JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Baruani Mshale (Twaweza): Hatuwezi tukafikia mahali ambapo tutaondoa sintofahamu kwa 100%

Hatuwezi kusubiri katika kuandaa Sera na Sheria za kusimamia Teknolojia mpya wakati maendeleo ya Kiteknolojia hayatusubiri

Tuendelee kutengeneza na kuboresha kadri tunavyoendelea kupata taarifa

#JamiiForums #DigitalRights #AccessToInformation #FactChecking #CSOWeek2023
👍1
Kutokana na Maendeleo ya Sayansi na #Teknolojia kumeibuka 'Application' nyingi za kutengeneza Picha, ambazo zinaweka kubadili Uhalisia wa Picha

Upotoshaji katika Picha huweza kufanyika kwa kubadili rangi, Mavazi, kubadili Mazingira, kuunganisha Picha mbili tofauti, kubadilisha muktadha au kuwashikisha wahusika vifaa n.k

Kufahamu zaidi tembelea Jukwaa letu la #JamiiCheck ndani ya JamiiForums.com

Soma https://jamii.app/UpotoshajiPicha

#FactChecking #Misinformation #InformationFactChecking #DigitalWorld #JamiiForums
👍1
Baada ya kuwepo mkanganyiko kuhusu athari za Matumizi ya Bangi kwenye Afya ya Binadamu, #JamiiCheck imefanya uhakiki juu ya suala hilo na kubaini baadhi ya athari za Bangi kwa Watumiaji ni pamoja na kuwa hatarini kupata Shambulio la Moyo na Kiharusi (Stroke)

Utafiti wa Mamlaka Udhibiti wa Dawa na Chakula ya Marekani (FDA) umeonesha Bangi ina Kemikali zaidi ya 100 zinazofahamika kama #Cannabinoids zenye athari tofauti mwilini, Kemikali 2 tu ndio zimetajwa kutumika kwenye baadhi ya Dawa kutibu #Saratani, Degedege, Shinikizo la Juu la Macho n.k

Kemikali zilizosalia zimetajwa kuwa na athari hasi kwa Binadamu ambapo Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Moyo ya Marekani (AHA) ulibaini 34% ya Watumiaji 150,000 walikutwa na Shambulio la Moyo na dalili za Kiharusi

Soma https://jamii.app/BangiMoyo

#JamiiForums #PublicHealth #JFAfya #JamiiCheck #FactChecking #HakikiHabari #JFAfyaJamii
👍31
Kumekuwapo Imani katika Jamii kwamba ukivaa Nguo nyekundu wakati wa Mvua unakuwa katika hatari ya kupigwa na Radi

Jukwaa la JamiiCheck.com limepitia tafiti mbalimbali za masuala ya Hali ya Hewa ambao wanasema hakuna uhusiano wowote kati ya Radi na Rangi ya Nguo

Aidha, Mazingira ya kupigwa na Radi yanategemea zaidi kama umekaa kwenye vitu virefu kama Miti, Milima, Minara n.k.

Soma https://jamii.app/NguoNyekunduRadi

#JamiiForums #Misinformation #Disinformation #VisitJamiiCheck #HakikiTaarifa #FactChecking
👍42
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Mobhare Matinyi amesema ili kufikisha taarifa sahihi kwa Jamii kuna umuhimu wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo kuwa na utaratibu wa kuhakiki Taarifa (#FactChecking)

Ameyasema hayo wakati akichangia mada katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari, Juni 18, 2024 Jijini Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/SektaYaHabari

#JamiiForums #JFUwajibikaji #PressFreedom #PressFreedom24
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo atakuwa Mzungumzaji katika Mkutano wa 14 wa Chama cha Mawasiliano cha Afrika Mashariki (EACA) kupitia Mjadala unaoratibiwa na JamiiForums na Twaweza.

Maxence anatarajiwa kuchambua nafasi ya Ubunifu unaolenga Wananchi katika kuchochea Uwajibikaji wa Serikali Nchini na kufafanua mikakati ya JamiiForums katika kudumisha uaminifu na kujenga imani katika nyakati za ambazo jamii inakabiliwa na ongezeko la Taarifa za Upotoshaji

#JamiiForums #EACA2024 #DigitalRights #HakiZaDijitali #JamiiCheck #FactChecking
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#DIGITALI: Jukwaa la Kidigitali katika Uhakiki wa Taarifa la #JamiiCheck linaloendeshwa na #JamiiForums limeshinda Tuzo ya U.S.-Tanzania Tech Challenge iliyokuwa ikiwaniwa na Taasisi 113 za Kiteknolojia kutoka Tanzania

Shindano hilo liliandaliwa na Marekani kupitia Ubalozi wake nchini ambapo JamiiForums kupitia Mradi wake wa "Mwananchi Makini" inalenga kuhakikisha Wananchi wanakuwa na Taarifa Sahihi ili kufanya Maamuzi Sahihi wakati wa Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025

Ikumbukwe, JamiiCheck inawapa Wananchi fursa ya kuwasilisha taarifa ambazo hazijathibitishwa, kushiriki katika mchakato wa kuzihakiki na kupokea tathmini ya ukweli wake ndani ya muda mfupi

