JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Mdau aliyejitambulisha kuwa ni Mkazi wa Kibamba CCM, anadai Wakazi wa maeneo hayo wanapata changamoto ya Barabara hasa ile “Barabara ya Polisi” akidai ni mbovu

Anadai Mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya zaidi na wanapolalamika kwa Serikali za Mtaa, kinachofanyika ni kumwaga michanga ambayo haisaidii

Anaomba Mamlaka zinazohusika kusikia kilio chao, kwani wakati wa Mvua mateso ni makali

Soma https://jamii.app/KibambaCCM

#JFHuduma #JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
👍3
#MICHEZO: Straika wa zamani wa Brazil, Ronaldo Nazario De Lima ambaye pia amewahi kuchezea Klabu za #Barcelona, #RealMadrid, #InterMilan, #ACMilan ametaja kikosi chake bora cha muda wote wakiwemo #LionelMessi na #CristianoRonaldo

Kikosi hiko ni; 1. Gianluigi Buffon 2. Cafu 3. Roberto Carlos 4. Fabio Cannavaro 5. Paolo Maldini 6. Zinedine Zidane 7. Pele 8. Diego Maradona 9. Ronaldo de Lima 10. Lionel Messi na 11. Cristiano Ronaldo

Unadhani nani mwingine alistahili kuingia kwenye kikosi hiki au kuwekwa benchi?

Soma https://jamii.app/C9Team

#JFSports #JamiiForums
👍8
Mbali na kumpatia mwanao Elimu ya Darasani (Awali, Msingi, Sekondari na Chuo) ni kwa namna gani unamwandaa na maisha? Ni ujuzi gani wa ziada unampatia?

#JamiiForums #JFChitChat #LifeStyle
3👍2😎1
BURUDANI: Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza kuwa Wadau wa Sekta ya Burudani watashiriki zoezi la Upigaji kura kwa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kuanzia Aprili 29 hadi Mei 29, 2024

Ujumuishwaji wa kura hizo utafanyika Juni 7, huku matokeo rasmi yakitangazwa katika tukio utoaji tuzo hizo, Jumamosi ya Juni 15, 2024

Vipi mdau, unategemea maboresho yapi katika Mchakato mzima wa Upigaji kura hadi sherehe za Utoaji wa tuzo?

Zaidi https://jamii.app/TuzoMuziki

#JamiiForums #Entertainment #Burudani #TMA2023
👍6
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mdau wa JamiiForums.com anasema kwa kuangalia mara kadhaa ‘clip’ inayoonesha utata wa linalobishiwa kuwa ni goli katika mchezo wa #MamelodiSundownsFC dhidi ya #Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika na amejiridhisha Mwamuzi hakufanya maamuzi ya haki kwa Yanga

Anaamini Mpira uliopigwa na Stephane Aziz Ki ulivuka mstari na Yanga ilistahili kupewa goli lakini Mpira ulivyorejea Uwanjani Beki wa Mamelodi akaupiga kwa Kichwa ukavuka mstari na kisha kurejea Uwanjani

Anaeleza, baada ya Kipa wa Mamelodi kuudaka ndipo Mwamuzi akasimamisha Mchezo, na VAR ilipokataa Goli aliwapa Mpira Mamelodi badala ya kuwa faida ya kona kwa Yanga

Je, Mdau yupo sahihi, Yanga ilistahili kupewa Goli au Kona?

Soma https://jamii.app/MpiraKuvukaMstari

#CAFCL #JFSports #JamiiForums
2👍2👎1😁1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PWANI: Siku chache baada ya Vijijini 23 vilivyopo Bonde la Mto Rufiji kuathiriwa na mafuriko yaliyotokana na Maji yaliyoachiwa katika Mradi wa Umeme wa #JNHPP, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowelle, amesema Mradi huo umesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa mafuriko na athari zilizokuwa zikitokea

Amesema “Miaka ya nyuma kulikuwa hakuna tahadhari, Wananchi walishtukia tu Maji yamejaa katika Nyumba na Mashamba yao, ndio maana mpaka sasa hakuna kifo hata kimoja kilichoripotiwa. Kwa sasa Wananchi wanajulishwa kabla ya Maji kuachiwa.”

Hivi karibuni, Mdau wa JamiiForums.com alitoa hoja kuwa ubunifu wa Mradi wa JNHPP ulitakiwa kuzingatia njia mbadala ya kudhibiti maji na kushauri Serikali kutafuta utatuzi wa kudumu kwani Wananchi wataendelea kuteseka ikiwa hali itabaki kama ilivyo

Soma https://jamii.app/MafurikoRufiji

#JFHuduma #JFUwajibikaji #Governance #HumanRights #CivilRights
👍13
Tunapojaribu kwenda mbele, ni vema kukubali mapito yetu, kujithamini, na kufanya uamuzi wa kuachia vitu vinavyotuzuia kufikia malengo yetu.

JamiiForums inakutakia Siku njema na Maandalizi mema ya Wiki mpya

#JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning #Maisha
👍4🔥1
Sheikh Abeid Amani Karume alifariki Aprili 7, 1972 akiwa na Umri wa Miaka 66 baada ya kupigwa risasi alipokuwa anacheza 'Bao' huko Zanzibar

Soma https://jamii.app/KarumeDay2024

#JamiiForums #KarumeDay2024 #JFKumbukizi
2👍2
Vipi Mdau, unakumbuka 'kamba' ipi ya Wachezaji wa Mpira wa Miguu?

Mjadala https://jamii.app/KambaZaSoka

#JamiiForums #Michezo #JFSports #JFChitchats
👍3
#AFYA: Umewahi kuathiriwa na Dawa na Daktari hakuwa amekupa Elimu yoyote kuhusu 'Side Effects' unazoweza kuzipata baada ya kutumia Dawa hiyo?

Shiriki Mjadala zaidi https://jamii.app/SideEffectsDawa

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability #AfyaBora2024
2👍1