JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kama kijana una wajibu wa kutambua sio kila kitu kwenye mitandao ni cha kweli

Kabla hujasambaza taarifa, hakiki. Jenga tabia ya kuuliza kama Chanzo ni sahihi na kama Habari imethibitishwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
1
Kutambua haki zako bila kuelewa na kutimiza wajibu wako ni sawa na kuwa na gari bila mafuta, linaweza kuwa la kisasa na lenye uwezo lakini haliwezi kukupeleka popote.

Jamii bora hujengwa na raia wanaotambua kuwa haki huambatana na wajibu

Vijana tushiriki katika shughuli za kimaendelo, mikutano ya kijamii na majukwaa mbali mbali ili kuhakikisha Haki zetu zimezingatiwa na kushauri maboresho tunayoyataka kwenye jamii yetu

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
1
Kuwa Mwananchi bora ni kuishi kwa Misingi ya Haki, Usawa na kuheshimu majukumu yetu katika Jamii. Tunapojifunza kuwa na maoni ya kujenga, kuuliza maswali ya msingi na kushiriki kikamilifu katika mambo yanayoathiri Maisha yetu, tunajifunza pia kuwa Viongozi wa kesho

Kiongozi mzuri huanza kwa kusikiliza, kuelewa matatizo ya Wananchi wake na kuyatatua kwa pamoja, hivyo Kijana usiache kushiriki, kuhoji na kusimamia Uwajibikaji kwa kila mmoja wetu

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
Usikubali kuwa raia mtazamaji wa mustakabali wa Nchi yako. Taifa linahitaji Vijana wenye maono, Maadili na Moyo wa kujitoa, Vijana wanaochukua hatua badala ya kungoja.

Simama kwenye Misingi ya Haki na Uwajibikaji, sema kwa ujasiri dhidi ya Ukatili, Rushwa na Ubaguzi na Shiriki kwa vitendo kwenye shughuli za Kijamii, mchakato wa Uchaguzi au hata kwa kutoa Elimu na msaada kwa wengine

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
Elimu si tu kwa Ajira, bali inapaswa kuwafundisha Wanafunzi Maisha ya kuwajibika kama Raia.

Shule na Vyuo havipaswi kufundisha maarifa ya kazi pekee, bali pia kusaidia Wanafunzi kuwa Watu wenye Uwajibikaji, Uadilifu, na Heshima kwa Jamii.

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #RestlessDevelopment #CivicEducation #UraiaWenyeUelewa
1
Uwajibikaji unaanza na vitendo kama kushiriki mijadala ya Kijamii, kutoa maoni, kusaidia wenye uhitaji, kufuatilia sera na maamuzi ya viongozi na kujifunza haki na wajibu wetu kama raia

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #RestlessDevelopment #CivicEducation #UraiaWenyeUelewa
Upatikanaji wa taarifa sahihi ni silaha ya kwanza ya Raia katika kulinda Uhuru, Haki na Maendeleo ya Taifa lao.

Kama Wananchi hawapewi au hakuna upatikanaji wa taarifa sahihi, huwezi kuwategemea kufanya maamuzi ya Busara kuhusu Nchi yao. Hii huacha nafasi kwa Udanganyifu, Uongozi mbovu na Ukandamizaji.

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #RestlessDevelopment #CivicEducation #UraiaWenyeUelewa
Usiishi kwa mazoea au kudhani mambo fulani ni sawa kwa sababu 'watu wengi wanafanya'. Zijue Sheria mapema ili uweze kujilinda wewe na wengine pia

Jifunze kidogo kidogo kwa kujisomea na kusikiliza Vyombo vya Habari na hata kutumia mitandao mbalimbali ya kijamii.

