This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katika hali ambapo #Miundombinu mtaani inaharibika kutokana changamoto mbalimbali, Wananchi huathirika kwa kukosa huduma muhimu ikiwemo usafiri, afya, maji, elimu n.k
Hali hii inahitaji Viongozi wa ngazi za chini kuwajibika kwa haraka ili kuwezesha Wananchi kuendelea na shughuli zao bila kusubiri msukumo kutoka juu.
Mdau, unaupima vipi utendaji wa viongozi Mtaa unaoishi?
Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/UwajibikajiViongoziMtaani
#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance

MAREKANI: Paris Saint-Germain (#PSG) itakuwa uwanjani kumenyana dhidi ya #Chelsea katika Fainali ya Klabu Bingwa Dunia (#FIFAClubWorldCup) kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey, leo Saa 4:00 Usiku (muda wa Afrika Mashariki)
Timu hizo zimekutana mara 10, kila upande ukiwa umeshinda michezo mitatu, sare zikiwa nne
Ikumbukwe, Mashindano hayo yaliongezwa kutoka timu 7 hadi 32, yakihusisha klabu bora kutoka Kanda 6 Duniani ambazo ni UEFA, CONMEBOL, AFC, CAF, CONCACAF na OFC
Unadhani, Timu ipi yenye silaha kali itaondoka kifua mbele?
Kushiriki mjadala soma https://jamii.app/ChelseaVsPSG
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports

❤3
Mdau wa JamiiForums.com anaomba ushauri baada ya mwenye nyumba wake kupotea kwa muda mrefu bila kudai kodi. Anasema amejitahidi kumtafuta bila mafanikio na amejenga, anataka kuondoka hapo lakini hajui afanye nini. Unamshauri nini?
Mjadala zaidi https://jamii.app/NyumbaSijuiNifanyaje
#JamiiAfrica #JamiiForums #Lifestyle

DODOMA: Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Mtaalamu wa Fedha na Uwekezaji wa #CHADEMA, Leonard Magere kwa tuhuma za jinai zinazomkabili, taarifa imetolewa baada ya CHADEMA kutoa taarifa kuwa Magere hajulikani alipo tangu alipokamatwa na Polisi, Julai 12, 2025
Awali, CHADEMA ilitoa taarifa kuwa Magere amefichwa na Jeshi la Polisi baada ya kukamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere na kuwa hawakupata taarifa sahihi walipohoji Jeshi hilo juu ya alipo mwenzao
Wakati huohuo, CHADEMA imesema Mkurgenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Brenda Rupia amehojiwa na Polisi kuhusu taarifa aliyoitoa Julai 2, 2025 kuwa kuna mipango ya kumuwekea sumu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akiwa gerezani
CHADEMA imesema licha ya kuwa kosa analotuhumiwa lina dhamana kwa mujibu wa Sheria, Jeshi la Polisi limeendelea kumshikilia kwa madai bado linafanya mawasiliano na Viongozi wake wa juu
Soma https://jamii.app/CHADEMAUpdatesJulai13
#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #JFMatukio #Democracy #HumanRights

MAREKANI: Timu ya Chelsea FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia baada ya kuishusha PSG kipigo cha Magoli 3-0 katika Fainali ya michuano hiyo ambayo ilishirikisha vikosi 37
Licha ya PSG ambaye ni bingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kupewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo, mambo yalikuwa magumu kwao. Waliofunga katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa MetLife ni Cole Palmer (22 na 30) pamoja na Joao Pedro (43)
Cole Palmer anakuwa Mwingereza wa tatu kufunga goli katika Fainali ya #FIFAClubWorldCup, wengine ni Wayne Rooney (2008) na Phil Foden (2023)
Chelsea inabeba kombe hilo kwa mara ya pili, ilitwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza Mwaka 2021 kwa kuifunga Palmeiras ya Brazil
Soma https://jamii.app/FIFAClubFinal

❤1
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita
#JamiiAfrica #JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons

