JamiiForums
โœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Uwekaji wa Tarehe sahihi unapotoa Taarifa au kueleza Tukio ni sehemu muhimu ya Muktadha wa Taarifa yoyote

Husaidia Jamii kuelewa uhalisia wa Muda wa tukio hilo hata baada ya muda wake kupita ili kuepusha taharuki

Ikiwa umepata taarifa ya tukio na ukashindwa kujua ni ya lini, iwasilishe katika Jukwaa la JamiiCheck.com kwa Msaada zaidi

Soma https://jamii.app/TareheYaTaarifa

#JamiiForums #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
โค1๐Ÿ‘1
Akiwa katika Kongamano la Kujadili Tasnia ya Habari kuelekea Uchaguzi, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani, Kalisha Holmes amesema "Mitandao ya Kijamii imefanya baadhi ya mambo kuwa na nguvu kuliko tulivyotarajia, yamekuwa yakisambaa kwa kasi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma"

Ameongeza "Tumeingia katika nyakati ambazo Wananchi wetu wanahitaji kuelewa umuhimu wa taarifa ambazo zimehakikiwa, kwani chombo cha Habari kikiwa huru kinakwepa kulaghaiwa"

Soma https://jamii.app/UTPCMkutano

#JamiiForums #PressFreedom #Democracy #CivilRights #UsawaHakiUwajibikaji #FactsCheck
๐Ÿ‘2๐Ÿ‘Ž1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo amesema baada ya kutembelea Mikoa tofauti ya Tanzania Bara na Visiwani, lilipatikana wazo la kuja na mfumo wa uhakiki wa taarifa, ndipo ikawa mwanzo wa kuanzishwa kwa JamiiCheck ambayo ilizinduliwa Mwaka 2022

Amesema JamiiCheck.com imekuwa msaada mkubwa kwa Wananchi wanaohitaji kuhakiki taarifa mbalimbali na kueleza kuwa ndani ya Miaka miwili kumefanyika uhakiki wa maudhui zaidi ya 600

Maxence ameyasema hayo wakati akichangia mada katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari, Juni 18, 2024 Jijini Dar es Salaam, ambapo Kauli Mbiu inaeleza โ€œJenga mustakabali endelevu kwenye Sekta ya Habari katika zama za Kidigitali.โ€

Soma https://jamii.app/SektaYaHabari

#JamiiCheck #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
๐Ÿ‘3โค1
Ni muhimu kila Mwanajamii kufanya jitihada binafsi kujifunza mbinu mbalimbali za kufanya Uhakiki wa Taarifa ili kuweza kuzibaini #TaarifaPotofu

Tembelea sasa JamiiCheck.com, Jukwaa linalohakiki Taarifa na kutoa mafunzo ya msingi ya namna ya kufanya Uhakiki wa Taarifa mbalimbali

#JamiiCheck #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
๐Ÿ‘2
JamiiForums kwa kushirikiana na #CIPESA kupitia Mfuko wa Haki za Kidijitali wa Afrika (The Africa Digital Rights Fund - ADRF) wameendesha mafunzo ya Uhakiki wa Taarifa kwa Wadau wa Tasnia ya Habari, Julai 26, 2024 Jijini Dar es Salaam

Lengo la mafunzo hayo ni sehemu ya kuwajengea uwezo katika majukumu kwa kuweza kutambua taarifa potofu pamoja na athari zake hususan kwenye kipindi cha #Uchaguzi na namna wanavyoweza kutumia ujuzi na nyenzo mbalimbali kuzihakiki

Washiriki walipata fursa ya kujifunza jinsi JamiiForums inavyopambana na taarifa potofu kupitia Jukwaa la JamiiCheck.com ambalo huwashirikisha Wananchi katika mchakato wa kuhakiki maudhui yanayopatikana ndani na nje ya Mtandao

Zaidi soma https://jamii.app/JamiiForumsMafunzoUhakikiTaarifa

#JamiiForums #InformationFactChecking #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
๐Ÿ‘3
JamiiForums kwa kushirikiana na #CIPESA kupitia Mfuko wa Haki za Kidijitali wa Afrika (The Africa Digital Rights Fund - ADRF) wameendesha mafunzo ya Uhakiki wa Taarifa kwa Wadau wa Tasnia ya Habari, Agosti 23, 2024 ambayo yalifanyika Dar es Salaam

Washiriki wamejifunza jinsi #JamiiForums inavyopambana na #TaarifaPotofu kupitia Jukwaa la JamiiCheck.com ambalo huwashirikisha Wananchi katika mchakato wa kuhakiki maudhui yanayopatikana ndani na nje ya Mtandao

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea Washiriki uwezo katika majukumu yao, kwa kuweza kutambua taarifa potofu pamoja na athari zake, hususan katika kipindi cha Uchaguzi na namna wanavyoweza kutumia Ujuzi na nyenzo mbalimbali kuzihakiki

Zaidi Soma https://jamii.app/UhakikiWaTaarifa

#InformationFactChecking #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
๐Ÿ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mdau wa JamiiCheck.com alitaka kufahamu Uhalisia wa Video inayosambaa katika Mitandao ya Kijamii ikimuonesha Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA (Bara), Tundu Lissu akizomewa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Septemba 11, 2024

#JamiiCheck imefanya Uhakiki wa Video hiyo na kubaini kuwa imehaririwa kwa kuongezewa sauti zinazosikika zikisema "Toka wee, Yuda huyo, tunamtaka Mwenyekiti" ambazo hazipo kwenye Video Halisi ya mkutano huo uliorushwa mbashara kupitia baadhi ya chaneli za Youtube.

