JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imesajili Waandishi wa Habari 2,900 kupitia Mfumo wa Kidigitali wa TAI-Habari. Amesema hayo leo Julai 9, 2025 wakati wa Mkutano wa Wadau wa Habari kujadili Mchango wa Sekta ya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ikumbukwe, Julai 4, 2025, Bodi hiyo iliagiza Waandishi wote wanaoendelea kufanya kazi kwenye Vyombo vya Habari vya uchapisho na kielektroniki, bila kusajiliwa wanatakiwa kuacha mara moja shughuli zao hadi pale watakapokamilisha usajili

Bodi ilieleza kufanyakazi bila kujisajili ni kuvunja Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari, kinachokataza mtu yeyote kufanya kazi za kihabari bila kibali rasmi

Zaidi soma https://jamii.app/WadauWaHabari

#PressFreedom #JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #KuelekeaUchaguzi2025 #UhuruWaHabari
UPDATES: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (#THBUB) imepokea malalamiko ya wafanyabiashara waliodaiwa kupigwa na askari wa Mamlaka ya Mji Mkongwe, kati ya tarehe 26 na 27 Juni 2025 katika eneo la Darajani, Wilaya ya Mjini, Zanzibar ambapo uchunguzi wa tukio hilo umeanza Julai 8, 2025 ili kubaini ukweli wake

Pia, THBUB imesisitiza juu ya Umuhimu wa Kuheshimu na kulinda haki za binadamu nchini, na kuviomba vyombo vinavyohusika na Usimamizi wa Haki Jinai na Mamlaka nyingine zenye mamlaka ya ukamataji kisheria kuzingatia Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora wakati wa utekelezaji wa majukumu yao

Hili limekuja baada ya taarifa ya wafanyabiashara hao kupigwa kusambaa katika mitandao ya kijamii ikiwemo JamiForums.com, ambapo mbali na kupigwa inadaiwa waliingizwa kwenye pipa la maji machafu

Soma zaidi https://jamii.app/ZanzibarKupigwaPolisi

#JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #HumanRights #Governance #JamiiForums #HakiZaBinadamu
Akizungumza katika Mkutano wa Wadau kujadili mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025, Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko amesema Vyombo vya Habari vimekuwa chanzo cha ajira kwa Watu katika upande wa Magazeti, Redio, Vyombo vya Habari vya Mtandaoni, Runinga pamoja na 'Blogs'

Zaidi soma https://jamii.app/WadauWaHabari

#PressFreedom #JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #KuelekeaUchaguzi2025 #JFDATA #UhuruWaHabari
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Wadau wa Sekta ya Habari na wengine kuwa kuelekea wakati wa Uchaguzi Mkuu kuwe na kuvumiliana na kukubali kuwapa nafasi Watu kutoa mawazo yao

Amesema hayo wakati wa Mkutano wa Wadau kujadili mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo pia amepata nafasi ya kuzindua Mfumo wa Vitambulisho kwa Waanahabari katika mfumo wa Kitigitali kupitia TAI-Habari, leo Julai 9, 2025

Zaidi soma https://jamii.app/WadauWaHabari

#PressFreedom #JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #KuelekeaUchaguzi2025 #JFDATA
2
Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (#NECTA) kutangaza matokeo ya Kidato cha Sita 2025, wanafunzi wamepokea matokeo hayo kwa hisia tofauti. Wapo waliopata alama nzuri na kufuzu kujiunga na vyuo vikuu, wakiwa na matumaini mapya ya Mafanikio ya Kielimu

Hata hivyo, wengine hawakufikia viwango vya kuendelea na elimu ya juu. Kwao, huu ni wakati wa tafakari, matumaini mapya na kutafuta njia mbadala za kujenga maisha yao

Kama Mdau wa Elimu, unamshauri nini mwanafunzi ambaye hakupata matokeo mazuri?

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/UshauriKidatoChaSita

#JamiiForums #JamiiAfrica #Elimu #Huduma #JukwaaLaElimu #JFElimu
1
Kampuni ya Novartis kwa kushirikiana na Shirika la Medicines for Malaria Venture (#MMV) imetangaza kupokea kibali kutoka Mamlaka ya Dawa nchini Uswisi kwa dawa ya kwanza Duniani ya kutibu #Malaria kwa watoto wachanga iitwayo 'Coartem Baby' au 'Riamet Baby' kwa baadhi ya nchi, ikilenga watoto wenye uzito kati ya kilo 2 mpaka 5, ambao awali hawakuwa na tiba iliyothibitishwa kutibu Ugonjwa huo

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la #Reuters, Nchi nane za Africa; Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Burkina Faso na Ivory Coast, zilishiriki katika tathmini ya dawa hiyo na zinatarajiwa kuidhinisha matumizi yake ndani ya siku 90, huku Ghana ikiwa tayari imeshaidhinisha

Dawa hiyo inatarajiwa kusaidia Kuboresha utoaji wa Huduma za Afya, Kupunguza Vifo vya Watoto na kuchangia katika lengo la muda mrefu la Kutokomeza Malaria Duniani


Zaidi soma https://jamii.app/TibaMalariaWatotoWachanga

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #JFAfya #Malaria
1
DAR: Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (#UTPC), Kenneth Simbaya amesema kuelekea katika #UchaguziMkuu2025, taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Wadau mbalimbali kutoa elimu ya masuala ya taarifa potofu ili kuhakikisha Jamii inapata taarifa sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi pia.

Amesema “Katika kutekeleza hilo tunashirikia na Wadau kuhakikisha Wanahabari wanakuwa Watu wa kwanza kutoa taarifa sahihi, baadhi ya Wadau tunaoshirikiana nao ni #JamiiAfrica katika kutoa elimu kwa Wanahabari na Wananchi kuhusu umuhimu wa Uhakiki wa Habari na njia za kuhakiki taarifa mbalimbali.”

Amesema hayo wakati akifanya wasilisho la Mada katika Mkutano wa Wadau kujadili mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025, leo Julai 9, 2025, ambapo ameongeza kuwa kuruhusu kusambaa kwa taarifa potoshi inaweza kuchangia kuharibu mchakato wa uchaguzi.

Zaidi soma https://jamii.app/UTPCNaJamiiAfrica

#HakikiTaarifa #JamiiForums #Democracy #FackChecking #FactsCheck
Lugha ya chuki kama maneno, jumbe au kauli zinazodhalilisha, huleta chuki na kuchochea vurugu dhidi ya watu hasa kupitia mitandao ya kijamii. Hii ni hatari kwa sababu inaweza kusababisha mgawanyiko wa kijamii, vurugu au hata vita

Hivyo ni muhimu watu kupewa elimu ya kuweza kutambua lugha ya chuki, kuelewa madhara yake na kujifunza namna ya kuwasiliana kwa heshima, uvumilivu na amani.

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo la Katoliki Musoma amesema watu hawatakiwi Kuhonga au Kuhongwa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, bali wasikilize Sera na Kuchagua wagombea Wanaostahili

Askofu Msonganzila ameyasema hayo akizungumza na Walei Siku ya Pentekoste, June 8, 2025, Kiabakari - Musoma

Soma https://jamii.app/AskofuMsongazila

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Democracy #Kuelekea2025 #Demokrasia #Uchaguzi2025
1
DAR: Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (#DCEA), Aretas Lyimo amesema "Mamlaka imebaini kuwa kwa sasa Dawa hizo zinasafirishwa kupitia maiti hususan maiti kupasuliwa kichwa na kuondoa ubongo na kisha dawa hizo kuwekwa kwa ajili ya kusafirishwa"

Aidha, amesema kuwa katika operesheni maalum iliyofanyika nchi nzima kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, wamefanikiwa kukamata kiasi cha kilo 37,197.142 za dawa hizo na watuhumiwa 64 wamekamatwa

Ameyasema hayo leo Julai 9, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa ya utendaji kwa kipindi cha Mwezi Mei hadi Julai, 2025

Soma https://jamii.app/RipotiDawaZaKulevya

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #DawaZaKulevya
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (#TARURA) kushughulikia haraka barabara ya Mbezi Beach-Makonde inayoelekea Kanisa Katoliki Mbezi Juu, akidai kuwa imekuwa Kero kwa watumiaji kutokana na mashimo mengi na miundombinu duni

Mdau huyo amehoji uwepo wa mkandarasi aliyelipwa bila kutekeleza kazi kwa viwango stahiki, hali inayozua wasiwasi wa Ubadhirifu wa fedha za umma, maana barabara hiyo ilikwanguliwa kwa greda kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini haikuboreshwa

Ametoa wito kwa TARURA kutenga bajeti ya kudumu kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo, kutokana na umuhimu wake kwa wakazi wa eneo hilo na kushauri kuwa na mpango endelevu kuzingatia maslahi ya wananchi

Soma https://jamii.app/MdauBarabaraMbeziMakonde

#JamiiAfrica #JamiiForums #ServiceDelivery #Uwajibikaji #JFHuduma #Accountability
Mkurugenzi Mtendaji wa X, Linda Yaccarino atangaza kujiuzulu kutoka nafasi hiyo kwa kushtukiza bila kutoa sababu za uamuzi wake

Kujiuzulu kwake kumekuja siku moja tu baada ya roboti wa mazungumzo ya AI (Grok) iliyotengenezwa na Kampuni ya xAI inayomilikiwa na Elon Musk kuchapisha maudhui yaliyomtaja Adolf Hitler kwenye jukwaa hilo

Aidha, machapisho hayo ya Grok yalifutwa baadaye kufuatia hasira na malalamiko kutoka kwa watumiaji

Soma https://jamii.app/LindaYaccairoKujiuzulu

#JamiiAfrica #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa wito kwa Wanahabari kuwa na kawaida ya kuhakiki Taarifa kabla ya kusambaza kama ambavyo imekuwa ikifanywa na JamiiCheck.com

Msigwa amezungumza hayo wakati akichangia mada katika Mkutano wa Wadau kujadili Mchango wa Sekta ya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, leo Julai 9, 2025

Amesema “Nimeona Watu wa JamiiForums wana kitu kinaitwa JamiiCheck, wanachofanya ndio kilekile tulichojifunza shuleni kwamba unachotaka kukichapisha jiridhishe kuwa ni sahihi?”

Soma https://jamii.app/MsigwaOnJamiiCheck

#JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck
2
Kuheshimu Muda si suala la saa pekee, ni kujifunza Kuthamini Ahadi na Juhudi zako katika kufanikisha jambo fulani, Kupanga Maisha kwa Nidhamu na kujipa Heshima Binafsi.

Unapojifunza kuwa na Utaratibu, unajenga tabia ya Kuwajibika, Kuaminika na kufikia Malengo yako kwa Ufanisi.

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Mdau wa JamiiForums kwenye Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali amependekeza mbinu bora za kusaidia wafanyabiashara kukuza na kuimarisha biashara zao zaidi.

Kama mteja au mfanyabiashara, mbinu gani nyingine unazozifahamu?

Soma https://jamii.app/MbinuBiashara

#JamiiAfrica #JamiiForums #JukwaaLaBiashara #Biashara #JFBiashara
1