JamiiForums
โœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kupitia somo la stadi za kazi Wanafunzi hujifunza sanaa na shughuli mbalimbali za uzalishaji kama, uchoraji, ushonaji, mapishi, kilimo, ufugaji

#JamiForums #SanaaYetu #Elimu
RAIS SAMIA: Makamishna niwaombe sana mkasimamie haki, Watanzania wote wana haki sawa. Juzi wamefurahi wamepanda madaraja kwa mserereko lakini hawajui wajibu wao

> Watumishi wetu hawajielewi, nidhamu yao ni mpaka wapate vitisho

Soma - https://jamii.app/WateuleWaapishwa

#JamiForums
LIGI KUU SOKA ENGLAND: Michezo ya mwisho ya Ligi Kuu England inachezwa sasa, huku macho yakiwa kwa timu za Liverpool na Manchester City

Ikiwa matokeo yatabaki hivi, Manchester City itachukua ubingwa kwa kuwa na tofauti kubwa ya magoli ya kufunga na kufungwa dhidi ya Liverpool

#JamiForums #JFSports
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (EWURA), Dkt. James Andilile amefafanua kuwa Petroli iliyopo inatosheleza matumizi ya siku 19 huku Dizeli ikiwepo ya kutumika kwa siku 18

Aidha, EWURA imevifungia kwa miezi 6 Vituo 2 vya Mafuta vya Camel Oil na Mtemba vilivyopo Msamvu na Turiani Morogoro kwa ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Uendesha wa Vituo vya Mafuta huku Kituo cha GBP Ipuli Tabora kikifungiwa kwa muda usiojulikana kwa maelezo ya kutouza Mafuta

Takwimu za Mahitaji ya Mafuta Nchini zinaonesha Tanzania inatumia Lita Milioni 4.5 za Petroli kwa siku na Dizeli Lita Milioni 6.6 kwa siku.

Soma https://jamii.app/EWURASept

#JamiForums #Governance #JFHuduma #JFUwajibikaji23
๐Ÿ‘7โค2
MDAU: NACTVET KUNA USUMBUFU WA โ€˜NJOO KESHOโ€™ WAKATI WA MAREKEBISHO YA VYETI

Anadai cheti chake kilikosewa, akafanya marekebisho Julai 2023 na kulipa gharama kwa โ€˜Control Numberโ€™ kama alivyoelekezwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) ambapo aliahidiwa kupata cheti kingine ndani ya wiki mbili

Mdau amedai imepita miezi mitatu hajapata Cheti chake na kila akienda anaambiwa mfumo unasumbua yaani 'System Iko Down', kitu ambacho kimekuwa kero kwake

Akizungumza na JamiiForums.com, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya NACTVET, Jeff Shellembi anasema โ€œUtaratibu wa Serikali, malalamiko kama hayo yawasilishwe kwa maandishi.โ€

Soma https://jamii.app/MalalamikoNACTVET

#JFHuduma #JFUwajibikaji #JamiForums
๐Ÿ‘1
NJOMBE: Kamanda wa Polisi Mkoa, Mahamoud Hassan Banga amesema uchunguzi wa awali kuhusu kesi ya mauaji ya Tumaini Luvanda (35) Mkazi wa Dombwela, umebaini Juma Kyando ambaye ni Mume wa Marehemu alifanya Mauaji kutokana na Mgogoro wa Ndoa

Kamanda amesema baada ya Mtuhumiwa kukamatwa alihojiwa ili kubaini sababu za mauaji hayo ambapo imebainika Familia ilikuwa na matatizo ya muda mrefu ambapo Mwanaume amekuwa akinyimwa unyumba lakini pia Siku ya tukio, Mke wake alichelewa kurudi Nyumbani

Hata hivyo, Kamanda Banga amesema kwa namna Mtuhumiwa alivyofanya tukio hilo ikiwemo kutenganisha Kichwa na Kiwiliwili huku baadhi ya Viungo akivitupa Mtoni, imeonesha uwezo wake wa kufikiri ulikuwa ni mdogo hali inayowafanya waendelee na uchunguzi wa Kidaktari ili kuona kama alikuwa mzima wa Afya wakati akitekeleza tukio hilo.