Soma https://jamii.app/TunduLissuMkutanoni

#JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck #MisDis04
๐Ÿ‘2
Mdau wa JamiiCheck.com alihitaji kufahamu Uhalisia wa chapisho linalosambaa mtandaoni linalodaiwa kuwa la #TheChanzo likionesha kuwa Mwenyekiti wa #CHADEMA, Freeman Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuungana na CHADEMA kuomboleza kifo cha Mzee Ali Kibao

Ufuatiliaji wa #JamiiCheck kwa kutumia #GoogleReverseImage umebaini kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli na haijachapishwa katika kurasa rasmi za Mitandao ya Kijamii ya The Chanzo. Pia, kupitia kurasa zake, The Chanzo imekanusha kuhusika na Taarifa hiyo

Aidha, JamiiCheck imebaini uwepo wa utofauti wa Nembo inayotambulisha mtandao wa X ambapo chapisho hilo limetumia nembo ya zamani ya alama ya Ndege wakati mtandao huo ukijulikana kama #Twitter tofauti na The Chanzo ambao hutumia nembo yenye herufi X

Soma https://jamii.app/MboweAmshukuruSamia

#JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck #MisDis04
๐Ÿ‘3๐Ÿ‘1
Mdau wa JamiiCheck.com ametaka kupata uhalisia wa barua inayosambaa Mtandaoni ikidaiwa kuandikwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) inayobainisha Mipango ya Siri kuelekea Maandamano yaliyopangwa kufanywa na chama hicho Septemba 23, 2024

Ufuatiliaji wa #JamiiCheck umebaini barua hiyo imetengenezwa na haijatolewa na CHADEMA kama inavyodaiwa. Uchunguzi wetu umebaini barua hiyo kukosa vipengele muhimu ikiwemo Saini na Tarehe ya kuandikwa kwake. Pia, Barua hiyo haina 'Letterhead' ya CHADEMA na ina makosa mengi ya kiuandishi.

Aidha, Chanzo cha kuaminika cha JamiiCheck ndani ya CHADEMA kimethibitisha kuwa barua hii haijatolewa na chama hicho na kimesisitiza kuwa kikundi cha #RedBrigade kilichotajwa hakiruhusiwi kuwepo kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura namba 258 iliyofanyiwa Marejeo mwaka 2019 chini ya kifungu cha 8E (1)

Soma https://jamii.app/MaandamanoCHADEMA

#FactsCheck #HakikiTaarifa #Misinformation #Disinformation #MisDis04
๐Ÿ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika hafla ya Utoaji wa Tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania, (#EJAT), Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, ametoa wito kwa Jamii kuwa makini na matumizi ya Akili Mnemba (AI), ili kuondoa Upotoshaji, Uzushi na kuepuka kusababisha taharuki

Soma https://jamii.app/EJATAwards2024

#JamiiForums #JFMatukio #EJATAwards #UhuruWaHabari #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
Uvumi wa Taarifa zisizo za Kweli kuhusu Afya unaweza kuwafanya Wananchi kupuuza ushauri wa wataalamu, hali inayoweza kusababisha madhara makubwa kwa afya za Watu.

Hakikisha Unathibitisha Taarifa zinazogusa Sekta ya Afya kabla ya kuziamini ili Kuhakikisha usalama wako na Jamii kwa ujumla

Soma https://jamii.app/ThibitishaKablaHujaamini

#VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis04
Upotoshaji hufanyika kwa njia nyingi ikiwemo kusambazwa kwa jumbe zinazodaiwa kuwa ni zawadi kutoka kwa Mashirika ya Kimataifa.

Ukutanapo na Taarifa za aina hii hakikisha Unathibitisha kuona kama ni Kweli imetolewa na chanzo husika ili kufanya maamuzi yaliyo sahihi na kujiepusha na #Upotoshaji.

Tumia Jukwaa la JamiiCheck.com kupata Uhalisia wa Taarifa mbalimbali.

Soma https://jamii.app/ZawadiMashirikaYaKimataifa

#VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis05
โค1
Ni muhimu kuthibitisha Picha unazokutana nazo Mtandaoni zikihusishwa na Matukio tofautitofauti ili kupata Uhalisia wake kabla ya kuendelea kuwasambazia wengine kwani baadhi ya Watu hutumia Picha za Matukio ya zamani kupotosha Umma

Kumbuka unapofanya Uhakiki wa maudhui unawalinda Watu wengi dhidi ya Upotoshaji unaosambaa ndani na nje ya Mtandao.

