JamiiForums
โœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Vipi Mdau, na wewe ni mpenzi wa Paa ndefu au huwa unazingatia nini kwenye Ujenzi wa Paa la Nyumba?

Shiriki Mjadala huu zaidi https://jamii.app/NyumbaBatiRefu

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFChitChats #JFStories
๐Ÿ‘1
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesema kuwa Ripoti ya Mkaguzi imeonesha maboresho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa hayawezi kukamilika kwa wakati kwa ajili ya kuandaa Mchezo wa Marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho uliopangwa kufanyika Mei 25, 2025

Taarifa ya CAF imeeleza kuwa (Kama ilivyotangaza awali) mchezo huo wa #Simba dhidi ya #RSBerkane unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Taarifa hiyo imeeleza kuwa #CAF itaendelea kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Serikali ya Tanzania na Wadau wote kuhakikisha Uwanja wa Mkapa na viwanja vyote vinakuwa tayari kwa Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) na kukidhi Kanuni na Viwango vya CAF yanayotarajiwa kuanza Agosti 2, 2025

Soma https://jamii.app/CAFMkapaStadium

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
๐Ÿ‘2โค1
USALAMA MTANDAONI: Jeshi la Polisi limetoa tamko kuhusu taarifa zilizosambazwa kupitia Akaunti za Jeshi la Polisi kwenye Mtandao wa X na kusema taarifa hizo ni za uongo, upotoshaji na zisizo na maadili

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema kuwa taarifa hizo si za kweli na wanaendelea kufuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo ili wakamatwe.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa aliyehusika na utengenezaji na utoaji wa taarifa hizo na yeyote yule ambaye ataendelea kuzisambaza

Soma https://jamii.app/TaarifaPotofuPolisiX

#JamiiForums #Misinformation #Accountability #DigitalSecurity
Taarifa ya Wizara ya Afya imesema vipimo vimeonesha hakuna kirusi kipya kinachoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha mlipuko aina ya Pandemiki. Ugonjwa wa #UVIKO19, umeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama yalivyo Magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa

Aidha, Wizara imesema hali ya kuongezeka na kupungua kwa Ugonjwa wa UVIKO-19 imekuwepo kila Mwaka tangu kutangazwa kwa Ugonjwa huu Mwaka 2020, kwa kipindi hiki ongezeko linaonekana zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam

Pia, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Nchi, hususan katika Mikoa ya Pwani, kumekuwa na ongezeko la hatari ya kuenea kwa Magonjwa yanayoenezwa na Mbu, kama vile Homa ya Dengue, Malaria, na Magonjwa mengine ya aina hiyo.

Soma zaidi https://jamii.app/OngezekoUvikoMbu

#JamiiForums #JamiiAfrica #PublicHealth #Afya
๐Ÿ‘2
Mwanachama wa JamiiForums.com anasema Nchi nyingi ambazo zilitafuta Amani bila kuzingatia Haki za Binadamu zilishindwa kwasababu Amani waliyoipata ilikuwa ya muda mfupi na isiyo na maana.

Tembelea Mjadala huu https://jamii.app/HakiAmani

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Democracy
MICHEZO: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com, Mei 13, 2025 kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya tukio la Viongozi wa Simba Queens kuwashambulia Waamuzi baada ya mchezo dhidi ya Mashujaa Queens, Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia Meneja wa Simba Queens, Selemani Makanya kwa Miezi 6 na kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5

Mchezo huo wa Mei 12, 2025 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo uliomalizika kwa sare ya 2-2, baadhi ya Viongozi wa Benchi la Ufundi la Simba Queens walianzisha vurugu na kuwavamia Waamuzi, wakipinga baadhi ya maamuzi yaliyotolewa uwanjani

Pia, Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Mgosi amefungiwa mechi tatu na kutakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5 kwa kuzingatia Kanuni ya 46(2) (1) ya Ligi za Wanawake.

Soma https://jamii.app/SimbaQueensAfungiwa

#JamiiForums #JFMichezo #JFSports #Accountability
โค1๐Ÿ‘1
DAR: Mwenyekiti wa zamani wa #CHADEMA, #FreemanMbowe ameeleza sababu ya kukaa kimya tangu Uchaguzi Mkuu wa chama hicho, Januari 22, 2025 ulipomalizika, akidai wanaotakiwa kuzungumza kwa sasa ni Viongozi waliokabidhiwa Mamlaka na chama

Mei 19, 2025, alipoulizwa sababu ya kuwa kimya, alijibu โ€œNiseme nini my brother!? Wasemao ni wenye mamlaka.... wasije wakadai tunawashwawashwa.โ€

Ikumbukwe Mei 18, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob โ€œBoni Yaiโ€, alitangaza hana mpango wa kuhama chama, akadaia anaamini baadhi ya Makada wa chama hicho wanaohama wakitumia jina la Mbowe hawajatumwa na Mwanasiasa huyo

Soma https://jamii.app/MboweNukuu

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
๐Ÿ‘2
GEITA: Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa Kilometa 3 na barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 1.66 umekamilika na unatarajiwa kuzinduliwa Juni 19, 2025

Ikumbukwe, mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamekuwa wakilalamikia matumizi ya vivuko eneo hilo kuwa yanachangia foleni na msongamano wa Abiria kutokana na changamoto ya kupata hitilafu mara kwa mara, wakawa wanatoa wito ujenzi wa Daraja ukamilike ili kupunguza usumbufu huo

Soma https://jamii.app/KigongoBusisiDaraja

#JamiiForums #ServiceDelivery
Huko Nchini Sweden, kuna hoteli ya barafu tupu ambayo hujengwa upya kila mwaka. Wasanifu wa Majengo kutoka duniani kote hualikwa kusanifu (design) vyumba vya hoteli hiyo, hivyo kuvifanya vya kipekee na vyenye mandhari ya kushangaza kila Msimu

Huko ndani je? Ni maajabu! Kila kitu ni barafu: Vitanda, taa, sanamu hadi glasi za vinywaji nazo ni barafu tupu! Kuhusu baridi usijali, japo joto hushuka hadi nyuzi -5ยฐC, wageni hulala vizuri kwenye mifuko ya kulalia yenye joto kali

Mdau, unaweza kulala siku ngapi kwenye hii hoteli?

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #Tourism #IceHotel
โค1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro leo Mei 20, 2025 akizungumza kuhusu Mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia Nchini kumtetea Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema "Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za Uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa Sheria zetu lakini kwanini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? Huu ni unafiki, na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la Haki za Binadamu tupo vizuri sana"

Soma https://jamii.app/NdumbaroZuioWakenya

#JamiiAfrica #JamiiForums #Diplomasia #Democracy #Governance
๐Ÿ‘Ž3๐Ÿคฎ1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Diwani wa Kata ya Kaloleni, Mji wa Tunduma, Hamis Chuma amesema analaani tukio la mauaji ya Katekista wa Kanisa Katoliki, Vincent Mwenda ambaye alifariki Mei 10, 2025 kwa kushambuliwa na Watu ambao bado hawajajulikana alipokuwa nyumbani kwake

Amesema tukio hilo linaumiza Jamii na linaogopesha Watu, ametoa ushauri Wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na kutoa taarifa kila wanapoona kuna dalili ambazo sio nzuri kwa kuwa ukimya unaweza kusababisha matukio ya aina hiyo kuendelea

Ibada ya kuuaga mwili wa marehemi ilifanyika katika Porokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Tazara Jimbo la Sumbawanga

Jitihada za kupata taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mkoa zinaendelea

Soma https://jamii.app/MauajiTunduma

#JamiiForums #HumanRights #Accountability #JFMatukio