JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akichangia hoja Bungeni, Mbunge wa Sumve, Wilayani Misungwi, Mwanza, Kasalali Mageni amesema huu ni Mwaka wanne amekuwa akiomba Barabara ya lami Jimboni kwake bila mafanikio huku akidai hakuna utekelezaji zaidi ya ahadi pekee kutoka kwa Mawaziri wanaohusika

Anasema "Ni lazima tuheshimiane, ni bora Watu wa Sumve tuambie hatuhusiki humu. Waziri Mkuu waambie Mawaziri wako wanaohusika waache kuwapa ahadi hewa Wananchi wa Sumve”

“Wabunge wote wa Mwanza tulienda kwa (Prof. Makame) Mbarawa alipokuwa Waziri wa Ujenzi akatuahidi lakini hakuna kitu, sasa hivi yupo (Innocent) Bashungwa napo hakuna kitu”

Soma https://jamii.app/MbungeWaSumve

#JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums #JFHuduma
👍2
Mwanasiasa #ZittoKabwe akizungumza katika Mjadala ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (#LHRC) kuhusu hoja ya Wananchi kupewa muda wa Miaka mitatu kuelimishwa kuhusu Katiba Mpya, amesema “Hoja ya miaka mitatu au mmoja ni kuchelewesha mchakato, kwani hata Watu kubishana wakati wa mchakato ni elimu tosha”

Zitto ameeleza kuwa taarifa za Wananchi zilizokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Joseph Warioba Mwaka 2011 zinaweza kutumika katika maamuzi ya Kisera kwa kuwa Wananchi walizungumzia mambo mengi mbali na Katiba huku akisisitiza kuwa hiyo ilikuwa elimu tosha kwa Watanzania na hakuna haja ya mchakato mwingine

Ameongeza “Wakati tunapata uhuru, tulikuwa na #Katiba ya Uhuru, Mkoloni hakutaka mchakato wa elimu ya miaka mitatu au mmoja kwa Wananchi, hata mwaka mmoja baada ya uhuru hakukuwa na hoja ya elimu kwa Wananchi”

Soma https://jamii.app/KatibaMchakato

#Democracy #Governance #FreedomOfExpression #Siasa #JamiiForums
👍3
Baadhi ya mijadala inayoendelea kwenye Jukwaa la Jamii Health (Jukwaa la Afya) ndani ya JamiiForums.com

1. Kupaka limao, sabuni na deodorant ni kati ya njia zilizoshauriwa na wadau baada ya mdau kuomba ushauri kuhusu tiba ya harufu kali ya kwapa.

Kufahamu njia nyingine bofya https://jamii.app/KwapaHarufuKali

2. Mdau anauliza, tatizo la watoto kuchelewa kuongea ni nini chanzo chake na jinsi gani linaweza kutatuliwa?

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/KuongeaMtoto

3. Wadau wajadili jinsi matumizi ya pedi mbalimbali zinavyoweza kubadili mzunguko wa hedhi.

Kufuatilia mada hii bofya https://jamii.app/PediHedhiBadili
👍3
Watu wengi huwa wanakimbilia Duka la Dawa kununua Dawa wanapopata Maumivu, Homa au Dalili ambazo wanaamini zinawakilisha Ugonjwa fulani

Hali ya kutumia Dawa kiholela bila Ushauri wa Daktari inaweza kusababisha Mtu kutumia Dozi kubwa au pungufu ya Kiwango kinachohitajika na kusababisha Usugu wa Dawa kwa Vimelea vya Magonjwa

Soma zaidi https://jamii.app/KujitibuMwenyewe

#JamiiForums #PublicHealth #AfyaBora2024 #Afya
👍2
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji Winfrida Beatrice Korosso kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT). Jaji Korosso ni Jaji wa Mahakama ya Rufani

Aidha, Rais amemteua Bibiana Joseph Kileo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Kabla ya uteuzi huu Kileo alikuwa Mkuu wa Mashtaka Mkoa (RPO), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mwanza

Soma https://jamii.app/UteuziAprili4

#Uteuzi #Governance #JamiiForums
👍31
UTEUZI: Rais #SamiaSuluhuHassan amemteua Alice Edward Mtulo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Mtulo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Kesi na Udhibiti Ubora, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

Soma https://jamii.app/UteuziAprili4

#Uteuzi #Governance #JamiiForums
UTENGUZI: Rais #SamiaSuluhuHassan ametengua uteuzi wa Catherine Michael Mashalla katika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

Soma https://jamii.app/UteuziAprili4

#Uteuzi #Governance #JamiiForums
Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates - UAE) ambapo ni kitovu cha Biashara na Viwanda katika Ukanda wa Mashariki ya Kati, umetangaza kusitisha uhusiano wa Kidiplomasia dhidi ya #Israel kufuatia mauaji ya Wafanyakazi saba wa Misaada ya Kibinadamu yaliyotokea Gaza

Wafanyakazi waliouawa katika shambulizi la anga la Israel walikuwa raia wa Uingereza, Poland, Australia, Palestina na wawili wa Marekani na Canada

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema Jeshi lake limewashambulia Watu wasiokuwa na hatia, hilo halikuwa kusudio lao na kuongeza “Inatokea kwenye vita, tunawasiliana na Serikali na tutafanya kila kitu ili jambo hili lisitokee tena."

Soma https://jamii.app/IsraelUAEDiplomacy

#Diplomacy #Governance #HumanRights #JamiiForums
👍21🖕1
Mdau wa JamiiFoums.com anasema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI kusema “Serikali iliamini Ujenzi wa Mradi wa #JNHPP utasaidia kuondoa mafuriko kwa Wakazi wa Rufiji” na baada ya hapo madhara yametokea chanzo kikiwa ni Mradi huo, ni uzembe wa wanaohusika na wanatakiwa kuwajibishwa

Anaeleza wakati huu ambapo Mradi umekamilika kwa asilimia kubwa kisha Serikali inatoa tamko la aina hiyo inamaanisha changamoto hiyo itaendelea kujirudia kila kunapokuwa na mvua kubwa, pia, waliohusika kufanya tathimini hawakutimiza majukumu yao

Soma https://jamii.app/UjenziJNHPPMafuriko

#JamiiForums #Governance #Accountability #ServiceDelivery
1👍1
Siku chache baada ya Rais #SamiaSuluhuHassan kusaini Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Masuala ya Vyama vya Siasa na Gharama za Uchaguzi zote za Mwaka 2024, maoni yametolewa kuwa Sheria hizo hazijazingatia baadhi ya mambo muhimu kama ilivyoshauriwa na Wadau kwenye mchakato wa kutoa maoni

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (#LHRC), Anna Henga, amesema “Wadau tulipendekeza maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kuhojiwa Mahakamani kwa njia za mapitio au mashauri ya Kikatiba hata hivyo bado maamuzi ya Tume yatakuwa ya mwisho na hayatahojiwa Mahakamani.”

Amesema “Vifungu vya 36(6), 53(6), na 65(7) vya Sheria kuhusu maamuzi ya Tume juu ya mgombea wa Urais, Ubunge na Udiwani kutohojiwa vinakiuka Ibara ya 13(6)(a) ya #Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.”

Soma https://jamii.app/MaoniYaSheria

#JusticeSystem #JFDemokrasia #Democracy #Governance #JamiiForums
👍6
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Ujerumani imekuwa Nchi ya tatu katika Jumuiya ya Ulaya kuidhinisha matumizi Binafsi ya Bangi. Wanaharakati wa matumizi ya Bangi walijumuika huko Berlin kusherekea kupitishwa kwa Sheria hiyo usiku wa Aprili Mosi, 2024 huku wengine wakisherekea katika kanisa la Cologne.

#JamiiForums
👍4👎1
TOGO: Vyama Vinne vya Upinzani vimeitisha Maandamano makubwa kuanzia Aprili 8, 2024 ili kupinga kucheleweshwa kwa Uchaguzi Mkuu uliotarajiwa kufanyika Aprili 20, 2024 huku tarehe mpya ikiwa bado haijawekwa wazi

Vuguvugu la Kisiasa limeongezeka Nchini humo baada ya #Bunge kupitisha mabadiliko ya #Katiba ambapo Vyama vya Upinzani vimelaani hatua hiyo vikidai inaweza kumruhusu Rais Faure Gnassingbé kusalia Madarakani

Rais #Gnassingbé amekuwa Madarakani tangu Mwaka 2005, alipomrithi Baba yake ambaye aliongoza #Togo kwa Miaka 38.

Soma https://jamii.app/TogoElectionsDelay

#JamiiForums #Democracy #Demokrasia #Governance
👍1
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, na Sheria ya Masuala ya Vyama vya Siasa na Gharama za Uchaguzi zilizosainiwa hivi karibuni hazijazingatia maoni muhimu ya Wadau

LHRC imesema ilipendekezwa Vyombo vya Habari vinavyokiuka taratibu wakati wa Kampeni na kumpendelea Mgombea mmoja kuwajibishwa

Pia, ilipendekezwa mabadiliko ya upatikanaji wa Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu uipe fursa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweka utaratibu lakini Vyama vya Siasa vimebaki kuwa na Mamlaka hayo

Soma https://jamii.app/MaoniYaSheria

#JusticeSystem #Demokrasia #Democracy #Governance #JamiiForums
👍2