Soma https://jamii.app/USTechChallenge

#JamiiForums #JamiiCheck #JFDigitali #FactChecking #Accountability #DigitalRights #USTZTech
🔥3
ARUSHA: Kuna changamoto ya baadhi ya Taasisi za Serikali kushindwa kuwa ‘Active’ katika kujibu kwa wakati kuhusu taarifa mbalimbali zinazokuwa zinasambaa Mtandaoni

Hayo yamesemwa na Nuzulack Dausen kutoka Nukta Africa ambaye ameongeza kuwa “Wanapofanya hivyo kuna Watu wanaweza kuwa wanaumizwa na Taarifa au Matukio yanayosambazwa kama hayana ukweli au hajayafafanuliwa.”

Amesema “Nadhani hiyo ni changamoto ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi kwa maana ya kwamba wahusika wawe wanajibu au wanatoa ushirikiano haraka wakati wa mchakato wa kuhakiki taarifa.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa #JamiiAfrica, Maxence Melo anasema “Katika kufanikisha elimu ya kukabiliana na taarifa potofu, tumewajengea uwezo Wadau wa Habari kukabiliana na changamoto ya taarifa potofu, tumekuwa tukifanya hivyo kwa Wadau mbalimbali.”

Ameongeza "Tuliamua kufanya uwezeshaji kwa Wadau wa Habari kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kwa zaidi ya Wanahabari 1,000.”

Ameongeza “JamiiAfrica iliingia makubaliano na redio mbalimbali za Kijamii kutoka katika Mikoa tofauti kwaajili ya kuwapa elimu ya masuala ya uhakiki wa Habari na ni mchakato ambao bado unaendelea.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Akizungumzia suala la uhakiki wa Taarifa, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema kupitia JamiiCheck.com wanashirikiana na Wanachi kuwaonesha kile kinachofanyika kwa kuwa ni sehemu ya Elimu ya kuelewa mchakato wa uhakiki wa Taarifa potofu

Ameongeza “Tunafanya kwa kushirikiana na Jamii kwa kuwaeleza na pia hata kwa Wanahabari na Wananchi wengine wana nafasi ya kushiriki ndani ya JamiiCheck kuhakiki taarifa kwa kuwa ni Jukwaa ambalo linawashirikisha Watumiaji.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, amesema Uwepo wa Sheria sio Mwarobaini wa taarifa za uzushi, kwani tukifanya hivyo Watu wengi watakamatwa na watawajibishwa

Ameongeza “Jambo muhimu ni kutoa Elimu kwanza kwa Jamii, kuna mambo mengi yanafanyika kutokana na Watu kutokuwa na Taarifa sahihi. Hivyo, Serikali na Wadau kwa pamoja wanatakiwa kushirikisha Wananchi

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Alphonce Shiundu, Mhariri Africa Check ya Kenya anasema wakati wa Uchaguzi mara nyingi Vyama na Wadau wa Siasa hutumia Fedha nyingi kusambaza uzushi, wanaweza kutumia njia mbalimbali ili kukamilisha jambo lao la kusambaza taarifa za propaganda

Ameongeza kuwa wakati mnapokuwa mnatengeneza Maudhui ni vizuri kuwa na mpango mkakati wa kudhibiti Taarifa hizo kwa kuwa taarifa nyingi za uzushi huwa zinavutia

Shiundu anasema ni vizuri kufikiria kuhusu njia sahihi na nzuri za kukabiliana na Taarifa potofu hasa wakati wa Uchaguzi

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Mwanahabari ambaye unajihusisha na uhakiki wa Habari hautakiwi kuegemea katika kitu kimoja au njia ile ile wakati unapofanya uhakiki wa Taarifa, unatakiwa kujiongezea Uwezo ili uweze kwenda mbele zaidi ya Akili Mnemba (AI)

Reagan Kiyimba kutoka Media Initiative (Uganda) amesema hayo na kuongeza kuwa Waandishi wa Habari wanapaswa kuboresha ujuzi wao ili wawe hatua moja mbele ya yanayopangwa wakati wa Uchaguzi, ikiwemo matumizi mabaya ya AI na Teknolojia nyingine mpya zinazoibuka

Amesema “Kabla ya kufuatilia Taarifa uwe unajua mambo ya muhimu kwa kuwa vitu vinabadilika. Pia, unaweza kushirikiana na Taasisi mbalimbali ndani na nje ya Nchi yako ili kupata Elimu zaidi, Mwanahabari wa Kuhakiki Taarifa ujuzi wako unatakiwa uwe unaboreshwa kila mara.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa anasema “Fact Checking ni msingi mzuri sana kwa Mwanahabari. Kuna namna mbili za kuifanyia kazi, kwanza ni mbinu za kiuandishi wa Habari na pili njia za Kidigitali ili kupata ukweli.”

Amesema “Tunalazimika kutoa mafunzo ya uhakiki kwa Wanahabari kutokana na kwamba Mitaala haina mafunzo ya nyenzo za Kidijitali za kufanya uhakiki.”

