MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com ameeleza hofu juu ya usalama wa Abiria katika Stendi Kuu ya Nyegezi, ambapo geti linalotumiwa na daladala kutoka stendi kwenda Barabara Kuu pia linatumika kupita Abiria wanaoingia stendi kutoka Barabara Kuu, huku mlango rasmi wa abiria ukiwa umefungwa
Pia, amedai eneo hilo, kuna vibaka wanaojifanya madalali wa tiketi na kuwaibia abiria, hasa wageni.
Mdau ameiomba Mamlaka husika kufungua mlango wa abiria
Soma https://jamii.app/MdauGetiStendiNyegezi
#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji

TABORA: Akiandika kupitia Akaunti yake ndani ya JamiiForums.com, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Watu walioshiriki kumuozesha Mwananchi Darasa la 6 Kata ya Mambali, Wilayani Nzega wamekamatwa na hatua za Kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao
Gwajima ambaye amesema alituma timu ifuatilie suala hilo baada ya kudokezwa na Mwananchi ameandika “Binti atarejea Shule na waliohusika watapambana na Sheria. Naitaka Jamii iache kuoa na kuoza Wanafunzi maana, utaratibu huo umepitwa na wakati, hivi sasa Wananchi wako macho na taarifa zinasafiri kwa kasi.”
Ameongeza “Ndugu Wananchi, mawasiliano ya Kidigitali ni msaada mkubwa kwenye Ulimwengu wa leo katika kuelimisha umma, kupokea na kupeleka taarifa na kuchukua hatua kwa gharama nafuu kabisa, wote mliowaoa Wanafunzi Watoto, warejesheni shule mara moja kabla hatujawafikia.”
Soma https://jamii.app/NdoaMtotoKusambaratishwa
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #DigitalRights #Accountability #ChildRights

Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Siasa anauliza unadhani mazungumzo baina ya Nape Nnauye (Mbunge) na Mwananchi huyu yalikuwa yanahusu nini?
Soma https://jamii.app/NapeNaWananchi
#Jamiiforums #JamiiAfrica #UchaguziMkuu #Siasa

❤1
Mdau wa Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki anadai walijuana na mpenzi wake Mwaka 2023 kupitia #Facebook, lakini sasa anachanganyikiwa na ndoto za kimapenzi ambazo mpenzi wake amekuwa akiota mara kwa mara kuhusu mpenzi wake wa zamani.
Je, unamshauri nini Mdau apeleke mahari au aache?
Kusoma kisa hiki https://jamii.app/MpenziKuota
#JamiiForums #JamiiAfrica #Lifestyle #JFChitChats

😁1
MOROGORO: Mdau wa #JamiiForums aliyelalamika juu ya ubovu wa Barabara ya Mazimbo–Manyuki, akieleza kuwa ilikuwa kero kubwa kwa wakazi na changamoto kwa madereva wa daladala na bajaji waliokuwa wakipata shida kuendesha shughuli zao za kila siku, hasa watumiaji wa vyombo vya moto.
Baada ya malalamiko, wahusika wameirekebisha barabara hiyo kwa Greda na hali imeimarika kwa sasa.
Hata hivyo, Mdau bado anatoa rai kwa mamlaka ifanyiwe maboresho ya kudumu kama kuweka lami kutokana na umuhimu wake
Soma Zaidi https://jamii.app/MazimboManyuki
#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Elimu #Uwajibikaji

Kiungo wa #YoungAfricans (Yanga), Peodoh Pacome Zouzoua ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Juni katika Ligi Kuu Bara 2024/2025, akiwashinda Clatous Chama wa #Yanga na Kibu Denis wa #Simba baada ya kuisaidia timu yake kushinda mechi tatu alizocheza Juni.
Kwa upande wa Kocha Bora, Miloud Hamdi wa Yanga amenyakua tuzo hiyo kwa kuiongoza timu yake kushinda mechi tatu akiwashinda kocha Rashid Taoussi wa Azam FC na Fred Felix wa Pamba Jiji.
Aidha, Meneja wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Jackson Mwendwa, ametangazwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi huo
Shiriki Mjadala https://jamii.app/PacomeTuzoJune
#JamiiForums #JFMatukio #JFSports

