Kaimu Katibu Mkuu wa #CHADEMA, John Mnyika amesema zuio la Jaji Hamidu Mwanga dhidi ya matumizi ya rasilimali za Chama limeathiri utendaji, kusababisha kusimamishwa kwa Wafanyakazi wote na kuacha ofisi zao bila ulinzi
Akizungumza Mahakamani katika shauri dogo la kumtaka Jaji Mwanga kujitoa katika Shauri hilo, kutokana na Washtakiwa kukosa imani nae, Mnyika amesema mali za CHADEMA zipo hatarini kuibiwa au kuharibiwa, huku akidai zuio hilo linakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano na linaathiri shughuli za Kisiasa za Chama
Ikumbukwe, Kesi ilifunguliwa mnamo Juni 10, 2025 dhidi ya Katibu Mkuu wa #CHADEMA pamoja na Bodi ya Wadhamini, ikiwa ni sehemu ya mvutano wa ndani kuhusu uhalali wa maamuzi na usimamizi wa mali za chama. Mchakato wa shauri hilo bado unaendeelea
Soma Zaidi https://jamii.app/BodiYaWadhamini
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio #KuelekeaUchaguzi2025

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya #CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama John Mnyika, ya kumtaka Jaji Hamidu Mwanga kujitoa katika Shauri hilo imeahirishwa hadi Julai 28, 2025 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar
Jaji Hamidu Mwanga aliyesimamia kesi hiyo amesema atatoa uamuzi kama anaendelea na shauri hilo au anajitoa kama ombi lilivyowasilishwa na upande wa CHADEMA wakitaka ajiondoe kwenye shauri hilo wakidai ana mgongano wa maslahi (Katika video ni Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala wa CHADEMA akifafanua kilichotokea Mahakamani leo Julai 14, 2025)
Soma https://jamii.app/KesiCHADEMAKumkaataaJajiMwanga
#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #KuelekeaUchaguzi2025 #Siasa #CivilRights

❤1
KENYA: Ofisi ya Msajili wa Ndoa imeanza rasmi zoezi la kuchapisha taarifa za Wanandoa watarajiwa kama majina yao, picha pamoja na sehemu watakazofanyia harusi Mtandaoni kupitia tovuti ya Serikali ya eCitizen
Kabla ya utaratibu huu mpya wa kuweka taarifa Mtandaoni, Wanandoa walitakiwa kuwasilisha Notisi ya Ndoa (Notice of Marriage) ambayo ilikuwa inabandikwa kwa siku 21 katika mlango wa Ofisi ya Msajili wa Ndoa, ili kutoa fursa kwa yeyote mwenye pingamizi la Kisheria kuwasilisha malalamiko yake
Wakati lengo la hatua hiyo limetajwa kuwa ni kuongeza uwazi na kurahisisha huduma kwa Wanandoa, baadhi ya Wakenya kupitia Mitandao ya Kijamii walilalamika, wakidai hatua hiyo inakiuka Sheria inayolinda Taarifa Binafsi za Wananchi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Kenya
Kupata taarifa zaidi soma https://jamii.app/MsajiliKenya
#JamiiAfrica #JamiiForums #DataPrivacy #DigitalRights #UlinziWaTaarifaBinafsi

UGANDA: Akiwa na umri wa Miaka 86, Jenerali mstaafu Moses Ali ameanza rasmi kampeni za kugombea Ubunge katika Jimbo la Adjumani West kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2026
Baada ya Rais Yoweri Museveni kuingia madarakani Mwaka 1986, Jenerali Moses alipandishwa vyeo hadi kuwa Jenerali na kushika nyadhifa Mbalimbali Serikalini, ikiwemo Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza (2016–2021) na Naibu Waziri Mkuu wa Pili (2021 hadi sasa)
Alichaguliwa tena kuwa Mbunge wa Adjumani Mwaka 2011 akiwa na umri wa Miaka 72
Shiriki Mjadala https://jamii.app/JeneraliMosesKampeni
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance

Kupitia Jukwaa la Entertainment ndani ya Jamiiforums.com Wadau wanajadili kuhusu tamthilia maarufu zilizovuma nchini Tanzania Miaka kadhaa nyuma
Tuambie Mdau, ipi ni tamthilia yako pendwa kati ya hizi na inakukumbusha nini?
Kushiriki mjadala huu bofya: https://jamii.app/TamthiliaZaZamani
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFBurudani #Zilipendwa
Tuambie Mdau, ipi ni tamthilia yako pendwa kati ya hizi na inakukumbusha nini?
Kushiriki mjadala huu bofya: https://jamii.app/TamthiliaZaZamani
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFBurudani #Zilipendwa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MARA: Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA, John Heche amesema kama mabadiliko wanayoyadai yatafanyika kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025, chama chake kitampelekea Mwenyekiti wao Taifa, Tundu Lissu fomu ya kugombea Urais akiwa Gerezani
Amesema hayo Julai 11, 2025, alipokuwa akizungumza na makada wa CHADEMA Mjini, Musoma
Soma https://jamii.app/MabadilikoFomuLissuRais
#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji

GEITA: Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imemkuta na hatia Mwalimu wa Shule ya Msingi Waja Springs, Josephat Masenema Shikome, na kumhukumu kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumuingilia kinyume na maumbile mwanafunzi wake wa darasa la 3 mwenye umri wa miaka 7
Katika kesi hiyo ya jinai Na. 32126 ya mwaka 2024, upande wa mashtaka ulileta mashahidi kadhaa wakiwemo Mama mzazi wa Mtoto, Mtoto mwenyewe, Afisa Ustawi wa Jamii, Daktari, na Maafisa wa Polisi, ambapo Mtoto alieleza kuwa tukio hilo lilitokea katika choo cha Shule
Ikumbukwe, Desemba 9, 2024, Mdau wa JamiiForums.com aliandika “Mamlaka fuatilieni kesi ya Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Waja anayedaiwa kulawitiwa na Mwalimu, kuna mazingira tata”. Mdau alidai kuna mazingira ya kuminywa kwa haki katika shtaka hilo
Soma https://jamii.app/HukumuGeita
#JamiiForums #Accountability #ChildRights #HumanRights #Governance #Uwajibikaji #HakiZaMtoto

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
JF KUMBUKIZI: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa kupitia (#CUF), Selemani Bungala (Bwege) aliwahi kusema Mbunge si wa chama, bali ni mwakilishi wa Wananchi, alisema hayo Bungeni Februari 6, 2020 alipokuwa akichangia mada katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati
Shiriki Mjadala https://jamii.app/MbungeSelemani
#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji #UtawalaBora #Siasa

Denmark itakuwa Nchi ya kwanza Ulaya kutoa Hakimiliki kwa raia wake juu ya matumizi ya Sura, miili na Sauti zao ili kukabiliana na video na sauti za kughushi "deepfakes" za Akili Unde zenye maudhui ya ngono, utapeli na propaganda za Kisiasa
Pendekezo hilo itamaanisha kuwa Mtu akichakachua au kutumia taarifa zako kutengeneza video, sauti au picha bandia bila ruhusa unaweza kudai ziondolowe na hata kulipwa fidia
Sheria hiyo inatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika rasmi kabla ya mwisho wa Mwaka 2025 na iwapo majukwaa ya #Teknolojia yatashindwa kuondoa maudhui yatakayoripotiwa yatakabiliwa na faini kubwa
Mdau unadhani Sheria kama hii inaweza kutumika kwa Nchi za Afrika?
Mjadala zaidi https://jamii.app/DenmarkFightsDeepfakes
#JamiiAfrica #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #DigitalRights

👍2❤1
Maisha hayahitaji ukamilifu bali moyo wa kuendelea hata baada ya kuanguka.
Kila ushindi una historia ya majaribu, machozi, na wakati wa kukata tamaa lakini tofauti ya mshindi ni kwamba hakuwai kuchoka.
#JamiiAfrica #JamiiForums
#AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Kila ushindi una historia ya majaribu, machozi, na wakati wa kukata tamaa lakini tofauti ya mshindi ni kwamba hakuwai kuchoka.
#JamiiAfrica #JamiiForums
#AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imeondoa shauri la awali lililofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Ufufuo na Uzima), linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kufuatia hatua ya Serikali kulifungia kanisa hilo.
Maombi ya kuondoa shauri hilo yaliwasilishwa na Wakili Alphonce Nachipyangu, baada ya Serikali kuwasilisha barua rasmi inayomtaja mteja wao kwa jina sahihi linalotambulika kisheria, hivyo wanasheria wa kanisa hilo wanatarajia kuwasilisha maombi mapya kwa kufuata taratibu zote.
Aidha, Juni 2, 2025, waumini wa kanisa hilo walizuiwa kufanya ibada baada ya Vyombo vya Dola kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya Kanisa hilo. Ikumbukwe pia, waumini 52 walifungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu na Mkuu wa Jeshi la Polisi wakidai kukamatwa na Polisi Juni 29, 2025 wakiwa katika ibada eneo la Ubungo, wakitekeleza haki yao ya kikatiba ya kuabudu.
Soma Zaidi https://jamii.app/ShauriKanisaGwajima
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Accountability #JFMatukio

DAR: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu inaendelea leo Julai 15, 2025, siku 14 tangu iliposikilizwa mara ya mwisho, ambapo unasubiriwa uamuzi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na jalada ambalo ilielezwa lipo mezani kwake.
Mara ya mwisho kesi hiyo inayotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliahirishwa baada ya Mahakama kukubali maombi ya Jamhuri ulioeleza mpaka Julai 1, 2025, bado DPP alikuwa hajafanya uamuzi wa jalada la kesi ambalo lipo mezani kwake.
Ikumbukwe, Lissu aliiomba Mahakama kuagiza upande wa Jamhuri kulipeleka shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kama wamekamilisha ushahidi au Mwendesha Mashtaka aonyeshe nia ya kutoendelea na shauri lake, hivyo amuachie huru (nolle prosequi).
Zaidi soma https://jamii.app/LissuKujiteteaMwenyeweLeo
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #CivilRights

Nchi ya #Kenya imeandika historia mpya hivi karibuni baada ya kuondoa rasmi hitaji la 'Visa' kwa raia wa nchi zote za Afrika isipokuwa kwa raia wa Somalia na Libya.
Kupitia sera hii mpya, raia kutoka nchi mbalimbali za Afrika wataruhusiwa kuingia Kenya bila Visa na kukaa kwa muda usiozidi miezi mitatu, upande wa raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wao wataruhusiwa kuishi nchini humo kwa muda usiozidi Miezi Sita.
Mbali na Kenya, nchi nyingine Afrika ambazo pia zimefuta masharti ya Visa kwa raia wa mataifa mengine ya Afrika ni pamoja na Benin, Ushelisheli, Rwanda na Gambia.
Zaidi soma https://jamii.app/KenyaYaondoaZuio
#JamiiAfrica #JamiiForums #Diplomasia #Governance

❤2👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza kupitia Kipindi cha One on One cha Wasafi TV, Mbunge wa Ilemela (Mwanza), Angelina Mabula amesema anapotoa fedha kwa Wananchi wake lengo lake ni zitumike katika maendeleo ya Jamii na siyo kwa ajili ya kununua Kura na kwamba haiendi kwa Mtu Binafsi.
Aidha, ameongeza kuwa tabia ya Wanasiasa kutoa fedha ili wapigiwe Kura si sahihi na ni kinyume cha utaratibu.
Shiriki Mjadala https://jamii.app/MabulaSitoiFedha
#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #Siasa

