Septemba 5 kila Mwaka ni siku ya Hisani Duniani, iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuongeza uelewa kwa Watu binafsi, Taasisi na Mashirika Duniani kusaidia na kuwahudumia wengine kupitia kazi za kujitolea na shughuli za Hisani
Ilichaguliwa kuadhimisha kifo cha Mama Teresa, aliyepata Tuzo ya Amani ya Nobel Mwaka 1979, kama Heshima ya juhudi zake za Hisani na Kibinadamu, ambapo alijitolea Maisha yake kusaidia na kuwahudumia Watu wasiojiweza
Siku hii sio tu kwaajili ya kutoa Fedha kusaidia wengine, bali kutoa Muda wako, Kujali, kutoa Upendo na Msaada. Kufanya tendo la Wema, kubwa au dogo linaloweza kuleta Mabadiliko makubwa kwa mwingine
Soma https://jamii.app/WorldCharityDay
#JamiiForums #InternationalDayOfCharity #GivingTuesday #CharityMakesADifference

β€1π1
ANTONY WA MAN. UNITED AONDOLEWA TIMU YA TAIFA KWA TUHUMA ZA KUMPIGA MPENZI WAKE
Uongozi wa #Brazil umechukua maamuzi hayo dhidi ya nyota huyo wa #ManchesterUnited ikidaiwa alimshambulia kwa kumpiga kichwa #GabrielaCavallin hotelini Januari 15, 2023
Gabriela ambaye kwa sasa hana uhusiano na Antony pia anadai aliumizwa kifuani na kulazimika kufanyiwa upasuaji ambapo Polisi wa Sao Paulo (Brazil) na Greater Manchester (England) wanaendelea na uchunguzi
Antony amesema uhusiano wao ulikuwa na misukosuko lakini hakuwahi kumpiga na kuwa hizo ni taarifa za kutungwa
Soma https://jamii.app/Antony
#Sports #JamiiForums

π6π€4β€1π1
ULINZI WA TAARIFA BINAFSI: Kifungu namba 46 cha Sheria ya Kuzuia VVU iliyopitishwa Mwaka 2008 kinamhukumu Mhudumu wa Afya atakayevunja usiri wa taarifa za Afya za Mgonjwa au Mtu yeyote atakayetoa taarifa kuhusu hali ya Kiafya ya Mtu kwamba ameambukizwa au hana VVU/UKIMWI faini isiyopungua Tsh. 500,000 na isiyozidi Tsh. 1,000,000 au kifungo kisichopungua Miezi 6 na kisichozidi Miezi 12 au vyote kwa pamoja.
Soma https://jamii.app/SheriaVVU
#JamiiForums #Afya #JFSheria #PersonalDataProtection #DataPrivacy

π3
#MALEZI: Maneno yanajenga taswira na matarajio, yanajenga na kukuza Saikolojia na hivyo kushawishi namna tunavyofikiri. Maneno tunayowaambia Watoto mara nyingine kwa kejeli na kuwatukana huathiri Maisha yao wanapokuwa Watu wazima
Tabia ya baadhi ya Wazazi kuwafananisha Watoto wao na Vitu au Wanyama, si tu inawaathiri Watoto Kisaikolojia lakini pia ni aina mojawapo ya Unyanyasaji wa Kihisia (#EmotionalViolence).
Soma zaidi https://jamii.app/ManenoWazazi
#JamiiForums #UkatiliWatoto #JFWomen #ChildSafety #ChildViolence #Parenting

π1
#JFWOMEN: Kuwapa Wanawake fursa sawa za kujipatia kipato na kushiriki katika shughuli za Kiuchumi kunaweza kuinua hali yao ya Kiuchumi na Kijamii
Wanawake wanapopata fursa za kazi bora, Ujuzi na #Elimu, wanaweza kujenga njia za Kujitegemea, kuwekeza katika Maendeleo yao Binafsi na Familia zao na hatimaye kuchangia katika Ujenzi wa Jamii yenye usawa na endelevu
Soma https://jamii.app/PengoLaKijinsia
#JamiiForums #WomenRights #HumanRights #GenderBalance #GenderGap

