JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Serikali ya Uingereza inatarajia kuchukua maamuzi dhidi ya Kundi hilo la Urusi ambapo itakuwa ni kinyume cha Sheria kuwa Mwanachama au kuunga mkono Shirika hilo

Mapendekezo hayo yakifikishwa Bungeni na kupitishwa, mbali na Wanachama, pia mali za kundi hilo nazo zitatambulika ni za magaidi ambapo Uingereza inaamini #Wagner inayotumiwa na Jeshi la Urusi chini ya Rais #VladimirPutin ni tishio kwa Usalama wa Kimataifa

Soma https://jamii.app/UKAgainstWagner

#Diplomacy #Governance #JamiiForums
πŸ‘6❀2🀬1
Rais wa Kenya, #WilliamRuto, amesema ni wakati wa kuwa na mazungumzo ya Kimataifa kuhusu kodi itakayotozwa kwa Nchi Wachafuzi wa Mazingira

Mataifa 17 kati ya 20 Duniani yalioathiriwa zaidi na Mabadiliko ya Tabianchi yako Barani Afrika, wakati Mataifa 20 tajiri zaidi Duniani ikiwemo Marekani yanazalisha asilimia 80 ya Hewa Ukaa ambayo inasababisha Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Soma https://jamii.app/AfricaClimateSummit23

#JamiiForums #AfricaClimateSummit23
πŸ‘4
MDAU-KIGOMA: ZOEZI LA β€˜KAMCHAPE’ LINALOLENGA KUONDOA UCHAWI NI UDHALILISHAJI NA UCHONGANISHI

Mdau wa JamiiForums.com anadai matukio hayo yamekuwa yakifanyika zaidi maeneo ya Kigoma Vijijini akitaja baadhi ya Vijiji vinavyokumbwa na kadhia hiyo ni Nyarubanda, Kalinzi, Mukigo, Muhinda, Nyaruboza, Rukoma, Igalula, Mgambo, Katumbi na Kalya

Anasema vitendo hivyo vina mazingira ya Utapeli na kuharibu Amani kwani KAMCHAPE inahusisha baadhi ya Watu wanaodai ni β€˜Waganga wa Jadi’ wanalazimisha kila Kaya kuchanga Tsh. 5,000 kuwawezesha wao kuzunguka katika makazi ya Watu kwa madai ya kuutoa uchawi

Anatoa wito kwa Mamlaka ziongeze nguvu ya kudhibiti KAMCHAPE kabla ya madhara kuwa makubwa zaidi ya ilivyo sasa

Soma https://jamii.app/KigomaUchawi

#Maisha #Lifestyle #SocialJustice #JamiiForums
πŸ‘4πŸ‘Ž1πŸ₯°1
#BUNGENI: Wizara wa Mambo ya Ndani imesema hadi kufikia Julai 31, 2023 jumla ya Watanzania 11,242,736 wamepewa Vitambulisho, sawa na asilimia 55 ya lengo la kuwapatia Wananchi 20,294,910 wanaostahili kupewa

Mpango wa Serikali ni kuwagawia Vitambulisho Watanzania 9,052,174 waliobaki ifikapo Machi, 2024

Soma https://jamii.app/BungeSept6

#JamiiForums #Governance
πŸ‘6
#BUNGENI: Akijibu swali Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Angelina Malembeka, aliyehoji idadi ya Madaktari Bingwa Wazalendo wa Magonjwa ya Binadamu na aina ya fani walizobobea, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Mollel amesema #Tanzania ina jumla ya Madaktari Bingwa Wazalendo 2,469 ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika wa fani mbalimbali za Udaktari Bingwa

Amesema kati yao Madaktari Bingwa 2,098 wapo katika Sekta ya Umma na Madaktari Bingwa 371 wapo Sekta Binafsi ambao wamegawanyika katika maeneo 28 ya Ubingwa

Soma https://jamii.app/BungeSept6

#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Governance #Accountability
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: SERIKALI HAITAMBUI GUNIA KUWA KIPIMO BALI NI KIFUNGASHIO

Waziri wa Viwanda na Biashara amesema Kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo β€œThe Weights and Measures Act (Amendment) Order, G.N. No. 725 of 2018”, kifungu cha (2) (b) cha Jedwali hilo ni kuwa Mazao ya Mashambani yatafungashwa kwa uzito usiozidi kilogramu 100, hivyo ameelekeza Wauzaji/Wanunuzi wa Mazao kutumia Mizani

Soma https://jamii.app/BungeSept6

#JamiiForums #Governance
πŸ‘5πŸ‘Ž1
Jiunge nasi katika Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini Alhamisi hii, Septemba 7, 2023, kupitia 'X Spaces' ya #JamiiForums

Tutaangazia Mchakato mzima wa Utoaji na Upatikanaji wa Vitambulisho ikiwemo Mafanikio na Changamoto wanazopata Wananchi na Mwitikio wa Mamlaka katika zoezi zima

'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces #JFToons
πŸ‘6
JE, ULISHIRIKI SHINDANO LA 'STORIES OF CHANGE' 2023? USIKAE MBALI NA PM YAKO

Mchakato wa kuwasiliana na wanaoelekea kuwa Washindi kwenye Shindano la #StoriesOfChange2023 na umeanza

Kama ulishiriki Shindano hili unashauriwa kukaa karibu na Private Message (PM) kupitia akaunti yako ya JamiiForums.com

Ni vyema kutoa Ushirikiano (PM) kama ilivyoelekezwa kwenye Vigezo na Masharti ya Shindano hili