Soma https://jamii.app/ThibitishaPicha

#VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis05
Kumekuwapo na Jumbe zinazotumwa katika Makundi Sogozi ya #WhatsApp na Mitandao mingine ya kijamii zinazoelekeza kubofya 'Links' (Viungo) ili upate zawadi ya MB ama Pesa

Link hizo mara nyingi zimekuwa si salama zikiwa na lengo la kulaghai na kuchukua Taarifa zako na wakati mwingine kupelekea Udukuzi wa Akaunti yako

Thibitisha links za aina hiyo kila unapokutana nazo ili kuepuka kupotoshwa. Hakikisha pia huendelei kusambaza links za aina hiyo ili kuwalinda wengine.

Soma https://jamii.app/LinksZaOfaNaZawadi

#VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis05
Upotoshaji umekuwa ukifanyika katika namna tofauti tofauti ikiwemo kuhariri Maudhui halisi yaliyo kwenye grafiki na kuleta maana tofauti.

Ili kuthibitisha uhalisia wa grafiki unayoitilia mashaka, angalia utofauti katika aina ya mwandiko(Fonts), maneno kupishana, au tafuta chanzo halisi kuona iwapo wamechapisha grafiki hiyo.

Unaweza pia kutumia Jukwaa la JamiiCheck.com kuwasilisha Taarifa unazohitaji uhalisia wake.

Soma https://jamii.app/GrafikiKuhaririwa

#VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis05
๐Ÿ‘1
Wakati wa uchaguzi, Taarifa Potofu zinaweza kusambazwa kwa kutumia vipande vya Video ili kuwasafisha au kuwachafua wanasiasa. Hakikisha Unathibitisha kila Taarifa kabla ya Kuiamini.

Tumia jukwaa la JamiiCheck.com kujifunza namna ya Kuthibitisha Maudhui ya Video, na kupata msaada wa Uhakiki kwa Taarifa zinazokutia mashakani.

Soma https://jamii.app/ThibitishaKipandeChaVideo

#VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis05
ARUSHA: Akizungumzia kuhusu kuwawezesha Wanawake kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 katika masuala ya Uhakiki wa Taarifa, Mkurugenzi Mtendaji wa #JamiiAfrica, Maxence Melo amesema Taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wadau wa Habari Wanawake na programu hizo zimekuwa zikiendelea

Amesema โ€œTulikuwa na Mradi maalumu pamoja na WiLDAF kuhusu kuwajengea uwezo Wanawake, pia kama kuna mapendekezo mengine yoyote kutoka kwa Wadau tupo tayari kuyapokea na ikiwezekana kushirikiana nao.โ€

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis04
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema Waandishi wa Habari wanao wajibu wa kusaidia umma kubaini Taarifa za ukweli na uongo, na wanaweza kutumia Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kuongeza tija licha ya kuwa nayo inachangia kuzalishwa kwa Taarifa za uongo

Ameyasema hayo Mei 2, 2025 katika mafunzo ya Siku moja ya Wanahabari 150, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambayo inaadhimishwa Mei 3, ambapo Kaulimbiu ya Mwaka 2025 ni โ€œUhabarishaji kwenye Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba/Unde kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari.โ€

Aidha, ametoa kongole kwa #JamiiAfrica ambayo imekuwa ikishughulikia kubaini Taarifa sahihi na zisizo sahihi kupitia Jukwaa la #JamiiCheck

Soma https://jamii.app/WPFD2025

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis04
DAR: Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (#UTPC), Kenneth Simbaya amesema kuelekea katika #UchaguziMkuu2025, taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Wadau mbalimbali kutoa elimu ya masuala ya taarifa potofu ili kuhakikisha Jamii inapata taarifa sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi pia.

Amesema โ€œKatika kutekeleza hilo tunashirikia na Wadau kuhakikisha Wanahabari wanakuwa Watu wa kwanza kutoa taarifa sahihi, baadhi ya Wadau tunaoshirikiana nao ni #JamiiAfrica katika kutoa elimu kwa Wanahabari na Wananchi kuhusu umuhimu wa Uhakiki wa Habari na njia za kuhakiki taarifa mbalimbali.โ€

Amesema hayo wakati akifanya wasilisho la Mada katika Mkutano wa Wadau kujadili mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025, leo Julai 9, 2025, ambapo ameongeza kuwa kuruhusu kusambaa kwa taarifa potoshi inaweza kuchangia kuharibu mchakato wa uchaguzi.

Zaidi soma https://jamii.app/UTPCNaJamiiAfrica

#HakikiTaarifa #JamiiForums #Democracy #FackChecking #FactsCheck
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa wito kwa Wanahabari kuwa na kawaida ya kuhakiki Taarifa kabla ya kusambaza kama ambavyo imekuwa ikifanywa na JamiiCheck.com

Msigwa amezungumza hayo wakati akichangia mada katika Mkutano wa Wadau kujadili Mchango wa Sekta ya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, leo Julai 9, 2025

Amesema โ€œNimeona Watu wa JamiiForums wana kitu kinaitwa JamiiCheck, wanachofanya ndio kilekile tulichojifunza shuleni kwamba unachotaka kukichapisha jiridhishe kuwa ni sahihi?โ€

Soma https://jamii.app/MsigwaOnJamiiCheck

#JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck
โค2