π4
Jiunge nasi katika Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini Alhamisi hii, Septemba 7, 2023, kupitia 'X Spaces' ya #JamiiForums
Tutaangazia Mchakato mzima wa Utoaji na Upatikanaji wa Vitambulisho ikiwemo Mafanikio na Changamoto wanazopata Wananchi na Mwitikio wa Mamlaka katika zoezi zima
'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO
#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces #JFToons

β€1
Kwa Nchi 146 zilizojumuishwa katika Ripoti ya Global Gender Gap Report 2023, kwa upande wa Afya na Uhai, pengo la kijinsia limezibwa kwa 96%. Hii inaonesha kuna mafanikio makubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa Huduma za Afya kwa wote bila kujali Jinsia
Katika eneo la Elimu, pengo la Kijinsia limezibwa kwa 95.2%, hii ni ishara ya kuongezeka kwa fursa sawa za Elimu kwa Wanawake na Wanaume
Soma https://jamii.app/GenderGapWorld
#JamiiForums #JFWomen #GenderGap #GenderEquality

π4β€1π€1
Anadai Wastaafu hao waliokuwa Watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa #Tanzania ambao wanaendelea kudai sehemu ya stahiki zao huku ikidaiwa wapo kwenye hatari ya kutapeliwa na watu wachache ambao si waaminifu
Mdau wa JamiiForums.com anadai Viongozi wanaowaongoza Wastaafu hao waliwajulisha wenzao kuwa wanatakiwa kumchangia Wakili anayesimamia kesi yao kiasi cha Dola za Marekani 82 (Tsh. 205,000) kwa kila mstaafu, idadi yao inadaiwa ni takribani 1,600
Mdau anatoa wito kwa Vyombo vya Usalama na #TAKUKURU kufuatilia kinachoendelea ili kama kuna mazingira ya rushwa, utapeli βupigajiβ wahusika wasaidiwe
Soma https://jamii.app/WastaafuEAC
#JFUwajibikaji23 #KemeaRushwa #Accountability #Diplomacy #JamiiForums

π5π2
MUHIMBILI: TUTAANZA KUPANDIKIZA INI MWAKA 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi amesema βKuelekea hatua hiyo safari ni ndefu na nzito, hadi sasa Kituo cha Mafunzo, Uchunguzi na Matibabu ya Kibobezi ya Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini cha MNH kina uwezo wa kutoa huduma kwa Wagonjwa waliofanyiwa Upandikizaji nje ya Nchi tofauti na awali ambapo walilazimika kurudi nje ya Nchi.β
Ameongeza kuwa maandalizi hayo yanaenda pamoja na uboreshaji wa maabara za kiuchunguzi wa patholojia, uchunguzi wa damu, uchunguzi wa radiolojia na tiba radiolojia na uboreshaji wa Vyumba vya Wagonjwa Mahututi
Soma https://jamii.app/UpandikiziIni
#Afya #JFHuduma #JamiiForums

π6π2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Wafahamu Marais watatu wa Afrika waliopo madarakani kwa muda mrefu zaidi
#JamiiForums #JFDemokrasia #Democracy
#JamiiForums #JFDemokrasia #Democracy
π8π2π€1
Jukwaa la #JamiiCheck linalopatikana ndani ya JamiiForums.com limefuatilia suala hili na kubaini kuwa upo uwezekano wa Mwanamke kupata Ujauzito wa Watoto Mapacha wa Baba tofauti
-
Hii huitwa 'Heteropaternal Superfecundation' na hutokea kwa baadhi ya Wanawake wanaopevusha yai zaidi ya moja kwenye Mzunguko mmoja wa Hedhi
-
Soma https://jamii.app/MapachaJC
#JamiiForums #FactsChecking #FactsCheck

