kuwa na Asilimia 23 ya Wagonjwa tofauti na Saratani nyingine zote

Ameongeza kuwa Kutibu au kujiuguza Saratani ni gharama kubwa ndio maana Serikali imeungana na Serikali nyingine Duniani kwa ajili ya kuhamasisha kupata Chanjo ya HPV ili kujikinga

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth
πŸ‘1
Meneja wa Mpango wa Chanjo katika Wizara ya Afya, Dkt. Florian Tinuga amesema Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ilianza 2014 Mkoani #Kilimanjaro, baadaye Mwaka 2018 ikaelekezwa Nchi nzima

Ameeleza ilianza kwa dozi mbili za Chanjo kwa Wasichana wa miaka 9-14, Mwaka 2024, kwa kuzingatia tafiti ilionekana kutoa dozi moja na mbili zote ni sawa, tafiti hizo zilizofanyiwa tathmini na Shirika la Afya Duniani likatolea mwongozo wa kutolewa Dozi moja

Amesema "Kuanzia Aprili 2024 kulikuwa na mabadiliko kutoka Dozi mbili na kuwa Dozi moja. Umri umezingatiwa kwa kuwa Sayansi imeonesha kwa umri huo ni wakati ambao dozi ya chanjo inaweza kufanya kazi kwa usahihi zaidi"

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘1
Meneja Mpango wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Florian Tinuga amesema Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ni ya hiyari na salama, na kundi kubwa inawalenga Watoto ambao wapo Shule na ndio maana wakafuatwa huko

Amesema hadi kufikia Aprili 26, 2024, walengwa wa Chanjo waliofikiwa katika Chanjo hii walikuwa 90%

Ameongeza Chanjo hii itaendelea kutolewa katika vituo mbalimbali hadi Septemba 2024, pia inatolewa katika vituo vya Serikali na vile vya Binafsi

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘2
Daktari Mkufunzi kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Norman Jonas, amesema Maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi yanaweza kusambaa kwa kujamiiana na ni moja ya Magonjwa yanayotokana na Ngono na kuathiri Watu wengi
-
Amesema Virusi wa #HPV hawasababishi Saratani ya Mlango wa Kizazi pekee, wanaweza kusababisha Saratani ya Koo, Mdomo, na Uume pia
-
Amefafanua kuwa, Maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi yanaweza kusababisha maumivu ya nyonga au maumivu wakati wa tendo la Ndoa

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘1
Daktari Mkufunzi kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Norman Jonas amesema ni vizuri Mwanamke akaanza uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi mapema

Pia, amewashukuru Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (#MEWATA) kwa kuwa mstari wa mbele kuongoza kampeni ya chanjo ambayo ni hiyari na inapatikana bila malipo Nchi nzima

Ameongeza, "Utoaji chanjo wa HPV unatolewa kwa Kampeni za Kitaifa kama inavyofanyika wakati huu pia unatumia kampeni ndogondogo mfano katika maeneo kama Wilaya au Mkoa"

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘2
Dkt. Norman Jonas ambaye ni Daktari Mkufunzi kutoka Wizara ya Afya, amesema Chanjo ya #HPV ni kinga namba moja ya Saratani ya Mlango wa Kizazi, kinga namba mbili ikiwa ni kutofanya ngono wakati wa umri mdogo

Amesema "Hii kinga namba mbili ipo kimaadili zaidi, kwa kuwa inawaepusha na maambukizi mengine mbalimbali"

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘1
Mtafiti kutoka Taasisi ya #NIMR, John Changalucha amesema kulingana na utafiti uliofanyika tokea 2017 unaonesha kuwa wasichana wadogo wanapokea kinga vizuri na inaweza kufanya kazi vizuri kuliko watu wazima

Pia ameongeza kuwa wanaopewa chango ya HPV ni wasichana ambao hawajaanza kujamiiana kwasababu maambukizi hayo husambaa kwa njia ya kujamiiana

Amesema β€œChanjo kutolewa kwa wasichana zaidi ya miaka 14 inawezekana lakini lengo ni kupunguza kuwapa chanjo ambao wameanza kujamiiana”

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘2
Mtafiti kutoka Taasisi ya #NIMR, John Changalucha amesema kulingana na tafiti zilizofanyika nchini, inaonesha kuwa dozi moja ina uwezo mkubwa katika kulinda mwili dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi

Pia, amesema tafiti zilizofanywa nchini Kenya kwa wanawake wenye Umri wa miaka 36 na zaidi lakini matokeo ya cha chanjo yaliokaonesha wasichana kutoka Tanzania wana kinga zaidi yao

Ameongeza kuwa, tafiti kwa wahusika 930 waliochanjwa zinaendelea nchini Tanzania kwa mwaka wa 7 tangu walipopata chanjo hiyo na hakuna madhara yaliyojitokeza

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘2
Mtafiti kutoka Taasisi ya #NIMR, John Changalucha, amesema Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza chanjo itolewe kwa Wasichana wenye umri wa Miaka 9 hadi 20. Lakini Nchi nyingine wanatoa hata kwa wasichana zaidi ya Miaka 20.

Amesema β€œ Hakuna utafiti ulioonesha Chanjo hiyo ikitolewa kwa MSI hana mwenye umri chini ya Miaka 9 atapata madhara”.

Pia, ameongeza kuna utafiti unaoendelea wa chanjo hiyo nchini Gambia kwa wasichana wenye umri wa Miaka 5 na ikikamilika tutapata majibu.

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘1🀝1
Daktari bingwa Afya ya Jamii #JHPIEGO, Mary Rose amesema watu wenye maambukizi ya UKIMWI wako hatarini zaidi kupata maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi hasa kwa wenye miaka kuanzia 25

Ameongeza kuwa chanjo ya HPV inatolewa katika nchi zaidi ya 150 Duniani kote. β€œKwa mfano Australia wanatoa dozi ya chanjo mpaka kwa Wavulana ili kudhibiti Saratani ya kizazi.

#JamiiForums #JFXSpaces #CancerAwareness #JFAfyaJamii #AfyaBora2024 #PublicHealth #Afya
πŸ‘4❀1