Soma https://jamii.app/MauajiNJMB

#JamiForums #HumanRights #JFMatukio
๐Ÿ‘8
Mdau wa JamiiForums.com ameshauri Watu kutofanya siri kwenye mambo yanayohusu Familia. Amesema fikiria umejenga, huna uliyemshirikisha; una pesa Benki, Biashara, hata Mtoto nje ya Ndoa ila hakuna Ndugu anayemjua. Likitokea la kutokea ghafla, kila kitu kinapoteza maana

Amesema tujifunze kushirikishana, tuache siri zisizo na tija

Mdau, ni jambo gani huwezi kumshirikisha Mtu au Watu wako wa karibu?

Mjadala https://jamii.app/TupunguzeSiri

#JamiiAfrica #JamiForums #Maisha
๐Ÿ‘1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai Desemba 2024, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, alitoa Miezi Mitatu kwa Mkandarasi wa Barabara ya Msongola - Mbande, kukamilisha Barabara hiyo kabla Mvua za masika kuanza, lakini hadi sasa ujenzi haujaisha na hali inazidi kuwa mbaya

Ametoa Wito kwa Wizara ya Ujenzi kufuatilia changamoto hiyo kwani Wananchi wengi wanategemea njia hiyo lakini kwa sasa wanaweza kutumia hadi Saa 3 kwenye kipande hicho

Zaidi https://jamii.app/BarabaraKisewe

#JamiForums #JamiiAfrica #HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #JFMdau2025 #Accountability #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Akizungumza katika tukio la Serikali kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kisasa wa Arusha Council Sports Complex, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema โ€œNawaomba tumrudishe Mama, tutafanya makubwa zaidi.....mtakaposhtaki hamuwezi kufanikiwa.โ€

Uwanja huo ambao utajengwa eneo la Bondeni City, utakuwa na uwezo wa kubeba Watu kati ya 8000 - 10,000 walioketi, ukiwa umezungukwa na Viwanja vya Mpira wa Kikapu 2, Uwanja wa Mpira wa Wavu (1) na Viwanja vya Tenisi (2)

Soma https://jamii.app/KariaArusha

#JamiForums #JamiiAfrica #JFSports
โค1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Akizungumza mbele ya Viongozi wa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amedai kuna Wagombea wa Kisiasa wamekuwa wakijaribu Kumshawishi kwa Fedha ili waweze kushinda katika kura za maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akimtolea mfano mmoja bila kumtaja jina

Chacha pia alikumbusha kuwa Rais Samia ameshatoa maelekezo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (#TAKUKURU) kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya #Rushwa wakati wa Uchaguzi

Zaidi bofya https://jamii.app/SiasaTabora

#JamiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Accountability #ElectionInformation2025
โค4๐Ÿ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TANGA: Mwanasiasa Rashid Kilua ambaye ni mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bumbuli aliingia katika hali ya mvutano na baadhi ya Watu mara baada ya kuchukua fomu ya Ubunge katika Ofisi za Wilaya, tukio hilo lilitokea Juni 28, 2025

Watu hao walimzuia kupiga picha na kufanya mahojiano mara baada ya kuchukua fomu, mvutano huo ulidumu kwa dakika kadhaa kabla ya kila Mtu kuondoka eneo la tukio kutokana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwepo eneo hilo kuingilia

Soma https://jamii.app/SiasaBumbuli

#JamiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Kiongozi wa #ACTWazalendo, Dorothy Semu akizungumza katika Mkutano wa hadhara, Julai 5, 2025 uliofanyika Sapiwi, Bariadi Vijijini alisema โ€œJeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Majeshi kwenye Uchaguzi wasitumike kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi wa Mwaka 2025."

Amedai kuwa Chaguzi za Mwaka 2020 na 2024 ziligubikwa na uwepo wa Kura feki hadi katika Vituo vya Kupiga Kura na kwamba kwa sasa wanakataa na hawataki uwepo wa Kura hizo

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKutumikaNaCCM

#JamiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Accountability
โค1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza punde baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kwenye Makao Makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC), leo Agosti 12, 2025, Mgombea Urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (#CHAUMMA), Salum Mwalimu amejinadi kuwa yeye pamoja na chama anachotokea ni wasafi na kwamba hawana dosari yoyote itakayowazuia kufanya uamuzi wowote kwa maslahi ya Taifa.

Zaidi Soma https://jamii.app/SalumMwalimuMsafi

#JamiiAfrica #JamiForums #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Siasa
โค1๐Ÿ˜1