🥰1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, #TunduLissu akipinga ahirisho la shauri la Uhaini linalomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amesema kuwa kesi inayomkabili ni ya kisiasa kwasababu ni mwaka wa uchaguzi mkuu, na yeye kukamatwa na kupewa kesi ya uhaini, siyo kwasababu ni mhaini, bali watu waende kwenye uchaguzi wasisumbuliwe na 'No Reforms, No Election'
Lissu ameongeza kuwa kesi yake imechafua nchi na kuendelea kuahirishwa kwake kunaharibu taswira ya #Tanzania kwenye Jumuiya za Kimataifa na Duniani kwa ujumla.
Soma zaidi: https://jamii.app/TunduLissuKesiKimataifa
#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #CivilRights
Lissu ameongeza kuwa kesi yake imechafua nchi na kuendelea kuahirishwa kwake kunaharibu taswira ya #Tanzania kwenye Jumuiya za Kimataifa na Duniani kwa ujumla.
Soma zaidi: https://jamii.app/TunduLissuKesiKimataifa
#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #CivilRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), #TunduLissu ameelezea kuwa amechoshwa na shauri lake kutofikia muafaka akitoa wito uamuzi ufanyike wa kupelekwa Mahakama Kuu au aachiwe huru kwa kuwa amekuwa Gerezani kwa Siku 97
Amesema hayo, leo Julai 15, 2025 wakati shauri la uhaini linalomkabili lilipokuwa likiendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Soma zaidi https://jamii.app/LissuMahabusu
#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #CivilRights
Amesema hayo, leo Julai 15, 2025 wakati shauri la uhaini linalomkabili lilipokuwa likiendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Soma zaidi https://jamii.app/LissuMahabusu
#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #CivilRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti #CHADEMA Taifa, Tundu Lissu akizungumza wakati wa kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Julai 15, 2025, amesema "Mimi siombi Huruma ya Mahakama, Sitaomba na sitaki huruma ya Mahakama, ninachotaka na ambacho nakisimamia ni utaratibu wa Mahakama usichezewe."
Soma https://jamii.app/SitakiHurumaLissu
#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #HumanRights
Soma https://jamii.app/SitakiHurumaLissu
#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #HumanRights
❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Taifa, #TunduLissu, imeahirishwa hadi Julai 30, 2025, hatua hiyo imekuja baada ya upande wa Jamhuri kuomba ahirisho, wakieleza Mahakama tayari wamewasilisha ombi la kuwakinga mashahidi, ambalo wamesema lipo Mahakama Kuu.
Hata hivyo, Lissu alipinga, akiomba Mahakama itumie mamlaka yake kufuta kesi hiyo kutokana na upande wa Jamhuri kuomba ahirisho mara kwa mara.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Mahakama ilitoa uamuzi kwamba licha ya hoja za Lissu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga ameutaka upande wa Jamhuri kuwa kama wana nia ya kuendelea na kesi hiyo, basi hatua zichukuliwe kwa haraka ili shauri hilo liweze kuwasilishwa Mahakama Kuu.
Soma https://jamii.app/UamuziKesiYaLissu
#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights

👎5❤3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Akizungumza kwenye kongamano la Vijana lililofanyika Viwanja vya Kanisa Kuu la KKKT USA River, Mchungaji wa Kanisa la KKKT Kijitonyama, Eliona Kimaro ametoa angalizo kwa Vijana kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vitakayosababisha kupata ulemavu wa mwili au kufunguliwa kesi katika kipindi hiki cha Uchaguzi
Akiwa katika kongamano hilo lililofanyika Julai 14, 2025, Mchungaji Kimaro alisema “Uchaguzi ni homa inayopita lakini Maisha yako yana thamani zaidi. Usibaki na ulemavu, usibaki na kesi Mahakamani kwa sababu ya Uchaguzi.”
Soma zaidi: https://jamii.app/MchungajiKimaroUchaguzi
#JamiiForums #JamiiAfrica #UchaguziMkuu #Siasa #Democracy