JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kufungwa kwa Viwanja vitatu vya Ndege katika Hifadhi za Taifa na Umma sababu ikitajwa kuwa ni za Kiutendaji

Taarifa iliyotolewa na Afisa Mkuu wa Hifadhi Mawasiliano wa #TANAPA, Catherine Mbena, imesema Viwanja vilivyofungwa ni #Serengeti Kusini hadi Mei 20, 2024, Lobo hadi Julai 1, 2024 na Lamai hadi Agosti 1, 2024

Amesema “Kwa sasa, tunapendekeza Viwanja vya Ndege vya Kogatende na Seronera kama njia mbadala, tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.”

Soma https://jamii.app/TANAPASerengeti

#JFHuduma #Governance #JamiiForums #Diplomacy
👍3
Nchini Tanzania, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (#DCEA) imekamata Kilogramu 4.623 za aina mpya ya #DawaYaKulevya iitwayo Methylene Dioxy Pyrovalerone (MDPV) Jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na Raia wa Comoro, Ahmed Bakar Abdou (32)

Akiongelea Dawa hiyo Aprili 4, 2024 Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo alisema ina Kemikali inayoweza kumwathiri haraka Mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya, pia imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi #Cocaine, Methamphetamine na Heroin

Zaidi https://jamii.app/VijanaDawaZaKulevya

#JamiiForums #Drugs #DawaZaKulevya #Governance #PublicHealth
👍21👎1
DAR: Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai 'lifti' tano kati ya sita za Millennium Tower 2 hazifanyi kazi, Wasimamizi wa Jengo hilo lenye zaidi ya ghorofa 25, wamekiri uwepo wa changamoto hiyo na kuwaomba Watumiaji kuwavumilia wakati mchakato wa marekebisho ukiendelea

Trude Henry, Meneja Mwandamizi wa Prolaty Consult Ltd ambao ni Wasimamizi wa Jengo hilo, amesema kulitokea tatizo na Wamiliki wa Jengo ambao ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (#PSSSF) wameagiza lifti tatu na tayari zimewasili Bandari ya Dar

Ameongeza “Kuna mchakato wa kubadilisha lifti tatu nyingine kwa kuwa zimekuwa zikisumbua kwa muda mrefu. Kwa sasa tuna lifti moja inayotumika ambayo ndio taarifa yake tuliiona JamiiForums, 'option' tuliyonayo na ile lifti mbadala inayoenda ghorofa ya tatu.”

Soma https://jamii.app/HudumaMillennium

#JFUwajibikaji #JFUwajibikaji #Accountability #JamiiForums
👍61👏1
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla amesema anasoma Mitandaoni na kuona baadhi ya Watu wanamkumbusha majukumu yake, amewaambia 'anayaelewa'

Anasema “Ninaposema nimerudi nyumbani naelewa majukumu ya Katibu wa Uenezi wa CCM maana nasoma Mitandaoni baadhi wananikumbusha majukumu, nawaambia nayaelewa yapo kwenye Katiba ya CCM, hii ya 107 kifungu cha pili A hadi F. Leo mnatupokea Sekretarieti yetu imeundwa, nataka niwahakikishie Timu imekamilika.”

Amesema hayo wakati wa Mapokezi ya Sekretarieti ya CCM Taifa katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Aprili 5, 2024

Soma https://jamii.app/MapokeziCCM

#Siasa #Governance #JamiiForums
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
BUNGENI: Akichangia mapendekezo ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Mbunge wa #Gairo (CCM), Ahmed Shabiby ameishauri Serikali kukata Tsh. 2,000 kila Mwezi kwenye laini za simu na Tsh. 10,000 kukatwa kwa Wabunge, Wafanyabiashara na Wafanyakazi ili fedha hizo ziwe chanzo cha mapato ya Bima ya Afya kwa wote

#Shabiby amesema kuna Wamiliki wa Laini za Simu Milioni 72 Nchini ambao makato yao kwa Mwaka yataingiza Tsh. Trilioni 1.72 na zikijumlishwa za Tsh. 10,000 kwa Mwezi za Wabunge, Wafanyabiashara na Wafanyakazi, Serikali itapata kwa Mwaka takriban Tsh. Trilioni 2

Zaidi soma https://jamii.app/MakatoYaLainiZaSimu

#DigitalRights #JamiiForums #Afya #ServiceDelivery #JFHuduma #PublicHealth #Accountability #Uwajibikaji
👎3👍21
Mojawapo ya madhara ya kutegemea Mtandao kupata utatuzi wa changamoto za Kiafya ni kupata Wasiwasi wa kuwa una tatizo kubwa kuliko uhalisia

Mtandao unaweza kufanya Uone unaumwa Magonjwa kama Saratani au VVU lakini kumbe ungeenda Hospitali ungegundua unasumbuliwa na Mchafuko wa Damu

Je, umeshawahi kupata wasiwasi wa kuumwa Ugonjwa wa kutisha baada ya ku-Google Dalili za kuumwa kwako?

Jifunze zaidi https://jamii.app/GoogleKujitibu

#PublicHealth #JamiiForums #AfyaBora2024 #Afya #SelfDiagnosis #SelfMedication
👍1
YANGA YAPOTEZA KWA PENATI 3-2, MAMELODI YAINGIA NUSU FAINALI

Licha ya Timu ya Young Africans “Yanga” kupambana kwa kupata matokeo ya 0-0 dhidi ya #MamelodiSundowns ya Afrika Kusini katika dakika 90 za kawaida za michezo miwili ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Timu hiyo imeondolewa kwa penati 3-2

Ikicheza ugenini kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, #Yanga ilionesha soka la ushindani muda mwingi wa mchezo huo

Kutokana na matokeo hayo, Mamelodi inatarajiwa kucheza na mshindi wa mchezo wa Espérance de Tunis ya Tunisia dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika Nusu Fainali

#JFSports #CAFCL #JamiiForums
👍51
#Simba imeshindwa kutimiza ndoto ya kuiondoa Al Ahly katika mechi za Mtoano kwa mara ya kwanza baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-0 katika mechi ya pili ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Hivyo, Simba inaondolewa kwa jumla ya magoli 3-0 kwa kuwa ilipoteza mchezo wa kwanza Jijini Dar es Salaam kwa goli 1-0, pia ni mara ya kwanza kufungwa 'nje ndani' na Al Ahly

Magoli yamefungwa na Amr Al-Sulaya dakika ya 47 na Kahraba dakika ya 90+9 kwa penati na Takwimu za jumla mechi baina ya timu hizo, Al Ahly imeshinda mechi 5, Simba imeshinda 3 na Sare 2

Soma https://jamii.app/SimbaOUT

#JFSports #CAFCL #JamiiForums
👍62
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Mkoani #Kilimanjaro anasema Stendi ya Bomang'ombe ina Mashimo yanayosababisha Madereva wa Mabasi na Costa kutishia kugoma kutoa huduma

Ametoa wito kwa Mamlaka hasa zinazopokea Ushuru wa kila siku kutumia fedha hizo kufanya ukarabati wa Stendi hiyo ili kuepusha Mgomo ambao utasababisha adha ya Usafiri kwa Watumiaji wa Stendi hiyo

Soma https://jamii.app/UbovuWaStendi

#JamiiForums #SerikaliBilaRushwa #JFHuduma #Accountability #Uwajibikaji
👍3
#KILIMANJARO: Mdau wa JamiiForums.com anadai kinachoendelea Wilayani #Moshi kwa maduka au sehemu za Biashara kufungwa bila wahusika kupewa nafasi ya kujieleza sio sawa kwa kuwa kinawaumiza Wafanyabiashara hata kama wanadaiwa Kodi

Anaomba Mamlaka za Juu kuingilia kati changamoto hiyo inayochangia kurudisha nyuma Maendeleo yao, akidai vitendo hivyo vinafanywa kwa maelekezo ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa

Anashauri mazungumzo yafanyike kwa kuwa kuna wakati wanapata hasara, hivyo inakuwa ngumu kutimiza malengo ndani ya muda uliowekwa

Soma https://jamii.app/BiasharaMoshi

#JFUwajibikaji #JFHuduma #JamiiForums #Governance
👍21