JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kutokana na Maendeleo ya Sayansi na #Teknolojia kumeibuka 'Application' nyingi za kutengeneza Picha, ambazo zinaweka kubadili Uhalisia wa Picha

Upotoshaji katika Picha huweza kufanyika kwa kubadili rangi, Mavazi, kubadili Mazingira, kuunganisha Picha mbili tofauti, kubadilisha muktadha au kuwashikisha wahusika vifaa n.k

Kufahamu zaidi tembelea Jukwaa letu la #JamiiCheck ndani ya JamiiForums.com

Soma https://jamii.app/UpotoshajiPicha

#FactChecking #Misinformation #InformationFactChecking #DigitalWorld #JamiiForums
👍1
Upotoshaji kwa kutumia Jina ni kitendo cha kutumia jina la Mtu, Kundi, Taasisi au Kampuni kwa lengo la kujinufaisha au kujiingizia kipato

Pia, hutumika kwa lengo la Kuchafua jina la Mtu au Heshima yake kwa jamii. Utumiaji huu hufanyika kwa kutumia jina fulani kuweka Maudhui yasiyokubaliwa na Jamii

Hivyo, ni muhimu unapotafuta jina la Mtu katika Mitandao ya Kijamii hakikisha akaunti yake ni halisi

Soma zaidi https://jamii.app/UpotoshajiJina

#JamiiForums #JamiiCheck #InformationFactChecking
👍5
JamiiForums kwa kushirikiana na #CIPESA kupitia Mfuko wa Haki za Kidijitali wa Afrika (The Africa Digital Rights Fund - ADRF) wameendesha mafunzo ya Uhakiki wa Taarifa kwa Wadau wa Tasnia ya Habari, Julai 26, 2024 Jijini Dar es Salaam

Lengo la mafunzo hayo ni sehemu ya kuwajengea uwezo katika majukumu kwa kuweza kutambua taarifa potofu pamoja na athari zake hususan kwenye kipindi cha #Uchaguzi na namna wanavyoweza kutumia ujuzi na nyenzo mbalimbali kuzihakiki

Washiriki walipata fursa ya kujifunza jinsi JamiiForums inavyopambana na taarifa potofu kupitia Jukwaa la JamiiCheck.com ambalo huwashirikisha Wananchi katika mchakato wa kuhakiki maudhui yanayopatikana ndani na nje ya Mtandao

Zaidi soma https://jamii.app/JamiiForumsMafunzoUhakikiTaarifa

#JamiiForums #InformationFactChecking #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
👍3
JamiiForums kwa kushirikiana na #CIPESA kupitia Mfuko wa Haki za Kidijitali wa Afrika (The Africa Digital Rights Fund - ADRF) wameendesha mafunzo ya Uhakiki wa Taarifa kwa Wadau wa Tasnia ya Habari, Agosti 23, 2024 ambayo yalifanyika Dar es Salaam

Washiriki wamejifunza jinsi #JamiiForums inavyopambana na #TaarifaPotofu kupitia Jukwaa la JamiiCheck.com ambalo huwashirikisha Wananchi katika mchakato wa kuhakiki maudhui yanayopatikana ndani na nje ya Mtandao

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea Washiriki uwezo katika majukumu yao, kwa kuweza kutambua taarifa potofu pamoja na athari zake, hususan katika kipindi cha Uchaguzi na namna wanavyoweza kutumia Ujuzi na nyenzo mbalimbali kuzihakiki

Zaidi Soma https://jamii.app/UhakikiWaTaarifa

#InformationFactChecking #FactsChecking #FactsCheck #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
👍2
Juni 16 hadi 20, JamiiAfrica iliendesha mafunzo kwa vitendo kwa Maafisa wa TAKUKURU kuhusu Usimamizi, Matumizi, Usalama na Utengenzaji wa Maudhui katika Mitandao ya Kijamii yaliyofanyika Dar es Salaam

Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo katika matumizi ya majukwaa mbalimbali ya Mitandao pamoja na uhakiki wa Taarifa Mtandaoni kwa ajili ya Mawasiliano ya Umma

Washiriki walijifunza namna ya kuandaa maudhui bora na kutumia zana tofauti ili kuendesha shughuli za kila Siku Mtandaoni. Pia, walipata Maarifa kuhusu kupanga Maudhui ya Wiki na kujilinda dhidi ya hatari za Usalama wa Kidigitali

#JamiiForums #JamiiAfrica #DigitalRights #SocialMediaManagement #InformationFactChecking