JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kesi ya Msingi Na. 8323/2025 iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed (aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA Zanzibar) na wenzake wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA inatarajiwa kuendelea leo Julai 10, 2025 mbele ya Jaji Hamidu Mwanga katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam. Awali, ilipangwa kusikilizwa Juni 24, 2025, lakini iliahirishwa kutokana na majukumu ya Jaji huyo mkoani Mtwara

Waleta maombi kupitia wakili wao Gido Simfukwe waliiomba Mahakama kutoa zuio kwenye shughuli za chama hicho hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa wakidai CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala ya msingi, ikiwemo mgawanyo wa rasilimali za chama

Soma https://jamii.app/KesiYaChadema

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #Siasa
ZANZIBAR: Kesi ya mauaji ya Sheikh Jabir Haidar Jabir imeahirishwa na Mahakama Kuu ya Zanzibar hadi itakapotajwa tena tarehe 16 Julai 2025. Watuhumiwa wote sita waliopandishwa kizimbani walikana shtaka hilo mbele ya Jaji Khadija Shamte Mzee

Wakili kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka, Anuwar Saaduni ameeleza kuwa watuhumiwa Salum Manja Ame (23), Idrisa Kijazi Kasim (41), Ali Mohamed Ali (30), Ali Machano Haji (30), Zahor Khamis Ali (54) na Mohamed Hassan Jongo (38), wote wakazi wa Zanzibar, walipanga na kutekeleza mauaji hayo kwa makusudi na wanaendelea kushikiliwa rumande kutokana na uzito wa kesi hiyo

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwezi Mei, 2025, ambapo Sheikh Jabir Haidar alikutwa amefariki Bumbwisudi polisi wakisema hakuwa na majeraha yeyote na mazingira hayakuonesha dalili zozote za vurugu

Zaidi soma https://jamii.app/MauajiYaSheikhJabir

#HumanRights #JamiiAfrica #HakiZaBinadamu #JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability
AFRIKA: Ripoti mpya ya Shirika la #Oxfam imebainisha kuwa watu wanne matajiri zaidi Barani Afrika wanamiliki Utajiri wa jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni 57.4 (Takriban Tsh. Trilioni 149), kiasi ambacho ni kikubwa kuliko kile kinachomilikiwa na nusu ya wakazi wote wa bara hilo wapatao Milioni 750

Matajiri hao ni Aliko Dangote wa Nigeria (Dola Bilioni 23.3), Johann Rupert na Familia yake (Dola Bilioni14.2) na Nicky Oppenheimer na Familia yake (Dola Bilioni 10.2) kutoka Afrika Kusini, pamoja na Nassef Sawiris (Dola Bilioni 9.4) kutoka Misri

Oxfam imesema Sera nyingi za Serikali barani Afrika zinawapa upendeleo matajiri hivyo kuongeza utajiri wao bila kikomo huku zikiwaumiza maskini

Shirika hilo limeonya kuwa Pengo hilo la Usawa linakwamisha Demokrasia, kuathiri juhudi za kupunguza Umasikini, na kuchochea mgogoro wa Mabadiliko ya Tabianchi barani Afrika.

Soma https://jamii.app/MatajiriZaidiAfrika

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchumiAfrika #JFUchumi
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais wa #Kenya William Ruto ameagiza Polisi kuwapiga risasi za miguu waandamanaji wanaoharibu mali za watu ili kuwazuia kufanya uharibifu huo bila kuwaua. Agizo hilo limekuja baada ya baadhi ya waandamanaji kuvamia maduka na ofisi na kuiba pamoja na kuharibu bidhaa kwenye maandamano yaliyofanyika Julai 7, 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa (#UN) na Mashirika ya Haki za Binadamu, yaliishutumu Polisi kwa matumizi makubwa ya nguvu katika Maandamano yanayojiri kuipinga serikali ya Kenya ambapo katika Maandamano ya 77 watu 31 waliripotiwa kuuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa

Kenya katika kipindi cha karibuni imekumbwa na wimbi la maandamano yanayodai kuondoka kwa Rais Ruto madarakani, yakiongozwa na kauli maarufu ya "Ruto must go" ambapo waandamanaji wanalalamikia hali ngumu ya maisha, ongezeko la kodi, pamoja na ukatili unaofanywa na Polisi kwa wananchi

