JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Tume ya Umoja wa Afrika imekuwa muhanga wa Uhalifu wa Mtandaoni baada ya Matapeli kutumia Teknolojia ya Akili Bandia (#AI) kughushi sauti na Taswira ya Mkuu wa Tume hiyo, #MoussaFaki na kisha kupiga video za kuomba mikutano kwenye Miji ya Ulaya

Katika taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imesema haijaweza kufahamika rasmi lengo la Matapeli japokuwa dalili zinaonesha walikuwa na nia ya kuiba Vitambulisho vya Kidijitali ili kuweza kufikia taarifa za siri zaidi

'#DeepFake' ni Teknolojia inayotumiwa na Wahalifu wa Mitandao, inazidi kukua na kupata umaarufu na wakati mwingine hutumiwa na Watu kueneza habari za uongo na propaganda

Soma https://jamii.app/DeepFakesAfricanUnion

#CyberCrimes #UlinziWaFaragha #DigitalWorld #DataPrivacy #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍5
#Deepfake ni aina ya ubunifu wa Kidijitali unaotumia Teknolojia ya Akili Mnemba (#AI) kubadilisha au kuunda Picha, Sauti na Video ambazo huonekana kama ni za kweli, lakini zimeundwa kwa njia bandia

#Teknolojia hii hutumia Taarifa za Awali kuunda Maudhui mapya yanayofanana na ya awali. Inaweza kubadilisha sura za Watu kwenye Video, kuingiza Watu kwenye matukio ambayo hawakuwepo au hata kutengeneza mazungumzo ya Video na Sauti za Watu ambao hawajasema

Kufahamu mengi kuhusu Teknolojia hii tembelea Jukwaa letu la #JamiiCheck ndani ya JamiiForums.com

Soma https://jamii.app/DeepfakeTechnology

#DigitalWorld #DataPrivacy #JamiiForums
👍4👏1
Kwa mujibu wa Ripoti mpya kutoka Shirika la Fedha Duniani (#IMF), Akili Mnemba (Artificial Intelligence) inatarajiwa kuathiri 40% ya Ajira Duniani kote na kuongeza pengo la Usawa

Karibu 60% ya Ajira zitaathiriwa katika Nchi za Uchumi wa juu. Katika nusu ya hali hii, Wafanyakazi wanaweza kunufaika na Matumizi ya #AI na kuimarisha ufanisi wao

Katika hali nyingine, AI itakuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu ambayo yanafanywa na Binadamu. Hii inaweza kupunguza mahitaji ya Ajira, kuathiri Mishahara, na hata kufukuzwa Kazi

Soma https://jamii.app/AIEffectsJobsIMF

#Employments #Equality #Technology #ArtificialIntelligence #DigitalWorld #JamiiForums
👍31
#TEKNOLOJIA: Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha Azimio la kwanza la Kimataifa kuhusu Akili Mnemba (Artificial Intelligence - AI), likiziomba Nchi kulinda #HakiZaBinadamu, kulinda Taarifa binafsi, na kufuatilia kwa karibu Teknolojia hiyo ili kubaini hatari zinazoweza kujitokeza

Azimio hilo linapigania kila Nchi kuimarisha Sera za Faragha kutokana na hofu kwamba #AI inaweza kutumiwa kuvuruga michakato ya Kidemokrasia, kuchochea udanganyifu au kusababisha Watu kupoteza kazi kwa kiasi kikubwa.

Soma https://jamii.app/UNRightsAI

#Accountability #DataPrivacy #DigitalRights #DataProtection #JamiiForums #Technology
👍3
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Lugangira, amesema "Changamoto ya upotoshaji wa taarifa inaendelea kukua kwa kutumia #AI (Akili Mnemba), mfano Mwaka 2023 kuna video ilisambaa ikimuonesha Rais wa #Zambia akitangaza kuwa hatagombea katika Uchaguzi unaofuata, Vyombo vya Habari vingi hadi vya Kimataifa viliripoti taarifa hizo hadi baadaye ilipokanushwa na Ofisi ya Rais

Ameongeza "Pia, hivi karibuni Nchini Marekani wakati wa Uchaguzi ilitolewa sauti ya Rais Joe Biden akiwaambia Wananchi wasiende kupiga kura jambo ambalo halikuwa kweli. Hiyo ni mifano jinsi Teknolojia inavyoweza kutumika kupotosha habari

Ameyasema hayo akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Jijini Dodoma

Soma https://jamii.app/WPFD2024Day2

#JamiiForums #WorldPressFreedomDay2024 #Accountability #Democracy #PressFreedom #WorldPressFreedomDay
👍9
Kuelekea Siku ya Faragha ya Taarifa Duniani ambayo inaadhimishwa Januari 28, Lawyers Hub kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali akiwemo JamiiForums wameandaa Mjadala wa Sera za Akili Mnemba (AI). Tukio hili litawaleta pamoja wadau muhimu kujadili faragha na usimamizi wa teknolojia za AI, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo masuala ya AI, ulinzi wa taarifa na haki za kidijitali ni muhimu

