Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), #FreemanMbowe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), huku nafasi ya Makamu wake ikienda kwa Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu
Uchaguzi huo umefanyika leo Juni 26, 2024 katika Mkutano Mkuu wa TCD uliokuwa na Wajumbe kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), CHADEMA, ACT-Wazalendo, Chama Cha Wananchi (CUF) pamoja na NCCR Mageuzi ambapo Mbowe amepokea kijiti kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba
Viongozi hao wanatarajiwa kutumikia uongozi wa TCD kwa kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa Katiba ya TCD, nafasi hiyo inapatikana kwa mzunguko kwa vyama
Soma https://jamii.app/TCDUchaguzi
#Siasa #JFMatukio #Democracy #Governance

👍3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), Tanzania Bara, Tundu Lissu amesema tuhuma zinazotolewa na Mchungaji Peter Msigwa (aliyehamia #CCM) kuhusu CHADEMA lazima zijibiwe
Lissu amesisitiza kuwa ufafanuzi kuhusu mali za chama ikiwemo mashamba na pesa, utasaidia kuwatoa Wananchi na Wanachama wao wasiwasi
Aidha, Lissu amesema hana tofauti na Mwenyekiti wake, #FreemanMbowe kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa Mitandaoni lakini amesema bado ana dhamira ya kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025
Soma https://jamii.app/LissuJulai26
#Siasa #JamiiForums

👍4
DEMOKRASIA: Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo kuzungumza na Waziri wake, Hamad Masauni kuona namna ya kuwaachia Viongozi wa CHADEMA waliokamatwa Mkoani Mbeya, akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho, #FreemanMbowe, leo Agosti 12, 2024
Nchimbi amesema hayo akiwa katika Mkutano wa hadhara Kata ya Katoro, Geita, ambapo amesema amefanya jitihada za kuwatafuta Viongozi wa Vyama vingine vya Siasa ili wazungumze kama Vyama vya Siasa
Viongozi wengine wa CHADEMA wanaoshikiliwa na Polisi ni, Makamu M/Kiti-Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu, John Mnyika, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi "Sugu", Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, John Pambalu, Viongozi wa Baraza la Vijana, Twaha Mwaipaya, Moza Ally, Deusdedith Soka, Wakili Deogratias Mahinyila
Soma https://jamii.app/CCMYaiagizaSerikali
#JamiiForums #JFMatukio #Governance #Siasa

👍4👎3❤2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, #FreemanMbowe amesema wanatarajia kupokea taarifa ya Uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Mshauri wa chama hicho, Ali M. Kibao aliyeripotiwa kuuawa na Watu wasiojulikana na kueleza ikiwa tofauti na walichoona wataipinga
Mbowe amesema hayo baada ya zoezi la uchunguzi (Autopsy) wa mwili wa Kibao kumalizika huku ukishuhudiwa na Wakili wa #CHADEMA. Kibao amepatikana siku 1 baada ya kuripotiwa kuchukuliwa na Watu waliodaiwa kuwa ni Askari Polisi kutoka kwenye Basi la Tashrif na kutoweka naye
Aidha, Mbowe amesema Mamlaka za Kiserikali zitambue zina wajibika kutoa maelezo yanayoridhisha kwa Watanzania juu ya matukio ya Utekaji na Watu kupotea yanayoendelea nchini na waseme nani anapaswa kuwalinda
Soma https://jamii.app/MboweAutopsy
#JamiiForums #HumanRights #JFDemokrasia #JFMatukio #SayNoToAbduction

👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
TANGA: Mwenyekiti wa #CHADEMA, #FreemanMbowe amemwambia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kuwa amfikishie salamu Rais #SamiaSuluhuHassan kuwa anatakiwa kuunda Tume ya Kijaji ya Mahakama kuchunguza matukio ya utekaji na mauaji Nchini
Amesema Tume hiyo ambayo itachunguza pia tukio la mauaji ya aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA, Ali Mohamed Kibao, akiongeza kuwa kuacha Polisi kufanya uchunguzi huku nao wakiwa wanashutumiwa, halitakuwa jambo lenye manufaa
Soma https://jamii.app/MboweTanga
#JFMatukio #JamiiForums

👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: #FreemanMbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesisitiza hawatajitoa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwa wanataka Wagombea wao wote walioenguliwa katika mchakato warejeshwe
Soma https://jamii.app/CHADEMANov19
#Democracy #JamiiForums #JFMatukio
Soma https://jamii.app/CHADEMANov19
#Democracy #JamiiForums #JFMatukio
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara, #TunduLissu amesema hatua yake ya kutaka nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho inalenga kulinda heshima ya Kisiasa ya Mwenyekiti wa sasa #FreemanMbowe kwa maelezo kuwa Miaka 21 aliyoongoza imetosha na hatakiwi kufikia hatua ya kufukuzwa
Lissu ameyasema hayo alipohojiwa na Kituo cha BBC
Soma https://jamii.app/LissuBBC
#JamiiForums #Democracy #Siasa
Lissu ameyasema hayo alipohojiwa na Kituo cha BBC
Soma https://jamii.app/LissuBBC
#JamiiForums #Democracy #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Mwenyekiti wa #CHADEMA, #FreemanMbowe akizungumzia madai ya tuhuma za Rushwa ndani ya chama hicho amesema kumekuwa kukitolewa tuhuma ambazo hazina uthibitisho
Amesema hayo wakati akihojiwa na Clouds FM kuhusu Uchaguzi wa Chama hicho
Soma https://jamii.app/MboweInterview
#JamiiForums #JFDemocracy
Amesema hayo wakati akihojiwa na Clouds FM kuhusu Uchaguzi wa Chama hicho
Soma https://jamii.app/MboweInterview
#JamiiForums #JFDemocracy
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Mwanasiasa Godbless Lema ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Kanda ya Kaskazini amezungumza na Wanahabari, leo Januari 14, 2025 na kutangaza kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu katika kuwania nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho dhidi ya #FreemanMbowe ambaye anatetea nafasi hiyo
Soma https://jamii.app/LemaPress
#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
Soma https://jamii.app/LemaPress
#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Aliyekuwa Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amesema Mwenyekiti wa chama hicho, #FreemanMbowe aliwahi kumwambia kuwa amechoka na anahitaji kupata watu wa kumsaidia kazi hiyo
Soma https://jamii.app/LemaPress
#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
Soma https://jamii.app/LemaPress
#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Ezekia Wenje, ambaye ni Mtia nia wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) - Bara amezungumza na Wanahabari, leo Januari 16, 2025, amesema kulikuwa na mpango wa kumpindua Mwenyekiti wa chama hicho #FreemanMbowe wakati akiwa gerezani
Soma https://jamii.app/WenjePress
#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
Soma https://jamii.app/WenjePress
#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
👍2❤1
DAR: Kupitia ukurasa wake wa X (Twitter), Mwanasiasa, #FreemanMbowe amempongeza na kumtakia heri #TunduLissu licha ya kuwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa #CHADEMA hayajatangazwa
Mbowe ameandika “Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.”
Baada ya andiko hilo, John Heche akajibu “Asante sana Mwenyekiti, umetujenga na kutulea, umeonesha Demokrasia kwa kuongoza timu kusimamia uchaguzi wa wazi, huru na haki. Historia ya Tanzania itakukumbuka, kama mtu uliejenga Demokrasia na kuleta mageuzi makubwa kwenye Nchi na chama chetu.”
Soma https://jamii.app/MboweAkubali
#JamiiForums #Siasa #JFDemocracy #Demokrasia

👍2✍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakati matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa #CHADEMA yakisubiriwa kutangazwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City, baadhi ya Wanachama wameonekana wakifurahia muziki wakiongozwa na #TunduLissu ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti akishindana na #FreemanMbowe na Odero Odero
Soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA
#JamiiForums #Siasa #Democracy #Demokrasia

❤2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Wakili #TunduLissu ametangazwa kuwa mshindi katika nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa kwa kupata Kura 513 (51.5%) akifuatiwa na #FreemanMbowe aliyepata Kura 482 (48.3%) pamoja na Odero Odero aliyepata kura moja tu (0.01%)
John Heche ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kwa kupata Kura 577 dhidi ya Ezekia Wenje aliyepata Kura 372 na Mathayo Gekul aliyepata Kura 49
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar ameshinda Said Mzee Said kwa Kura 625 sawa na 89% ya Kura 706 huku halali zikiwa 700 na sita zimeharibika
Soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA
#JamiiForums #Siasa #Democracy #Demokrasia
John Heche ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kwa kupata Kura 577 dhidi ya Ezekia Wenje aliyepata Kura 372 na Mathayo Gekul aliyepata Kura 49
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar ameshinda Said Mzee Said kwa Kura 625 sawa na 89% ya Kura 706 huku halali zikiwa 700 na sita zimeharibika
Soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA
#JamiiForums #Siasa #Democracy #Demokrasia
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, #FreemanMbowe, amesema Uchaguzi wa kuchagua Viongozi Wakuu wa Chama hicho umeacha majeraha mengi ndani mwao, hivyo Viongozi wapya wakakiponye Chama
Soma https://jamii.app/MboweKaongea
#JamiiForums #Demokrasia #Governance #UchaguziCHADEMA #Accountability
Soma https://jamii.app/MboweKaongea
#JamiiForums #Demokrasia #Governance #UchaguziCHADEMA #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu #CHADEMA Bara, Benson Kigaila amesema baada ya Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho, Mwenyekiti wao mpya Taifa, #TunduLissu aliendeleza mashambulizi dhidi ya Wanachama waliokuwa wakimuunga mkono #FreemanMbowe hali ambayo anadai iliwaonesha kuwa bado wapo katika kipindi cha Uchaguzi
Aidha, amesema baada ya uchaguzi huo, waliomuunga mkono Mbowe waliendelea kushambuliwa na wafuasi wa Lissu na kwamba suala hilo limeleta ubaguzi, huku akidai baadhi ya wafausi kadhaa ambao walimuunga mkono Mbowe wanavuliwa Uanachama
Soma https://jamii.app/G55Mei7
#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025

DAR: Mwenyekiti wa zamani wa #CHADEMA, #FreemanMbowe ameeleza sababu ya kukaa kimya tangu Uchaguzi Mkuu wa chama hicho, Januari 22, 2025 ulipomalizika, akidai wanaotakiwa kuzungumza kwa sasa ni Viongozi waliokabidhiwa Mamlaka na chama
Mei 19, 2025, alipoulizwa sababu ya kuwa kimya, alijibu “Niseme nini my brother!? Wasemao ni wenye mamlaka.... wasije wakadai tunawashwawashwa.”
Ikumbukwe Mei 18, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob “Boni Yai”, alitangaza hana mpango wa kuhama chama, akadaia anaamini baadhi ya Makada wa chama hicho wanaohama wakitumia jina la Mbowe hawajatumwa na Mwanasiasa huyo
Soma https://jamii.app/MboweNukuu
#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Mei 19, 2025, alipoulizwa sababu ya kuwa kimya, alijibu “Niseme nini my brother!? Wasemao ni wenye mamlaka.... wasije wakadai tunawashwawashwa.”
Ikumbukwe Mei 18, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob “Boni Yai”, alitangaza hana mpango wa kuhama chama, akadaia anaamini baadhi ya Makada wa chama hicho wanaohama wakitumia jina la Mbowe hawajatumwa na Mwanasiasa huyo
Soma https://jamii.app/MboweNukuu
#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), #FreemanMbowe akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa Habari kuhusu msimamo wa “No Reforms No Election” amesema yeye sio mzungumzaji wa chama na kupendekeza waulizwe viongozi
Amesema hayo mara baada ya kushiriki katika uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, leo Julai 17, 2025
Soma https://jamii.app/MboweNoReforms
#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Uchaguzi2025
Amesema hayo mara baada ya kushiriki katika uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, leo Julai 17, 2025
Soma https://jamii.app/MboweNoReforms
#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Uchaguzi2025
❤2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), #FreemanMbowe amesema kitendo cha yeye kushiriki katika Uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ni kwasababu amealikwa na amefanya hivyo kwa kuwa ni Mzalendo, ni Haki yake kujua hatma ya Taifa inapangwaje.
Amesema hayo, leo Julai 17, 2025 baada ya uzinduzi huo na kuongeza, “Lazima ukweli utamalaki katika Taifa, tuache Unafiki, Viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wawe na utashi wa Kisiasa kurekebisha tulikotoka.”
Soma zaidi https://jamii.app/MboweNoReforms
#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Uchaguzi2025 #Demokrasia

❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Yericko Nyerere akiwa Kada wa #CHADEMA, Januari 21, 2025 wakati wa Uchaguzi wa Chama alipokuwa akimuunga mkono #FreemanMbowe aliyewania Uenyekiti Taifa na kushindwa na #TunduLissu, alinukuliwa akisema "Hiki chama unapigwa, unatulia, unaendelea na Maisha, tumeshawaambia hakuna kuhama.''
Hata hivyo, Agosti 6, 2025, Yericko akiwa pamoja na kada mwingine wa CHADEMA, James Mbowe wametangaza kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (#CHAUMMA).
Soma https://jamii.app/YerickoHakunaKuhamaChama
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFKumbukizi #Democracy #JFDemocracy #Siasa

❤4