❤1👍1
Jeshi la Polisi usiku huu wa Julai 12, 2025 limethibitisha kumkamata Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), Brenda Rupia kwa ajili ya mahojiano kutokana na Tuhuma za kutoa Taarifa za Uongo na za Uchochezi na kwamba baada ya kumhoji hatua nyingine za Kisheria zitafuata kulingana na taratibu za nchi
Kabla ya taarifa hiyo, CHADEMA kilitoa taarifa kikieleza kuwa Brenda Rupia alizuiwa kuingia nchini #Kenya na kushikiliwa na mamlaka za mpakani eneo la Namanga ambako alikuwa safarini kuelekea Nairobi kwa ajili ya kikao kabla ya kuelekea Munich, Ujerumani, kushiriki mafunzo kuhusu Demokrasia na Uchaguzi
Zaidi soma https://jamii.app/BrendaPolisi
#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #Governance #Uchaguzi2025 #Democracy

Safari ya Ukuaji haijawahi kuwa kamilifu. Huwa ni polepole, imejaa changamoto na wakati mwingine unarudi nyuma.
Kila kosa linakufundisha na kila hatua ndogo huongeza hatua nyingine.
Kila mara unapojitokeza, unajenga kasi ya mafanikio.
#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha

Mwaka 2009, Timu ya #Yanga chini ya Kocha Kostadin Papic raia wa Serbia ilikuwa ikicheza soka la kuvutia, kikosi kikiundwa na wachezaji wengi mafundi
Mdau kama ulianza kufuatilia mpira kipindi cha wachezaji kama Fiston Mayele na Stephane Aziz, basi ni nafasi kwa Mashabiki wakongwe kutoa ushuhuda wao ili kizazi kipya wakijue kikosi cha 2009.
Soma Zaidi https://jamii.app/KikosiYanga2009
#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica #Football

Kwa kanuni hizi za uvaaji wa suti, mdau utatoboa kweli?
Kushiriki mjadala huu bofya :https://jamii.app/KanuniKuvaaSuti
#Jamiiforums #JamiiAfrica #JFlifestyle #JFChitChat

Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amemuandikia barua Rais Samia akitangaza kujiuzulu nafasi ya uwakilishi wa Tanzania nchini Cuba, eneo la Karibe, Amerika ya Kati pamoja na nchi rafiki za Colombia, Venezuela na Guyana
Katika barua hiyo, Polepole ameeleza kuwa ameamua kujiuzulu kutokana na mwelekeo wa kiuongozi unaokosa msimamo thabiti katika kusimamia haki za watu, amani, na heshima kwa wananchi
Aidha, ameeleza kutoridhishwa na kufifia kwa dhamira ya kweli ya uwajibikaji na kushughulikia changamoto za wananchi, sambamba na kudorora kwa maadili ya uongozi
Amesisitiza hawezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi na chama, haki, maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi
Polepole aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Novemba 2020 – Machi 2022), Balozi Malawi (Machi 2022 – Aprili 2023) na Cuba (Aprili 2023 – Julai 2025)
Soma https://jamii.app/PolepoleAjiuzuluUbalozi
#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #UtawalaBora

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM) lililokuwa katika eneo la Ubungo Kibo limeonekana katika hali ya kuvunjwa, leo Julai 13, 2025. Ikumbukwe baadhi ya Waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Ufufuo na Uzima) walihamia Kanisa la #KKAM kwa ajili ya ibada baada ya kufungwa kwa kanisa lao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Maximilian Machumu "Mwanamapinduzi", amesema hatua ya kuvunjwa kwa Kanisa la KKAM imetekelezwa kwa madai kuwa limejengwa katika eneo la barabara.
Soma https://jamii.app/KanisaKuvunjwa
#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #JFMatukio

MTWARA: Aliyekuwa Mbunge wa Mtwara Mjini na Makamu Mwenyekiti wa CUF, Maftaha Nachuma akiwahutubia wakazi wa Mtwara Julai 12, 2025, amesema aliamua kugombea Ubunge Mwaka 2015 licha ya kutokuwa na uhakika wa kuchaguliwa, kwa kuwa aliona mateso na manyanyaso kwa wakazi wa Mtwara, ikiwemo ukosefu wa miundombinu, maji na bandari kusahaulika.
Nachuma ambaye kwa sasa yupo #ACTWazalendo anadai juhudi zake zilivurugwa na Viongozi wa CUF walioshirikiana na CCM hali iliyomvunja moyo
Soma https://jamii.app/MaftahaNachumaSababuKuhamaCUF
#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Democracy #UchaguziMkuu2025

Uongozi si nafasi ya kufaidika, ni wajibu wa kutumikia Wananchi kwa uaminifu.
Kabla ya kuchagua Kiongozi, angalia anasimamia nini na ana uwezo gani, sio kumchagua kwa ushabiki au hisia.
#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa

❤2👏1