Lengo ni kuhamasisha uelewa wa athari za AI katika faragha Barani Afrika, kutengeneza Sera zinazozingatia muktadha wa Kiafrika na kuimarisha ushirikiano wa wadau. Pia, kuainisha mbinu bora za matumizi ya taarifa na utekelezaji wa Akili Mnemba kwa uwajibikaji, kuhakikisha uwiano kati ya ubunifu na haki za faragha.

Ili kujisajili bofya https://jamii.app/AIPolicyDialogue

#JamiiForums #LawyersHub #ArtificialIntelligence #AI #AkiliMnemba
Lawyers Hub kwa kushirikiana na JamiiForums na wadau wengine wameandaa Mjadala wa Sera za Akili Mnemba (AI). Tukio hili litawaleta pamoja wadau muhimu kujadili faragha na usimamizi wa teknolojia za AI, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo masuala ya AI, ulinzi wa taarifa na haki za kidijitali ni muhimu

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo atakuwa miongoni wa wazungumzaji wa mjadala huu wenye Lengo la kuhamasisha uelewa wa athari za AI katika faragha Barani Afrika huku ukijadili namna ya kutengeneza Sera zinazozingatia muktadha wa Kiafrika na kuimarisha ushirikiano wa wadau.

Ili kujisajili bofya https://jamii.app/AIPolicyDialogue

#JamiiForums #LawyersHub #ArtificialIntelligence #AI #AkiliMnemba
Katika kuadhimisha Siku ya Faragha ya Taarifa Duniani, Lawyers Hub kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali akiwemo JamiiForums wameandaa Mjadala wa Sera za Akili Mnemba (AI) kuanzia Saa 8:00 Mchana hadi Saa 10:00 Jioni, leo Januari 28, 2025

Wadau watajadili kuhusu faragha na usimamizi wa teknolojia za AI, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo masuala ya AI, Ulinzi wa Taarifa na Haki za kidijitali ni muhimu wakiwa na lengo la kuhamasisha uelewa wa athari za AI katika faragha Barani Afrika

Kushiriki bofya https://jamii.app/DialogueDataPrivacy

#JamiiForums #LawyersHub #ArtificialIntelligence #AI #AkiliMnemba
👍2
Unaweza kugundua Video iliyotengenezwa kwa Teknolojia ya #AkiliMnemba (AI) kwa kuangalia uhusiano kati ya Midomo ya Mtu na maneno anayozungumza.

Katika video halisi, uelekeo wa Midomo huendana kwa usahihi na Sauti inayotoka. Lakini kwenye video za #AI, mara nyingi kuna ucheleweshaji au kutolingana kati ya matamshi na jinsi Midomo inavyofunguka na kufungwa.

Pia, video hizo zinaweza kuwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida kwenye Sura, kama mwanga kwenye Midomo kubadilika ghafla au kuwapo kwa mwonekano wa Midomo usio halisi

Soma https://jamii.app/UhakikiAkiliBandia

#JamiiCheck #Misinformation #Disinformation #FactsMatter #MisDis05
👍1
Moja ya Changamoto kubwa inayoonekana kwenye Picha zinazotengenezwa kwa #Teknolojia ya Akili Mnemba (#AI) ni madhaifu katika muonekano wa viungo vya Binadamu, hasa Vidole na Masikio.

Picha za aina hii zinaweza kuonesha Vidole vichache au vingi kupita kawaida au hata kuwa na umbo lisilo la kawaida. Vilevile, Masikio yanaweza kuwa katika umbo lisilo la kawaida au kutolingana.

Ikiwa utakutana na Picha inayokupa mashaka, anza kwa kukagua Vidole na Masikio kama havina mapungufu

Soma https://jamii.app/ChangamotoZaAI

#JamiiCheck #FactsMatter #Disinformation #Misinformation #MisDis05
👍1
CHINA: Uongozi wa Mji wa Beijing umetoa maelezo kuwa Shule zote za Jiji hilo zinatakiwa kutoa angalau Saa Nane ndani ya Mwaka wa Masomo kwa Wanafunzi kufundishwa kuhusu Akili Mnemba (AI)

Wanafunzi wanatakiwa kufundishwa AI katika somo linalojitegemea au linaweza kuingia katika masomo yaliyopo ya Sayansi na Teknolojia ya Habari

Wanafunzi wenye umri wa Miaka 6 hadi 12 watatakiwa kupata elimu hiyo kisha itaendelea hadi kwa Ngazi za Juu huku kila ngazi ikiwa na levo yake ya kujifunza #AI

Soma https://jamii.app/AIInChina

#JamiiForums #JFDigital #Technology #DigitalWorld
👍1
Je, AI inachukua nafasi za ajira za Wanahabari na ianaathiri uhuru wa Vyombo vya Habari na uandaaji wa taarifa?

