AFYA: Wizara ya Afya imethibitisha uwepo wa Watu wawili wenye Maambuziki ya Ugonjwa wa Mpox waliogundulika kupitia Mifumo ya Ukusanyaji Taarifa na ufuatiliaji wa magonjwa
Taarifa ya Wizara iliyotolewa leo Machi 10, 2025 imesema kuwa mmoja wa wagonjwa hao ni dereva wa magari ya mizigo aliyetoka nchi jirani kuelekea Dar es Salaam
Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa Wananchi kujilinda dhidi ya Ugonjwa huo kwa kuwashauri kunawa mikono mara kwa mara kwa maji na sabuni au vitakasa mikono na kuwa makini wakati wa kuhudumia Wagonjwa wenye Maambukizi hayo
Soma https://jamii.app/WawiliWanaMpox
#JamiiForums #PublicHealth #MpoxCase #Afya

❤1👍1
Wizara ya Afya imesema magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi hayana tiba mahususi, ila mgonjwa anahudumiwa kulingana na dalili alizonazo, hivyo Wananchi wametakiwa kuzingatia na kuchukua hatua na tahadhari za kujikinga
Soma https://jamii.app/WawiliWanaMpox
#JamiiForums #PublicHealth #Afya
Soma https://jamii.app/WawiliWanaMpox
#JamiiForums #PublicHealth #Afya
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
IRINGA: Dkt. Godfrey Mtunzi kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa, amethibitisha uwepo wa Watu Wawili wenye dalili za kuwa na Ugonjwa wa Mpox katika Kata ya Kiesa na Kitanzini na kwamba wamefanyiwa vipimo ambavyo vimepelekwa Maabara Kuu kufanyiwa uchunguzi zaidi
Soma https://jamii.app/MpoxIringa
#JamiiForums #PublicHealth #Afya
Soma https://jamii.app/MpoxIringa
#JamiiForums #PublicHealth #Afya
Watu wenye Usonji hukabiliwa na changamoto za mawasiliano na mahusiano ya Kijamii, hivyo Mzazi/Mlezi anapaswa kuhakikisha Mtoto anapata huduma za Kitaalamu kama mazoezi ya Lugha, tabia na viungo
Aidha, mbinu mbadala za mawasiliano kama picha, ishara au teknolojia zinaweza kuwasaidia kuelewa na kujieleza
Kwa kuwa Watoto wenye Usonji mara nyingi hupenda kujitenga, Wazazi wanapaswa kuwahamasisha kushiriki katika Michezo na shughuli zinazowajenga, huku wakiwapa faraja na msaada wa kihisia
Kulea mtoto mwenye Usonji huweza kusababisha Mzazi/Mlezi kuhisi uchovu na Msongo wa Mawazo kutokana na mahitaji maalum ya Mtoto, hivyo Wazazi/Walezi wanashauriwa kushirikiana na Wazazi wengine kwa msaada wa Kisaikolojia na uzoefu
Soma https://jamii.app/UsonjiDay25
#JamiiForums #Afya #WorldAutismDay

DODOMA: Serikali imesema imefanya utafiti wa kina Nchi nzima kuhusu Saratani na imebaini upande wa Kanda ya Ziwa Saratani zinazoongoza ni ya Kibofu cha Mkojo, Mji wa Uzazi (Wanawake), Damu, Macho na Figo
Akijibu swali #Bungeni kuwa lini Serikali itatoa majibu ya tafiti za Saratani upande wa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya Saratani iliyokithiri, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema visababishi vinavyotajwa bado ni nadharia na kwamba utafiti bado unaendelea kubaini vyanzo.
Soma https://jamii.app/SarataniTaarifa
#JamiiForums #Afya #PublicHealth

DODOMA: Akijibu hoja ya Mbunge Joseph Mkundi aliyesema takwimu zinaonesha Wagonjwa wengi wa Saratani waliopo Hospitali ya Ocean Road wanatokea Kanda ya Ziwa, hivyo kushauri Serikali iboreshe Hospitali ya Rufaa ya Bugando Kitengo cha Saratani ili kusaidia mgawanyo wa Huduma, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema dhana hiyo ya utafiti sio sahihi
Dkt. Mollel amesema utafiti unaonesha Wagonjwa wengi waliopo kwenye Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini na sio Kanda ya Ziwa kama ambavyo imekuwa ikiaminika
Soma https://jamii.app/SarataniUtafitiMpya
#JamiiForums #Afya #PublicHealth
Dkt. Mollel amesema utafiti unaonesha Wagonjwa wengi waliopo kwenye Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini na sio Kanda ya Ziwa kama ambavyo imekuwa ikiaminika
Soma https://jamii.app/SarataniUtafitiMpya
#JamiiForums #Afya #PublicHealth
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema Wananchi wanaoishi Mbagala - Sabasaba, wanapata changamoto ya Mazingira kuchafuliwa na kuwa hatari kwa #Afya kutokana na Machinjio ya Ng’ombe ambayo yapo kwenye Makazi ya Watu
Anaeleza Maji machafu ambayo yanatoka kwenye Machinjio hayo tanatiririka kwenye Makazi ya Watu na hakuna jitihada zinazofanywa na Mamlaka kudhibiti hali hii, akidai hali imekuwa mbaya zaidi msimu huu wa Mvua
Soma https://jamii.app/MajiMachinjioMBG
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #PublicHealth

