JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ukimuuliza Mtanzania kuhusu Nchi za #Nordic, yaani Sweden, Norway, Denmark, Finland au Iceland, wengi watasema: “Aaah zile nchi za maisha bora! Kule hakuna rushwa! Elimu ni bure na watu wao wana furaha kweli kweli”

Lakini, ni hayo tu unayoyajua?

Je, unajua uhusiano wao na Afrika ukoje? Wanavyotumia teknolojia kusaidia jamii? Tamaduni zao za kipekee? Au ushirikiano wao wa kimataifa unaoleta maendeleo ya kijamii?

Ni muda wa kuonesha maarifa yako. Bofya link na uone ni kwa kiasi gani unaelewa kuhusu Nchi za Nordic:

https://jamii.app/NordicDodoso

#JamiiAfrica #JamiiForums #NordicWeek
👍1
#MALEZI: Sera ya Uzazi na Malezi nchini Sweden inawapa Wazazi jumla ya Siku 480 za likizo ya Uzazi na Malezi yenye malipo pale Mtoto anapozaliwa au kuasiliwa. Iwapo kuna Wazazi wawili, kila mmoja anapewa Siku 240

Kwa Watoto waliozaliwa mwaka 2016 au baadaye, kila Mzazi ana siku 90 ambazo haziwezi kuhamishiwa kwa Mzazi mwingine kama hazitatumika. Mzazi mmoja (single parent) anapewa Siku zote 480

Wazazi pia wanaweza kuamua kuhamisha hadi Siku 45 za likizo yao kwa Babu, Bibi au Rafiki wa karibu wa Familia, anayewasaidia kulea. Wanaostahili likizo hii ni wanaolea badala ya kufanya Kazi, Kusoma au kutafuta Kazi

#JamiiForums #NordicWeek #ParentHood #LifeStyle
👍1
Raia wa Norway huwa na utaratibu wa kuwaacha Watoto wao nje iwe ni msimu wa joto au wa baridi kali kwa madai kuwa ni njia moja wapo ya Watoto hao wachanga kupata hewa safi na kujenga kinga dhidi ya Magonjwa kama Mafua na kikohozi

Utaratibu huu ukifanyika wakati wa baridi Watoto huvishwa nguo za joto na kuachwa kwenye Magari ya Kutembelea Watoto (Stroller) na mara nyingine hutumia Kipima Joto kufuatilia hali ya hewa

Mdau unaweza kumuacha mwanao nje kwenye baridi ili kuimarisha kinga yake dhidi ya Magonjwa ya Msimu wa Baridi?

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #ParentHood #Lifestyle
👍1
Ukimuuliza Mtanzania kuhusu Nchi za #Nordic, yaani Sweden, Norway, Denmark, Finland au Iceland, wengi watasema: “Aaah zile nchi za maisha bora! Kule hakuna rushwa! Elimu ni bure na watu wao wana furaha kweli kweli”

Lakini, ni hayo tu unayoyajua?

Je, unajua uhusiano wao na Afrika ukoje? Wanavyotumia teknolojia kusaidia jamii? Tamaduni zao za kipekee? Au ushirikiano wao wa kimataifa unaoleta maendeleo ya kijamii?

Ni muda wa kuonesha maarifa yako. Bofya link na uone ni kwa kiasi gani unaelewa kuhusu Nchi za Nordic: https://jamii.app/NordicDodoso

#JamiiAfrica #JamiiForums #NordicWeek
Finland inakadiriwa kuwa na Sauna (Bafu la Mvuke) Milioni 3.2 huku likiwa ni Taifa lenye idadi ya Watu zaidi ya Milion 5.5 (Takwimu za Mwaka 2023), hali ambayo inaonesha uwepo wa mabafu hayo sio fasheni au kitu cha gharama kubwa kwa Watu fulani kama ilivyo katika baadhi ya Nchi nyingi, bali kwao ni sehemu ya maisha na sehemu ya tamaduni

Baadhi ya faida za Sauna zinazoaminiwa na Wakazi wa #Finland ni kuwa: Matumizi ya mara kwa mara yanazuia matatizo makubwa ya Kisaikolojia, yanapunguza hatari ya kupata Ugonjwa wa Akili ikiwemo wa Dementia (kupoteza ufahamu)

Pia, inaongeza mabadiliko ya mapigo ya moyo na kuboresha kazi ya moyo, huboresha mzunguko wa damu na kuimarisha ulegevu wa mishipa ya damu. Wanaotumia mara kwa mara huwa na mfumo wa kinga wenye nguvu zaidi

#JamiiAfrica #JamiiForums #NordicWeek
2
Huko Nchini Sweden, kuna hoteli ya barafu tupu ambayo hujengwa upya kila mwaka. Wasanifu wa Majengo kutoka duniani kote hualikwa kusanifu (design) vyumba vya hoteli hiyo, hivyo kuvifanya vya kipekee na vyenye mandhari ya kushangaza kila Msimu

Huko ndani je? Ni maajabu! Kila kitu ni barafu: Vitanda, taa, sanamu hadi glasi za vinywaji nazo ni barafu tupu! Kuhusu baridi usijali, japo joto hushuka hadi nyuzi -5°C, wageni hulala vizuri kwenye mifuko ya kulalia yenye joto kali

Mdau, unaweza kulala siku ngapi kwenye hii hoteli?

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #Tourism #IceHotel
1
Handaki la Lærdal nchini #Norway ndilo handaki refu zaidi la barabarani Duniani ambalo inauunganisha Miji ya Lærdal na Aurland

Ujenzi wake ulianza Mwaka 1995 na kuanza kutumika rasmi Mwaka 2000.

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #Tourism #LærdalTunnel
Mwaka 2021, Denmark ilizindua Shamba kubwa zaidi la Upepo katika eneo la Skandinavia (Scandnavia) linaloitwa "Kriegers Flak." Shamba hili lina uwezo wa kuzalisha Umeme wa kutosha kuhudumia takriban Kaya 600,000 za Denmark

Hata hivyo, Upepo sio Nishati mbadala pekee inayotumiwa Nchini Denmark, nafasi ya kwanza inashikiliwa na Nishati ya Mimea (Bioenergy), ikifuatiwa na Upepo, Jua na Nishati kutoka kwenye Joto la Ardhini (Geothermal).

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #WindEnergy #RenewableEnergy
1
Wakati Barani Ulaya inajulikana wazi kuwa mchezo wa soka (Football) ndio namba moja kwa kupendwa na kufuatiliwa zaidi na Watu, Nchini #Finland hali ni tofauti, wao mchezo wao namba moja ni Ice Hockey

Mchezo huo unaongoza kwa umaarufu na kwa kufuatiliwa na watu wengi, hii inajumlisha wanaofuatilia kupitia TV (TV Viewership) na wanaofika uwanjani

Finland ilitwaa Ubingwa wa Dunia wa IIHF World Championship Mwaka 2022, 2019, 2011 na 1995, pia mpinzani wao wa jadi katika mchezo huo ni Sweden, licha ya kuwa mara kadhaa kumekuwa na ushindani mkali dhidi ya Canada na Marekani

Soma https://jamii.app/FinlandIceHockey

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #JFSports
Je, Viongozi wetu wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa Wananchi? Uwajibikaji wao unahusiana moja kwa moja na Maendeleo endelevu?

Usikose kuungana nasi kwenye mjadala kupitia #XSpaces ya JamiiForums, ambapo tutachambua mifano hai ya Nchi zenye Utawala bora, njia walizotumia kupata Mafanikio na nafasi ya Wananchi katika kuwawajibisha Viongozi wao

Usikose fursa hii ya kipekee ya kujifunza, kushiriki hoja mbalimbali, Mei 28, 2025 kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku

Kujiunga bofya https://twitter.com/i/spaces/1eaKbWqZegXGX

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSpaces #TheNordics #NordicWeek #Uwajibikaji #Accountability
Uwajibikaji una nafasi gani katika kuleta maendeleo endelevu? Na wale waliofanikiwa, walifanya nini tofauti?

Usikose kushiriki nasi kwenye mjadala huu muhimu, tukijifunza kutoka kwa mifano halisi na kuchambua hatua zinazoweza kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi na maendeleo ya jamii

Njoo utoe maoni, jifunze na kuwa sehemu ya mjadala wa kujenga Tanzania tunayoitaka, Jumatano hii, Mei 28, 2025, kuanzia Saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku, kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kujiunga bofya https://twitter.com/i/spaces/1eaKbWqZegXGX

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSpaces #TheNordics #NordicWeek #Uwajibikaji #Accountability
Mchezo wa #Handball ni mojawapo ya Mchezo mkubwa Nchini Denmark ambao ulivumbuliwa Nchini humo Mwaka 1898 na ni moja ya Michezo inayopendwa sana

Mpira wa 'handball' ni mkubwa, una ukubwa sawa na Tikiti Maji dogo, tofauti na Mpira mdogo unaojulikana Nchi nyingine. Mchezo huu ni wa kasi na ushindani mkubwa, ambapo Mabao 30 au zaidi yanaweza kufungwa katika Mechi ya Saa moja.

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #JFSports
1👍1