π2β€1
DR-CONGO: Maafisa 2 wa Jeshi (Mkuu wa Kikosi cha Walinzi na Kiongozi wa Jeshi katika Mji wa Goma) wamekamatwa kwa madai ya kuhusika katika kutoa maagizo yaliyosababisha Wanajeshi kuwaua Waandamanaji 43 na wengine 56 kujeruhiwa
Mauaji yalitokea baada ya Waandamanaji kuingia Mitaani kupinga uwepo wa Vikosi vya Jeshi la Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa
Wizara ya Mambo ya Nje imeahidi kufanya Uchunguzi utakaokuwa Huru na Wazi kuhusu mauaji hayo
Soma https://jamii.app/DRCMilitia
#JamiiForums #Governance #HumanRights #SocialJustice #Accountability

β€4π1π1
Je, umewahi kukumbana na Changamoto za Kupata Kitambulisho cha Taifa? Jiunge nasi katika Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini Alhamisi hii, Septemba 7, 2023, kupitia 'X Spaces' ya #JamiiForums
Tutaangazia Mchakato mzima wa Utoaji na Upatikanaji wa Vitambulisho ikiwemo Mafanikio, Changamoto wanazopata Wananchi na Mwitikio wa Mamlaka
'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO
#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces

π5β€4
ZAMBIA: Akiwa katika ziara eneo la #Kanyama, Mji Mkuu wa #Lusaka, Rais #HakaindeHichilema amewataka wanaopanga Mapinduzi ya Kijeshi wasitishie mipango yao mara moja
Amesema "Kwa wenzetu wanaofikiri sisi ni dhaifu kwa kuwa wema na kuwa wanaweza kuvunja Sheria na kufikiria kuchukua madaraka kwa njia isiyo ya Kidemokrasia, tunakuja kuwakabili"
Onyo hilo linakuja baada ya Mapinduzi kadhaa yaliyotokea hivi karibuni katika Nchi za Afrika (#Niger na #Gabon) huku kukiwa na malalamiko ya Wananchi kuhusu ongezeko la gharama za maisha
Soma https://jamii.app/MapinduziZambia
#JamiiForums #AfricanCoups #Demokrasia #Democracy

π6β€1
ERIC BAILLY WA MANCHESTER UNITED ATUA BESIKTAS
Beki huyo wa Kati ambaye msimu uliopita aliitumikia #Marseille ya Ufaransa kwa mkopo, amekamilisha mchakato wa kutua #Besiktas ya Uturuki baada ya kukosa nafasi chini ya Kocha Erik ten Hag
#EricBailly ambaye alisajiliwa Mwaka 2016 chini ya Utawala wa Kocha #JoseMourinho akitokea #Villarreal amecheza mechi 113 akiwa na jezi ya #ManUnited na kufanikiwa kufunga goli moja
Soma https://jamii.app/BaillyTransfer
#JFSports #JamiiForums

π7β€2π1
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa #Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Utatu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao
Pamoja na mambo mengine wamejadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa #DR Congo
Baada ya mkutano huo ulifuata Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC MCO), ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi, Dkt. Stergomena Tax kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje, #JanuaryMakamba
Soma https://jamii.app/SADCKikao
#JFDiplomacy #Governance #JamiiForums

π7
Mamlaka ya Nishati na Maji (EWURA) imetangaza Bei Kikomo za Mafuta zinazoanza kutumika leo Septemba 6, 2023 ambapo imesema mabadiliko yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi 21%, gharama za uagizaji wa mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi Agosti, 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+)
#DaresSalaam Petroli itauzwa Tsh. 3,213, Dizeli Tsh. 3,259 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,943. #Tanga Petroli Tsh. 3,259, Dizeli Tsh. 3,305 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,989. #Mtwara Petroli Tsh. 3,285, Dizeli Tsh. 3,332 na Mafuta ya Taa Tsh. 3,016 kwa Lita
Vipi Mdau, una maoni gani kuhusu kupanda huku kwa bei za mafuta Nchini?
Soma https://jamii.app/Fuel0609

π7π5π€2
Kujifunza na kushiriki Mijadala mbalimbali kuhusu Ujenzi na Makazi Tembelea https://jamii.app/MakaziUjenzi
#JamiiForums #Ujenzi
#JamiiForums #Ujenzi
π2