JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GABON: Jenerali Brice Oligui Nguema anatarajiwa kuapishwa leo, Septemba 4, 2023 kuwa Rais wa Mpito akichukua Madaraka baada ya kupindua Utawala wa Familia ya #Bongo uliodumu kwa miaka 55 nchini humo

Septemba 1, 2023, Jenerali Nguema aliahidi kuunda Taasisi za Kidemokrasia zinazoheshimu #HakiZaBinadamu, japokuwa Wapinzani wamedai Jenerali huyo hana dalili ya kurejesha Utawala wa Kiraia

Soma https://jamii.app/JeneraliKuapishwaGabon

#JamiiForums #Governance #GabonCoup #Accountability #Demokrasia
πŸ‘3❀1πŸ‘1
Vipi Mdau, umeelewa nini hapa?

Credit @MasoudKipanya

#JamiiForums #JFToons
πŸ‘4
Kukataa kutoa Rushwa si uamuzi rahisi. Watu wengi wanaweza kujikuta katika hali ngumu ya kuchagua kati ya kukataa Rushwa na mahitaji yao ya msingi au fursa za kuboresha Maisha yao. Lakini Mfumo wa Sheria na Utawala katika Nchi unaweza kuwa na mapungufu, hivyo kuleta changamoto kubwa kwa Watu kushikilia msimamo wa kukataa kutoa Rushwa

Jamii inayoelewa umuhimu wa Maadili na #Uwajibikaji, Watu wanaokataa kutoa Rushwa wanaweza kuchukuliwa kama waanzilishi wa Mabadiliko chanya. Kwa kushikilia Maadili na kusimama imara dhidi ya Mfumo wa Rushwa, wanaweza kuwa mfano bora kwa wengine

Mjadala zaidi https://jamii.app/KukataaRushwa

#JamiiForums #KemeaRushwa #SerikaliBilaRushwa #Corruption
😁4πŸ‘3πŸ‘1
Je, umewahi kukumbana na Changamoto za Kupata Kitambulisho cha Taifa? Jiunge nasi katika Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini Alhamisi hii, Septemba 7, 2023, kupitia 'X Spaces' ya #JamiiForums

Tutaangazia Mchakato mzima wa Utoaji na Upatikanaji wa Vitambulisho ikiwemo Mafanikio, Changamoto wanazopata Wananchi na Mwitikio wa Mamlaka

'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO

#NIDASpaces #JFVoiceBasedSessions #VitambulishoVyaNIDA #JFSpaces
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
BURUDANI YA JESHI LA POLISI

Rais #SamiaSuluhuHassan akishuhudia burudani wakati akishiriki katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, leo Septemba 4, 2023, Oysterbay Polisi, Dar es Salaam

#Burudani #JamiiForums
πŸ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akiongea katika Kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, leo Septemba 4, 2023, Oysterbay Polisi, Dar es Salaam

#Governance #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Spika wa Bunge, Dkt. #TuliaAckson ameshauri Serikali kuweka utaratibu maalumu wa kuwazingatia kwanza Watumishi wanaofanya kazi za kujitolea wakati Serikali ikiendelea kufanya maboresho ya Sheria ya Ajira ili kuwasaidia kupata ajira bila kikwazo pindi zinapotangazwa

Katika swali la msingi, Mbunge wa Kiteto (CCM), #EdwardOlelekaita alihoji ni lini Serikali itapeleka Bungeni marekebisho ya Sheria ya Ajira ya Utumishi wa Umma ili kuongeza kigezo cha kujitolea katika kupata ajira

Akitoa mchango wa nyongeza, Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, #GeorgeSimbachawene amesema β€œHaipendezi kuona Daktari akilima Matikiti wakati sisi tunauhitaji wa Madaktari au Walimu, tunakuja na mpango mkakati wa kumaliza tatizo hilo."

Soma https://jamii.app/SpikaAjira

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #JFUwajibikaji23
❀3πŸ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza leo Sept. 4, 2023 wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, Rais Samia amesema wananchi bado wanalalamikia tatizo la Rushwa hasa kwa Askari wa Barabarani

Amesema β€œMfano tukiweka Kamera za Barabarani hakutakuwa na sababu ya Askari kusimama Barabarani kusimamisha Magari, Teknolojia itatoa mwongozo wa kila kitu na Rushwa haitakuwepo,”

Rais amesema β€œWimbo wa Polisi ni mzuri na leo kabla ya kuja hapa nilifungua YouTube nikausikiliza kisha nikaangalia Jeshi langu na kujiuliza ingekuwa yanayoimbwa hapa ndiyo yanayotendeka tungekuwa na Jeshi la Malaika"

Soma https://jamii.app/SamiaRushwa

#JamiiForums #Governance #SerikaliBilaRushwa #Accountability #KemeaRushwa
πŸ‘8
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kujitafakari utendaji wao kwasababu bado amekuwa akipokea Malalamiko ya Wananchi kubambikiwa kesi wanapofika kwenye Vituo vya Polisi Nchini

Rais amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi kulifanyia kazi tatizo hilo ili wanaofikishwa kwenye Mikono ya Sheria wawe na Makosa ya Kweli na sio ya kukomoana

Hivi karibuni, Tume ya kuangalia namna ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai iliwasilisha Ripoti kwa Rais iliyoonesha malalamiko ya Wananchi kubambikiwa Mashtaka na baadhi ya Askari yameongezeka katika Vituo vya Polisi Nchini.

Soma https://jamii.app/SamiaKesi

#JamiiForums #Governance #SocialJustice #SerikaliBilaRushwa #JFUwajibikaji23
πŸ‘5
KILIMANJARO: Aliyekuwa Mlinzi wa Shule ya Sekondari #Scolastica, iliyopo Himo-Moshi, Hamis Chacha (34) aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kumuua kwa makusudi mwanafunzi wa shule hiyo, Humphrey Makundi, ameachiwa huru baada Mahakama kukubali Rufaa yake na kubadili shitaka lake kutoka mauaji ya kukusudia na kuwa ya bila kukusudia

Baada ya kusikiliza Rufaa yake Majaji waliamua Mtuhumiwa aliua bila kukusudia kwa kuwa hakuwa na nia ovu ya kuua, hivyo kufuta na kubatilisha adhabu ya kifo aliyohukumiwa Juni 3, 2019 na kuamuru aachiwe huru kwa kuwa muda aliokaa gerezani unafidia muda wa adhabu ya kuua bila kukusudia

Soma https://jamii.app/MlinziAachiwaHuru

#JamiiForums #SocialJustice #Accountability #Uwajibikaji #Governance
πŸ‘8πŸ‘Ž4😁1
Kifungu namba 47 cha Sheria ya Kuzuia VVU iliyopitishwa Mwaka 2008 kinasema, Mtu yeyote kwa makusudi akisambaza Virusi vya UKIMWI kwa Mtu mwingine atakuwa ametenda kosa na akithibitika adhabu ni kifungo kisichopungua Miaka mitano na kisichozidi Miaka 10

Soma https://jamii.app/SheriaVVU

#JamiiForums #Afya #JFSheria
πŸ‘3πŸ‘1
Kwa mujibu wa utafiti wa Taasisi ya American Lung Association (ALA), vijana wenye kati ya miaka 18 hadi 24 duniani wanazidi kuingia katika matumizi ya 'Shisha' licha ya Kilevi hicho kuwa na madhara ya Kiafya

Tafiti za ALA za mwaka 2020 zinaonesha 52.1% ya Watumiaji wa Shisha duniani wanapatikana Afrika na Mashariki ya Kati ambapo watumiaji wenye kati ya miaka 15 hadi 23 waliovuta Shisha walikiri Kilevi hicho kimewasukuma pia Kuvuta Sigara

Ikumbukwe, Sigara ya Kawaida inahitaji kuvuta pumzi ndani kati ya Mara 8 hadi 10 kwa Sigara, Uvutaji Shisha umetajwa kuhusisha Uvutaji Pumzi kati ya mara 100 hadi 200 (Kwa Saa 1) kitendo kinachoingiza Sumu ya Nikotini mara 1.7 zaidi ya Wanaovuta Sigara

Mbali na kusababisha aina zaidi ya 7 za Saratani, Shisha imetajwa kuwa sababu kuu ya Saratani ya Mapafu kutokana na Mtumiaji Kuvuta Kiasi kinachofikia Mikrogramu 90,000 za Hewa yenye Sumu kwa muda mfupi

Soma https://jamii.app/ShishaCigar

#JamiiForums #PublicHealth #JFAfya #CancerAwareness #JFAfyaJamii
πŸ‘4
GABON: Rais wa Mpito, Jenerali Brice Nguema ambaye ni kati ya Wanajeshi waliohusika kumuondoa Madarakani Rais #AliBongo, ameapishwa rasmi na kuahidi kufanya Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi, Sheria za Adhabu na Katiba

Nguema amesema uamuzi wa kumuondoa Rais aliyekuwepo ulikuwa muhimu kwa manufaa ya Taifa hilo huku akimnukuu Rais wa zamani wa #Ghana, Jerry John Rawlings, β€œWananchi wanapoumizwa na Viongozi, basi Wanajeshi wanapaswa kuwarudishia Utu na Uhuru wao."

Soma https://jamii.app/NguemaNewGabon

#JamiiForums #Democracy #Governance #Gabon
πŸ‘7πŸ‘1
Mtu Mzima anayependa/kuvutiwa kufanya Mapenzi na Watoto wadogo (ambao hawajafikia umri wa kubalehe), Kitaalamu anajulikana kama #Pedophile

Pedophile anaweza kuwa yeyote (Kijana au Mzee, Mwanaume au Mwanamke), Watu wa aina hii huwa na tabia ya kujitenga na Watu wazima na kufurahia zaidi kuwa na Watoto

Mara nyingi hujaribu kuwarubuni Watoto kwa kutumia vitu kama zawadi, Pesa, Michezo ya video na vitu vingine vya kuchezea ili kuwashawishi kufanya nao Mapenzi, kuwashika maungo yao ya siri au kuwapiga Picha/Video za Utupu

Soma zaidi https://jamii.app/Pedophile

#JamiiForums #JFWomen #HakiMtoto #ChildAbuse #UkatiliWatoto #ChildSafety
#JFAFYAAKILI: Kuwa na Mwenza asiyechaguliwa na mhusika mwenyewe kunaweza kusababisha uhusiano wa dhati kutoweka. Hii husababisha mtu kukosa uhusiano wa furaha na Mwenza wake, hali ambayo inaweza kuathiri furaha na ubora wa maisha yake yote

Vile vile, katika Jamii ambayo Mila ya kupangiwa Mume kabla ya Kuzaliwa inazingatiwa, mtu anayekataa maamuzi hayo anaweza kutengwa na kubaguliwa. Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya Kihisia, Kujisikia kutengwa na hata matatizo ya Kisaikolojia, kama Upweke na Msongo wa Mawazo ambayo huweza kusababisha hisia za kujidhuru

Soma Zaidi https://jamii.app/AhadiZaNdoaKablaYaKuzaliwa

#JamiiForums #JFWomen #HakiMtoto #SocialJustice #Depression #MentalHealth #MentalWelliness #ChildProtection #WomenRights
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kwa takriban Wiki 2 kumekuwa na taarifa kutoka maeneo mbalimbali Nchini zinazoeleza uwepo kwa tatizo la upatikanaji wa Mafuta katika Vituo vinavyotoa huduma hiyo

Kuna madai kuwa baadhi ya Wamiliki wa Vituo vya Mafuta wamezuia uuzaji wakisubiri Bei mpya za Mafuta zinazotarajiwa kutangazwa Wiki hii

Hali ya upatikanaji wa Mafuta ikoje katika eneo ulipo?

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #SocialJustice #Uwajibikaji
πŸ‘2
#BURUDANI: #Barbie imekuwa Filamu rasmi yenye Mauzo Bora kwa Mwaka 2023 baada ya mapato yake kuipita Filamu ya #SuperMarioBros kwa kuingiza zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 1.38 (Takriban Tsh. Trilioni 3.45)

Filamu ya Super Mario Bros imeingiza Dola za Marekani Bilioni 1.36 (Tsh. Trilioni 3.4), #Oppenheimer Dola za Marekani Milioni 853 (Tsh. Trilioni 2.13), #GuardiansOftheGalaxy Vol. 3, Dola za Marekani Milioni 846 (Tsh. Trilioni 2.11), #FastandFuriousX Dola Milioni 705 (Tsh. Trilioni 1.76) na #Spiderman Tsh. Trilioni 1.71

Soma https://jamii.app/BarbieYavunjaRekodi

#JamiiForums #JFEntertainment #Movies #MovieOfTheYear
πŸ‘2❀1
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (EWURA), Dkt. James Andilile amefafanua kuwa Petroli iliyopo inatosheleza matumizi ya siku 19 huku Dizeli ikiwepo ya kutumika kwa siku 18

Aidha, EWURA imevifungia kwa miezi 6 Vituo 2 vya Mafuta vya Camel Oil na Mtemba vilivyopo Msamvu na Turiani Morogoro kwa ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Uendesha wa Vituo vya Mafuta huku Kituo cha GBP Ipuli Tabora kikifungiwa kwa muda usiojulikana kwa maelezo ya kutouza Mafuta

Takwimu za Mahitaji ya Mafuta Nchini zinaonesha Tanzania inatumia Lita Milioni 4.5 za Petroli kwa siku na Dizeli Lita Milioni 6.6 kwa siku.

Soma https://jamii.app/EWURASept

#JamiForums #Governance #JFHuduma #JFUwajibikaji23
πŸ‘7❀2
SIMIYU: MADAI YA STENDI KUTELEKEZWA, MEYA AKIRI MIUNDOMBINU SI RAFIKI KWA WAFANYABIASHARA

Mstahiki Meya wa Mji wa #Bariadi, Elias Masanja ametoa majibu hayo baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza Stendi ya Mizigo ya Kidulya ya Wilayani Bariadi iliyojengwa Kilometa 7 kutoka katikati ya Mji kwa gharama ya zaidi ya Tsh. Bilioni 1 imetelekezwa na hakuna hatua zinazochukuliwa

Meya amesema β€œStendi ilikamilika Mwaka 2021 lakini sehemu ya maegezo si nzuri, hakuna ghala la kuhifadhia mizigo, mvua ikinyesha inaweza kuharibu mizigo, kazi zinaendelea lakini si kwa kiwango tulichotarajia. Mkandarasi alijenga kama alivyotakiwa kwa kuwa mkataba wake haukuwa na vipengele vya kuongeza vitu ambavyo vinatakiwa kuongezwa.”

Soma https://jamii.app/StendiBariadi

#JFUwajibikaji23 #JFHuduma #Governance #JamiiForums
πŸ‘7
DODOMA: Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, linatarajiwa kuchunguza Malalamiko ya Ukiukwaji wa Maadili dhidi ya Julius Kenneth Ningu (Mkuu wa Wilaya ya Ulanga - #Morogoro) na Mathew P. Mbaruku (Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto - #Tanga)

Viongozi hao watajadiliwa Septemba 5 hadi 6, 2023 kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika Kikao cha Baraza la Maadili kitakachofanya Uchunguzi kuhusu Malalamiko yaliyotolewa juu yao

Kwa mujibu wa Taarifa ya Sekretarieti, uchunguzi utafanyika kwa uwazi kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo Wananchi wanaalikwa kuhudhuria katika kikao hicho

Soma https://jamii.app/Maadili

#JamiiForums #Governance #JFuwajibikaji23
πŸ‘4❀3