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
👍1
Usikae pembeni ukisubiri taarifa zikutafute, nenda kwenye vikao, sikiliza, uliza maswali na toa mawazo yako

Hapo ndipo unakuwa sehemu ya mabadiliko yanayokuhusu moja kwa moja

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
Kuwa Mtu anayefikiri kwa uhuru, si kufuata tu kila kitu bila tafakari, fikra zako huru zinaweza kubadili Jamii au hali uliyonayo

Usikubali kila unachoambiwa bila kuchambua, usiamini kila taarifa au kauli bila kupima uhalisia wake

Uliza, chunguza, hakikisha unapata ukweli kabla ya kukubaliana

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
Kama raia, una nafasi ya kujielimisha kila siku. Tumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu, soma mabango ya Serikali barabarani, na sikiliza mijadala ya Bunge. Ndipo utaelewa haki zako, wajibu wako, na jinsi ya kushiriki kwenye maamuzi yanayogusa maisha yako.

Uraia ni zaidi ya kupiga kura ni kushiriki, kujua na kuwajibika

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
Uongozi si nafasi ya kufaidika, ni wajibu wa kutumikia Wananchi kwa uaminifu.

Kabla ya kuchagua Kiongozi, angalia anasimamia nini na ana uwezo gani, sio kumchagua kwa ushabiki au hisia.

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
2👏1
Uhuru wa kujieleza Mtandaoni ni haki ya Msingi kwa kila Mtu — lakini unakuja na Wajibu.

Toa maoni yako kwa hoja zenye Heshima ili kujenga Jamii yenye Fikra Pana na Maelewano.

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
1
Demokrasia inahitaji ushiriki wako ili iwe hai.

Ukikaa kimya, unawapa wengine mamlaka ya kuamua hatma yako bila mchango wako.

Tembela https://jamii.app/JukwaaJamiiForums

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Serikali za Mitaa zina wajibu wa kuandaa bajeti, kutunza fedha na kutoa taarifa katika vikao husika na kubandika katika mbao za matangazo kuhusu mapato na matumizi ya fedha kwa kila kipindi cha Mwaka wa Fedha kinapoisha.

Ni wajibu wa kila Mwananchi kufuatilia taarifa hizo ili kulinda maendeleo ya mtaa.

Je, ni mara ngapi umekuwa ukifuatilia taarifa za usimamizi wa fedha za Serikali ya Mtaa wako? Je, unaridhishwa na matumizi ya pesa hizo?

Zaidi soma https://jamii.app/MapatoMatumiziMtaa

VIDEO CREDITS: STAR TV

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
2
Uraia sio tu kupiga Kura au kudai Haki zako, ni pia kujitokeza kwa vitendo. Unaposaidia kusafisha mtaa, kuwasaidia watoto shuleni au kuwasaidia ambao wapo kwenye hali ngumu, unajenga jamii bora zaidi.

Mdau, wewe kama Raia unayewajibika huwa una tabia ya kujitolea kwenye jamii yako?

Tembela https://jamii.app/JukwaaJamiiForums

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
Simu yako ina nguvu ya kubadilisha Dunia sio kuumiza Watu. Tuitumie kwa hekima: kuelimisha, kuhamasisha na kujenga Jamii, sio kueneza uongo, chuki au udhalilishaji

Tembelea https://jamii.app/JukwaaJamiiForums

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
1
Ukikaa kimya mtu anapodhulumiwa, unakuwa mshirika wa dhuluma.

Sio kila vita ni ya silaha, nyingine ni ya kusimama na kusema; “Hii siyo sawa.”

Tembelea https://jamii.app/JukwaaJamiiForums

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
3
Tukipanda haki, wajibu na heshima kwa taifa la leo kesho tutavuna taifa bora.

Tembelea https://jamii.app/JukwaaJamiiForums

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
👍1
Bila uhuru wa vyombo vya habari, wananchi hukosa sauti na ukweli hukandamizwa.

Uhuru huu ni msingi wa haki, uwajibikaji na demokrasia.

Tembelea https://jamii.app/JukwaaJamiiForums

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa