JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#BURUDANI: Baada ya taarifa kusambaa zikimhusisha Msanii wa #BongoFleva, Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' kufunguliwa madai ya Uchochezi, #JamiiForums imezungumza na Wakili wake, #JebraKambole ambaye amethibitisha kuwa Mteja wake alipata wito wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati-Dar kwa tuhuma za uchochezi kupitia baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa '#Amkeni'

Kuhusu Madai ya Nay wa Mitego kuzuiwa na #BASATA kufanya matamasha, Jebra amesema hakuna taarifa rasmi kutoka BASATA, japokuwa BASATA walikuwa wakiwasiliana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa ambao ndio walimnyima Mteja wake vibali.

Pia, Jebra amesema BASATA imempa Nay wa Mitego wito wa kwenda Ofisini kwao bila Mwanasheria Septemba 8, 2023

Soma https://jamii.app/UchocheziNayWaMitego

#JamiiForums #Entertainment #Democracy #FreedomOfSpeech #FreedomOfExpression
πŸ‘8❀2😁1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema wito huo kwa Msanii wa Bongo Fleva, #NayWaMitego ulihusu mazungumzo kuhusu wimbo wake wa #Amkeni lakini hakutokea na hiyo ndio sababu ya kuzuia vibali vya kufanya shoo Mkoani #Njombe

Mwanasheria wa #BASATA, Christopher Kamugisha amesema β€œTumempa wito kwa mara ya tatu afike Ijumaa hii (Septemba 8, 2023), tunasubiri kuona kama atafika au la.”

Awali, Mwanasheria wa Nay, Wakili Jebra Kambole akiongea na JamiiForums alisema β€œBASATA wamempa wito wa maandishi Nay afike ofisini kwao Ijumaa hii kwa sharti kuwa anatakiwa kwenda peke yake bila Mwanasheria, bado tunatafakari sharti hilo na kwa nini iwe hivyo.”

Soma https://jamii.app/NayNaBASATA

#Entertainment #Democracy #FreedomOfSpeech #FreedomOfExpression #JamiiForums
πŸ‘5😁2πŸ‘Ž1
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesitisha shughuli za Sanaa, Starehe na Burudani katika Kumbi 504 za Tanzania Bara kutokana na kutotimiza vigezo baada ya kuhuisha vibali kuanzia Machi 28, 2024 mpaka watakapolipia vibali kupitia Mfumo wa AMIS

#BASATA imesema imefikia hatua hiyo baada ya Wamiliki wa Kumbi 149 kutimiza maelekezo ya usajili kati ya 653 waliyopewa maelekezo ya kufanya hivyo awali mnamo Februari 19, 2024 ambapo walipewa Siku 14 wakamilisha mchakato huo

Baadhi ya Kumbi hizo ni #BilicanasClub (Arusha), #Fuego Lounge, Dar Live, Lango la Jiji, Dar West Inn na Lamada Hotel

Zaidi soma https://jamii.app/BASATAFungia

#JFEntertainment #Governance #JamiiForums
πŸ‘4❀1
DAR: Baraza la Sanaa la Taifa (#BASATA) limefuta Leseni ya kuendesha Shindano la Miss Tanzania kwa Kampuni ya The Look Company Limited kwa kueleza imeshindwa kutekeleza maagizo halali ya Baraza licha ya kupewa maelekezo kupitia barua Aprili 15, 2025 na Mei 9, 2025

BASATA imesema kibali chao cha kufanya kazi hakijahuishwa kwa zaidi ya Miezi sita, kukaidi agizo la Baraza kwa kutowasilisha nyaraka muhimu kama nakala ya Cheti/Leseni ya kushiriki Shindano la Dunia, kushindwa kuandaa Shindano la Miss Tanzania kwa Mwaka 2023/2024 na kutowakilisha kwenye β€œMiss World 2024/2025”

Kampuni hiyo inasimamiwa na Basilla Mwanakuzi (Mshindi wa Taji la Miss Tanzania 1998) ambaye pia ni Mwanasiasa. Hivi karibuni (Mei 2025) kupitia ukurasa wake wa Instagram alitoa kauli kadhaa akikosoa baadhi ya maamuzi na Utendaji wa Chama chake cha CCM

Soma https://jamii.app/MissTZKufutwa

#Entertainment #JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability
❀2
Mdau katika Jukwaa la Celebrities la JamiiForums.com amehoji hatma ya Tuzo za Muziki Tanzania kwa Mwaka 2025, akieleza kuwa tofauti na miaka mitatu iliyopita, hadi sasa hakuna dalili za kufanyika kwake.

Amebainisha kuwa Mwaka 2022 na 2023 tuzo hizo zilifanyika Aprili, Mwaka 2024 zilifanyika Septemba, lakini hadi Julai 2025 hakuna taarifa yoyote kuhusu mchakato wa tuzo hizo, jambo linalozua mashaka huenda zisifanyike kabisa.

Mdau anatoa wito kwa mamlaka husika, ikiwemo #BASATA ambao ndio waandaaji wa tuzo hizo, kutoa mwongozo kuhusu hatma ya tuzo hizo kwa kuwa ni sehemu ya Burudani kwa mashabiki wa muziki.

Zaidi soma https://jamii.app/TuzoZaMuziki2025