👍1
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change 2024, anasema ifikapo Mwaka 2035 Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa (UVIMADA), itakuwa janga kubwa zaidi kwani Tanzania imo kwenye orodha ya Nchi 14 za Kusini mwa Jangwa la Sahara zenye kiwango kikubwa cha UVIMADA
Anapendekeza uanzishwe Mfumo maalumu wa kukusanya taarifa (Kanzi Data) za Kimaabara za Wagonjwa wenye UVIMADA, utakaoratibiwa kwenye ngazi ya kanda ili kufuatilia ukubwa wa Janga, kupanga mipango Kisera na kibajeti, kuratibu tafiti pamoja na kutoa miongozo
Soma zaidi Andiko hili https://jamii.app/UVIMADASOC2024
#JamiiForums #JamiiAfrica #PublicHealth #Afya

ZANZIBAR: Mdau wa JamiiForums.com kutokea Pemba anasema kuna changamoto ya kukosekana Gari la Majitaka kwenye Mitaa yao, huku akidai kipindi hiki cha mvua, kama jitihada hazitafanyika inawezekana athari zikawa kubwa ikiwemo Majitaka kuanza kusambaa Mtaani
Soma https://jamii.app/PembaGariMajitaka
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #PublicHealth #Afya

🥴1
Taarifa ya Wizara ya Afya imesema vipimo vimeonesha hakuna kirusi kipya kinachoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha mlipuko aina ya Pandemiki. Ugonjwa wa #UVIKO19, umeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama yalivyo Magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa
Aidha, Wizara imesema hali ya kuongezeka na kupungua kwa Ugonjwa wa UVIKO-19 imekuwepo kila Mwaka tangu kutangazwa kwa Ugonjwa huu Mwaka 2020, kwa kipindi hiki ongezeko linaonekana zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam
Pia, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Nchi, hususan katika Mikoa ya Pwani, kumekuwa na ongezeko la hatari ya kuenea kwa Magonjwa yanayoenezwa na Mbu, kama vile Homa ya Dengue, Malaria, na Magonjwa mengine ya aina hiyo.
Soma zaidi https://jamii.app/OngezekoUvikoMbu

👍2
AFYA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza anakunywa Soda Nne aina ya Cola kwa siku, Mtaalam wa #Afya ameeleza unywaji wa soda na vitu vingine vya Sukari kwa wingi inasababisha hatari ya kupata magonjwa kama Kisukari, anashauri ni vyema kuepuka vitu hivyo kwa wingi ikiwemo juisi, energy drinks n.k.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Figo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mlonganzila, Dkt. Anthony Gyunda anaeleza “Matumizi mengi ya Sukari yanasababisha uraibu, hiyo pia ipo katika vinywaji vya chupa na makopo sababu vinatunzwa kwa kuweka ‘preservatives’ ambazo zingine zinaleta uraibu kama Dawa za Kulevya tu.”
Kuhusu kuachana na uraibu huo, Dkt. Gyunda anasema “Kuondokana na Uraibu wa Sukari ni sawa tu na Uraibu mwingine kama wa Dawa za Kulevya, ushauri nasaha, maamuzi ya muathirika mwenyewe na matumizi ya dawa za kukakata uraibu.”
Soma https://jamii.app/UnywajiSoda
#JamiiForums #PublicHealth #JFMdau2025 #JamiiAfrica

RUVUMA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mmalaka husika kurekebisha mazingira ya Vyoo vya Shule ya Msingi Miembeni, iliyo Kata ya Msamala, Manispaa ya Songea
Amedai hali ya uchafu wa Vyoo hivyo, inaweza kusababisha mlipuko wa Magonjwa, hivyo kuhatarisha afya za Walimu na Wanafunzi wa Shule hiyo
Soma https://jamii.app/ShuleYaMiembeni
#JamiiForums #PublicHealth #Afya #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji

❤2
Siku ya Baiskeli Duniani huadhimishwa kila Mwaka Juni 3 na ilianzishwa rasmi na Umoja wa Mataifa (UN) Mwaka 2018, kwa kutambua umuhimu wa Baiskeli kama chombo cha Usafiri, Burudani na #Afya
Siku hii inaenzi Baiskeli kama njia rafiki kwa Mazingira kwasababu haizalishi Hewa chafu na hupunguza Msongamano wa foleni za Magari
Inasisitiza Afya na Maisha bora kwani kuendesha Baiskeli husaidia kudhibiti uzito, kupunguza hatari ya Magonjwa ya Moyo na Kisukari. Pia, ni njia ya Usafiri inayopatikana kwa Watu wengi kwa gharama ndogo na inafika hata maeneo ya Vijijini.
Vipi Mdau, Baiskeli yako ya kwanza uliimiliki ukiwa na Umri gani?
Soma https://jamii.app/WorldBicycleDay2025
#JamiiForums #JamiiAfrica #WorldBicycleDay2025 #PublicHealth

Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia kero ya mazingira duni ya vyoo vya Stendi Kuu ya Mkanaledi ya Mtwara, akidai hali hiyo inahatarisha #Afya za Watumiaji na wanavyovizunguka
Soma https://jamii.app/VyooVichafuMkanaledi
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025

❤1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema walipokaa muda mrefu kusubiri Huduma ya 'Ambulance' katika Hospitali ya Amana, walimuhoji mmoja wa Wahudumu ili kufahamu Changamoto ni nini na aliwaambia Hospitali hiyo ina Gari mbili tu za Wagonjwa na Dereva yupo mmoja
Pia, ameomba Uongozi wa Hospitali uangalie ‘customer care’ ya Wauguzi, wana majibu ya ovyo sana na yanayokera, utadhani umeenda Hospitali kuomba msaada wakati ile ni Huduma na wao wapo kazini
Soma zaidi https://jamii.app/HudumaAmbulanceAmana
#JamiiForums #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #PublicHealth #Afya

Utafiti mpya uliochapishwa katika Jarida la The Lancet Global Health na kikundi cha Watafiti kutoka Marekani na Afrika umefichua tatizo linalotia wasiwasi mkubwa, ambapo karibu Dawa moja kati ya sita (Asilimia 17) za Saratani zinazopatikana Nchini Ethiopia, #Kenya, Malawi na #Cameroon ni bandia au zina Viambato visivyo sahihi
Watafiti walikusanya taarifa za vipimo vya Dozi, mara nyingine kwa siri, kutoka Hospitali 12 na Maduka ya Dawa 25 katika Nchi hizi nne, wakipima takriban bidhaa 200 tofauti za Dawa za Saratani kutoka chapa mbalimbali. Matokeo yanaonesha hata bidhaa zinazotumika katika Hospitali kubwa zilikuwa na kasoro
Athari kwa Wagonjwa ni kubwa. Wale wanaopokea dozi zisizotosheleza Viambato muhimu wanaweza kuona Uvimbe wao ukiendelea kukua na hata kuenea, badala ya kudhibitiwa au kupunguza kama ilivyokusudiwa.
Soma zaidi https://jamii.app/DawaBandiaSaratani
#JamiiForums #JamiiAfrica #Afya #PublicHealth

GEITA: Mdau ametoa wito kwa mamlaka kushughulikia utupaji ovyo wa taka kwenye Makazi ya Watu, Mtaa wa Ntengere, Kata ya Igulwa, Ushirombo ambao umegeuza eneo hilo kuwa 'dampo' akidai ni hatari kwa #Afya
Anashauri kuwepo na utaratibu maalum wa kudumu wa usimamizi wa taka, pia eneo hilo kurejeshwa kwenye matumizi yake ya awali kama Makazi au Ofisi za Umma
Zaidi soma https://jamii.app/DampoUshirombo
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #JFMdau2025 #PublicHealth

DODOMA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Uongozi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Nanenane kushughulikia hali ya vyoo kituoni hapo, akidai mazingira yalivyo sio salama kwa #Afya za Watumiaji.
Anadai Vyoo vya upande wa Wanaume mazingira yake siyo mazuri na kuwa sehemu za haja ndogo miundombinu haijakaa sawa licha ya kuwa kila Mtumiaji analipia Tsh. 300 kupata huduma, anahoji mapato yanafanya kazi gani?
Anadai kwa ujumla hali ya usafi ni changamoto, pia maji yanayotumika yapo kwenye ndoo yametuama na kwamba upande wa Choo cha Watu Wenye Ulemavu kimefungwa, hakitumiki.
Soma Zaidi https://jamii.app/KituoMbasiDodoma
#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFMdau2025 #PublicHealth

Ili kujenga #Afya yako jaribu kuacha tabia kwa kuanza kufanya maamuzi madogo kila siku
Tembela https://jamii.app/JukwaaJamiiForums
#JamiiAfrica #JamiiForums
#AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha

❤2👏1
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka kuwasaidia Wafanyabiashara wa Buguruni hususani katika kipande cha barabara kinachoelekea Buguruni kwa Mnyamani, akidai ujenzi unaoendelea wa barabara ya Mwendokasi, Mkandarasi anamwaga maji upande wa Barabara ya Mandela na Uhuru lakini upande wa Mnyamani hafanyi hivyo.
Anasema, vumbi linalotoka hapo linaathiri #afya na biashara katika maeneo hayo, na kwamba hali hiyo imedumu kwa muda wa mwezi sasa.
Zaidi Soma https://jamii.app/BuguruniMnyamaniVumbi
#JamiiAfrica #JamiiForums #ServiceDelivery #Uwajibikaji #ServiceDelivery #JFHuduma