Mdau wa JamiiForums.com ameandika kuwa mfumo wa mkopo kupitia Employee Self Service (ESS) una changamoto hasa kwenye marejesho ya mkopo.
Anaomba baadhi ya vipengele viboreshwe ili kuwasaidia Watumishi urejeshaji wa mikopo bila kulazimika kufika ofisi husika kwa kuwa kama Serikali imeamua kuirahisisha kwa kupeleka mambo Kidigitali basi hilo liendelezwe.
Soma https://jamii.app/BenkiMarejeshoESS
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #Uwajibikaji #Accountability #DigitalRights

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya #CHADEMA na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika inaendelea leo Julai 14, 2025 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo Mahakama itaanza kusikiliza shauri dogo la kumtaka Jaji Hamidu Mwanga kujitoa katika Shauri hilo, kutokana na Washtakiwa kukosa imani nae
Kwa mujibu Mawakili wa walalamikiwa wanadai hawana imani na Jaji huyo hasa kutokana na uamuzi wake wa kusitisha Shughuli za Kiutendaji za Chama na utumiaji wa rasilimali ambao unaendelea mpaka kesi ya Msingi itakapoanza kusikilizwa
Ikumbukwe Julai 10, 2025 Jaji Hamidu Mwanga alisema suala hilo hatalitolea uamuzi bila kutoa nafasi kwa upande wa waliofungua kesi nao kupitia hoja. Ambapo upande wa wafungua shauri kupitia Wakili wao waliomba ahirisho ili kupata nafasi ya kupitia ombi hilo
Soma https://jamii.app/KesiCHADEMAKumkaataaJajiMwanga
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio #KuelekeaUchaguzi2025

CAMEROON: Rais Paul Biya, ambaye ana umri wa Miaka 92, akishikilia rekodi ya kuwa Rais mwenye umri mkubwa zaidi Duniani kwa sasa, ametangaza kutetea nafasi ya Urais katika muhula wa Nane katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12, 2025.
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Rais Biya alisema uamuzi wake wa kugombea umetokana na wito kutoka kwa Wananchi wa mikoa yote 10 ya #Cameroon pamoja na raia wa Nchi hiyo wanaoishi nje ya nchi.
Biya alichukua madaraka rasmi Mwaka 1982 baada ya mtangulizi wake, Ahmadou Ahidjo kujiuzulu, tayari ameongoza kwa zaidi ya Miongo minne, iwapo atashinda Uchaguzi ujao, anaweza kuongoza hadi atakapofikisha Miaka 99.
Kusoma zaidi bofya https://jamii.app/RaisWaCameroon
#Jamiiforums #JamiiAfrica #Demokrasia #Governance #UtawalaBora #Demokrasia

LINDI: Chama cha #ACTWazalendo kimetoa taarifa kuwa Kiongozi mstaafu wa chama hicho, #ZittoKabwe, alishikiliwa na Jeshi la Polisi, Saa Sita Usiku, Julai 14, 2025, baada ya kuvamiwa akiwa hotelini, baadaye alipelekwa Kituo cha Polisi akazuiwa kwa zaidi ya dakika 30 bila kuelezwa kosa lake mara moja
ACT imeeleza baada ya majibizano ya muda mrefu Askari walisema wanamshikilia kwa kosa la kutoa kauli za vitisho alivyotoa wakati wa hotuba yake ya Julai 10, 2025 kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini, ambapo chama kimeeleza aliachiwa Saa Nane Usiku bila masharti
Ikumbukwe, Zitto alinukuliwa akisema Askari yeyote au Watendaji wa Serikali watakaojihusisha na Kura Bandia wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 basi mhusika au Wahusika “watakuwa halali yao”
Soma Zaidi https://jamii.app/ZittoPolisi
#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #JFMatukio #Democracy #Siasa

Mitandao si mahali pa kuficha chuki. Tumia sauti yako kwa Hekima, Heshima na Huruma.
Chuki haijengi Jamii. 'Comment' Kistaarabu
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa