JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kumuelimisha Binti ni suala kubwa zaidi ya kumpeleka Shuleni tu, Kunahusisha kuhakikisha anahisi kuwa salama akiwa Shuleni; Kuwa na Fursa ya kukamilisha Ngazi zote za #Elimu na Kupata Ujuzi wa kushindana katika Soko la #Ajira

Wasichana wanaopata #Elimu kwa Usawa wana Uwezekano mkubwa wa kuwa na Maisha Bora na kuepuka Ndoa katika Umri mdogo

Soma https://jamii.app/ElimuMtotoWaKike

#DayOfTheGirl
πŸ‘8
Wahalifu wa Kimtandao hutumia tatizo la Ukosefu wa #Ajira kufanya Ulaghai kwa kuweka Matangazo ya Kazi ili kukusanya Taarifa Binafsi za Watu

Umewahi kukutana na aina hii ya Ulaghai kwenye harakati za kuomba Kazi Mtandaoni?

Uliathirika kwa namna gani?

#DigitalRights #JFDigitali
πŸ‘2
#Teknolojia inaendelea kupenya katika nyanja mbalimbali za Maisha yetu, ikiwemo Ajira. Umuhimu wa Ujuzi wa Kidigitali unaendelea kujidhihirisha katika Soko la #Ajira na hata kwa wanaojiajiri

Mfumo wetu wa #Elimu unatuandaa kuendana na kasi ya Mabadiliko ya Teknolojia?

#DigitalSkills #DigitalRights #JFDigitali
πŸ‘2
Ukuaji wa Sekta ya #Teknolojia umekuja na fursa mbalimbali kwa Jamii, ikiwemo #Ajira, Biashara na Ujasiriamali

Ni muhimu kwa Wananchi kupatiwa Ujuzi wa Kidigitali ili Maendeleo ya Teknolojia yawanufaishe na wajikwamue kiuchumi

#DigitalSkills #Technology #JFDigitali
πŸ‘2❀1
Imezoeleka kuwa Mtu anahitajika kutoa kiasi fulani cha fedha au mali ili apate anachostahili hasa katika huduma za #Afya, nafasi za #Ajira na #Elimu

Kauli maarufu ya 'Mkono mtupu haulambwi' inasababisha Jamii kuamini hiyo ndiyo njia sahihi ya kurahisisha Maisha huku ikileta madhara makubwa

Ni muhimu kutambua kuwa sio wote wenye uwezo wa kutoa #Rushwa, hivyo kauli hiyo inawagharimu wakati mwingine hata Maisha yao

Soma https://jamii.app/AthariZaKilaSikuZaRushwa

#KemeaRushwa
πŸ‘6❀1
DKT. MPANGO: ELIMU YETU HAIKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA

Amesema "Uwezo wa Kusoma na Kuandika unakadiriwa kuwa 92% lakini bado Vijana wengi wanaomaliza Masomo hawapati fursa za Ajira. Pia, #Elimu yetu haikidhi mahitaji ya Soko la #Ajira wala kuwezesha Wahitimu kujiajiri"

Soma https://jamii.app/DiraYa2025

#Governance
πŸ‘7
Je, Mikopo ya Biashara ikitolewa kwa Vijana inaweza kuondoa tatizo la Ajira Nchini?

#JamiiForums #Maisha #Ajira #Uchumi
Kilio cha Rushwa kipo karibu kila sekta kuanzia Vyombo vya Utoaji Haki, #Elimu, Afya, #Ajira na nyinginezo

Katika Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania (2022), Rushwa ilibainishwa kuwa kikwazo kikubwa katika kupata Haki

Kama Taifa, tunakwama wapi katika kuwajibika ipasavyo ili kupunguza vitendo vya Rushwa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/Rushwa01

#KemeaRushwa #Uwajibikaji #JFHuduma
Kuhakikisha Watu wanapata #Ajira zenye hadhi ni changamoto kubwa ambayo inahitaji juhudi za pamoja za Serikali, Wafanyakazi, Waajiri, na Jamii nzima

