JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini Taifa, Ameir Hassan Ameir amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, atahakikisha kila mwananchi analipwa mshahara wa Tsh. 500,000 kwa mwezi, akilenga kujenga Zanzibar yenye Usawa wa Kiuchumi na mustakabali bora kwa wote

Amesema hayo Julai 10, 2025, kwenye kikao kazi, kilichojadili utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 hadi 2025 na matarajio ya ilani ya mwaka 2025 hadi 2030

Zaidi, soma https://jamii.app/AmeirNikichaguliwaRais

#JamiiForums #JamiiAfrica #KuelekeaUchaguzi2025
Kama raia, una nafasi ya kujielimisha kila siku. Tumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu, soma mabango ya Serikali barabarani, na sikiliza mijadala ya Bunge. Ndipo utaelewa haki zako, wajibu wako, na jinsi ya kushiriki kwenye maamuzi yanayogusa maisha yako.

Uraia ni zaidi ya kupiga kura ni kushiriki, kujua na kuwajibika

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
Chukua hatua kwa ajili ya mafanikio yako mwenyewe.

Maisha hayaendi kwa huruma wala msaada kila wakati, ukitaka kufika mbali, ni lazima ujitoe na uweke juhudi zako mwenyewe.

Hakuna atakayekupigania kama hujajitokeza kujipigania kwanza.

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
3👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kwa mara ya kwanza, China imeandaa mechi ya Soka inayochezwa na Roboti wa umbo la binadamu (humanoid robots) wanaojiendesha kwa kutumia Akili Unde (#AI), bila msaada wa Binadamu

Mechi hiyo ilifanyika mwishoni mwa mwezi Juni, 2025 katika Chuo Kikuu cha Tsinghua, Beijing, kama maandalizi ya Mshindano ya Dunia ya Roboti (World Humanoid Robot Games) yatakayofanyika Agosti 2025. Roboti hao walitumia AI kutambua mpira, kuchambua mazingira, kufanya maamuzi na kucheza

Licha ya Roboti hao kuangukaanguka na kuwaacha watazamaji 'wakifa mbavu' kwa vicheko, tukio hili linaonesha mafanikio makubwa Kiteknolojia nchini humo na huenda kwa miaka ijayo yakashuhudiwa Mapinduzi makubwa kwenye ulimwengu wa Soka

Fuatilia zaidi https://jamii.app/ChinaRobotiSoka

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFTeknoloji #JFTech #AkiliUnde #AI #Soka #Michezo #JFSports #HumanoidRobots
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mchambuzi wa Masuala ya Siasa, Deus Kibamba, amaesema 'Unono' wa #Siasa unafanya watumishi wengi wa umma wakimbilie huko kwasababu inaonekana ndio njia pekee ambayo mtu anaweza kutajirika na kuishi mazuri hivyo maeneo mengine yanakosa watu wenye weledi, na kwamba usipodhibitiwa basi nchi itachelewa sana kupata maendeleo

"Tusipodhibiti unono wa kazi ya siasa nchi hii maendeleo tutasubiri sana. Kwasabbabu Prof. wa Chuo Kikuu, Daktari Bingwa wa Upasuaji wanaacha (majukumu) yao wanakimbilia bungeni. Sijasema tuwe masikini, lakini huwezi kuwa nchi ambayo ili Utajirike ni lazima uingie Bungeni tu. Haiwezekani hata kidogo!"

Deus ameyasema hayo Julai 10, 2025, Dar es Salaam akiwa katika Kipindi cha Mada Kuu - TBC

Soma https://jamii.app/DeusKibambaMaslahiYaNchi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #UchaguziMkuu2025 #Siasa
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, akiwa kizimbani Mahakamani aliingia kwenye mvutano mkali na Askari Magereza wakati anajadiliana jambo na Mawakili wake ambao inadaiwa kuwa alizuiliwa kuongea nao Mahakamani hapo.

Ikumbukwe leo Julai 11, 2025, Lissu alifika Mahakama Kuu masijala ndogo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza shauri la maombi alilofungua, akipinga uamuzi uliotolewa Juni 2, 2025 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa kesi yake ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni

Soma https://jamii.app/MzozoWaibukaMahakamani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Accountability
1
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuandika “Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuweni 'serious' na elimu yetu, kuna uzembe mkubwa unaosababisha kuchelewesha mambo”, akitaja Mtaala Mpya wa Kidato cha 5 na 6 kuchelewa kuanza, kasi ndogo ya kugawa vitabu, Walimu kutoelimishwa vizuri kuhusu Mtaala huo na kutolipwa posho za mafunzo, TET imefafanua

