JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#Twaweza, #JamiiForums, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (#UTPC), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (#TAMWA) na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (#MISATan) kwa pamoja zinatarajiwa kuzindua Ripoti ya Sauti za Waaandishi, leo Februari 16, 2024

Ripoti itaelezea Uzoefu na Maoni ya Waandishi wa Habari Nchini Tanzania, kuhusu Sekta ya Vyombo vya Habari, lengo likiwa ni kutoa taarifa (Data) zilizopatikana kati ya Septemba na Novemba 2023

Soma https://jamii.app/RipotiYaWaandishi

#DigitalRights #SautiZaWaandishi #Twaweza #Governance #FreedomOfExpression #TanzaniaMedia
👍21
#WPFD2024: Wadau wa Tasnia ya Habari wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri wameshiriki mbio za Kilomita 10 ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2024 yanayofanyika Mei 1-3, Dodoma

Akizungumza kabla ya zoezi hilo kuanza, leo Mei 1, 2024, Shekimweri amesema Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni “Uandishi wa Habari katika Kukabiliana na Mgogoro wa Mazingira”, amewataka Wanahabari kutumia taaluma yao kutoa Elimu ya utunzaji wa Mazingira

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (#UTPC), Kenneth Simbaya ambao ni waratibu wa maadhimisho, amesema “Kauli Mbiu yetu itumike vizuri kuweka mazingira safi na mikusanyiko kama hii iwe kichocheo cha kupeana elimu na kufikisha ujumbe kwenye jamii kuhusu mazingira.”

Soma https://jamii.app/WPFD2024Day1

#JamiiForums #WorldPressFreedomDay2024 #ClimateChange #Democracy #PressFreedom #WorldPressFreedomDay
👍1👎1
#WPFD2024: Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2024 yanaendelea Jijini #Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, leo Mei 2, 2024. Ni siku ya pili ya maadhimisho hayo ambapo Kauli Mbiu ni Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi

Baadhi ya viongozi wanaotarajiwa kushiriki ni Spika wa Bunge la Tanzania - Tulia Ackson, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari - Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Rose Senyamule Staki, Mratibu Mkazi wa UN - Zlatan Milisic, Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (#UTPC) - Deogratius Nsokolo, Mwakilishi wa UNESCO - Michel Toto na Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC - Kenneth Simbaya

Soma https://jamii.app/WPFD2024Day2

#JamiiForums #WorldPressFreedomDay2024 #Accountability #Democracy #PressFreedom #WorldPressFreedomDay
👍2
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (#UTPC) umepinga Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (#TCRA) kuifungia kwa muda wa Siku 30 leseni za huduma za maudhui Mtandaoni za Kampuni ya Mwananchi Communications Limited

UTPC imesema kitendo hicho ni kinyume na misingi ya Uhuru wa Vyombo vya Habari na haki ya Wananchi kupata Taarifa ambapo imesema inapinga vikali matumizi ya Sheria zinazoruhusu Taasisi moja au mtu mmoja kutoa hukumu bila kuzingatia haki ya msingi ya kusikilizwa kwa upande wa pili

Taarifa ya UTPC imesema Mwananchi walipaswa kupewa haki yao ya kujitetea mbele ya Chombo Huru cha Kisheria kabla ya uamuzi wa kufungia chombo hiki kutekelezwa na kuwa uamuzi huo unarudisha nyuma juhudi za Waandishi wa Habari kuuhabarisha Umma na kudidimiza Haki ya Wananchi kupata taarifa.

Soma https://jamii.app/UTPCTamko

#DigitalRights #Governance #JamiiForums
👍5
DAR: Akichangia mada kuhusu changamto za Wanahabari, Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (#UTPC), Kenneth Simbaya amesisitiza haja ya Wanahabari kupata uangalizi wa huduma ya masuala ya Afya ya Akili kulingana na majukumu yao

Ameeleza hayo baada ya awali kusema kazi za Waandishi wa Habari zinawapitisha katika mazingira magumu na hivyo bila kuwa na msaada huo wa kiafya inawezekana wakawa wanapata athari za kiafya na kupungua uwezo wa kufanya maamuzi sahihi

Amesema “Suala hili likitazamwa linaweza kuwasaidia kurejea katika hali yao, hali hiyo imezidisha mgogoro wa Afya kwao kwa asilimia kubwa, imesababisha kuongezeka kwa likizo kwa sababu ya ugonjwa, wengine wanakimbia taaluma.”

Soma https://jamii.app/SilaaNaWanahabari

#JamiiForums #CivilRights #Accountability #Democracy #UchaguziSerikaliMtaa #Kuelekea2025
1👎1
DAR: Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (#UTPC), Kenneth Simbaya amesema kuelekea katika #UchaguziMkuu2025, taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Wadau mbalimbali kutoa elimu ya masuala ya taarifa potofu ili kuhakikisha Jamii inapata taarifa sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi pia.

Amesema “Katika kutekeleza hilo tunashirikia na Wadau kuhakikisha Wanahabari wanakuwa Watu wa kwanza kutoa taarifa sahihi, baadhi ya Wadau tunaoshirikiana nao ni #JamiiAfrica katika kutoa elimu kwa Wanahabari na Wananchi kuhusu umuhimu wa Uhakiki wa Habari na njia za kuhakiki taarifa mbalimbali.”

Amesema hayo wakati akifanya wasilisho la Mada katika Mkutano wa Wadau kujadili mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025, leo Julai 9, 2025, ambapo ameongeza kuwa kuruhusu kusambaa kwa taarifa potoshi inaweza kuchangia kuharibu mchakato wa uchaguzi.

Zaidi soma https://jamii.app/UTPCNaJamiiAfrica

#HakikiTaarifa #JamiiForums #Democracy #FackChecking #FactsCheck