JamiiForums
56.2K subscribers
32.8K photos
1.86K videos
30K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) kuzingatia suala la utambuzi katika mchakato wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuepuka malalamiko kuhusu uwepo wa Wapigakura Feki au Wasio na Sifa kama ambavyo imekuwa ikitajwa

Anaeleza kama mchakato wa kukosekana Wakaguzi ukiendelea ni rahisi kujipenyeza au kupenyezwa kwa kundi la Watu wasio na sifa na hivyo kuharibu Uchaguzi baadaye

Ikumbukwe zoezi hilo kwa Dar es Salaam limeanza Machi 17, 2025 na litaendelea hadi Machi 23, 2025

Soma https://jamii.app/UandikishajiMaoni

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Waziri Kivuli, Ofisi ya Waziri Mkuu-Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira (#ACTWazalendo), Ndolezi Petro amesema ugawaji Majimbo uzingatie maslahi mapana ya Nchi na haupaswi kulenga maslahi binafsi au Kisiasa bali uzingatie idadi ya Watu, Jiografia, upatikanaji wa huduma za kijamii na uchocheaji wa maendeleo ya Kiuchumi

Amesema ugawaji ukiongozwa na tafiti makini na takwimu sahihi, utasaidia kuleta maendeleo badala ya kuwa mzigo kwa Taifa na hautakiwi kuchukuliwa kama nyenzo ya Kisiasa

Soma https://jamii.app/NdoleziUandikishaji

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Rushwa ndani ya Vyama vya Siasa inahatarisha misingi ya #Demokrasia, inadhoofisha #Uwajibikaji na kuzuia maendeleo jumuishi

Je, Vyama vya Siasa vina jukumu gani katika kupambana na #Rushwa ili kujenga Taifa lenye usawa na haki?

Jiunge nasi katika mjadala huu muhimu kujadili changamoto, athari na suluhisho kuhusu Rushwa ndani ya Vyama vya Siasa

Ni Alhamisi, Machi 20, 2025 kuanzia Saa 12:00 Jioni – 2:00 Usiku, kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kujiunga Bofya; https://jamii.app/XSpacesMachi20

#Uwajibikaji #Demokrasia #Maendeleo #KemeaRushwa #RushwaVyamaVyaSiasa #JFWomen
DAR: Akielezea msimamo wa Kisheria wa Sheria ya Huduma za Habari, Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula amesema Serikali na nchi kwa jumla imekubali Uandishi wa Habari ni taaluma kama zilivyo nyingine, hivyo ni lazima kufuata matakwa ya Kisheria

Amesema hata kama Mtu ana kipaji kikubwa kiasi gani, kama hajasoma Taaluma ya Uandishi wa Habari haruhusiwi Kisheria kufanya kazi za Habari

Ameeleza “Kifungu cha 19 (1) cha Sheria ya Huduma za Habari, kinasema Mtu hataruhusiwa kufanya kazi ya Uandishi wa Habari, isipokuwa mtu huyo awe amethibitishwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria.”

Soma https://jamii.app/IthibatiMaelekezo

#PressFreedom #JamiiForums #Governance #FreeSpeech #Democracy #FreedomOfExpression
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, ameagiza kuanza kwa operesheni maalum ya kufuatilia malalamiko kuhusu uwepo wa bidhaa feki na watu wanaofanya biashara kinyume na Sheria katika Soko la Kimataifa la Kariakoo

Ametoa agizo hilo Machi 17, 2025 jijini Dar, wakati akipokea ripoti ya Uchunguzi kutoka kwa wajumbe wa kamati maalum iliyochunguza Biashara za Wafanyabiashara wa Kiigeni hasa katika eneo la Kariakoo

Amesema "TBS na FCC wahakikishe wanashirikiana kufuatilia malalamiko ya bidhaa zisizo na ubora zinazoharibu soko na uchumi wa ndani. Lengo letu ni kulinda maslahi ya Watanzania na kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa nchini zinakidhi viwango vya ubora,”

Soma https://jamii.app/BiasharaHaramuKariakoo

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Ingawa AI inaweza kuharakisha usambazaji wa taarifa na mawazo, jambo linalochochea kwa kiasi kikubwa Uhuru wa Kujieleza, pia inaleta hatari mpya ikiwemo Ukatili wa Kijinsia, Hotuba za Chuki, Upotoshaji wa taarifa na Unyanyasaji Mtandaoni (#Cyberbullying)

Global Digital Compact, ambayo ni nyaraka shirikishi ya Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ya Septemba 2024, inasisitiza kukuza Uadilifu, Uvumilivu na Heshima katika anga za Kidijitali