Shiriki nasi mjadala huu ili uweze kufahamu kwa undani kuhusu nafasi ya #AI katika Vyombo vya Habari, siku ya Jumanne Aprili 15, 2025, kuanzia Saa 12:00 hadi Saa 2:00 Usiku, kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki bofya https://twitter.com/i/spaces/1eaKbWezOjZGX

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍1
ARUSHA: Balozi wa Uswisi-Tanzania, Nicole Providoli amesema Mijadala iliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025 imeonesha faida na changamoto zinazoweza kusababishwa na Akili Manemba (AI), pia imegusia suala la uhakiki wa Taarifa ambalo nalo ni la muhimu

Ameeleza kuwa AI inaweza kuwa msaada mkubwa katika stori za uchunguzi na kumsaidia Mwanahabari kupata taarifa nyingi lakini tukumbuke kuwa #AI inafanya kazi kutokana na taarifa zilizopo na sio ambazo zipo nje ya Mtandao

Tutambue kuwa AI sio adui wala Mwokoaji, bali inaakisi kile kilichopo kwenye Ulimwengu wa Mtandao, ndio maana Uswisi inashirikiana na Wadau mbalimbali Tanzania wakiwemo; Serikali ya Tanzania, UTPC, SJMC na JamiiAfrica

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala kuhusu Matumizi ya Akili Mnemba (AI) kwa kuzingatia Maadili (Ethical use of AI) akilalamikia suala la baadhi ya Watu kuitumia AI kudhalilisha wengine, badala ya kujinufaisha kwa kuongeza Maarifa na kipato

Ametoa mfano wa kauli iliyotolewa na mmoja wa Watumiaji wa Mtandao wa X ya kukemea matumizi mabaya ya AI kufuatia matukio ya hivi karibuni

Wewe unaitumia #AI kufanyia nini?

Mjadala https://jamii.app/MatumiziAI

#JamiiForums #JamiiAfrica #AIBenefits #Technology #Cyberbullying
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kwa mara ya kwanza, China imeandaa mechi ya Soka inayochezwa na Roboti wa umbo la binadamu (humanoid robots) wanaojiendesha kwa kutumia Akili Unde (#AI), bila msaada wa Binadamu

Mechi hiyo ilifanyika mwishoni mwa mwezi Juni, 2025 katika Chuo Kikuu cha Tsinghua, Beijing, kama maandalizi ya Mshindano ya Dunia ya Roboti (World Humanoid Robot Games) yatakayofanyika Agosti 2025. Roboti hao walitumia AI kutambua mpira, kuchambua mazingira, kufanya maamuzi na kucheza

Licha ya Roboti hao kuangukaanguka na kuwaacha watazamaji 'wakifa mbavu' kwa vicheko, tukio hili linaonesha mafanikio makubwa Kiteknolojia nchini humo na huenda kwa miaka ijayo yakashuhudiwa Mapinduzi makubwa kwenye ulimwengu wa Soka

Fuatilia zaidi https://jamii.app/ChinaRobotiSoka

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFTeknoloji #JFTech #AkiliUnde #AI #Soka #Michezo #JFSports #HumanoidRobots
Tafiti iliyofanyika nchini Marekani inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya Vijana wanatumia Akili Unde (Artificial Intelligence -#AI) kwa ushauri wa mahusiano, kama rafiki wa karibu zaidi ya Uhalisia na Msaada kitaaluma.

Ripoti mpya kutoka Shirika la Common Sense Media 2025 inaonyesha zaidi 70% ya Vijana tayari wametumia #AI kama rafiki, huku nusu yao wakiitumia mara kwa mara, takriban 31% wamesema mazungumzo yao na AI yanaridhisha hata zaidi ya yale na marafiki wa kweli. Sababu kubwa ni AI hupatikana muda wote, haikuhukumu na hujibu kihisia, ikitoa hisia ya kuwa na rafiki wa karibu.

Aidha, ripoti hiyo inashauri kuwe na uangalizi zaidi na kuwahimiza Vijana kujenga 'mahusiano' halisi badala ya kutegemea marafiki wa Kidijitali (AI).

Je, Vijana wanabadilisha mahusiano ya kweli na ya Kibinadamu kuwa bandia?

Soma zaidi https://jamii.app/VijanaAkiliUnde

#JamiiAfrica #JamiiForums #Elimu #DigitalRights #JFDigitali
3🔥1