JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mara nyingi tunadhani furaha inatokana na kuwa na kila kitu tunachotamani, lakini ukweli ni kwamba furaha hutokana na kuthamini na kufurahia kile tulicho nacho

Furaha si lazima itokane na vitu vikubwa, inatoka ndani yetu tunapojifunza kushukuru na kufurahia vitu vilivyopo

#JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #LifeStyle #LifeTips #MorningQuote
πŸ‘1
Leo ni fursa nyingine ya kujaribu tena, jifunze, na songa mbele. Usiruhusu muda upite bila kufanya kitu cha maana, na kujijenga kuwa bora zaidi.

Maisha hayangoji, na kila siku ni hatua moja mbele kuelekea Ndoto zako.

#JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #LifeStyle #LifeTips #MorningQuote
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com anasema katika zama hizi hakuna haja ya kuwekeza pesa nyingi kwenye elimu rasmi, badala yake Wazazi wawekeze kwenye kuwapatia Watoto ujuzi mbalimbali, ili waweze kujiajiri badala ya kusota wakisubiri ajira

Unakubaliana na hoja za Mdau?

Mjadala https://jamii.app/AjiraAfterChuo

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle #LifeTips
πŸ‘1
Mdau wa JamiiForums.com anasema hawaelewi watu wanaosema kujenga nyumba na kuzika pesa badala ya fursa ya uwekezaji wenye faida kubwa baadae

Amehoji, hivi Mtu aliyejenga Nyumba #Kariakoo Miaka ya 1970 kwa Tsh. laki 1 halafu amekuja kuiuza Mwaka 2021 kwa Tsh. Bilioni 5 utamwambiaje kwamba alizika pesa?

Vipi mdau, upi mtazamo wako?

Mjadala https://jamii.app/GharamaKujenga

#JamiiForums #LifeTips #LifeStyle #JFChitChats
πŸ‘1
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha mjadala na kudai unatakiwa kuchukulia suala la kutengwa na Watu wa karibu kama vile familia, ndugu na marafiki katika hali ya kawaida

Je, Wewe huwa unatumia mbinu gani unapokutana na hali kama hii?

Soma https://jamii.app/WapotezeeWanaokutenga

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
πŸ‘2
Kuna mambo mengi huwa tunapitia na kupambana kuweka sawa. Muda mwingine hakuna anayejua wala kutambua kuwa unapambana

Usikate tamaa endelea kupambana na kuweka mambo sawa kwani baada ya muda utaona matokeo

#JamiiForums #LifeTips #MorningQuote #AmkaNaJF
πŸ”₯3
Mdau ndani ya JamiiForums.com anadai kila akijaribu kufanya maendeleo kwa Wazazi anashindwa kutokana na pesa alizochanga kuishia kwenye mambo ya ovyo bila yeye kujua

Unamshauri nini Mdau huyu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/RohoYaUmaskini

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Ulishawahi kuambiwa "Kuna mishe naisikilizia ikitiki nitakutumia" halafu aliyekuambia akaingia Mitini?

Mjadala zaidi https://jamii.app/UsitegemeeMfukoMwenzako

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips #JFStories #JFChitChats
Mdau ndani ya Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala kuhusu mkewe kudai kuwa ni wajibu wa mume kuijulia hali familia hasa pale anapokuwa mbali na familia

Je, jukumu la kujulia Hali familia ni la mume tu kwenye familia?

Mjadala zaidi https://jamii.app/WajibuKusalimiaFamilia

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Mdau ndani ya Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki ndani ya JamiiForums.com amemeelezea kisa kilichomfanya amfukuze mke wake kisa ndugu na sasa anajuta

Je, unamshauri mdau achukue hatua gani ili mkewe arudi nyumbani?

Mjadala zaidi https://jamii.app/TumeachanaKisaNdugu

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
❀1
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala akielezea kuwa baada ya kupambana kwa muda mrefu sasa amejipata lakini tabia ya Ubahili imezidi kuliko mwanzo

Soma https://jamii.app/NimejipataIlaBahili

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Mdau, uliweza kupata Tsh. Milioni 1 yako ya kwanza ukiwa na umri gani?

Uliipataje?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MilioniYaKwanza

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Mwanachama ndani ya Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki ndani ya JamiiForums.com ameomba ushauri wa nini cha kufanya kwani ana tatizo la kumchukia Mtu anayefanana na adui yake kwa sura

Unamshauri nini Mdau?

Mjadala zaidi https://jamii.app/AkifananaNaAduiYangu

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Mwanachama wa Jukwaa la Habri na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameelezea kisa cha ndugu yake wa karibu kujaribu kumharibia biashara yake baada ya kumshirikisha

Anasema hadi sasa hajamwambia ukweli ila anaumia na hajui achukue hatua gani

Unamshaurije?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KumshirikishaNduguMipango

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Mwanachama wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameelezea kisa chake cha kudhulumiwa mara mbili, lakini amepata moyo wa kusamehe japo anaumia sana kwa kurudishwa nyuma kimaendeleo

Mdau, ulichukua hatua gani ulipodhulumiwa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/UlifanyaNiniUlipodhulumiwa

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
πŸ‘2
Mwanachama wa JamiiForums.com amesema ni muhimu kuwa na Elimu ya pesa β€œFinancial Literacy” ili usijiingize kwenye mikopo ya kifedha na kujikuta na Madeni yasiyoisha

Mdau, pesa ya mkopo haipaswi kutumika kufanyia nini?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KulipaMkopoMajuto

#JamiiForums #LifeTips #Lifestyle
❀2
Mwanachama wa JamiiForums.com amesema baada ya kuomba msaada kwa ndugu zake na kuambiwa afanye kwanza kazi za ndani ndiyo asaidiwe, ilimfanya ajiambie kwamba ni lazima 'atafute hela' hata iwaje

Mdau ulipitia nini hadi ukajiapiza kwa udi na uvumba ni lazima utafute pesa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/LazimaUtafutePesa

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
❀2
Mdau wa Jukwaa la 'Jamii Health' ndani ya JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akihoji ni kwa muda gani soksi au nguo za ndani zinapaswa kuvaliwa kabla ya kufuliwa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/AfyaUvaajiNguo

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
Mdau wa Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki ndani ya JamiiForums.com, anaomba ushauri baada ya kugundua Mpenzi wake ana Watoto Watano, wakati walipoanza Mahusiano alimwambia ana mtoto mmoja

Anasema amemuuliza kama akimuoa atakuwa tayari kuishi na hao Watoto, lakini amekosa jibu

Unamshauri afanye nini?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NimegunduaAnaWatoto5

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
πŸ‘1
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameelezea kuwa alifanya kazi ya Afisa Mauzo 'Sales', ambapo kutafuta wateja kulimtesa na hawezi kuifanya tena

Ni kazi gani uliwahi kuifanya 'ukaapa' hutakaa uifanye tena?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KaziHuweziKuifanya

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
πŸ‘1