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Leo Machi 18, 2025 akiwa katika maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yaliyofanyika Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Mjadala wa VETA ufanyiwe kazi kwani una tija

Amesema "Mjadala huu haupiti tu hovyo na mimi nimehushuhudia na naufatilia kwa ukaribu. Hakika una tija kwa sababu wapo ambao wanapinga na kuna ambao wanaongea kurekebisha na wapo ambao wamesema namna nzuri ya kwenda vizuri"

Soma https://jamii.app/MjadalaVetaTija

#JamiiForums #Governance #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji #Ajira #UnemploymentCrisis
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, akizungumza na Wananchi wa Mlowo, Wilaya ya Mbozi, amesema Sera ya CCM inaeleza huduma ya kujifungua pamoja na Watoto wenye umri kuanzia 0 hadi Miaka Mitano kutotozwa fedha, hivyo ni marufuku kuwatoza fedha katika Hospitali za Serikali

Wasira amesema hayo baada ya kujulishwa wanaoenda kujifungua wanatozwa hadi Tsh. 300,000 ili kupata huduma ya kujifungua

Soma https://jamii.app/WasiraSongwe

#JamiiForums #Governance #HumanRights
Mwanachama wa JamiiForums.com amesema baada ya kuomba msaada kwa ndugu zake na kuambiwa afanye kwanza kazi za ndani ndiyo asaidiwe, ilimfanya ajiambie kwamba ni lazima 'atafute hela' hata iwaje

Mdau ulipitia nini hadi ukajiapiza kwa udi na uvumba ni lazima utafute pesa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/LazimaUtafutePesa

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa Kukusanyika ni Haki zinazohusiana moja kwa moja

Huwezi kuwa na Uhuru wa kusema ikiwa huna Haki ya Kukusanyika na wengine, ili kuwasilisha ujumbe wako kwa pamoja

Maandamano ya Amani, Mikutano ya hadhara na Mijadala ya wazi ni sehemu muhimu za Jamii huru na ya Kidemokrasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akipokea ripoti ya Uchunguzi kutoka kwa wajumbe wa kamati maalum Machi 17, 2025, Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo amesema, wamegundulika Wafanyabiashara wa kigeni ambao wanaendesha biashara zao kwa kutumia vibali na nyaraka za Wazawa Nchini kinyume na sheria, na tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa

Ikumbukwe, Februari 2, 2025 Rais Samia Suluhu alitoa agizo kwa Jafo kuunda kamati ya Uchunguzi kuhusu Biashara za Wafanyabiashara wa Kigeni hasa eneo la Kariakoo

Soma https://jamii.app/WageniVibaliWatanzania

#JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji
Upotoshaji umekuwa ukifanyika katika namna tofauti tofauti ikiwemo kuhariri Maudhui halisi yaliyo kwenye grafiki na kuleta maana tofauti.

Ili kuthibitisha uhalisia wa grafiki unayoitilia mashaka, angalia utofauti katika aina ya mwandiko(Fonts), maneno kupishana, au tafuta chanzo halisi kuona iwapo wamechapisha grafiki hiyo.

Unaweza pia kutumia Jukwaa la JamiiCheck.com kuwasilisha Taarifa unazohitaji uhalisia wake.

Soma https://jamii.app/GrafikiKuhaririwa

#VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis05
DAR: Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemuhukumu kifungo cha Miaka Miwili jela, Mchungaji Daud Nkuba 'Komando Mashimo', baada ya kupatikana na hatia ya kuharibu ujenzi wa nyumba mali ya Flora Jonas Mwasha, katika eneo la Mbezi Luis

Hakimu Rugemalira amesema "Kwa shtaka la kuingia kwa jinai, mshtakiwa atatumikia kifungo cha Miezi Sita, kosa la kuharibu mali, atatumikia kifungo cha Miaka Miwili gerezani, vifungo hivyo vitaenda kwa pamoja."

Makosa aliyoshtakiwa; kuingia kwa jinai katika ardhi ya Flora Mwasha, Novemba 22, 2023, kuharibu nyumba (mali) ya Flora Mwasha na kumtishia kwa vurugu Ramson Vicent, shtaka ambalo Jamhuri imeshindwa kulithibitisha, hivyo Mahakama ikamuachia huru

Aidha, baada ya hukumu hiyo, Mchungaji 'Mashimo' aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu, akidai ana familia inayomtegemea

Soma https://jamii.app/MashimoHukumu

#JamiiForums #CivilRights #Governance