Soma zaidi https://jamii.app/RutoRisasiMiguuni

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #KenyanPolitics #Uwajibikaji #HakiZaBinadamu #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Iddy Kimanta amesema matatizo yanayotokana na Lishe duni kwa mtoto yanaweza kusababisha #Udumavu na kuathiri uwezo wa kufanya maamuzi na utendaji wake kwa ujumla akitolea mfano uwezo wa viongozi wa Umma katika nafasi mbalimbali kufanya maamuzi

Akizungumza katika Mafunzo ya Waandishi wa Mtandao wa Mapambano dhidi ya Udumavu, Juni 26, 2025 na kutoa mifano ya Udumavu alisema "Unaweza ukakuta Afisa Mkubwa tu mwenye 'degree' mbili lakini faili likienda kwake siku nne halijatoka, anasoma na kurudisha, unashindwaje kutoa maamuzi? Au pale Bungeni, unakuta Mbunge anaongea mapaka unasema 'Eh, ni Mbunge huyu?'"

Soma https://jamii.app/MwenyekitiCCMKatavi

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Accountability #JFHuduma #Udumavu #LisheBora
MBEYA: Mdau amelalamikia ukosefu wa taa za kuangaza usiku katika Kituo cha Mabasi cha Nanenane Jijini Mbeya akisema hali hiyo imekuwa kero kwa watumiaji wa kituo hicho kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa

Anahoji Mamlaka ziko wapi mpaka kushindwa kuchukua hatua ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kwa kukosa mwanga usiku?

Soma https://jamii.app/KituoChaMabasiNanenane

#JamiiAfrica #JamiiForums #Huduma #Uwajibikaji #Accountability
DAR: Kesi ya mgawanyo wa rasilimali za #CHADEMA iliyokuwa inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeahirishwa hadi Julai 14, 2025.

Ahirisho la kesi hiyo limekuja baada ya Mawakili wa upande wa waleta maombi kuiomba mahakama kupata muda wa kwenda kuisoma na kutafakari barua iliyopelekwa mahakamani hapo na upande wa wajibu maombi (Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu)

Aidha, Wakili Mpoki ameileza mahakama kuwa walichelewa kuupatia upande wa waleta maombi nakala ya barua kutokana na kwamba barua hiyo ilikuwa ni ya mahakama tu hivyo hawakufahamu kama upande wa waleta maombi wanapaswa kupatiwa nakala ngumu

Kuahirishwa kwa kesi hiyo kunaathiri maombi ya CHADEMA ya kuhusu mahakama kufuta uamuzi wa kusimamishwa kwa shughuli za chama ambapo Jaji Mwanga amesema maombi hayo madogo yatafanyiwa kazi baada ya uamuzi kutoka wa yeye kuendelea na kesi hiyo au lah

Soma https://jamii.app/KesiZuio

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #KuelekeaUchaguzi2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo la Katoliki Musoma amehoji kwanini Mtu anaposema Mauaji yanatendeka anachukuliwa kuwa Mbaya? Akiuliza kuna kigugumizi gani kusema yanatendeka? Pia, ameongeza kuwa, wauaji wa #Albino walipatikana haraka sana, sasa kwanini wauaji wa watu wengine ndio hawapatikani?

Askofu Msonganzila ameyasema hayo akizungumza na Walei Siku ya Pentekoste, June 8, 2025, Kiabakari - Musoma

Soma https://jamii.app/AskofuMsonganzilaMauaji

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #WatuWasiyojulikana #HumanRights #HakiZaBinadamu
3👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KUMBUKIZI: Balozi wa Tanzania nchini #Cuba, Humphrey Polepole aliwahi kutoa kauli kuhusu mwenendo wa baadhi ya Viongozi wa Umma kujificha kwenye Mitandao ya Kijamii, akitolea mfano Mtandao wa #WhatsApp akisema huo ni Ulaghai na Uhuni

"Wewe Kiongozi wa Umma simu yako kwenye WhatsApp ukitumiwa ujumbe kwanza haunokeni 'last seen' yako, ukiwa 'online' hauonekani, akikutumiwa ujumbe kwenye WhatsApp umeweka tiki za grey (kijivu) badala ya kuwa bluu na wewe ni Kiongozi wa Umma, huo ni Ulaghai yaani huo ni Uhuni"- alisema Balozi Polepole