TET imesema Mtaala uliahirishwa na taarifa iliwekwa wazi, kuhusu vitabu vimeshasambazwa, pia Walimu waliopo kazini walipata mafunzo ya muda mrefu (Pre-service) na sasa Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo endelevu (MEWAKA) ngazi ya shule katika siku moja ya kila wiki

Taarifa imeeleza “Malipo ya posho yanahusisha kuwasilisha taarifa sahihi za Kibenki, baadhi ya Walimu hawakuzingatia hilo, hivyo kukatokea ucheleweshaji wa malipo, tuliwasiliana nao, wakarekebisha na wakalipwa, bahati mbaya baadhi walichelewa kurekebisha taarifa zao na ikafika mwisho wa Mwaka wa Fedha.”

Soma https://jamii.app/TETUfafanuzi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Elimu
1
Julai 11 ya kila mwaka ilipitishwa na Umoja wa Afrika (#AU) kuwa Siku ya Mapambano dhidi ya #Rushwa Barani Afrika. Kwa Mwaka 2025, maadhimisho haya yamebeba kaulimbiu “Kudumisha Hadhi ya Binadamu katika Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika.”

Mdau, ni kitu gani huwa kinakufanya Usitoe Taarifa unapoona Tukio la Rushwa?

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/MapambanoRushwa2025

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #AfricaAgainstCorruption #KemeaRushwa
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Maombi ya Tundu Lissu ya kutaka kurejelewa kwa uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kisutu wa kuahirisha kesi yake ya kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni, imetupiliwa mbali na Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo Julai 11, 2025 ikieleza kuwa maombi hayo yalipaswa kusubiri hadi kesi ya msingi itakapokamilika ndipo yaweze kuwasilishwa Mahakama Kuu

Awali, Hakimu Mfawidhi Godfrey Mhini aliahirisha kesi hiyo Juni 2 baada ya upande wa Jamhuri kuomba mashahidi wao watoe ushahidi kwa kificho, jambo ambalo Wakili wa Lissu, Hekima Mwasipu, alisema halikuwa na msingi wa kisheria

Baada ya uamuzi huo wa Mahakama Kuu leo, Wakili Mwasipu amesema wameridhika na watachukua hatua zaidi pale itakapohitajika.

Zaidi https://jamii.app/KesiYaTunduLissuKuahirishwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Kiongozi Mstaafu wa #ACTWazalendo, #ZittoKabwe amesema Chama hicho hakitavumilia majaribio ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuingiza Kura bandia, amesema hayo Julai 10, 2025, Tunduru Kaskazini katika mwendelezo wa Operesheni Majimaji ya Chama hicho, ambapo ametoa angalizo kwa Jeshi la Polisi kutojiingiza katika "mchezo" wa Kura Bandia

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiNaKuraBandia

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Governance
Mdau wa JamiiForums.com ameandika “Naomba Maafisa wa TAKUKURU - Uyui, mfuatilie na kuleta mrejesho stahiki na wa haki, suala la mama Mkazi wa Kijiji cha Izumba ambaye Askari wa Kituo cha Polisi Kigwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kigwa walimlaghai na kuchukua pesa zake ili mume wake aachiwe huru baada ya kukaa Kituo cha Polisi Kigwa kwa zaidi ya wiki moja.”

Anaongeza “Suala hilo lilielekezwa na Kamanda TAKUKURU Mkoa lishughulikiwe na Kamanda TAKUKURU Wilaya ya Uyui lakini limekwama vipi? Mbona waathirika wa Rushwa hawapati haki yao?”

Upande wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (#TAKUKURU) imesema inafahamu suala hilo na taarifa hiyo inafanyiwa kazi, kwa sasa uchunguzi unaendelea kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.

Zaidi soma https://jamii.app/TAKUKURUTabora

#Accountability #JamiiForums #Uwajibikaji #JamiiAfrica
1
Ripoti ya #UNAIDS iliyozinduliwa Julai 10, 2025 nchini Afrika Kusini imeonya kuwa kusitishwa ghafla kwa Ufadhili wa Marekani kupitia mpango wa #PEPFAR kumeacha pengo kubwa katika mapambano dhidi ya #UKIMWI. Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima amesema bila hatua za haraka, watu wengine milioni sita wataambukizwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne ijayo, huku vifo vikikadiriwa kuwa milioni nne zaidi

UNAIDS imetoa wito kwa nchi kuchukua hatua za haraka kupambana na Janga la UKIMWI hasa kipindi hiki ambapo hakuna uhisani wa PEPFAR