#JamiiForums #SoC2023 #StoriesOfChange #Accountability #Governance
❀5πŸ‘1
Watoa taarifa (#Whistleblower) wanabeba jukumu muhimu katika kutengeneza Dunia yenye usawa. Utoaji wa taarifa husaidia kulinda Fedha za Umma, kuchochea Uwazi na Uwajibikaji pamoja na kuimarisha Huduma za Kijamii

Mtu yeyote kwa manufaa ya Umma anaweza kufichua maovu yaliyofanyika, yanayofanyika au kuelekea kufanyika ikiwemo Ubadhirifu, Utapanyaji wa Mali au Matumizi mabaya ya Mali ya Umma au matumizi mabaya ya Madaraka

Watu wanaweza kuogopa kutoa taarifa ikiwa hatari za kuripoti taarifa hizo zinaonekana kuwa kubwa au ikiwa wanahofia kwamba hawatapewa uzito unaostahili

Soma https://jamii.app/WhistleblowerProtection

#JamiiForums #WhistleblowerProtection #FreedomOfSpeech #Accountability
πŸ‘5
UPDATE: Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Dkt. Julius Ningu ameshtakiwa katika Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma kwa tuhuma za kutoa Lugha za Matusi, Vitisho na kuwaweka Mahabusu Watumishi wa Umma akiwemo Mtendaji wa Kata ya #Rwinga, Mario Fabian

Upande wa Mashtaka umedai Mshtakiwa hakutoa maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusiana na kukamatwa kwa Watumishi wa Halmashauri na Mafundi waliokuwa wanatekeleza Miradi ya UVIKO-19, Wilayani Namtumbo, ikiwa ni kinyume cha Sheria inayomtaka Mkuu wa Mkoa au Wilaya kutoa maelezo kwa Maandishi kwa Polisi kabla au muda mfupi baada ya kuamuru kumuwekwa ndani akieleza sababu za Msingi za kumuweka ndani Mtuhumiwa

Soma https://jamii.app/DCMoroAshtakiwa

#JamiiForums #Governance #Accountability #SocialJustice
πŸ‘7❀1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kisiwa cha Chippewa ni kivutio cha asili huko Marekani. Kisiwa hiki husukumwa na boti ili kisifike kwenye makazi ya watu

#JamiiForums #Entertainment #JFEntertainment #Chippewa
πŸ‘3❀1
#HISTORIA: MWAMI THERESA NTARE VI, CHIFU WA KWANZA MWANAMKE

Alikuwa Kiongozi wa Jamii ya Heru huko Kasulu na alishika wadhifa wa kuwa Mkuu wa Machifu wote #Tanganyika kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle 1958

Baada kutawazwa Uchifu alitafutiwa Mchumba ambaye ni George Shinganya. Kulingana na Mila za Kiha, Mwami haolewi, akiolewa inabidi ahame milki yake ya Uchifu ili akawe Mke. Familia ya Mwami ndiyo iliyolipa Mahari kwa Familia ya George, hivyo, Jina la Shinganya likaondolewa na akaitwa George Ntare

Fahamu zaidi https://jamii.app/TheresaChifuMwanamke

#JFHistoria #JFWomen #WomenInPower #AfricanHistory
😁8πŸ‘5
NIGERIA: Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi leo Septemba 6, 2023 baada ya kusikiliza maombi ya Wagombea wa Upinzani wa People’s Democratic Party, Labour Party na Allied People’s Movement wanaotaka kubatilisha tangazo la Rais #BolaTinubu kuwa Mshindi wa Uchaguzi huo wa Februari 2023

Matarajio ya hukumu hiyo yamezua hali ya wasiwasi kote nchini humo ambapo katika Mji Mkuu idadi kubwa ya Askari na Maafisa wa Polisi wameweka vizuizi vya Barabarani katika maeneo ya katikati ya Jiji na maeneo jirani

Soma https://jamii.app/HukumuUchaguziNigeria

#JamiiForums #NigeriaElections #Democracy #Governance
πŸ‘4❀1
#BURUDANI: Baada ya taarifa kusambaa zikimhusisha Msanii wa #BongoFleva, Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' kufunguliwa madai ya Uchochezi, #JamiiForums imezungumza na Wakili wake, #JebraKambole ambaye amethibitisha kuwa Mteja wake alipata wito wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati-Dar kwa tuhuma za uchochezi kupitia baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa '#Amkeni'

Kuhusu Madai ya Nay wa Mitego kuzuiwa na #BASATA kufanya matamasha, Jebra amesema hakuna taarifa rasmi kutoka BASATA, japokuwa BASATA walikuwa wakiwasiliana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa ambao ndio walimnyima Mteja wake vibali.

Pia, Jebra amesema BASATA imempa Nay wa Mitego wito wa kwenda Ofisini kwao bila Mwanasheria Septemba 8, 2023

Soma https://jamii.app/UchocheziNayWaMitego

#JamiiForums #Entertainment #Democracy #FreedomOfSpeech #FreedomOfExpression
πŸ‘8❀2😁1
#UCHUMI: Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameiomba Benki Ya Dunia kuharakisha upatikanaji wa Dola za Marekani zaidi ya Milioni 500 ifikapo Novemba 2023 ili zisaidie kukabiliana na uhaba wa Fedha hizo katika mzunguko wa Fedha Nchini

Dkt. Mwigulu ameuambia ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) unaosimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kuwa changamoto ya upatikanaji wa Dola inachangia Mfumuko wa Bei na kukwamisha uagizaji wa Bidhaa muhimu ikiwemo Mafuta

Aidha, amesema Serikali kupitia Bunge imefanya maboresho na kupitisha Mabadiliko mbalimbali ya Sheria na Kanuni zitakazowezesha kuvutia Uwekezaji wa Mitaji na Teknolojia

Soma https://jamii.app/DollarBill

#JamiiForums #Governance #EconomyCrisis #Accountability
πŸ‘1