Anaongeza “Tulichelewa hapo kati kuingiza suala la Uhakiki wa Habari katika masomo yetu ya Habari, lakini kuongezeka kwa Habari potoshi hasa za Kijamii ndio kumezidi kuleta uhitaji kwenye tasnia ya Habari.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Kuna wakati Utani unaweza kwenda tofauti na vile ambavyo Watu walitarajia, kuna vitu vinaweza kufanyiwa utani na Watu wakaamini kuwa kilichoandikwa au kuchapishwa ni cha kweli

Hayo yamesemwa na Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa ambaye amesema “Kuna maelekezo kuwa unapotengeneza Maudhui unatakiwa kuweka angalizo la kuwa unachokifanya ni Utani lakini sidhani kama Watu wote wanazingatia hilo, matokeo yake kile kinachochapishwa kinasambaa na kuaminika.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema “JamiiAfrica ipo tayari kuwapokea Watu kutoka Vyuoni kuwajengea Uwezo wa masuala ya Uhakiki wa Taarifa kwa Wanahabari, tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ni wakati muhimu ambao tunaweza kutoa Elimu hiyo.”

Ameongeza “Tuna Mkataba wa ushirikiano na Vyuo kadhaa ikiwemo UDSM, SAUT na UDOM. Tunapoelekea hatuwezi kufanya kila kitu peke yetu, ndio maana tuna Mikataba na Redio za Kijamii 15 kwaajili ya kutoa Elimu hiyo, hatuwezi kufanikiwa kupitia ushirikiano wa UTPC peke yake"

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
👍1
ARUSHA: Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa anasema kuna Watu wanaanzisha taarifa potoshi wakiwa na lengo la kujiingizia kipato kutokana na kuamini wanapofanya hivyo wakitumia njia za kuvutia inaweza kuwavutia Watu kubonyeza au kufuatilia taarifa zao

Ameeleza kuwa wengine wanafanya taarifa hizo makusudi kwasababu zao za Kisiasa. Wanaweza kufanya hivyo kwa lengo la kuhamisha fikra za Watu ili waache kujadili kitu fulani na wajadili suala analotaka yeye

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
DAR: Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema moja ya changamoto inayosumbua Sekta ya Habari ni suala la Upotoshaji wa Taarifa unaofanyika kwa makusudi ama kwa kutofahamu

Amesema hali hiyo imetokana na maendeleo ya Teknolojia ambayo yanatengeneza fursa kwa usambaaji wa Taarifa Potoshi, ambapo ameeleza hoja za kukabiliana na changamoto hizo ni sehemu ya Mada zitakazojadiliwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika (Julai 14 - 17, 2025)

Aidha, ameongeza kuwa Mkutano huo utajadili mijadala ya kitalaamu kuhusu changamoto zinazoathiri Tasnia ya Habari na namna Mabaraza ya Habari kote Duniani yanavyokabiliana na changamoto hizo

Soma https://jamii.app/MabarazaYaHabari

#JamiiForums #JamiiAfrica #FactChecking #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
1
DAR: Akizungumzia umuhimu wa kuwa na Watu wanaohusika Uhakiki wa Taarifa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema “Uwepo wa Wadau kama #JamiiAfrica unahitajika kutumika kusaidia kutoa elimu ya Uhakiki wa Taarifa kama ambavyo wamekuwa wakifanya (kupitia #JamiiCheck).”

Ameongeza “Tunahitaji Wadau aina hiyo waongezeke kusaidia kukabiliana na Taarifa Potoshi hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, kwani kupotosha Sera, Ilani au Taarifa za Watu wakati huu tunapoelekea katika kampeni kunaweza kuwa na madhara makubwa.”

Amesema hayo wakati akizungumzia ujio wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika (Julai 14-17, 2025) unaoandaliwa na MCT kwa kushirikiana na Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA), Umoja wa Mabaraza ya Habari ya Afrika Mashariki (EAPC) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Soma https://jamii.app/MCTFactChecking

#JamiiForums #JamiiAfrica #FactChecking #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
Juni 16 - 17, 2025, JamiiAfrica iliendesha mafunzo maalum kuhusu Akili Unde katika Uandishi wa Habari (AI in Journalism) yaliyolenga kukuza Uelewa na Ujuzi wa Teknolojia katika Taaluma ya Habari

Mafunzo hayo yalilenga kuendana na Mabadiliko ya Dunia na Teknolojia ya Habari ambapo Wanafunzi walijifunza na kujadiliana masuala anuai kuhusu AI ikiwemo matumizi, faida na changamoto zinazotokana na Teknolojia hiyo hususan suala la Upotoshaji wa Taarifa

Mafunzo haya yaliyohusisha Wakufunzi na Wanafunzi wa Shahada ya Uandishi wa Habari pamoja na Uhusiano wa Umma yalitoa fursa ya kujua namna teknolojia inavyobadilika mara kwa mara na namna ya kukabiliana na taarifa zisizo sahihi zinazozalishwa na AI.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AIJournalism #FactChecking
1