Zaidi soma https://jamii.app/HumphreyPolepoleUwaziNaUwajibikaji

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji #UtawalaBora #Siasa

Video: Swahili Digital
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Chama cha ACT Wazalendo, leo Julai 10, 2025, kimetoa taarifa kuwa Jeshi la Polisi kupitia Makamanda na Maofisa wake Waandamizi wamekuwa wakifanya mawasiliano na baadhi ya Viongozi wao kuomba majina ya wagombea wa Ubunge na Udiwani, huku baadhi ya Wakuu wa Wilaya pia wakipiga simu kuhitaji taarifa hizo

Maeneo yaliyoripotiwa kwa Jeshi la Polisi kuhitaji taarifa hizo ni Kilwa, Kigamboni, Kinondoni, Magu na Tarime, jambo ambalo ni kinyume cha sheria

#ACTWazalendo imelalamikia hatua hiyo kwa IGP, Msajili wa Vyama na Tume ya Uchaguzi, na kuwataka viongozi wake kupuuza maombi hayo yasiyo halali

Soma https://jamii.app/ACTPolisinaWakuuWaWilaya

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Democracy #Demokrasia #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Siasa
DODOMA: Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi kufuatia madai ya Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu kuwa Chama hicho kimemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi kuhusu baadhi ya Viongozi wake kutakiwa kuwasilisha taarifa na majina ya watia nia wa kugombea Ubunge na Udiwani

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, tarehe 10 Julai, 2025 imesema barua hiyo haijamfikia Mkuu wa Jeshi la Polisi lakini endapo itamfikia, itafanyiwa kazi haraka ili kubaini ukweli wake na chanzo cha mawasiliano hayo

Soma https://jamii.app/ACTNaPolisi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Accountability
Mradi wa Mji wa Kisasa wa Msanii Aliaune Thiam 'Akon' - 'Akon City', wenye thamani ya Tsh. Trilioni 15.5, umefutwa rasmi baada ya kufeli kukamilisha ujenzi. Serikali ya Senegal imechukua eneo hilo la ardhi na sasa inapanga kuwekeza Tsh. Trilioni 3.1 kujenga Hoteli na Nyumba za Kupanga kwa ajili ya watalii katika eneo hilo lenye utajiri wa fukwe

Akon City ilipangwa kukamilika Awamu ya Kwanza Mwaka 2023 na Awamu ya Pili Mwaka 2030, lakini ujenzi ulisimama kutokana na janga la UVIKO-19 pamoja na ukosefu wa Fedha. Hadi mwaka 2024, ujenzi ulikuwa umefikia msingi wa jengo la mapokezi pekee

Zaidi soma https://jamii.app/AkonCityYafeli

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #AkonCity
Mdau ameeleza kutoridhishwa na utendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) akitoa mfano kwa kudai Mafunzo ya Mtaala mpya kwa Walimu yamefanyika haraka haraka katika mazingira ya ‘juujuu’ jambo linaloweza kusababisha wengi wao kutoelewa vizuri

Pia, anadai Walimu wengi walioshiriki mafunzo hayo na kuahidiwa posho hawajalipwa kama ilivyopangwa hali anayodai inaweza kuchangia kurudisha nyuma morali kwa Walimu

Mdau ameitaka TET ambayo ni Taasisi ya Umma iliyo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha utekelezaji wa Sera za Elimu unafanyika kwa ufanisi na kwa wakati.

Soma https://jamii.app/KeroMtaalaMpyaWaElimuTET

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Elimu
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (#TEC), Padri Charles Kitima amesema kuwa Kazi ya Kanisa ni kutetea Uhai wa Binadamu na kukemea Uovu bila Hofu, na kufanya hivyo ni kutimiza wajibu wa Kidini na Kibinadamu

Ameongeza kuwa "Unaposema tusitetee Uhai wa Mtu, Mdude honekani, Ali Kibao amekamatwa kwenye halaiki mchana, Soka haonekani, halafu unasema tunyamaze? Uovu lazima tuukemee!”

Padri Kitima ameyasema hayo Julai 8, 2025, Dar es Salaam akiwa katika mahojiano na Jambo TV

Soma https://jamii.app/KitimaWajibuWaKidini

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Uwajibikaji #Accountability #HakiZaBinadamu
MICHEZO: Mdau, wewe kama mpenzi wa #Soka kindakindaki ulikuwa unafahamu kuhusu Historia ya Mchezo huo?

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/HistoriaMpiraMiguu

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica #Football