Aidha, Aprili 9, 2025 akiwasilisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema watu elfu 60 hupata maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini kila mwaka ambapo 34.3% ya maambukizi hayo ni kundi la vijana

Soma https://jamii.app/MaambukiziUKIMWIKuongezeka2029

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #JFAfya
1
Mahakama ya Rufaa ya Paris nchini Ufaransa imewafutia kesi wanawake wawili ambao ni Amandine Roy na Natacha Rey waliodaiwa kueneza madai ya kwamba mke wa Rais Ufaransa Brigitte Macron alibadili jinsia kuwa mwanamke, madai ambayo yalichapishwa kwenye mtandao wa Youtube mwaka 2021 

Awali, mahakama moja huko nchihi Ufaransa iliwaamuru wawili hao walipe fidia ya euro 8,000 kwa Brigitte na euro 5,000 kwa kaka yake, kutokana na kauli hizo ambazo Rais Emmanuel Macron aliwahi kuziita kuwa ni za  “uongo” na “zinazokera.”

Kwa miaka kadhaa sasa, tetesi kuhusu jinsia ya Brigitte Macron zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini Ufaransa, zikidai kwamba Brigitte alizaliwa mwanaume lakini baadaye alibadili jinsia na kuwa mwanamke alipokuwa mtu mzima.

Kushiriki mjadala huu pitia: https://jamii.app/MkeWaMacron

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Governance 
Kila hatua ndogo ya ujasiri unayochukua huleta mwelekeo mpya, inaweza kufungua mlango wa fursa, matumaini na mwanga wa kesho.

Usingoje hadi mambo yote yawe sawa, anza na kilichopo

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuimarisha doria na misako nchi nzima, Usiku na Mchana, kuelekea Uchaguzi Mkuu na hata baada ya Uchaguzi ili kuhakikisha hakuna Wageni wenye nia ya kuvuruga amani

Amesema hayo Julai 11, 2025, wakati wa uzinduzi wa jengo la Uhamiaji, Wilaya ya Busega lililofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), ambapo ameagiza mapingamizi ya uraia kwa Wagombea yashughulikiwe kwa haraka na kwa kufuata Sheria kwa kushirikiana na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutoa elimu kwa Umma kuhusu masuala ya uraia.

Pia, amewataka Wananchi kuwa raia wema kwa kutoa taarifa kwa Vyombo vya Dola pindi wanapohisi uwepo wa mgeni au tukio lolote linaloashiria uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

Shiriki Mjadala https://jamii.app/BashungwaWageni

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Accountability #JFDiplomasia
DAR: Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Kiomoni Kibamba akizungumza na ITV, Julai 11, 2025 amesema atawapeleka Mahakamani Mawakili waliomdhalilisha akidai wamlipe Tsh. Bilioni 2

Awali, Wakili Doris Kafuku akizungumza kwa niaba ya Mawakili wanaopinga mchakato wa Uchaguzi huo alisema “Huyu anayejiita Wakili Kiomoni aliyetajwa kuongoza Kamati ya Uchaguzi hajahuisha leseni ya Uwakili tangu Mwaka 2023, Mtu kama huyu tunamchukulia kama Kishoka na tutamchukulia hatua za Kisheria.”

Ikumbukwe Julai 4, 2025, Wakili Kiomoni akizungumzia kuenguliwa kwa Wagombea Wanne wa Urais huku akisalia Wallace Karia kuwa Mgombea pekee, alisema “Ukisikia Mawakili wanavyoongea utasema wana mambo ya maana ya msingi, waache kukurupuka, wakasome upya Ibara ya 14 ya Kanuni za FIFA (toleo la Mwaka 2024).”

Soma https://jamii.app/WakiliKibamba

#JFSports #JamiiForums #Accountability
1
Opportunity Alert: Consultant for Quarterly Media Monitoring: Data Collection and Preparation

JamiiAfrica, through the “Empowering Journalists for Informed Communities (2025–2027)” funded by the European Union and jointly implemented with IMS and UTPC, is seeking a consultant to monitor the media landscape and to collect and prepare data on mis-/disinformation, hate speech and online gender-based violence (OGBV).

Key Deliverables
• Provide a convincing strategy on how to conduct the monitoring
• Provide access to a functional database or dashboard containing all the data categorized by type
• Timely submission of high-quality and well-structured quarterly reports entailing all the relevant data.
• End of Activity Report explaining the procedure and all lessons learned.

Submit Your Proposal with cover letter, previous experience, CV and/or company portfolio and consultancy budget breakdown by 17th July 2025.

For more info visit https://jamii.app/ConsultantMediaMonitoring