Kwa mfano, kupatia Watu Elimu bora na mafunzo yanayolingana na mahitaji ya Soko la Ajira ni muhimu kwani inaweza kuimarisha Mifumo ya Elimu, kutoa Mafunzo ya Ufundi Stadi, na kuendeleza Programu za Mafunzo ya kuendeleza Ujuzi

Kuunda Mazingira mazuri ya #Ujasiriamali na kukuza Sekta Binafsi ni eneo muhimu kufanyiwa kazi. Serikali zinaweza kutoa Sera na Rasilimali za kuchochea Ujasiriamali, kusaidia #Biashara ndogo na za kati, na kukuza Mazingira ya Biashara yenye urafiki kwa ukuaji wa Ajira

Soma https://jamii.app/KaziHadhi

#JamiiForums #Employment #HumanRights
πŸ‘1
#SikuYaKimataifaYaVijana 2023 inakumbusha juu ya umuhimu na nguvu za Vijana katika Ujenzi wa Jamii Bora na kusisitiza Umuhimu wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili ili kuboresha Mazingira ya Ukuaji na Mafanikio ya Vijana

Lengo la siku hii ni kuongeza uelewa kuhusu changamoto mbalimbali wanazopitia Vijana Duniani kote, ikiwa ni pamoja na #Elimu, #Ajira, #AfyaYaAkili, #Umaskini na Kushirikishwa

Soma https://jamii.app/IYD2023

#JamiiForums #IYD #IYD2023 #GreenSkills #YouthDay #GlobalGoals
πŸ‘5
Kuna mazingira ya Rushwa ya namna mbalimbali katika Taasisi za #Elimu ambayo husababisha madhara Makubwa katika Jamii. Kwa Mfano, Utoaji wa Rushwa ili kupata vibali vya kuanzishwa kwa Vyuo Binafsi

Vibali hivi hutolewa kwa kuzingatia miundombinu na uajiri wa kutosha wa Wafanyakazi wanaostahili. Baadhi ya Taasisi hujaribu kuwahonga Wakaguzi wa Ubora ili kupata vibali hivi

Rushwa inasababisha Elimu kutolewa bila Viwango Stahili

Soma https://jamii.app/MadharaRushwa

#JamiiForums #KemeaRushwa #Accountability #Governance #Ajira #ElimuBilaRushwa
πŸ‘4
Kufahamu zaidi kuhusu nafasi hizi tembelea Jukwaa la Ajira na Tenda ndani ya JamiiForums.com

Kufikia Jukwaa hili bofya https://jamii.app/AjiraNaTenda

#JamiiForums #JFAjiraNaTenda #Ajira #Tenda
πŸ‘4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Tembelea Jukwaa la Ajira na Tenda kufahamu zaidi kuhusu nafasi hizo

Kufikia jukwaa hilo bofya https://jamii.app/NafasiZaKaziAjiraNaTenda

#JamiiForums #AjiraNaTenda #NafasiZaKazi #Ajira
πŸ‘4
Mdau wa JamiiForums.com anasema Tatizo la ukosefu wa Ajira limekuwa ni kilio kwa Vijana wengi, na limeibua fursa kwa upande mwingine hasa Kampuni, Biashara binafsi, Taasisi Zisizo za Kiserikali (NGO's) na Mashirika

Anasema kwa kiasi kikubwa Sekta Binafsi wamekuwa hawatoi #Ajira kama zamani badala yake wanatumia Watu Wanaojitolea ili kupata uzoefu wa kazi kwa malipo kidogo au bila malipo kabisa na kuwaweka wengi kwenye hatari ya kufukuzwa kazi muda wowote

Ukubaliana na Mdau? Je, unadhani hali hii inasababishwa na nini?

Kushiriki Mjadala zaidi https://jamii.app/AjiraVolunteering

#JamiiForums #Accountability #Employment
πŸ‘8
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Tembelea Jukwaa la Ajira na Tenda ndani ya JamiiForums.com ili kufahamu zaidi kuhusu nafasi hizi na nyingine zilizotangazwa

Kufikia Jukwaa hili bofya https://jamii.app/NafasiZaKaziAjiraNaTenda

#JamiiForums #AjiraNaTenda #NafasiZaKazi #Ajira
πŸ‘4
AFRIKA KUSINI: Chama Tawala cha African National Congress (#ANC) kimekubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kupoteza idadi kubwa ya viti vya Ubunge

Akitoa taarifa hiyo baada ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama (NEC), Rais Cyrill Ramaphosa amesema β€œTumeridhia kuvialika Vyama vya Siasa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo ndio njia bora ya kuipeleka mbele Nchi yetu"

Ameongeza kuwa lengo la Serikali hiyo itakuwa ni kuhakikisha yanapatikana majibu ya kero zinazowakabili Wananchi ikiwemo tatizo kubwa ukosefu wa #Ajira, Gharama za Maisha na Kukuza Uchumi

ANC ambacho kilikuwa na kawaida ya kupata zaidi ya 60% katika Chaguzi, ilianza kushuka mwaka 2019 kwa kupata 57.5%, na katika Uchaguzi wa Mei 29, kilipata 40.18% ya Kura zote.

Soma https://jamii.app/ANCDecides

#JamiiForums #Democracy #Governance #SocialJustice #JFDemokrasia #SAElections #SAUnemploymentRate
πŸ‘4❀1
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOENDA KWENYE 'INTERVIEW'

Vaa Vizuri: Saikolojia ya kuvaa vizuri ni kama umeweza kujipangilia mwenyewe katika Mavazi yako hata kazi yao utaifanya kwa uangalifu na unadhifu

Wahi Kufika: Inashauriwa kufika sehemu ya usaili Nusu Saa kabla ya muda ili kuyasoma Mazingira na kutuliza akili yako

Uliza maswali ya Msingi: Ukipewa nafasi ya kuuliza maswali uliza mambo yaliyo ndani ya #Ajira au #Fursa uliyoitiwa, usiongee 'sana'

Zaidi https://jamii.app/UsailiAjira

#JamiiForums #UsahiliWaKazi #JobInterviews #Interviews #Internships #Opportunities
❀2πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kwa taarifa zaidi kuhusiana na nafasi hizi na ili kuona nafasi nyingine za kazi na tenda mbalimbali zilizotangazwa tembelea Jukwaa la Ajira na Tenda ndani ya JamiiForums.com

Kufikia Jukwaa hilo bofya https://jamii.app/AjiraNaTenda

#JamiiForums #AjiraNaTenda #Ajira #Tenda
πŸ‘2
Swali la 'Tell us about yourself' (tuambie kuhusu wewe) kwenye usaili, huwa linaogopeka sana lakini ni swali muhimu ambalo ukishindwa kujibu vizuri linaweza kukupunguzia nafasi ya kupata fursa au ajira uliyoitiwa

Lengo la Swali hili ni kujenga picha kamili na thabiti ya jinsi ulivyo na jinsi unavyoweza kuleta thamani katika nafasi unayoiomba, hivyo jibu kwa ufupi kuhusu elimu yako, uzoefu wako wa kazi, majukumu uliyokuwa nayo, na jinsi yanavyohusiana na nafasi unayoomba

Vile vile, kwa ufupi elezea ujuzi maalum na stadi ulizonazo zitavyosaidia katika kazi unayoiomba. Pia, eleza jinsi nafasi unayoomba inavyoendana na malengo yako ya muda mrefu kulingana na taaluma yako.

Zaidi https://jamii.app/InterviewTips

#JamiiForums #Fursa #Ajira #InterviewTips
πŸ‘3❀2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Leo Machi 18, 2025 akiwa katika maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yaliyofanyika Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Mjadala wa VETA ufanyiwe kazi kwani una tija

Amesema "Mjadala huu haupiti tu hovyo na mimi nimehushuhudia na naufatilia kwa ukaribu. Hakika una tija kwa sababu wapo ambao wanapinga na kuna ambao wanaongea kurekebisha na wapo ambao wamesema namna nzuri ya kwenda vizuri"

Soma https://jamii.app/MjadalaVetaTija

#JamiiForums #Governance #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji #Ajira #UnemploymentCrisis